twfou_ndation
TWF inashughulika na
1. Michezo na burudani
2. Utalii
3. Kulea makundi maalumu
16/10/2022
Taasisi ya TWF iliandaa na kutekeleza mchezo wa mbio za pole (jogging) tarehe 15.10.2022
Ambapo vilabu vyote vya jogging toka wilaya ya Mbeya vilialikwa.
Mbio za pole zilimaliza Km 5.7 na baadae watu walifanya mazoezi ya viungo kabla ya kutawanyika.
13/10/2022
Wakazi wa Mbeya ni wakati wenu huu mnaalikwa kushiriki katika mchezo wa mbio za pole tarehe 15/10/2022. Mwambie na mwenzio si yakukosa... itakua ni wakati mzuri sana wa jamii kukutana pamoja na kuweza kuitambua vizuri TWENDE WOTE FOUNDATION 🔥🔥
08/10/2022
Wafuasi wa Twende Wote Foundation tukiongozwa na Katibu Mkuu Dada Elizabeth Kaponela, tulishiriki mazishi ya baba mzazi wa Mfuasi mwenzetu,, Severina Mwakateba.
Mazishi hayo yalifanyika Vwawa Mbozi.
twfou_ndation
06/10/2022
Hizi ni baadhi ya picha za matukio ya tarehe 01/10/2022 ndani ya Hospitali ya rufaa mkoa wa Mbeya
Tarehe 1.10.2022 TWF ilijitambulisha kwa jamii kwamba ipo na kuelezea kwa ufupi malengo yake kwamba ni kuifanya jamii kuwa ya watu wanaofurahia kuishi na kuwakumbusha watu kwamba wana wajibu wa kuwahudumia wengine,
Ilifanya ziara Hospital ya Rufaa ya Kanda, Mbeya. Ambapo ilifanya usafi hospitalini Rufaa, ofisi kuu iliyoko mjini Mbeya, na kitengo cha wazazi, Meta.
Baadae saa 5 asubuhi Twf iligawa zawadi chache kwa wagonjwa zaidi ya 150 waliolazwa wadi za wanawake na watoto katika maeneo hayo. Na hatimaye kutoa mapipa 6 ya kuhifadhia taka taka kwenye wadi za hospitali hizo.
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Contact the organization
Website
Address
Mbeya