Dunia Rafiki

Dunia Rafiki

Share

Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Dunia Rafiki, Non-Governmental Organization (NGO), Nera Street. Makongoro Road Isamilo, Mwanza.

Dunia Rafiki's mission is to promote early childhood development by uplifting and empowering childre and women through early education and care - advancing women entrepreneurship opportunities to foster a brighter future for every Tanzanian family.

09/04/2025

Mabadiliko ya hali ya hewa yanatishia kuvuruga wakati muhimu wa maisha ya mtoto na kuwafanya kuwa katika hatari zaidi ya athari kutoka kwa uhaba wa chakula hadi kuhamishwa kutoka kwa hali mbaya ya hali ya hewa.

Katika kukabiliana na kupunguza athari za mabadiliko ya tabia nchi, tunawaelimisha watoto na kuwashirikisha katika afua mbalimbali ikiwemo upandaji miti.

31/03/2025

Children in Actions for Climate Change ni programu yetu mpya inayoangazia kuwashirikisha kikamilifu watoto wadogo; kutetea mabadiliko ya tabianchi kupitia mipango mbalimbali ikiwemo elimu, upandaji miti na kampeni huku pia wakitaka nafasi katika meza za majadiliano ya sera ya tabianchi.



Children in Actions for Climate Change, our new program that focuses on actively engaging young children in advocating for climate change through various initiatives including education, tree planting and campaigns while also demanding a seat at the table in climate policy discussion.

17/03/2025

Takriban theluthi moja ya watoto walio chini ya miaka 5 nchini Tanzania wamedumaa, na upungufu wa virutubishi unasalia kuwa suala la afya ya umma.

Ni wajibu wetu sote kuchukua hatua madhubuti kuhakikisha kuwa kila mtoto anapata lishe bora kwa wakati kwa ustawi wake na jamii kwa ujumla.

13/03/2025

Dhamira yetu ni kukuza Maendeleo ya Utotoni kwa kuwainua na kuwawezesha watoto na wanawake kupitia matunzo ya mapema sambamba na kuendeleza fursa za ujasiriamali za wanawake ili kukuza mustakabali mwema kwa kila familia ya Kitanzania.

10/03/2025

Lishe ni Moja ya kichocheo muhimu katika ukuaji wa ubongo wa mtoto mdogo.

Mtoto asiye pata lishe bora, yupo katika hatari ya kuto kukua na kufikia utimilifu wake kamili.

Dunia Rafiki tunatekeleza program za lishe ili kuhakikisha Kila mtoto anakua na afya bora katika kipindi muhimu Cha ukuaji wa ubongo wake.

05/03/2025

Kuelekea siku ya wanawake duniani, tunapaswa kukumbuka kuwekeza katika elimu na uwezeshaji wa mtoto wa k**e kwa maisha yao ya baadaye - lakini pia katika siku zijazo kwakua binti wa leo ni mama wa kesho.

10/02/2025

Elimu ya awali ni muhimu na haki ya kila mtoto. Kwa bahati mbaya, si watoto wote wana fursa ya kupata elimu ya awali nchini Tanzania huku idadi kubwa ikiwa ni watoto wanatoka katika familia duni.

Dunia Rafiki ina lenga kukuza fursa za ujifunzaji wa mapema ili kuhakikisha kila mtoto anakua na mwanzo mzuri maishani.

05/02/2025

Zana za kuchezea ni muhimu katika maendeleo ya ukuaji na ujifunzaji wa mtoto hasa katika miaka ya mwanzo ya mtoto.

Ni jukumu letu sote kuhakikisha kila mtoto anapata fursa ya malezi bora na ujifunzaji wa mapema lakini pia kuhakikisha uwepo wa zana muhimu zinazo msadia mtoto kukuza uwezo wake wa kiakili, kimwili, kihisia na kimahusiano.

29/01/2025

22/01/2025

Kila mtoto anahitaji mwanzo mzuri wa maisha.

Ni jukumu letu sote kuhakikisha kila mtoto ana kua bila kizuizi, anapata elimu iliyo bora na anafikia ndoto zake.

21/01/2025

Unakaribishwa kusaidia na kufanikisha juhudi zetu za kuhakikisha kila mtoto wa Kitanzania ana kuwa na mwanzo mzuri wa maisha

17/01/2025

Mwanamke alie wezeshwa anaweza sio tu kukuza mtoto mwenye afya na furaha lakini pia atakae kua na kufikia utimilifu wake kamili.

Want your organization to be the top-listed Non Profit Organization in Mwanza?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Telephone

Address


Nera Street. Makongoro Road Isamilo
Mwanza

Opening Hours

Monday 08:00 - 16:00
Tuesday 08:00 - 16:00
Wednesday 08:00 - 16:00
Thursday 08:00 - 16:00
Friday 08:00 - 16:00