Singida Manispaa

Singida Manispaa

Share

Karibu Katika Ukurasa Rasmi wa Halmashauri ya Manispaa ya Singida.

Karibu katika Ukurasa wa Halmashauri ya Manispaa Singida
Lengo la Ukurasa huu ni kuwaleta watumishi na wakazi wote wa Singida Manispaa Kwa pamoja na kupeana taarifa mbali mbali za kiutendaji ndani ya Manispaa Singida, Pia kupeana matangazo mbali mbali

05/08/2026
Photos from Singida Manispaa's post 04/08/2026

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Singida, Bi Joanfaith Kataraia, leo Agosti 4, 2026 alikuwa miongoni mwa viongozi waliomsindikiza Waziri wa Kilimo wa Jamhuri ya Sudan Kusini, Mhe. Clement Juma Mbugoniwia, alipotembelea mabanda mbalimbali katika Maonesho ya Kitaifa ya Nane Nane 2026 yanayoendelea Viwanja vya John Malecela, Nzuguni, Dodoma.

Photos from Singida Manispaa's post 04/08/2026
Photos from Singida Manispaa's post 04/08/2026

NAIBU WAZIRI KAMANI APONGEZA WAJASIRIAMALI BANDA LA SINGIDA MANISPAA NANE NANE

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Ngw'asi Damas Kamani, leo Agosti 4, 2026 ametembelea Banda la Halmashauri ya Manispaa ya Singida katika Maonesho ya Kilimo ya Nane Nane yanayoendelea kwenye Viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma.

Akiwa katika banda hilo, Mhe. Kamani alijionea bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na wajasiriamali wa Manispaa ya Singida na kupongeza juhudi zao za kuongeza thamani ya mazao na bidhaa za ndani, hatua ambayo amesema inachangia kukuza uchumi wa wananchi na Taifa kwa ujumla.

Kiongozi huyo amewataka wajasiriamali hao kuendelea kuimarisha ubora wa bidhaa zao ili ziweze kushindana katika masoko ya ndani na nje ya nchi, sambamba na kuongeza uzalishaji ili kukidhi mahitaji ya soko linaloendelea kukua.

Mhe. Kamani pia alisisitiza matumizi ya Maonesho ya Nane Nane k**a jukwaa muhimu la kutangaza bidhaa, kubadilishana uzoefu na kufungua masoko mapya yatakayowezesha wajasiriamali kuongeza kipato na kuchochea maendeleo ya sekta ya uzalishaji.

Maonesho ya Nane Nane ya mwaka huu yanaongozwa na kaulimbiu isemayo, "Tambua Soko; Ongeza Tija Kutekeleza Dira 2050," ikihamasisha wazalishaji na wajasiriamali kuzingatia mahitaji ya soko ili kuongeza tija na kuchangia maendeleo endelevu ya nchi.

04/08/2026

RC DENDEGO: SINGIDA NA DODOMA KUONGOZA MAPINDUZI YA TASNIA YA MAFUTA YA KUPIKIA

Serikali imeeleza kuwa Mkoa wa Dodoma na Singida utakuwa kitovu cha utekelezaji wa Mkakati wa Taifa wa Mafuta ya Kula (NEOS 2026–2035), unaolenga kuongeza uzalishaji wa mafuta ya kupikia nchini, kuvutia uwekezaji, kuongeza ajira na kuchochea utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Singida. Halima Dendego leo Agosti 4, 2026 katika mjadala wa kukuza uwekezaji Tasnia ya mafuta ya kupikia chini, uliofanyika jijini Dodoma katika viwanja vya Dkt. John Samwel Malecela. Dendego ameongeza kuwa hatua hiyo inalenga kukuza uwekezaji katika Tasnia ya Mafuta ya kupikia nchini.

Mjadala huo umefanyika leo siku chache baada ya uzinduzi wa Mkakati wa Taifa wa Mafuta ya Kula uliofanywa Julai 30, 2026 na Waziri wa Kilimo, Daniel Chongolo, ukiwakutanisha viongozi wa Serikali, sekta binafsi, wakulima na wataalamu kujadili mikakati ya kutekeleza NEOS, hususan katika mikoa ya Dodoma na Singida ambayo imepewa nafasi ya kimkakati katika kukuza tasnia hiyo.

Imeelezwa kuwa Tanzania bado inaagiza kutoka nje zaidi ya asilimia 60 ya mafuta ya kupikia na ya kula yanayotumika nchini, hali inayosababisha matumizi ya zaidi ya dola za Marekani milioni 200 kila mwaka.

Wakati huo huo, mahitaji ya mafuta ya kupikia yanatarajiwa kuongezeka kutoka tani 732,000 mwaka 2025 hadi zaidi ya tani 1,037,145 mwaka 2035, ilhali uzalishaji wa sasa ni tani 305,906 pekee, sawa na takribani asilimia 40 ya mahitaji ya taifa.

Want your organization to be the top-listed Government Service in Singida?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Address


Ipembe
Singida
236

Opening Hours

Monday 07:30 - 15:30
Tuesday 07:30 - 15:30
Wednesday 07:29 - 17:00
Thursday 07:30 - 15:30
Friday 07:30 - 15:30