bfm_radio
Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from bfm_radio, Radio Station, Njombe.
29/08/2022
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassani akiwa kwenye picha ya pamoja na Majaji aliyowaapisha muda mfupi baada ya kuwaapisha.
29/08/2022
KUBWA.
Halmashauri ya wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera kupitia kikosi maalum cha kudhibiti magendo
imefanikiwa kuk**ata tani 21 za kahawa magari 4 pikipiki na baiskeli kadhaa katika zoezi la kudhibiti magendo ya kahawa.
Akizungumzia tukio hilo kupitia kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri hiyo mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Bahati Henerico amesema Zoezi la udhibiti wa magendo limefanikiwa kuk**ata kahawa iliyokuwa katika harakati za kutoroshwa kwenda nje ya nchi pamoja na kumilikiwa kinyume na sheria katika mazingira mbali mbali.
29/08/2022
Stars yamtimua kocha wake na wasaidizi wake wtoe
29/08/2022
Mwanaume mmoja nchini Afrika Kusini mwenye umri wa miaka 57, aliyetambulika kwa jina la Joseph Kagiso Ndlov alikimbia mbio za kilometa 90 sawa na maili 56 ili kumchumbia mwanamke aitwaye Prudence.
Mwanaume huyo alipigwa picha akiwa ameshika bango la kumtaka mwanamke huyo aoane naye alipokaribia kumaliza mbio za Marathon za Comreds.
Bango lilikuwa na ujumbe unaosomeka hivi, "Prudence utakubali kuwa mke wangu? Nimekimbia kilometa 90 kwa ajili yako".
Unahisi Prudence alikubali? Weka maoni yako hapa πππ
29/08/2022
π¨ A N N O U N C E M E N T π¨
Tumefikia makubaliano ya pande mbili na kocha wetu, Abdihamid Moallin, na msaidizi wake, Omary Nasser, kuachia ngazi k**a kocha mkuu na msaidizi mtawalia.
Hata hivyo, makocha hao wataendelea kubaki k**a sehemu ya idara ya ufundi klabuni kwetu katika nafasi nyingine ambazo tutazitangaza hapo baadaye.
Kwa sasa timu itakuwa chini ya Daniel Cadena, ambaye ni kocha wa makipa, hadi tutakapotangaza kocha mpya.
Cadena ni kocha mwenye leseni ya juu kabisa ya ukocha, UEFA Pro License.
.amin
29/08/2022
*NTOMA ORPHANAGE MARUKU WATIMIZA MIAKA 70 YA HUDUMA.*
Na Dulla Uwezo
Kituo cha kulelea Watoto Wadogo cha Ntoma Orphanage kinachosimamiwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Dayosisi ya Kaskazini Magharibi, kimetimiza Miaka Sabini ya Huduma huku Taarifa zikionesha kuwa Watoto 290 wamelelewa Kituoni hapo.
Akisoma Risala mbele ya Wageni na Mgeni Rasmi Mkuu wa Kituo hicho katika Tukio Kubwa la Unyonyeshaji Watoto hao, ambalo limeratibiwa na Kamati iliyoongozwa na Mbunge wa Jimbo la Bukoba Vijijini Dkt. Samson Jasson Rweikiza, Bi Penina Kaimukirwa (Mtawa) Amesema Kituo hicho Mwaka huu kimetimiza Miaka 70 ya Huduma hiyo ya kulea Watoto Wadogo ambao huletwa hapo kufuatia Matukio mbalimbali katika Jamii husika, zikiwemo Changamoto za Kifamilia, huku akitaja changamoto mbalimbali kubwa ikiwa ni chakula cha Watoto hao.
Awali akiongoza Ibada Maalum ya kuombea Kituo hicho Mchungaji Dkt. Elimerek Kigembe amewakumbusha Wageni na waumini waliohudhuria, juu ya umuhimu wa kuendelea kuwalea Watoto hao, huku akisisitiza Maneno matakatifu Yanayosema kuwa "Dini Safi ni Ile inayojali Mayatima na Wajane katika Dhiki zao.."
Kwa upande Dkt. Samson Rweikiza ambaye Ni Mwenyekiti wa Kamati ya Shughuli hiyo ya Unyonyeshaji, ameendelea kuwaomba Wananchi kuguswa Mara kwa Mara na kutembelea Kituo hicho bila kujali Dini Wala itikadi, licha ya kuwa Kituo kipo chini ya Kanisa, lakini hata Watoto wenye Madhehebu na Dini nyingine wamekuwa wakilelewa hapo.
Katika Tukio hilo lililoambatana na Harambee ya Kuchangia Kituo hicho, Zaidi ya Milioni 30 zimechangwa ikiwemo ahadi na Pesa Taslimu, Harambee iliyoongozwa na Mhe. Charles Mwijage Mbunge.
28/08/2022
Simba yashinda 4 - 2 Sudani dhidi ya Asante kotoko
28/08/2022
Simba 2 - 1 Asante Kotoko
28/08/2022
Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars imekubali kipigo Cha goli moja kwa bila akiwa nyumbani dhidi ya aTimu ya Taifa ya Uganda Uganda the cranse.
Kwa Matokeo haya Stars inakuwa na kibarua kigumu Cha kufuzu kushiriki Mashindano CHAN kwa kuwa anahitaji kumfunga Uganda kwenye mechi ya marufiano zaidi ya goli 2 bila au zaidi.
28/08/2022
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania imeongeza timu ya wanawake ya Simba Queens kwa kutwaa ubingwa wa ligi ya wanawake SAMIA CUP na kuitakia kila raheli katika Mashindano ya kimataifa ambayo yatafanyika nchini Morocco.
28/08/2022
Uongozi wa BFM RADIO 92.5Mhz unaitakia timu ya Taifa ushindi katika mechi yake ya kufuzu CHAN 2023.
26/08/2022
: Rais Samia Afanya uteuzi wa viongozi mbalimbali muda huu tazama hapa chiniπππ
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Website
Address
Njombe