Ruvuma
center of business How to get employed after completion of your studies like university. Get being into rich celebrating your work commenced by yourself.
I offer to give a good direction of community skills becoming employer wherever will you live. HOW.........?
1.Through allocating a capital of your program idea.
2.Granting an asserts for your program.
3.To employ those who are able to work for non-formal employment.
4.Loading..........
Usicheke, kuwa siriaz
Kajichanganya
Tulipigwa hapa
11/06/2023
Kupata vichekesho zaidi like page hii ya Ruvuma
01/06/2023
MKUU WA WILAYA YA MBINGA AYATAKA MAKAMPUNI YA UCHIMBAJI WA MAKAA YA MAWE KUTHIBITI VITENDO VIOVU VINAVYO FANYWA NA WATUMISHI WAO ILI KULINDA NA KUZUIA KUPOROMOKA KWA MAADILI
Mkuu wa Wilaya Mbinga *Mheshimiwa Aziza Mangosongo* alitoa wito huo alipokutana na kuzungumza na Meneja wa Migodi ya madini ya makaa ya mawe, Maafisa usafirishaji wa migodi ya, BECO, TANCOAL, RUVUMA COAL, JITEGEMEE, MILCOAL, viongozi wa Chama wa Ccm, Pamoja na wenyeviti, watendaji na wadau wa Maendeleo wa kata ya ruanda. Kikao hicho kilifanyika katika ukumbi wa parokia ya kanisa katoliki ruanda.
Ambapo Mhe. Mangosongo, Mkuu wa Wilaya Mbinga alisema kwamba lengo la kikao hicho ni kujadili na kuweka mikakati ya Kupambana na wimbi kubwa la kuporomoka kwa maadili pamoja na kupokea taarifa ya utekelezaji wa wa barabara ya kitai-ruanda inayojengwa kwa kiwango cha lami na mkandarasi CSRg kutoka china na barabara ya ruanda kuelekea katika maeneo ya uchimbaji wa makaa ya mawe.
Sambamba na hilo aliwataka watumishi na madereva kuacha tabia za kuwarubuni na kujihusisha na mapenzi na wanafunzi jambo ambalo huleta athari za mimba, kusababisha maradhi na kuacha shule kwa baadhi yao, Vilevile kuacha tabia ovu za kujihusisha na vitendo vya rushwa, uvunjaji wa sheria kwa kumwaga makaa ovyo barabarani, uharibifu wa mazingira kwa wamiliki wa migodi pasipo kufuata sheria za uhifadhi wa mazingira.
Aidha, Mhe. Mangosongo, Mkuu wa Wilaya ya Mbinga alipokea taarifa ya mradi wa barabara ya kitai-ruanda.Ambapo Mhandisi Rubara Narando Kutoka TANROADS Mkoa alisema mkandarasi yupo eneo la kazi na Mradi utakamilika ndani ya muda uliopangwa, alikadhalika alisema kwamba barabara ya ruanda kuelekea katika maeneo ya uchimbaji, mkandarasi ameshapatikana na kazi itaanza hivi karibuni na fedha zimeshatengwa.
Hata hivyo,Mhe.Mangosongo Mkuu wa Wilaya
aliwataka madereva kufunika vizuri makaa ya mawe ili kuondoa adha ya kuyamwaga ovyo, Pia alimtaka Mtendaji kata kuandaa taarifa ya idadi ya makampuni yanayojishughulisha na uchimbaji na taarifa hiyo ifike ofisi ya Mkuu wa Wilaya, Vilevile Aliwataka Mameneja wa migodi kushiriki vikao Kila vinapoandaliwa.
Vilevile alitoa agizo kwa makampuni hayo kutekeleza ujenzi wa ofisi ya Kijiji cha Ntunduwalo ndani ya kipindi cha miezi sita, Pia alimwagiza Meneja wa TARURA Wilaya kuhakikisha mkandarasi wa mradi wa barabara ya ruanda kuelekea katika maeneo ya uchimbaji jumatatu aanze kazi, Aidha alimtaka Mtendaji kata kuwachukulia hatua wale wanaojihusisha na matumizi ya madawa ya kulevya hususani bangi, vijiwe hivyo vife.
Naye, Kamanda wa TAKUKURU Wilaya ya Mbinga Ndugu Fredrick Msae alitoa rai kwa viongozi wa migodi kutenda haki wakati wa kutoa ajira, Hivyo wazingatie weledi na vigezo, kwasababu kupokea au kufanya upendeleo wakati wa kuajiri hivyo ni vitendo vya rushwa na ni kosa kisheria, vilevile ni makosa ambayo hayana dhamana kwa mujibu wa sheria.
Mwisho, Afisa Tarafa ya Namswea Ndugu Karimu Mzee alimshukuru Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya kwa kufanya ziara hiyo, alisema kupitia Kikao hicho kitaleta mabadiliko chanya kwa maslahi mapana ya taifa na ufanisi wa utekelezaji wa maendeleo ya Migodi.
*IMETOLEWA NA*
*OFISI YA MKUU WA WILAYA YA MBINGA*
*LEO MAY 31, MWAKA 2023*
Video ya Feisal iliyovuja wakimshauri vibaya kuichafua Yanga
Like page hii ya Ruvuma ujionee mengi yajayo...
Click here to claim your Sponsored Listing.
Telephone
Website
Address
P. O. Box 50 Mbinga
Songea