Mwauwasa
Ukurasa rasmi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA)
Kwa msaada piga simu namba (0800110023) BURE
Mwanza Water Supply and Sanitation Authority (MWAUWASA) was established in July 1996 under Water Works Ordinance Cap 281 (as amended) as a semi autonomous executive agency of the government for provision of adequate, reliable and sustainable portable water and wastewater management services in Mwanza City at affordable and cost effective prices. It was declared full autonomous from January 1998 an
30/05/2026
MWAUWASA YATOA SOMO LA USAFI WA MAZINGIRA NA MAJI
Jamii imekumbushwa umuhimu wa utunzaji wa mazingira pamoja na ushirikiano wa pamoja katika kuhakikisha upatikanaji endelevu wa huduma ya maji.
Hayo yameelezwa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano MWAUWASA, Vivien Temu, wakati wa semina maalum iliyowakutanisha wajasiriamali na wadau kutoka taasisi mbalimbali za Umma na sekta binafsi Mei 29, 2026.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji, Bi. Vivien alisema wajibu wa MWAUWASA ni kuhakikisha inatoa huduma ya Maji safi na salama, kuondoa maji taka, na kuacha mazingira safi, huku wananchi wakiwajibika kuhakikisha wanatumia maji kwa usahihi, kulipia huduma na kutunza miundombinu ikiwemo mabomba.
"Maji ni Uhai, ili huduma hii iwe endelevu ushirikiano wa pamoja ni muhimu sana, na hii inaanzia kwenye ngazi ya familia" Alisisitiza.
Semina hiyo iliyoratibiwa kwa ushirikiano kupitia Taasisi ya Sudama Group iliwakutanisha Wajasiriamali na Wadau zaidi ya 150 kutoka taasisi mbalimbali
30/05/2026
KUELEKEA SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI, MWAUWASA YAANZA KWA VITENDO
Katika kuungana na wadau kuhakikisha na kuhamasisha umuhimu wa usafi wa mazingira, Watumishi wa MWAUWASA wameungana kufanya usafi kwenye maeneo ya vyanzo vya maji kikiwemo chanzo cha Butimba.
Hatua hiyo ni kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya usafi wa Mazingira ambayo huadhimishwa tarehe 5 ya kila mwaka Duniani kote.
Siku ya Mazingira Duniani (World Environment Day), Iliwekwa rasmi na Umoja wa Mataifa mwaka 1972 kwa lengo la kuongeza uelewa na kuhamasisha hatua za kulinda mazingira duniani.
Kwa Mwaka huu Tanzania inaadhimisha siku hiyo kwa kaulimbiu isemayo "Dira 2050, Tuwajibike Kukijanisha Tanzania"
26/05/2026
21/05/2026
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt, Mwigulu Nchemba akiambatana na viongozi wa Sekta ya maji walioongozwa na Waziri wa maji Mhe. Jumaa Aweso wametembelea na kukagua banda la maonesho la MWAUWASA katika maadhimisho ya siku ya Ziwa Victoria.
Wakizungumza katika tukio hilo muhimu, pamoja na mambo mengine viongozi hao wamesisitiza umuhimu wa wadau wote wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuendelea kushirikiana kwa pamoja katika utunzaji wa Ziwa Victoria kwa manufaa ya wote kwaajili ya kizazi cha sasa na baadae.
21/05/2026
MWAUWASA YAIBUKA KIDEDEA - LAKE VICTORIA DAY
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA) imepatiwa tuzo mbili kwa kutambua mchango wake katika utunzaji wa Ziwa Victoria kwa usimamizi thabiti wa uondoshaji Majitaka katika Jiji la Mwanza (Sludge water Management), pamoja na kushiriki kikamilifu katika maadhimisho ya siku ya Ziwa Victoria ( Best Exhibitors).
Tuzo hizo zimetolewa na Kamisheni ya Bonde la Ziwa Victoria ( LVBC ) na kukabidhiwa na Mhe. Jumaa Aweso (Mb) Waziri wa Maji katika hafla iliyowakutanisha wadau wa sekta ya maji, taasisi na Viongozi mbalimbali kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na wadau wa Ziwa Victoria tarehe 20 Mei, 2026.
19/05/2026
KATIBU MKUU MAMBO YA NJE, ATEMBELEA BANDA LA MWAUWASA - MAONESHO SIKU YA ZIWA VICTORIA
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya nje Balozi Said Shaibu M***a ni miongoni mwa Viongozi ambao wametembelea banda la MWAUWASA kwenye maonesho ya maadhimisho ya Siku ya Ziwa Victoria viwanja vga Nanenane - Nyamhongolo.
Baada ya kupata maelezo kutoka kwa wataalam waliopo hapo, ameipongeza MWAUWASA k**a mdau muhimu kwa kushiriki kikamilifu katika maadhimisho hayo na kutambua kazi kubwa inayofanywa na Serikali kupitia Wizara ya Maji na MWAUWASA kuhakikisha utunzaji wa ziwa ikiwemo utekelezaji wa miradi mbalimbali ya usafi wa mazingira inayosaidia uondoshaji na utibuji wa Majitaka kuepusha uchafuzi wa Ziwa.
19/05/2026
MWAUWASA inawakaribisha kutembelea banda lake la maonesho kwenye maadhimisho ya Siku ya Ziwa Victoria yanayofanyika katika viwanja vya Nanenane - Nyamhongolo.
Tumia fursa hii kupata elimu na ufafanuzi kuhusu huduma ya Maji na Usafi wa Mazingira.
Kilele cha Maadhimisho hayo yaliyoanza rasmi tarehe 18 Mei, ni tarehe 21.05.2026 ambapo Mhe. Waziri Mkuu anatarajiwa kuwa Mgeni rasmi.
18/05/2026
Katika kuadhimisha Siku ya Ziwa Victoria, Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA) kwa kushirikiana na Bodi ya Maji Bonde la Ziwa Victoria, leo Mei 18, 2026 wameungana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Said Mtanda pamoja na viongozi wengine wa serikali akiwemo Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji Bi. Rose Ambrose kupanda zaidi ya miti 2,000 katika chanzo cha maji Butimba. Zoezi hili linaongeza idadi ya miti iliyokwisha pandwa kufikia zaidi ya 6,500 katika eneo hilo muhimu.
Akizungumza katika kilele cha maadhimisho hayo, Mkuu wa Mkoa Said Mtanda aliwapongeza wananchi na wadau mbalimbali kwa kujitokeza kwa wingi kushiriki katika juhudi za uhifadhi wa mazingira. Alisema hatua hiyo ni muhimu katika kulinda rasilimali za maji, hususan Ziwa Victoria ambalo lina mchango mkubwa katika maisha ya watu.
Aidha, Mkuu wa Mkoa alieleza kuwa kwa mwaka huu, maadhimisho ya Siku ya Ziwa Victoria yamefanyika kwa mara ya kwanza katika ngazi ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, ambapo wakuu wa nchi na mawaziri wa sekta za maji na mazingira walikubaliana kuwa na siku maalum ya kuenzi na kulinda ziwa hilo.
“Ziwa Victoria ni muhimu sana kwa huduma mbalimbali za kijamii na kiuchumi. Maji ni afya, maji ni uchumi na maji ni maendeleo,” alisisitiza Said Mtanda huku akiwataka wananchi kuhakikisha wanatunza miti iliyopandwa ili iweze kudumu na kutoa manufaa yaliyokusudiwa.
Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Bi. Rose Ambrose, alimshukuru Mkuu wa Mkoa kwa kushiriki kikamilifu katika tukio hilo, na kupongeza juhudi za wadau wote wanaoshiriki katika uhifadhi wa vyanzo vya maji.
Aliongeza kuwa Wizara ya Maji kupitia Bodi ya Maji Bonde la Ziwa Victoria imejiwekea lengo la kupanda miti 10,000 rafiki kwa vyanzo vya maji katika eneo la Butimba, ambapo hadi sasa miti zaidi ya 6,500 tayari imepandwa.
Miti iliyopandwa inalenga kulinda vyanzo vya maji, kuzuia mmomonyoko wa ardhi, kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi na kuboresha mazingira kwa ujumla katika eneo la chanzo cha Butimba.
Maadhimisho hayo yameongozwa na kauli mbiu isemayo: “Maji yetu, mustakabali wetu – tuungane kwa uendelevu wa Bonde la Ziwa Victoria.”
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Contact the organization
Telephone
Website
Address
P. O. Box 317
Mwanza
255
Opening Hours
| Monday | 08:00 - 17:00 |
| Tuesday | 08:00 - 17:00 |
| Wednesday | 08:00 - 17:00 |
| Thursday | 08:00 - 17:00 |
| Friday | 08:00 - 17:00 |
| Saturday | 08:00 - 18:00 |