Pastor Emmanuel Chatanda

Pastor Emmanuel Chatanda

Share

Pastor Emmanuel Chatanda Is The Senior Pastor(SNP) Of Glory Of Christ Church (GCTC)

01/09/2026

TAARIFA RASMI YA KUKANUSHA

TAARIFA YA KUKANUSHA KUHUSIKA KWA ASKOFU DKT. JOSEPHAT GWAJIMA NA TUKIO HILI

Tunapenda kutoa ufafanuzi rasmi kwa umma kwamba Askofu Dkt. Josephat Gwajima hahusiki na Semina ya “SEPTEMBER TO REMEMBER” inayotangazwa kufanyika tarehe 3–6 Septemba 2026.

Picha na jina la Askofu Dkt. Josephat Gwajima vimetumika kwenye tangazo hilo bila kuthibitisha ushiriki wake katika tukio hilo. Hivyo, umma usipotoshwe wala kuhusisha uwepo, ushiriki au idhini ya Askofu Dkt. Josephat Gwajima na tukio hilo.

Tunaomba taarifa hii izingatiwe na isambazwe ili kuwafikia wote ambao wanaweza kuwa wameona au kupokea tangazo hilo.

Asanteni kwa kuzingatia taarifa hii.

01/09/2026

Mtu mdhaifu sana kuliko wote kwenye Familia Muogope, ana kasi ya kwenda mbele kuliko waliomtangulia.

� KABLA HUJAZALIWA ULIKUWEPO
� Askofu Dr. Josephat Gwajima
� 31 August 2026

01/09/2026

Njooo Ufunguliwe jumla na Yesu kristo

Ukianza biashara zinakufa
Hupati wateja kabisa kwenye biashara yako n.k

Ni JUMAPILI ZOTE ZA MWEZI HUU WA TISA, USIKOSE.

27/08/2026

BIBLIA INASEMA NINI KUHUSU UFUFUKO WA WAFU SIKU YA MWISHO.

Utukufu kwa Yesu kristo, aliye Alfa na Omega, Mungu wa milele nakuarika kusoma Makala hii inayohusu kufufuka kwa watu waliokufa siku ya Mwisho.

Biblia Inasema kwamba maisha ya watu duniani hayaishii pale mtu akifa na kuzikwa kaburini bali maisha ya mtu aliyekufa huwa yanaendelea.

Watu wameshindwa kuelewa kwamba Miili tuliyonayo ndiyo huwa inazikwa kaburini kwa sababu, Miili ni udongo tu.

Mwanzo 3:19b kwa maana u mavumbi wewe, nawe mavumbini utarudi.

Mungu alivyomuumba mwanadamu alimuumba akiwa na Vipande Viwili Yaani Mwili pamoja na Pumzi yaani Roho.

Mtu ni roho(sio Roho Mtakatifu) roho yako, inayokaa ndani ya nyumba inaitwa mwili.

Mwanzo 2:7 Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi(mwili), akampulizia puani pumzi ya uhai(roho); mtu akawa nafsi hai.

Maneno ya u mavumbi wewe na mavumbini utarudi aliyeambiwa ni Mwili uliotengenezwa kwa udongo.

Na ndio Maana sote mashahidi Mtu akifa huzikwa kaburini Ila kinachozikwa ni Mwili wa mtu na sio roho ya mtu.

Kifo sio tukio bali ni utengano wa Roho ya Mtu na Mwili wa Mtu, Roho ikichomoka ndani ya mwili, Mwili huwa haufai tena hauna nguvu, hauwezi kutembea wala kukaa unaanguka unaenda kuzikwa.

Yohana 6:63a Roho ndiyo itiayo uzima, mwili haufai kitu;

Sasa kwa kawaida mwili wa mtu ukizikwa kaburini, Roho huendelea kuwa hai na hurudi kwa Mungu kwa ajiri ya Hukumu.

Waebrania 9:27 Na k**a vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu;

Hukumu hii hutoa Mungu mwenyewe na hii hukumu sio ile ya mwisho wa dunia atakayohukumu Mwanakondoo Yaani Yesu kristo bali, hukumu hii ni mwanzo tu wa kuamua huyo mtu aende wapi.

Ukifa hakuna mapumziko bali Roho yako inaenda kukutana na Mungu mwenyewe na anatoa hukumu kwa haki.

K**a ulikuwa ujamwamini Yesu Yaani kuokoka Basi, Unahukumiwa kwenda kuzimu kwenye mateso makali, na K**a ulikuwa umeokoka Duniani ulimwamini Yesu kristo basi, utapelekwa paradiso Yaani eneo la mapumziko au kifuani pa Ibrahim.

Mtu anayehukumiwa na kutupwa kuzimu ananza kulipia hukumu yake kwa mateso makali sana na huu sio Mwisho wa yote ni mwanzo tu,

Luka 16:23 Basi, kule kuzimu aliyainua macho yake, alipokuwa katika mateso, akamwona Ibrahimu kwa mbali, na Lazaro kifuani mwake.

Tajiri huyu alivyokufa alizikwa mwili wake kaburini lakini Roho yake ilienda kwa Mungu na ikahukumiwa kutupwa kuzimu na kuzimu kule alipata mateso.

Lakini mtu ambaye anahukumiwa kuingia paradiso Basi kule anapata pumziko la kweli na huu ni mwanzo wa raha na atapata raha zaidi, Lazaro Masikini alipokufa alichukuliwa na Malaika akapelekwa kupumzika.

SASA BIBLIA INASEMA NINI KUHUSU UFUFUKO WA WAFU.

Siku yaja ambayo Mambo yote yataisha duniani,

1 Wakorintho 15:52 kwa dakika moja, kufumba na kufumbua, wakati wa parapanda ya mwisho; maana parapanda italia, na wafu watafufuliwa, wasiwe na uharibifu, nasi tutabadilika. 53 Maana sharti huu uharibikao uvae kutokuharibika, nao huu wa kufa uvae kutokufa.

Japo linaloongelewa hapa ni:

🔹 Wafu watafufuliwa.

Huu ndio unaitwa ufufuko wa wafu, Maana yake kinachotokea Zile Roho zilizokufa zitapewa miili tena isiyoharibika na kurudi hai kwa ajiri ya Hukumu ya Siku ya Mwisho.

Roho ambazo zilikuwa kuzimu zitapewa miili na zitahukumiwa Sasa hukumu ya Pili yaani kutupwa Jehanamu kwenye ziwa la Moto na huu ndio utungu wenyewe.

Ufunuo wa Yohana 20:12 Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi; na vitabu vikafunguliwa; na kitabu kingine kikafunguliwa, ambacho ni cha uzima; na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu, sawasawa na matendo yao.

Hukumu hii ni kutupwa Motoni, kuendelea na mateso, mateso ya Jehanamu ni mara mia ya mateso ya kuzimu.

Lakini na zile Roho za watu zilizoingia Paradiso na zenyewe zitaingia Mbinguni na huko kutakuwa na sherehe na shangwe.

Na huu ndio Mwisho wa maisha ya wanadamu Yaani ama utupwe Motoni uishi milele Motoni, au uingie Mbinguni uishi milele kwa starehe.

Ili uingie Mbinguni fanya Mambo haya:

🔹 Okoka
Yaani mwamini Yesu wewe binafsi ndani ya Moyo wako.

🔹 Maisha matakatifu
Acha dhambi ishi kwa usafi.

Wagalatia 5:19 Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi,
20 ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi,21 husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, k**a nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu.

Tuishie Hapa, Mungu akubariki na akupe Neema ya Wokovu.

Kwa Sala ya Toba na Ushauri
Namba: WhatsApp au 0621002308.

Njoo nikuunge group la Whatsapp la Neno la Mungu, weka namba yako hapa.

Share kwa marafiki


Na Pastor Kijana Zaidi.
Pastor Emmanuel Chatanda

27/08/2026

SWALI K**A HILI MAJIBU YAKE NI HAYA

MUNGU NI MMOJA, YAANI, WAKRISTO NA WAISLAMU HUMWOMBA MUNGU MMOJA AU KUMUABUDU?

NA MHUBIRI KIJANA

Q&A with Pastor Emmanuel chatanda

25/08/2026

Ndege wenye rangi moja huruka pamoja.

23/08/2026

SWALI K**A HILI MAJIBU YAKE NI HAYA

Waislam Huuliza NINYI WAKRISTO MNAABUDU MUNGU WATATU YAANI BABA MWANA NA ROHO MTAKATIFU? JIBU HILI KWENYE VIDEO

NA MHUBIRI KIJANA

Q&A with Pastor Emmanuel chatanda

21/08/2026

SWALI K**A HILI MAJIBU YAKE NI HAYA

JE YESU KRISTO ALIKUFA MSALABANI NA VIPI WAISLAMU WANASEMAJE?

NA MHUBIRI KIJANA

Q&A with Pastor Emmanuel chatanda

21/08/2026

JUMAPILI HII

MAOMBI
SIFA NA KUABUDU
NENO LA MUNGU
MAOMBEZI

19/08/2026

KWANINI YUDA ALIMSALITI YESU KRISTO.

Luka 22:3 Shetani akamwingia Yuda, aitwaye Iskariote, naye ni mmoja wa wale Thenashara.

Sote tunajua Yuda alimsaliti Yesu Kristo pale alipoingiwa na Shetani ndani yake kwa sababu hiyo Shetani alianza kumhubiria Yuda, na Yuda akaona anafaa kumsaliti Yesu japo kuwa ulikuwa ni uongo wa Shetani.

Sikiliza Shetani anatenda kazi hata Sasa anaweza kukuingia ndani K**a utakua unajichanganya na dhambi kisiri Siri, akipata upenyo tu anaingia ndani ndipo utashangaa mtu anaacha wokovu, anaacha Ibada n.k

Kwa Hiyo Yuda alikuwa na sababu nzuri na zenye mashiko japo kuwa ulikua Ni uongo wa Shetani.

SABABU NJEMA ILA ZINA UONGO WA SHETANI NDANI YAKE EBU ONA..

1. Unajua Yesu Kristo katika Huduma yake alikuwa Hana mahali pa kulala kwa hiyo walikuwa wanalala kwa watu au mahali popote.

Luka (Luk) 9:58 Yesu akamwambia, Mbweha wana pango, na ndege wa angani wana viota, lakini Mwana wa Adamu hana pa kujilaza kichwa chake.

Sasa pengine Shetani alianza kumuwazisha Yuda mbona mnateseka, mbona Yesu mkatili anawalaza nje, au kwa watu au milimani achana nae muuze tu.

2. Huduma ya Yesu ilijaa miujiza mingi na wakati Fulani Yesu alitenda Muujiza wa chakula wakala watu wengi Sana chakula kile Ila Yesu akawaambia Wanafunzi wake kusanyeni masazo,

Huwenda Yuda ilimuuma Maana Shetani huwenda alipanda mawazo K**a vile Yesu hawajali, Yesu hawapendi anawalisha makombo akaamua kumsaliti.

3. Huwenda Yuda alimzoea Sana Yesu,(MAZOEA)
Walicheka pamoja, alimwona Yesu analia mara Nyingi, mara Yesu alalamike njaa inauma mara akasirike n.k

Sasa pengine Yuda akaanza kumuona Yesu kuwa sio Mungu tena, mbona analia lia njaa, roho ya MAZOEA akaamua kumsaliti.

Zipo sababu Nyingi Sana ambazo Yuda alizitumia kumsaliti Yesu na kwa Yuda zilikuwa na mashiko Sana Ila kumbe ulikuwa Ni uongo wa Shetani.

Sikiliza ikifika wakati ukaanza kumuona mchungaji wako au Baba Yako wa kiroho K**a mwanadamu wa kawaida ujue upo kwenye hatari Sana na unaweza ukaishia kujinyonga K**a Yuda.

Kukaa karibu na mtu wa Mungu Kuna baraka zake na pia ukicheza vibaya Kuna laana zake.


Mhubiri Kijana
Pastor Emmanuel Chatanda.

Want your place of worship to be the top-listed Place Of Worship in Njombe?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Website

Address


IBANI, Ludewa
Njombe