JETBanking
Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from JETBanking, Financial service, Mwanza.
JetBanking is a digital platform that aims at empowering Individuals, Groups and Financial Institutions by providing them with a digital platform to automate their day to day activities securely ,fast and affordably.
Karibu asilimia 95 ya vikundi vilivyojiunga na JETBanking vinafurahia urahisi wanaoupata kwa kutumia app ya JETBanking, lakini pia kwa elimu tunayotoa kwa ajili ya kurahisisha shughuli zao za kila siku.
Tunajivunia kwa kuviwezesha vikundi hivi vya VICOBA kuweza kufikia malengo yao.
JETBanking, Benki yako ya kidigitali inayoaminika.
17/05/2023
Muhasibu usipate tabu kufungua makaratasi na kupiga hesabu nani anadaiwa na nani hadaiwi, au nani kanunua hisa na nani hajanunua.
Ukitumia JETBanking hutopoteza muda tena kuumiza kichwa na kupekua madaftari, vitu vyote hivi unavipata kwa urahisi na kwa kubofya tu, ukitakata ripoti ya walionunua hisa ni kubofya tu na mkeka wote unao.
Ukiwa na JETBanking, utazipata taarifa zote za kifedha za kikundi chako.
Pakua App ya JETBanking kupitia Playstore au Apple Store(Link Kwenye Bio) na uanze kuendesha kikundi chako kidigitali.
16/05/2023
Tusingependa lugha ikawa kikwazo kwenye kutumia mfumo wetu. na Tunaelewa watumiaji wetu wanatumia lugha tofauti. Na ndiyo maana tumerahisisha kwa kuiweka JETBanking kutumika kwa lugha ya Kiswahili na Kiingereza.
Pakua sasa app ya JETBanking na uone urahisi wa kuendesha kikundi chako kidigitali.
15/05/2023
Hii ni kwa wale wenye vikundi zaidi ya kimoja.
JETbanking imekurahisishia kwa kuweza kujiunga na kufatilia vikundi vyako vyote sehemu moja.
Kupitia JETbaking utaweza kupata taarifa za kila kikundi ulichonacho. Iwe ni kununua hisa, kuomba na kufatilia marejesho ya mikopo, vyote utavipata kwenye App ya JETBanking.
Pakua App ya JETBanking sasa na urahisishe shughuli za kikundi chako.
11/05/2023
Tunapenda kuwahakikishia kuwa hakuna gharama yoyote ya kujiunga na mfumo wa JETBanking. Tunajivunia kuviwezesha vikundi vya VICOBA, kwa kurahisisha shughuli za vikundi kuwa rahisi na kufanyika wakati wowote na mahali popote.
Jiunge nasi leo na ufurahie urahisi wa kuendesha kikundi chako kidigitali. JETBanking, Benki yako ya kidigitali inayoaminika.
# .
09/05/2023
Je, wewe ni mmoja wao?
Jiunge na sisi leo uwe sehemu ya familia hii ya vicoba kidigitali.
05/05/2023
Asimilia kubwa ya vikundi vya VICOBA bado vinatumia madaftari kutunza na kuhakiki taarifa na shughuli zote za kikundi. Hii inaweka ugumu kwenye uhakiki na utafutaji wa taarifa, hasa kwa vikundi vinavyoendelea au visivyovunjwa.
JETBanking imerahisisha, huna haja tena ya kumtafuta muweka hazina usiku wa manane akuangalizie hisa zako au mkopo umebaki kiasi gani. Shughuli zote na taarifa zote utazipata kwenye application ya JETBanking muda wowote, wakati wowote.
Madaftari tuwaachie wanafunzi.
Pakua application ya JETBanking kupitia playstore au apple store na uone urahisi wa kuendesha kikundi chako kidigitali.
04/05/2023
VICOBA na Vikundi vya Hisa hii ni yenu.
Mfumo wa JETBanking haujafungamana na utaratibu wa aina moja wa kuendesha kikundi. Tumeviwezesha pia vikundi vyenye utaratibu tofauti tofauti, kuweza kuweka taratibu zao kwa urahisi zaidi. Kila kitu ni uamuzi na uchaguzi wenu.
Sajili na jiunge kwenye kikundi chako kupitia JETBanking, mfumo unapatikana kupitia Playstore na Apple Store. (Link Kwenye Bio)
28/04/2023
Hapana!🚫
Mfumo wa VICOBA si sawa na upatu, maana mfumo huu umeboreshwa katika utaratibu wa uongozi, mfumo wa utunzaji wa kumbukumbu, utaratibu wa mifuko ya kuchangia, mfumo wa uendeshaji na taratibu za utoaji wa huduma kwa ujumla.
Ila upatu hauna uongozi bali una kijumbe ambaye anakuwa na jukumu la kujua nani ni mwanachama, nani kapewa, nani hajapewa na nani anafuata.
Ifahamike kuwa upatu ni michezo na siyo mfumo. Na kwa nchi k**a Tanzania michezo ya upatu haitambuliki kisheria, na ikitokea mmezurumiana, hakuna pa kushtaki, kila kitu ni juu yenu.
Endelea kutufatilia kujifunza zaidi kuhusu VICOBA.
27/04/2023
Iwe ni ripoti kuhusu waliorejesha mikopo, walionunua hisa mwezi wa kwanza, au taarifa za wanachama wapya. Zote hizi utazipata kwa urahisi kabisa, ni kubofya tu na ripoti zote unazo. Hivyo tu.
Hakuna tena kupekua madaftari, VICOBA KIDIGITALI.
Pakua sasa App ya JETBanking kupitia Google playstore au Apple Store, na uone urahisi wa kupata taarifa zote za kikundi chako.
25/04/2023
Kuna muda mambo yanakuwa mengi, kiasi kwamba tunasahau hata kurejesha mikopo na kuishia kupigwa faini/penalty.
Kuepukana na hili, Ukitumia App/mfumo wa JETBanking utapata taarifa za ukumbusho kuhusu mkopo wako na taarifa zote za marejesho.
Sajili na Jiunge kwenye kikundi chako kupitia JETBanking, na uone urahisi wa kuendesha kikundi chako kidigitali.
JETBanking, Benki yako ya kidigitali inayoaminika.
22/04/2023
Tunawatakia wafanyakazi wetu na wateja wetu wote sikukuu njema ya Eid!
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Contact the business
Website
Address
Mwanza
Opening Hours
| Monday | 09:00 - 17:00 |
| Tuesday | 09:00 - 17:00 |
| Wednesday | 09:00 - 17:00 |
| Thursday | 09:00 - 17:00 |
| Friday | 09:00 - 17:00 |
| Saturday | 09:00 - 14:00 |