UTUME FM RADIO 97.3MHz
Utume Fm Radio, North Eastern Diocese- Evangelical Lutheran Church Tanzania. Box 10 Lushoto Tanga, E-mail [email protected] - Lushoto – Tumaini Hostel.
MOTTO OF THE RADIO
‘TUNAKUFIKIA ULIPO’ TUSIKILIZE LIVE KUPITIA http://onlineradiobox.com/tz/utume973/player/... TUAMBIE UNATUSIKILIZA KUTOKA WAPI
29/11/2025
Umepanga kuabudu usharika gani kesho?
.k.k.t_vijana_taifa
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto amewataka wananchi kudumisha michezo kwaajili ya kuimarisha afya zao na utimamu wa miili yao.
Hayo ameyazungumza hii leo 29/11/2025 wakati wa kuhitimisha Bonanza la kimichezo lililohusisha Tarafa zote za Jimbo la LUSHOTO na mlalo.
Aidha Dkt. Ikupa Mwasogye amewataka wananchi kulinda afya zao na kuendelea kupima ili kujijua hususani katika kipindi hiki kuelekea kilele cha week ya UKIMWI Duniani ifikapo 1/12/2025.
Akihitimisha Risala yake Dkt. Mwasogye amezipongeza Taasisi na Asasi za kiraia na binafsi ikiwemo UTUME FM RADIO kwa kuendelea kutimiza amani kupitia Matamasha ya kimichezo na hamasa mbali mbali ambazo wamekuwa wakianzisha.
dc
22/11/2025
Tujiandae kwa Ibada.
RAIS Samia Suluhu Hassan amewatakiwa kheri ya wanafunzi 595,816 wa kidato cha nne ambao wameanza mtihani wa kuhitimu elimu ya sekondari leo katika shule takribani 5,868 nchini.
Katika ujumbe alioutoa kupitia mitandao yake ya kijamii loe Rais Samia amesema idadi hiyo ya shule inatokana na nyongeza ya shule 305 mpya, ambazo ni mara yake ya kwanza kufanya mtihani wa kidato cha nne.
Amesema shule hizo ni matokeo ya kazi wanayoendelea kufanya kuhakikisha kila mtoto wa Tanzania ana uhakika wa kupata elimu bora.
“Mwenyezi Mungu Mtukufu aliyewaongoza tangu elimu ya awali hadi leo awajalie utulivu mwifanye na kukamilisha vyema hatua hii muhimu kwenye maisha yenu.
Ikawe ibada njema.
27/09/2025
Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Dkt. Msafiri Joseph Mbilu, amewataka Watheolojia wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki waliopata mafunzo ya kozi maalumu ya Theologia katika Chuo Cha Kolowa Technical Training Institute (KOTETI) kuhakikisha wanakwenda kufundisha neno la Mungu kwa usahihi ili jamii iweze kuondokana na mafundisho potofu yanayoenea kwa kasi.
Askofu Dkt. Mbilu ameyasema hayo leo tarehe 27/9/2025 katika mahafali ya wahitimu wa kozi ya Theologia ngazi ya cheti ambapo amesema kwa sasa kumekuwa na mafundisho potofu ya neno la Mungu na yanayoenea kwa kasi hivyo wahitimu wa kozi hiyo maalumu wametakiwa kwenda kuhakikisha wanahuburi neno la Mungu kwa usahihi wake.
Askofu Dkt. Mbilu amesema Kanisa la Mungu linahitaji watumishi walio elimishwa vizuri ili kufundisha kweli ya neno la Mungu, huku akiwataka wahitimu hao kuhakikisha wanaendelea kujifunza zaidi juu ya Neno la Mungu.
Kwa upande wake Askofu Johan Tyrberg kutoka Dayosisi rafiki ya Lund-Sweden alipokua akihuburi amewaasa Wahitimu hao kwa kusema kuwa sasa wanatumwa rasmi kwenda kuifanya kazi ya Mungu lakini katika utumishi wao hawako peke yao bali uwepo wa Mungu utakuwa pamoja nao katika wajibu waliyoitiwa shambana mwa Bwana.
Kwa upande wao wahitimu hao wapatao 13 wametoa shukrani zao kwa Baba Askofu Dkt. Mbilu pamoja na Halmashauri Kuu ya KKKT-DKMs kwa kuona vema wao kupata mafanzo hayo maalumu yanayopelekea kubarikiwa kwao kuwa Wachungaji ifikapo tarehe 16/11/2025 katika Usharika wa Kanisa Kuu Lushoto.
27/09/2025
Tanzia
27/11/2024
Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Dkt. Msafiri Joseph Mbilu, amepiga kura kwa ajili ya kuchagua viongozi kwenye uchaguzi wa serikali za mtaa katika Kituo cha kupigia kura cha Uwalu kilichopo Wilayani Lushoto Mkoani Tanga tarehe 27 Novemba, 2024.
27/11/2024
Mkuu wa Wilaya ya Lushoto Mkoa wa Tanga Zephania Sumaye amesema zoezi la upigaji kura katika Halmashauri ya Lushoto linaendelea vizuri huku wananchi wakiendelea kusisitizwa kujitokeza katika vituo vya kupiga kura ili kuwachagua viongozi wanaowataka.
Sumaye ameyasema hayo mapema leo mara baada ya kuzindua zoezi la upigaji kura katika kituo cha kupigia kura kilichopo katika Kitongoji cha Chakechake na kuongeza kuwa hali ya usalama ni shwari na hakuna changamoto yoyote iliyojitokeza hivyo kila mwananchi aliyejiandikisha ajitokeze akapige kura katika kituo alichojiandikisha.
Ameongeza kuwa kamati ya ulinzi na usalama imejipanga vizuri kuimarisha ulinzi ambapo hata kubali kuona matukio yoyote yanayoashiria uvunjifu wa amani huku akiwataka wananchi wote mara baada ya kupiga kura kuondoka katika mazingira ya vituo vya kupigia kura.
Kwa upande wake Msimamizi wa uchaguzi wa Halmashari ya Wilaya ya Lushoto Ikupa Harsoni Mwasioge amesema kuwa katika Kitongoji hicho cha Chake Chake vipo vituo vya kupigia kura vilivyoongezwa ili kupunguza umbali kwa wapiga kura ambapo katika kitongoji hicho kina jumla ya vitu 30 hivyo wananchi waendelee kujitokeza katika zoezi hilo.
Nao baadhi ya wananchi ambao wamejitokeza katika zoezi hilo wamesema kuwa zoezi la kupiga kura linaendelea vizuri licha ya kuwepo changamoto ndogo ya utafutaji wa majina lakini wanashukuru uwepo wa wasimamizi kuwasaidia katika kutafuta majina yao na kupiga kura
26/11/2024
Msemaji Mkuu wa Serikali, Thobias Makoba, amesema idadi ya vifo vilivyotokana na kuporomoka kwa ghorofa Kariakoo Jijini Dar es salaam imefikia 29 hadi kufikia leo November 26,2024 huku akisema lipo pia zoezi linaloendelea la kutambua miili mingine kwa kutumia teknolojia ya vinasaba(DNA) na wakishathibitisha watatoa taarifa.
Akiongea mchana huu Kariakoo, Makoba amesema "Mpaka kufikia muda huu ambao tunazungumza kwa bahati mbaya namba ya marehemu ambao tumethibitisha ni 29, kwahiyo namba imeongezeka kidogo tunaendelea kuwaombea wenzetu wapumzike kwa amani"
"Lipo zoezi linaloendelea la kutambua miili mingine kutumia teknolojia ya vinasaba (DNA) na wenyewe tutatoa taarifa tukishathibitisha Ndugu pamoja na miili ya wenzetu, kwa upande wa majeruhi idadi ipo palepale"
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Contact the business
Telephone
Address
Lushoto
Tanga