CCM MKOA Ruvuma

CCM MKOA Ruvuma

Share

Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from CCM MKOA Ruvuma, Tutor/Teacher, Barabara ya Sokoine, Songea.

29/03/2025

๐—–๐—›๐—”๐—ง๐—œ ๐—ก๐—” ๐—–๐—–๐—  ๐—จ๐—ฃ๐—”๐—ง๐—˜ ๐—จ๐—›๐—”๐—ž๐—œ๐—ž๐—” ๐—ช๐—” ๐— ๐—”๐—๐—œ๐—•๐—จ ๐—ฌ๐—” ๐— ๐—”๐—ฆ๐—ช๐—”๐—Ÿ๐—œ ๐—ฌ๐—”๐—ž๐—ข

Huna haja ya ku-google kupata majibu ya maswali yako kuhusiana na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwakuwa mpango mzima ni ku-chat nasi moja kwa moja na kupata majibu yaliyo nyooka ya maswali yako wakati wowote ule.

๐˜พ๐™๐™–๐™ฉ๐™ž ๐™ฃ๐™– ๐˜พ๐˜พ๐™ˆ ๐™ ๐™ช๐™ฅ๐™ž๐™ฉ๐™ž๐™– ๐™’๐™๐™–๐™ฉ๐™จ๐˜ผ๐™ฅ๐™ฅ ๐™ฃ๐™–๐™ข๐™—๐™– 0761825659 ๐™–๐™ช ๐™ฉ๐™š๐™ข๐™—๐™š๐™ก๐™š๐™– ๐™ฉ๐™ค๐™ซ๐™ช๐™ฉ๐™ž ๐™ฎ๐™š๐™ฉ๐™ช ๐™ฎ๐™– ๐’˜๐’˜๐’˜.๐’„๐’„๐’Ž.๐’๐’“.๐’•๐’›

#๐™†๐™–๐™ฏ๐™ž๐™‰๐™–๐™๐™ฉ๐™ช๐™๐™ช๐™ฃ๐™–๐™จ๐™ค๐™ฃ๐™œ๐™–๐™ˆ๐™—๐™š๐™ก๐™š๐™‹๐™–๐™ข๐™ค๐™Ÿ๐™–

23/05/2024
05/01/2024

๐Ÿ“Œ๐Ÿ“Œ TUPO WHATSAPP: TUFUATILIE KUPITIA CHANELI YA CHAMA CHA MAPINDUZI TAIFA. Link ipo kwenye Bio

Chama Cha Mapinduzi Taifa ndilo jina la chaneli rasmi ya CCM katika mtandao wa WhatsApp.

Fuatilia Chama Cha Mapinduzi Taifa channel on WhatsApp: Link kwenye Bio kwa wepesi wa kujiunga

Usichelewe wala kupitwa, wakati ni sasa. Ndugu mwanachama, mkereketwa, mpenzi, shabiki, mfuasi na mwananchi pata taarifa, habari na matukio mbalimbali ya CCM kiganjani mwako.

"Tunasonga Mbele Kidijitali."

๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ

๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ

24/10/2023

๐Ÿ“Œ๐Ÿ“Œ HONGERA NDG.RABIA ABDALLAH HAMID.

Hongera Ndg. Rabia Abdallah Hamid kwa kuaminiwa na kuteuliwa kuwa Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi Idara ya Siasa na Ushirikiano wa Kimataifa (SUKI).

Tunakutakia heri katika majukumu yako mapya.

24/10/2023

OFISI KUU YA UVCCM WILAYA YA SONGEA MJINI

Tarehe 23/10/2023 Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Songea Mjini Ndug, Mwl. JOACHIM KOMBA Akiwa ameambatana na Wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji UVCCM na Kamati ya Uendeshaji ya Chipukizi UVCCM Wilaya ya Songea Mjini amefanya Ziara ya Kikazi katika Kata ya LIZABONI

Akiwa katika Ziara hiyo Ametembelea na Kukagua Mradi wa Ujenzi wa Ofisi ya Serikali ya Mtaa wa Kichangani ambayo inajengwa kwa nguvu ya wananchi na kushirikiana na ofisi ya serikali ya Mtaa wa Kichangani amefurahishwa na Ujenzi huo ambao umefikia katika hatua ya Kuezekwa ambapo Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Songea Mjini ameahidi kuchangia kiasi cha Tsh. 100,000/= katika Ujenzi huo kwa ajili ya kuunga Mkono Kuhudi hizo za Wananchi pamoja na Serikali ya Mtaa wa Kichangani

Pia katika Ziara hiyo Mwenyekiti amemtembelea Mzee Mapunda ambaye ana Uhitaji Maalum wa Msaada wa kuezekewa Nyumba yake kutokana na nyumba hiyo kutokuwa katika hali mzuri kwa Makazi ya kuishi Watu hivyo Serikali ya Mtaa wa kichangani imefanikisha kumpatia bati Mzee huyo ambapo Mwenyekiti ameunga mkono juhudi hizo za Serikali ya Mtaa kwa Kumchangia Mzee huyo Boriti 20 kwa ajili ya kuezekea nyumba hiyo.

Aidha katika Ziara hiyo Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya Songea Mjini amepita Kupandisha Bendera za Chama Cha Mapinduzi Nyumbani kwa Mabalozi wa katika Kata hiyo ya Lizaboni.

Pia katika ziara hiyo amefungua Shina la Vijana wa Chama Cha Mapinduzi katika tawi la Madizini

Pia katika Ziara hiyo Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Songea Mjini alipata Fursa ya kufanya kikao cha ndani na Viongozi pamoja na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi.

Katika Kikao hicho amewashukru na kuwapongeza Viongozi na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi kata ya Lizaboni kwa Mapokezi Makubwa na Mazuri waliyompatia katika ziara hiyo

Pia amewapongeza kwa Ushirikiano Mkubwa waliokuwa nao baina ya viongozi wa Chama na Viongozi wa Serikali amewataka waendelee na Ushirikiano huo ili wananchi waendelee kupata Maendeleo kwa haraka zaidi.

Aidha Amewataka Vijana kujiandaa kikamilifu kuhakikisha wanajitokeza kwa wingi kugombea nafasi Mbalimbali katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa Mwaka 2024 na kuhakikisha Chama Cha Mapinduzi kinapata Ushindi wa kishindo katika Uchaguo huo wa Serikali za Mitaa

Pia amewataka Viongozi wa vijana kuepuka kuwa Madalali wa Viongozi wanaotaka Madaraka katika nafasi mbalimbali amewataka kuendelea kutimiza Majukumu yao ya kikanuni na kikatiba kuahakikisha wanawalinda Viongozi waliopo Madarakani ili wafanye kazi ya kuwatumikia wananchi kwa kuleta maendeleo katika Jamii zao.

Aidha amewataka Vijana kuendelea kuunga Mkono Juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe Rais DKT.SAMIA SULUHU HASSAN

Pia katika ziara hiyo Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Songea Mjini ameshiriki katika Mechi ya WENYEVITI UVCCM KATA&MATAWI Vs MAKATIBU UVCCM KATA &MATAWI ambapo katika Mechi hiyo Weneyeviti wameibuka na Ushindi wa goli Moja kwa Bila

WANA LIZABONI, HAKIKA LIZABONI IMEITIKA๐Ÿ™๐Ÿ™๐Ÿ™



๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ’ช๐Ÿ’ช_*

๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ๐Ÿƒโ€โ™‚๏ธ๐Ÿƒโ€โ™‚๏ธ

Imeandaliwa na kutolewa na Cde. KALELA- K/HAMASA NA CHIPUKIZI UVCCM WILAYA YA SONGEA MJINI._

23/10/2023

๐Ÿ“Œ KAZI IMEMPATA MWENYEWE, KAA TAYARI. TUFUATILIE.

Mwanachama, Mkereketwa, Mfuasi na Mpenzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) tufuatilie kupitia mitandao yetu ya Kijamii ya CCM; Instagram, X (zamani Twitter), Threads, Facebook, YouTube, Tik Tok, CCM App na Tovuti ya Chama(www.ccm.or.tz) .

Usikubali kupitwa, Kazi imempata mwenyewe.

Karibu Sana Ndg. Paul C. Makonda - Katibu wa NEC-Itikadi na Uenezi.

Photos from CCM MKOA Ruvuma's post 05/10/2023

Hongera sana Mh Judith kapinga na hakika umefanya jambo kubwa na ambalo halitasaulika kwenye historia ya UVCCM Mkoa wa Ruvuma.Mungu akutunze kwa maslahi mapana ya Nchi yetu,Serikali na Chama chetu na Zaidi Vijana wote wa Tanzania na mkoa wa Ruvuma.Wewe ni hazina ambayo inapaswa kulindwa na Vijana wa Nchi hii kwa Nguvu Zote

05/10/2023

TAYARI UMEJISAJILI KIELEKTRONIKI? JISAJILI SASA NA CCM APP

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinahimiza wanachama wapya na wazamani kujisajili kielektroniki kupitia simu ya kisasa ya mkononi (smartphone) kwa kupakua programu ya CCM App inayopatikana Playstore au AppStore kisha kulipa Ada, kuchangia michango, kuhariri taarifa za uanachama na kufuatilia matukio na Habari za CCM.

05/10/2023

Komred Jokate Urban Mwegelo
Katibu Mkuu wa Wanawake Tanzania

26/09/2023

UVCCM MKOA WA RUVUMA
26 SEPTEMBA, 2023

UJUMBE WA MWENYEKITI UVCCM TAIFA NDG.MOHAMED KAWAIDA KWA VIJANA WENZAKE.
MATATIZO HUISHA KWA KUSEMEZANA NA SIO KWA KUSEMANA

TUPENDANE.

Photos from CCM MKOA Ruvuma's post 25/09/2023

KAZI KUBWA INAFANYIKA YA UTEKELEZAJI WA ILANI KWA VITENDO.

Ruvuma, Tanzania.

SERIKALI IMEWATUA NDOO KICHWANI KWA SH BIL 20
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan ametoa zaidi ya shilingi bilioni 20 kutekeleza miradi ya maji katika Halmashauri ya wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma.

Katika kutekelza azma hiyo njema ya serikali ya awamu ya sita ,katika Kijiji cha Hongi Kata ya Liuli wilayani Nyasa serikali imepeleka mradi wa maji wenye thamani ya shilingi bilioni 4.7.

Miradi inayoendelea kutekelezwa katika wilaya hiyo pamoja na mradi wa maji Mwerampya kata ya Lituhi unaogharimu shilingi bilioni 6.5,mradi wa maji Kilosa Mbambabay unaogharimu zaidi ya shilingi bilioni 4 na mradi wa maji Ngumbo unaogharimu shilingi bilioni 2.5



Sauti Ya Watanzania
Ccm Makao Makuu
Comred Makao Makuu
CCM MKOA Ruvuma
Wazazi Ccm Ruvuma

Want your school to be the top-listed School/college in Songea?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Category

Website

Address


Barabara Ya Sokoine
Songea