Dray Wadray
Daily~wisdom
10/11/2025
SOMO:MAOMBI YA USIKU WA MANANE
UTANGULIZI
Katika Biblia, usiku wa manane ni kipindi cha kipekee—kati ya saa 6 usiku hadi 3 usiku, au kile tunachokiita watches of the night.
Ni wakati ambapo:
••Ulimwengu wa roho huwa na shughuli nyingi,
••Adui hufanya kazi zaidi,
••Na Mungu hufunua mambo makubwa kwa watu wake.
Whatsapp Group
https://chat.whatsapp.com/IkMhhdEDNAdGnWi2H7sadf?mode=wwt
Watu wengi wenye ushindi wa kiroho katika Biblia walipata miujiza yao wakati wa usiku wa manane.
Leo tunatazama kwa nini, na jinsi ya kuomba kwa nguvu katika kipindi hicho.
SEHEMU YA 1:
*KIPINDI CHA USIKU WA MANANE NI NINI?*
Biblia inataja:
Watch ya kwanza: 6 pm – 9 pm
Watch ya pili: 9 pm – 12 am
Watch ya tatu: 12 am – 3 am
Watch ya nne: 3 am – 6 am
Usiku wa manane *(12 am – 3 am)* ni kipindi ambacho:
✓ Milango ya kiroho huwa wazi
✓ Shughuli za giza hutawala
✓ Roho Mtakatifu hutenda kazi bila kuvurugwa
✓ Malaika hupewa maagizo
✓ Watakatifu hupata maono, ufunuo na vita vya kiroho
SEHEMU YA 2:
*KWA NINI MAOMBI YA USIKU WA MANANE NI YA KIMKAKATI?*
1. Ni wakati adui anafanya mashambulizi yake makubwa
Mathayo 13:25
— “Walipo lala usingizi, adui akaja akapanda magugu…”
Hii inaonyesha kuwa mashambulizi mengi hutokea usiku.
Adui huanzisha:
°°Laana
°°Uchawi
°°Mashambulizi ya ndoto
°°Kuzuia baraka
°°Kuweka vifungo vya kifamilia
°°Kufunga riziki
*Kwa nini?*
1.Kwa sababu muda huo binadamu wengi wanakuwa katika hali ya udhaifu wa kimwili.
2. Ni wakati ambao viongozi wa kiroho waliomba na kuona matokeo
a) Paulo na Sila
– Matendo 16:25–26
“Usiku wa manane Paulo na Sila waliomba… mara tetemeko la nchi likatokea… milango ikafunguka… minyororo ikaondoka.”
*Matokeo:*
🔥Minyororo ya kiroho ilivunjika
🔥Milango ya hatima ikafunguliwa
🔥Wokovu ukaingia kwa mkuu wa gereza
Hii inaonyesha maombi ya usiku huleta uhuru na kuvunjika kwa vifungo pamoja na kuruhusu majira mapya kwa muhusika haswa uhuru na kufunguliwa kwa nafsi ya muombaji.
b) Petro
— Matendo 12:6–10
Petro alikuwa gerezani, malaika akamtoa usiku wa manane.
Kuna;
🔥Minyororo ikaanguka
🔥Mlango ukafunguka wenyewe
🔥Ulinzi wa Mungu ukamfunika
*Ujumbe:*
Maombi ya usiku hutoa miujiza isiyotarajiwa.
c) Yakobo
— Mwanzo 32:24–28
Yakobo alipigana na Malaika usiku kucha.
*Matokeo:*
🔥Jina lake likabadilika
🔥Ukombozi ukaingia katika ukoo
🔥Hatima yake ikafunguliwa
d) Samueli
— 1 Samweli 3:3–10
Samueli alisikia sauti ya Mungu usiku.
Hii inaonyesha:
Wakati wa usiku ndicho kipindi cha kupokea ufunuo mzito wa Mungu.
e) Yesu mwenyewe
— Luka 6:12
“Yesu alitoka kwenda mlimani kuomba, akakesha usiku kucha akimwomba Mungu.”
Alipoamka, aliwachagua mitume 12.
Maamu*i makubwa ya Yesu yalifanyika baada ya maombi ya usiku.
SEHEMU YA 3:
*NINI HUTOKEA KATIKA ULIMWENGU WA ROHO USIKU WA MANANE?*
1. Kiti cha enzi cha giza huinuka
(Isaya 29:15)
_“Ole wao wanaojitahidi kumficha Bwana mashauri yao, na matendo yao yamo gizani, nao husema, Ni nani atuonaye? Nani atujuaye?”_
2. Laana huzungumzwa sana usiku
(Zaburi 91:5–6)
_⁵ Hutaogopa hofu ya usiku, Wala mshale urukao mchana,⁶ Wala tauni ipitayo gizani, Wala uele uharibuo adhuhuri,_
3. Malaika wa Bwana huzunguka wenye haki usiku
(Zab 34:7)
_“Malaika wa Bwana hufanya kituo, Akiwazungukia wamchao na kuwaokoa.”_
*Usiku ni kipindi cha:*
🔥Ulinzi
🔥Uokozi
🔥Ufunuo
🔥Sauti ya Mungu
4. Ndoto za kiroho hutokea usiku
Katika Mathayo 2:13; 2:19—Mungu alimuonya yusufu
5. Maagizo ya Mungu hutolewa usiku
(Ayubu 33:14–15)
_¹⁴ Kwa kuwa Mungu hunena mara moja, Naam, hata mara ya pili, ajapokuwa mtu hajali.¹⁵ Katika ndoto, katika maono ya usiku, Usingizi mzito uwajiliapo watu, Katika usingizi kitandani;_
Mungu hunena katika ndoto na maono ya usiku.
SEHEMU YA 4:
*MATOKEO YA MAOMBI YA USIKU WA MANANE*
1. Milango iliyofungwa hufunguliwa
K**a kwa Petro na Paulo & Sila.
2. Ngome za shetani zinaporomoka
2 Kor 10:4 — silaha za vita zetu zina nguvu za kubomoa ngome.
3. Mizani ya kiroho hubadilika
Adui alipanda usingizini, lakini wakristo wanaamka kuvunja kazi zake.
4. Uwepo wa Mungu hushuka kwa ukaribu zaidi
*Watu wengi hupata:*
🔥Maono
🔥Sauti ya Mungu
🔥Ufunuo
🔥Maelekezo
🔥Wito wa huduma
5. Ndoto mbaya zinashindwa
*Maombi ya usiku yanaweza:*
❌Kufuta ndoto za laana
❌Kuzuia ndoto za mapepo
❌Kuzuia mashambulizi ya usiku
6. Hatima hubadilishwa
K**a Yakobo alivyopata jina jipya.
SEHEMU YA 5:
*JINSI YA KUFANYA MAOMBI YA USIKU WA MANANE KWA UFAUZI*
1. Jitenganishe na kelele
Anza kwa ukimya, kusoma Zaburi au Ayubu ili kujiweka rohoni.
2. Anza kwa sifa na shukrani (Zaburi 100:4)
Sifa hujenga uwepo wa Mungu.
3. Tubu dhambi zote
Usiku ni kipindi ambacho roho nyeti ya mtu inahitaji utakaso.
4. Vunja kila agano la giza lililotolewa usiku
(Isa 28:18)
*Shetani huwa anapenda kufanya maagano usiku.*
5. Tangaza vita vya kiroho
Zaburi 35, Zaburi 27, Zaburi 91.
6. Ombea hatima yako
*Vitu vikuu vya kuomba:*
🟢Kitu unachotaka Mungu afungue
🟢Msimu mpya
🟢Kibali
🟢Mafanikio
🟢Kuhamishwa kiroho
🟢Ulinzi wa familia
🟢Undoaji wa vifungo
7. Piga kelele za ushindi k**a Paulo & Sila
Hili huvuta nguvu ya wingu la uwepo wa Mungu.
8. Maliza kwa amani ya Mungu (Isa 26:3)
Toa utukufu kwa Mungu.
SEHEMU YA 6:
*MUDA GANI NI BORA KUOMBA USIKU?*
✓ Kuanzia saa 6 usiku – 9 usiku — kipindi cha usalama na utulivu
✓ Kuanzia saa 9 usiku – 12 — kipindi cha kufunga milango ya adui
✓ Usiku wa manane (12 – 3 asubuhi) — kipindi cha kupigana vita
✓ Macho ya alfajiri (3 – 6 asubuhi) — kipindi cha ushindi, mwanga na kutolewa maagizo
Usiku wa manane ni k**a *“mahak**a ya kiroho”* ambapo:
👉🏿Maamu*i hufanyika
👉🏿Hukumu za Mungu hutolewa
👉🏿Ukombozi huanza
SEHEMU YA 7:
*SABABU 7 ZA KUANZA MAOMBI YA USIKU WA MANANE*
1. Kuzuia kazi za giza
2. Kufungua milango ya mafanikio
3. Kupokea ufunuo wa hatima
4. Kuvunja vifungo vya kizazi
5. Kuamsha karama za kiroho
6. Kuimarisha maisha ya kiroho
7. Kusikia sauti ya Mungu kwa uwazi zaidi
*HITIMISHO*
Usiku wa manane si kawaida:
Ni kituo cha maamu*i,
ni eneo la vita,
ni mlango wa miujiza.
Kila muamini anayejifunza siri hii, hushinda ngome nyingi ambazo adui alikuwa ameweka.
Maombi ya usiku wa manane yana nguvu kwa sababu:
👉🏿Yanavunja kazi za giza
👉🏿Yanageuza misimu au majira
👉🏿Yanatoa uhuru au ukombozi
👉🏿Yanakuimarisha rohoni
👉🏿Yanakufungua kwa baraka ambazo usingepata kwa urahisi katika maombi ya mchana
KUMBUKA KUWA;
*Wakati mwingine mafanikio yako yaliyokwama hayahitaji kuongea na mtu bali yanahitaji maombi ya usiku wa manane.*
MUNGU AKUBARIKI SANA 🙏🏽
ALTAR OF GRACE WhatsApp Group Invite
*SOMO:BADO LIKO TUMAINI*
*UTANGULIZI*
Kila mtu anayesafiri katika maisha hukutana na vipindi vya giza, maumivu, kukatishwa tamaa na hali zinazojaribu kumvunja moyo.
Wengine wanakata tamaa kwa sababu ya hali ya kiuchumi,
wengine za kifamilia,
wengine kimwili,
kiimani au katika huduma.
Lakini ujumbe wa leo ni mmoja tu:
*Bado lipo tumaini!*
Tumaini ni u*i mwembamba unaotufunga na mustakabali wa Mungu;
ni nguzo inayotuweka wima hata upepo unapovuma.
Whatsapp Group
https://chat.whatsapp.com/IkMhhdEDNAdGnWi2H7sadf?mode=wwt
*SEHEMU YA 1:*
*MAANA YA TUMAINI KIBIBLIA*
Neno *“tumaini”* kwenye Biblia mara nyingi linatokana na neno la Kiebrania *“Tikvah”* lenye maana ya kamba inayovutwa, kitu cha kushikilia, au matarajio ya kuelekea mbele.
Hii ina maana;
•Tumaini sio hisia tu bali;
•Tumaini si kufikiria mambo mazuri yasiyo na msingi,
Tumaini ni kuk**ata ahadi za Mungu na kujua kuwa Mungu aliyeahidi ni mwaminifu.
1. Tumaini ni nguvu ya ndani *(Waebrania 6:19)*
Biblia inasema:
“Tumaini tulilo nalo ni k**a nanga ya roho, imara na yenye salama…”
Nanga inazuia chombo kisipeperushwe. Kadhalika tumaini linazuia roho yako isipotezwe na mawimbi ya maisha.
2. Tumaini linaangalia kile Mungu atafanya *(Rum 8:24–25)*
Paulo anasema, “Kile tunachotarajia, k**a tumekiona tayari, si tumaini…”
Hivyo tumaini huzaliwa kwenye maeneo yasiyoonekana; mahali ambapo bado hatujaona matokeo, lakini tunaamini Mungu anafanya kazi.
*SEHEMU YA 2:*
*KWA NINI WATU WANAPOTEZA TUMAINI?*
*(i) Kuangalia mazingira kuliko Mungu*
(Mathayo 14:29–31)
_"²⁹ Akasema, Njoo. Petro akashuka chomboni, akaenda kwa miguu juu ya maji, ili kumwendea Yesu.³⁰ Lakini alipouona upepo, akaogopa; akaanza kuzama, akapiga yowe, akisema, Bwana, niokoe.³¹ Mara Yesu akanyosha mkono wake, akamshika, akamwambia, Ewe mwenye imani haba, mbona uliona shaka?"_
*(ii) Kuchelewa kwa majibu ya maombi*
(1 Samweli 1:7–8)
_⁷ Tena mumewe akafanya hivyo mwaka kwa mwaka, hapo yule mwanamke alipokwea kwenda nyumbani kwa Bwana, ndivyo yule alivyomchokoza; basi, kwa hiyo, yeye akalia, asile chakula.⁸ Elkana mumewe akamwambia, Hana, unalilia nini? Kwani huli chakula? Kwa nini moyo wako una huzuni? Je! Mimi si bora kwako kuliko watoto kumi?_
*(iii) Msimamo dhaifu wa kiroho*
(Methali 24:10)
_“Ukizimia siku ya taabu, Nguvu zako ni chache.”_
*(iv) Kupitia majaribu makubwa kuliko uwezo wa mwanadamu*
(2 Kor 1:8–10)
_⁸ Maana ndugu, hatupendi, msijue habari ya dhiki ile iliyotupata katika Asia, ya kwamba tulilemewa mno kuliko nguvu zetu, hata tukakata tamaa ya kuishi.⁹ Naam, sisi wenyewe tulikuwa na hukumu ya mauti katika nafsi zetu ili tusijitumainie nafsi zetu, bali tumtumaini Mungu, awafufuaye wafu,¹⁰ aliyetuokoa sisi katika mauti kuu namna ile; tena atatuokoa; ambaye tumemtumaini kwamba atazidi kutuokoa;_
Lakini, hata kwenye hali hizo, Mungu haachi kutoa tumaini.
*SEHEMU YA 3:*
*UFUNUO WA BIBLIA KUHUSU TUMAINI*
1. MWANA MPOTEVU
Luka 15:11–24
Kijana alipotea, akaharibu kila kitu, akashuka mpaka chini, lakini bado lilikuwepo tumaini.
Tumaini lilikuwa:
•Baba alikuwa bado anamsubiri,
•Mlango wa nyumbani haukufungwa,
•Utambulisho haukupotea,
•Neema haikumkatiza.
*Ujumbe:*
Haijalishi ulifikaje hapo ulipo, bado Mungu ana mlango wa kurudi kwako na kukupa mwanzo mpya wa matumaini
2. AYUBU
Ayunu 14:7–9
Ayubu anasema:
“Kwa mti kuna tumaini… ukikatwa hutoa machipuko tena… hata ikiwa shina limezeeka, harufu ya maji litachipuka k**a mche.”
Maneno haya yanaonyesha:
•Tumaini linaweza kuonekana limekufa, lakini ndani yake kuna uhai,
•Hata ukiharibikiwa na maisha,
ukipata “harufu ya maji” yaani — *Neno la Mungu na uwepo wa Roho mtakatifu* — uhakika ulio wazi ni kuwa utainuka tena.
3. EZEKIELI NA BONDE LA MIFUPA
Ezekieli 37:1–14
Israeli walikuwa wamekufa kiroho, kimwili na kitaifa. Walijiona k**a mifupa iliyokauka.
Lakini ujumbe wa Mungu ulikuwa: *“Bado mtaishi!”*
Hata k**a:
•Ndoa yako imekauka,
•Huduma yako imekauka,
•Biashara yako imekauka,
•Ndoto zako zimekauka,
Bwana anaweza kuachilia uhai tena.
*SEHEMU YA 4:*
*SABABU KUU KWANINI BADO LIPO TUMAINI*
1. Mungu hawezi kubadilika
(Malaki 3:6)
Anasema, “Mimi Bwana sibadiliki.”
Hali zako zinazobadilika hazibadilishi asili ya Mungu.
2. Ahadi za Mungu hazipotei (Isaya 55:11)
Neno la Mungu halirudi bure.
Ikiwa aliahidi — hata k**a imechelewa — bado kuna tumaini.
3. Rehema za Bwana ni mpya kila siku (Maombolezo 3:21–23)
Yeremia anasema:
“Ndilo nalolikumbuka, kwa hiyo najitia tumaini.”
Tumaini lako halijengwi juu ya mapenzi ya binadamu; linajengwa juu ya wema wa Mungu.
4. Mungu yuko katika udhibiti hata wakati wewe huelewi (Rum 8:28)
Hata mambo mabaya anaweza kuyageuza kuwa mema.
*SEHEMU YA 5:*
*BAADHI YA MIFANO HALISI KIBIBLIA INAYOTHIBITISHA TUMAINI*
1. Hana – 1 Samweli 1
Alilia kwa miaka, lakini bado lilikuwepo tumaini la kuwa mama.
2. Yusufu – Mwanzo 37–50
Alipitia shimo, utumwa na gereza, lakini tumaini lilimfikisha kwenye kiti cha pili kwa Farao.
3. Petro – Luka 22:54–62; Yohana 21
Alimkana Bwana mara tatu, lakini bado kulikuwepo tumaini la kurudishwa kwenye huduma.
*SEHEMU YA 6:*
*JINSI YA KUJENGA TENA TUMAINI*
1. Shikilia Neno la Mungu (warumi 15:4)
*“Kwa kuwa yote yaliyotangulia kuandikwa yaliandikwa ili kutufundisha sisi; ili kwa saburi na faraja ya maandiko tupate kuwa na tumaini.”*
Neno la Mungu ndilo msingi wa tumaini.
2. Omba bila kukata tamaa
(1 wathesalonike 5:17)
*“ombeni bila kukoma;”*
Maombi huamsha tumaini ndani ya roho.
3. Jenga ushirika na watu wanaojenga
(Waebrania 10:24–25)
*²⁴ tukaangaliane sisi kwa sisi na kuhimizana katika upendo na kazi nzuri;²⁵ wala tusiache kukusanyika pamoja, k**a ilivyo desturi ya wengine; bali tuonyane; na ku*idi kufanya hivyo, kwa kadiri mwonavyo siku ile kuwa inakaribia.*
Kundi baya linaua tumaini; kundi nzuri linaunda tumaini jipya.
4. Kumbuka mambo Mungu aliyokwisha kukutendea
(Zaburi 103:2)
*“Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana, Wala usizisahau fadhili zake zote.”*
Kumbukumbu ya matendo ya Mungu ni mafuta ya tumaini.
5. Tazama mwisho Mungu aliouahidi, si hali uliyonayo sasa
(2 Kor 4:17–18)
*¹⁷ Maana dhiki yetu nyepesi, iliyo ya muda wa kitambo tu, yatufanyia utukufu wa milele u*idio kuwa mwingi sana;¹⁸ tusiviangalie vinavyoonekana, bali visivyoonekana. Kwa maana vinavyoonekana ni vya muda tu; bali visivyoonekana ni vya milele.*
*HITIMISHO*
✓ Hali yako ya sasa si hukumu yako ya mwisho.
✓ Kilio chako cha leo si tamati ya maisha yako.
✓ Kushuka ulipo shindwa si mwisho wa hadithi yako.
*BADO LIPO TUMAINI* kwa sababu:
> Mungu yupo,
> Neno linasimama,
> Roho Mtakatifu anatenda,
> Na ahadi za Mungu hazibadiliki.
Tembea leo na mtazamo mpya, kwa ujasiri mpya, ukijua kuwa wakati wa Mungu bado haujachelewa — na kwa sababu hiyo:
kuna tumaini hata k**a ulikata tamaa.
*Mungu akubariki sana*
*UHUSIANO WA SADAKA NA MAFANIKIO YAKO BINAFSI*
Whatsapp group
https://chat.whatsapp.com/IkMhhdEDNAdGnWi2H7sadf?mode=wwt
*UTANGULIZI*
Kila mwanadamu hutamani kufanikiwa—kimwili, kiroho, kifamilia, kifedha, na katika huduma.
Lakini Biblia inaweka kanuni za wazi kuhusu nafasi ya sadaka katika kuleta mafanikio ya mtu binafsi.
Sadaka sio tu kutoa kitu; ni kanuni ya kiroho inayofungua milango ambayo nguvu za kawaida haziwezi kuifungua.
Katika somo hili tutachunguza biblia inasema nini kuhusu:
••Maana ya sadaka
••Sababu sadaka ni mlango wa mafanikio
••Uhusiano wa mbegu unayopanda na matokeo unayopata
••Nguvu ya Madhabahu unayotoa juu yake
••Jinsi ya kutoa sadaka kwa namna inayovuta baraka za Mungu
*SEHEMU YA 1: MAANA YA SADAKA KIBIBLIA*
*Sadaka ni:*
1. *Ishara ya utii kwa Mungu* (Kumb 12:11).
_“wakati huo itakuwa kwamba mahali pale atakapopachagua Bwana, Mungu wenu, alikalishe jina lake, hapo ndipo mtakapoleta kila kitu ninachowaamuru; sadaka zenu za kuteketezwa, na dhabihu zenu, na zaka zenu, na sadaka ya kuinuliwa ya mikono yenu, na nadhiri zenu zote teule mtakazoweka kwa Bwana.”_
2. *Kutoa kilicho na thamani kwa Bwana*
(2 Samweli 24:24).
_“Lakini mfalme akamwambia Arauna, La, sivyo; lakini kweli nitavinunua kwako kwa thamani yake; wala sitamtolea Bwana, Mungu wangu, sadaka za kuteketezwa nisizozigharimia. Hivyo Daudi akakinunua hicho kiwanja cha kupuria na wale ng'ombe kwa shekeli hamsini za fedha.”_
3. *Mbegu ya rohoni inayozaa matokeo ya kimwili*
(2 Kor 9:6–10).
_⁶ Lakini nasema neno hili, Apandaye haba atavuna haba; apandaye kwa ukarimu atavuna kwa ukarimu.⁷ Kila mtu na atende k**a alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa lazima; maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu.⁸ Na Mungu aweza kuwajaza kila neema kwa wingi, ili ninyi, mkiwa na riziki za kila namna siku zote, mpate ku*idi sana katika kila tendo jema;⁹ k**a ilivyoandikwa, Ametapanya, amewapa maskini, Haki yake yakaa milele.¹⁰ Na yeye ampaye mbegu mwenye kupanda, na mkate uwe chakula, atawapa mbegu za kupanda na ku*izidisha, naye atayaongeza mazao ya haki yenu;_
4. *Kuelekeza moyo — Yesu alisema, “Mali yako ilipo, ndipo na moyo wako utakuwa”*
(Math 6:21).
_“kwa kuwa hazina yako ilipo, ndipo utakapokuwapo na moyo wako.”_
Hii ina maana sadaka ni zaidi ya fedha; ni ushuhuda wa moyo wa mtu kwa Mungu.
"SEHEMU YA 2:*
*KANUNI YA MWONGOZO*
— Mwanzo 8:22
_“Wakati wote nchi idumupo, MBEGU NA MAVUNO… hayatakoma.”_
Hii ni sheria ambayo Mungu mwenyewe aliweka.
Sadaka ni mbegu, na mbegu huwa na:
1️⃣Kanuni (unapanda kabla ya kuvuna)
2️⃣Samaki (kila mbegu hulipa kwa aina ileile)
3️⃣Nguvu ya kuongeza (mbegu moja huongeza mavuno mengi)
Kutoelewa kanuni ya mbegu kunawafanya watu wengi washangae kwa nini maisha yao hayasongi mbele.
*SEHEMU YA 3:*
*MIFANO YA BIBLIA INAYOONYESHA UHUSIANO WA SADAKA NA MAFANIKIO*
1. KAINI NA ABELI
— Mwanzo 4:3–7
Abeli alitoa sadaka bora — Mungu akaikubali.
Kaini akatoa ilimradi tu — Mungu hakukubali.
*Matokeo:*
🟢Abeli alifanikiwa kiroho,
🔴Kaini akafungiwa mlango wa neema na kutengwa.
💬 *Ujumbe:*
Ubora wa sadaka unaamua ubora wa matokeo.
2. IBRAHIMU
— Mwanzo 22:1–18
Alipokuwa tayari kutoa kitu chake kikubwa (Isaka), Mungu akatangaza:
_“Kwa kuwa umefanya neno hili… nitakubariki sana.”_
Sadaka ya utii ya Ibrahimu ilifungua:
☑️Agano la baraka,
☑️Ulinzi wa vizazi vyake,
☑️Kila mlango wa mafanikio.
💬 *Ujumbe:*
Kiwango cha utii katika sadaka kinafungulia mtu kiwango cha baraka.
3. MFALME SULEMANI
— 1 Wafalme 3:4–13
Sulemani aliitoa sadaka ya ng’ombe elfu moja.
Usiku ule ule, Mungu akamtokea na kumwambia:
“Omba lolote utakalo.”
Sadaka hiyo ilifungua:
☑️Hekima isiyo ya kawaida,
☑️Utajiri,
☑️Utawala ulioimarishwa,
☑️Heshima isiyo ya kawaida.
💬 *Ujumbe:*
Sadaka ina uwezo wa kuleta fursa ambazo maombi pekee hayawezi kutoa.
4. MJANE WA SAREPTA
— 1 Wafalme 17:8–16
Alitoa sadaka kwa nabii Eliya wakati njaa ilikuwa kali.
*Matokeo:*
☑️Uhai ukaingia nyumbani mwake,
☑️Makopo ya mafuta hayakuisha,
☑️Hali yake ikabadilishwa.
💬 *Ujumbe:*
Sadaka inayotolewa kwenye mazingira magumu ina uwezo wa kuleta miujiza mikubwa na matokeo ya haraka sana kwa mtoaji.
5. YESU NA MVULANA
— Yohana 6:1–13
Mvulana alitoa sadaka ya mikate mitano na samaki wawili.
Yesu akavunja, akashukuru, akagawa.
Zikazidi — wakabakisha makapu 12.
💬 *Ujumbe:*
Sadaka yako ikishaguswa na Yesu huwa haitabaki vile vile; hu*idishwa na kuongezwa mara nyingi zaidi.
*SEHEMU YA 4:*
*JINSI SADAKA INAVYOONGEZA MAFANIKIO*
*1. Sadaka inavunja vizuizi vya rohoni*
Katika 1 Samweli 7:9–13, Samweli alitoa sadaka ya kuteketezwa.
Ghafla:
▶️Adui alishindwa,
▶️Milango ya ushindi ikafunguliwa.
Sadaka inafanya kile maombi pekee hayafanyi
— inazungumza na kutoa sauti kubwa katika ulimwengu wa roho.
*2. Sadaka inavuta kibali*
Mithali 18:16:
“Zawadi humfungulia mtu njia.”
Si tu kwa wanadamu, hata mbele za Mungu.
Sulemani alipotoa
— Mungu akatokea usiku ule ule.
*3. Sadaka inaharibu nguvu na roho za umaskini*
Zaburi 20:1–3 inasema Mungu
_“hukumbuka sadaka zako.”_
Sadaka ni ushuhuda unaowasilisha mbele za Mungu kwamba unavunja mzunguko uliokuzuia.
*4. Sadaka inabadilisha misimu ya mtu*
Mfano wa mjane wa Sarepta unaonyesha:
Sadaka ina uwezo wa kugeuza kipindi cha njaa au ukame kikawa kipindi cha wingi au utele.
*5. Sadaka inasababisha mavuno kulingana na mbegu ulizopanda*
2 Kor 9:6:
_“Apandaye haba atavuna haba; apandaye kwa wingi atavuna kwa wingi.”_
Mafanikio yako yanalingana na kiwango cha utoaji wako.
*SEHEMU YA 5:*
*SADAKA NA MADHABAHU UNAYOTOA JUU YAKE*
Kila sadaka inaongea kulingana na madhabahu ilikotolewa.
*Madhabahu ni:*
⏩Nafasi ya kukutana na Mungu,
⏩Chanzo cha nguvu ya kiroho,
⏩Mlango wa baraka au laana.
*A. Madhabahu safi huleta thawabu*
(Mwanzo 8:20–22)
Nuhu alijenga madhabahu
— Mungu akabariki dunia nzima.
*B. Altare chafu huleta maangamizi*
(Waamu*i 6:25–32)
Gideoni alibomoa madhabahu ya Baali na kujenga ya Bwana, ndipo mafanikio yakaanza.
*Ujumbe:*
Mafanikio yanayokuja kupitia sadaka yako yanategemea mazingira ya kiroho unayotoa ndani yake.
*SEHEMU YA 6:*
*JINSI YA KUTOA SADAKA INAYOVUTA MAFANIKIO*
*1. Toa kwa utii*
Sadaka isiyo ya utii haina nguvu (1 Sam 15:22).
*2. Toa kwa moyo mkunjufu na kwa shukrani*
Mungu apenda watoao kwa moyo wa furaha (2 Kor 9:7).
*3. Toa kwa hekima na katika madhabahu sahihi*
Usitoe sadaka yako mahali Mungu hajakuelekeza.
*4. Toa sadaka iliyo na kiwango cha maumivu (sacrifice level)*
Daudi alisema:
“Sitatoa kwa Bwana kitu kisichonigharimu chochote.” (2 Sam 24:24)
*5. Toa kwa uwazi wa moyo kwa Mungu, si kwa kutafuta sifa*
Yesu alisema wanaotoa kwa kujionyesha tayari wamepokea thawabu yao (Math 6:1–4).
*6. Toa kwa kujenga kipindi — usiwe mtu wa sadaka ya bahati nasibu*
Zaburi 126:5–6 — “Wapandayo kwa machozi watavuna kwa kelele za furaha.”
*SEHEMU YA 7:*
*FAIDA ZA KUTOA SADAKA KATIKA MAISHA YA MWAMINI*
1. Kufunguliwa kwa milango iliyofungwa
2. Kuongezeka kwa baraka
3. Kuongezeka kwa neema ya kiroho
4. Kubadilishwa kwa misimu mibaya au kuingizwa katika majira mapya ya baraka
5. Kuvunjwa kwa laana za ukoo
6. Kukumbukwa na Mungu kwa wakati wa shida au taabu (Zab 20:1–3)
7. Kupata kibali mbele ya watu
8. Kupokea ulinzi usio wa kawaida
*(divine preservation)*
*HITIMISHO*
Mafanikio ya mtu si matokeo ya juhudi za kibinadamu pekee.
Biblia inafunua wazi kwamba:
•••Sadaka ni mlango,
•••Sadaka ni sauti,
•••Sadaka ni mbegu,
•••Na sadaka ni nanga ya mafanikio ya mtu.
K**a mbegu inavyopandwa ardhini na kutoa mavuno kwa wakati wake, ndivyo sadaka yako inavyopandwa katika ulimwengu wa roho na kutoa matokeo yanayoonekana katika maisha yako ya kila siku.
*Kwa hiyo, kumbuka:*
Kiwango cha mbegu unayopanda leo kinaamua ukubwa wa mavuno utakayovuna kesho.
*Mungu akubariki sana*
Mhubiri 4:9-11
"Afadhali kuwa wawili kuliko mmoja; Maana wapata ijara njema kwa kazi yao.Kwa maana wakianguka, mmoja wao atamwinua mwenzake; lakini ole wake aliye peke yake aangukapo, wala hana mwingine wa kumwinua!Tena, wawili wakilala pamoja, hapo watapata moto; lakini mmoja aliye peke yake tu awezaje kuona moto?"
21/04/2024
```KANAANI MPYA MINISTRY```
TABIA YA MUNGU YA KUSAMEHE NDANI YAKO
Mw.C Mwakasege
Ulipompokea Kristo kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yako, ulipokea tabia ya aina gani?
" Bali wote waliompokea (Kristo) aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake; waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu." (Yohana 1:12,13)
Whatsapp Group
https://chat.whatsapp.com/IkMhhdEDNAdGnWi2H7sadf
Web
https://draywadray.blogspot.com
Ulipozaliwa mara ya pili kwa Neno la Kristo ulifanyika kuwa mtoto wa Mungu.
Watoto wa Mungu wana tabia ya namna gani?
Kwa kuwa wamehamishwa toka ufalme mwingine na uzazi mwingine, na kuingizwa katika ufalme wa Mungu na uzazi wake (Wakolosai 1:13); watoto hawa wanatakiwa wawe na tabia nyingine.
Kabla ya kuzaliwa mara ya pili, kabla ya kumkiri Kristo ya kuwa ni Bwana: ulikuwa na tabia ya dunia hii iliyoongozwa na mfalme wa dunia hii ambaye ni shetani.
Ulipozaliwa mara ya pili na kuukiri wokovu katika Kristo, ulipokea tabia mpya inayoongozwa na Mungu mwenyewe aliye ndani yako.
" Kwa kuwa uwezo wake wa Uungu umetukirimia vitu vyote vipasavyo u*ima na utauwa (Utakatifu), kwa kumjua yeye aliyetuita kwa utukufu wake na wema wake mwenyewe. Tena kwa hayo ametukirimia ahadi kubwa mno; za thamani,ili kwamba kwa hizo mpate kuwa Washirika wa TABIA YA UUNGU, mkiokolewa na uharibifu uliomo duniani kwa sababu ya tamaa." (2 Petro 1:3,4)
Mistari hii inatuonyesha wazi kabisa kuwa kwa uweza ule ule uliokuwezesha kuwa mwana wa Mungu, unakuwezesha kuipokea tabia ya Mungu.
Tabia ya Mungu iliyo wazi ni Upendo kwa kuwa Mungu ni Upendo
(1 Yohana 4:8)
Ni upendo ambao huvumilia, hufadhili, hauhusudu, hautakabari, haujivuni, haukosi kuwa na adabu, hautafuti mambo yake, hauoni uchungu, hauhesabu mabaya, haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli,huvumiliayote,huamini yote, hutumaini yote, hustahimili yote, haupungui neno wakati wowote.K**ailivyoandikwa katika (1 Wakorintho 13:4 - 8)
Mungu anavyosamehe:
Ndani ya upendo, kuna tabia ya kusamehe na kusahau. Ili kuifahamu zaidi na tuitafakari tabia ya Mungu ya kusamehe na kusahau. Mungu anasema hivi:
" Mimi, naam, mimi, ndimi niyafutaye makosa yako kwa ajili yangu mwenyewe; wala sitazikumbuka dhambi zako." (Isaya 43:25)
Na tuitafakari tabia hii ya Mungu katika mafungu mawili yafuatayo:
1. Mimi, naam, mimi, ndimi niyafutaye makosa yako kwa ajili yangu mwenyewe; na;
2. Wala sitazikumbuka dhambi zako.
Haya ni maneno ya Mungu ambayo aliyasema kwa kutumia kinywa cha nabii Isaya, kwa ajili ya watu, baada ya kufunga agano jipya katika damu ya Yesu Kristo pamoja nao. Kwa kuwa katika agano la kale makosa (au dhambi) yalikuwa hayafutwi ila yanafunikwa tu kwa damu ya wanyama waliotolewa sadaka (Waebrania 10:1 - 25)
Lakini katika agano jipya, makosa yanafutwa kwa uwezo wa damu ya Yesu iliyomwagika msalabani.
Kuna tofauti kubwa kati ya kuifunika dhambi kwa damu na kuifuta dhambi kwa damu. Unapofunika, kosa haliondoki linabaki pale pale, lakini linakuwa halionekani. Unapofuta, kosa linaondolewa kabisa, inakuwa k**a hakuna kosa lililowahi kufanyika.
Ukiwa darasani, mwalimu akifuta maandishi ya chaki ubaoni, ubao unabaki hauna maandishi; unakuwa safi. Lakini utakuta yale yaliyokuwa yameandikwa, ingawa hayapo ubaoni, katika akili za watu yanakuwa yapo. Na wakati mwingi inachukua muda kufutika mawazoni.
Sasa, ile sehemu ya kwanza ya mstari, Mungu anasema anayafuta makosa yetu kwa ajili yake mwenyewe, Mungu hakusema "Anayafunika makosa," bali amesema, "anayafuta makosa".
Soma tena:
"Mimi, naam, mimi, ndimi niyafutaye makosa yako kwa ajili yangu mwenyewe."
Soma na maneno haya:
"Tukiziungama dhambi zetu, yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote" (1Yohana 1:9)
Ukitubu dhambi zako kwa Mungu katika Roho na Kweli, Mungu anakusamehe, na anafuta dhambi zako na mbele yake unaonekana k**a hukufanya kosa lo lote. Hivyo ndiyo maana ya kuhesabiwa haki mbele za Mungu katika Kristo. Kusamehe ni kufuta au kuondoa kosa na kulisahau au kutokulikumbuka tena.
Kusamehe kosa = kufuta + kutokulikumbuka kosa
Wakati huu tunatizama jinsi Mungu anavyotusamehe. Hatua ya kwanza anafuta kosa machoni pake.
Kwa nini Mungu atusamehe?
Kwa nini Mungu ayafute makosa yetu?
Umewahi kujiuliza kwa nini Mungu aliamua kukusamehe mabaya yote uliyoyafanya maishani mwako?
Watu wengine wanafikiri wokovu unakuja kwa kumpendeza Mungu kwa matendo yao. Na matokeo yake wanajihesabia haki wenyewe badala ya kuhesabiwa haki na Mungu.
Utamsikia mtu anasema mimi sina dhambi, siibi, sizini, silewi, sijatengwa na kanisa, na naitunza Sabato kwa hiyo sina kosa kwa Mungu!
Lakini neno la Mungu linatuambia mambo tofauti, kwa mfano neno linasema hivi:
" Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu; wala SI KWA MATENDO, mtu awaye yote
asije akajisifu (Waefeso 2:8,9)
Kwa hiyo, unaona kuwa matendo yako peke yake hayawezi kukupa wokovu, na ondoleo la dhambi, bila ya imani ndani ya Kristo. Imani lazima iambatane na matendo. Imani pasipo matendo imekufa (Yakobo 2:26).
Kitu kinachomfanya Mungu akusamehe si uzuri wa matendo yako; bali anakusamehe KWA AJILI YAKE MWENYEWE.
Mungu anasema; "Mimi, naam, Mimi, ndimi niyafutaye makosa yako KWA AJILI YANGU MWENYEWE"
Huu ndiyo upendo wa ajabu!
Kumbuka si kwa matendo yako bali kwa ajili yake mwenyewe Mungu, unapata kusamehewa makosa yako.
Mungu akisamehe anasahau:
Hatua ya pili ambayo Mungu anaichukua mara tu anapofuta makosa yako ni kuyasahau aliyokwisha yafuta.
Yeye mwenyewe ameahidi kwamba ".... Wala sitakumbuka dhambi zako". WALA SITAKUMBUKA DHAMBI ZAKO!
Ina maana kuwa Mungu akiisha kukusamehe kwa ajili yake mwenyewe; anafuta na kusahau makosa uliyofanya, anakuhesabia haki bure mbele zake. Unasimama ndani yake k**a mtu ambaye hajawahi kufanya kosa wala dhambi yo yote.
Sasa k**a Mungu amekwishafuta na kuyasahau mambo uliyofanya kabla hujaokoka na ukatubu, kwa nini wewe unayakumbuka? Jifunze kujisamehe mwenyewe! Mungu akikusamehe na wewe jisamehe. Mungu asipoyakumbuka makosa yako, na wewe usiyakumbuke!
Huduma za watumishi wengi zinakwama mara tu anapokumbuka mambo aliyoyafanya zamani au maneno aliyoyasema - hata k**a wamekwishayatubia!
Kwa sababu hiyo, badala ya kusonga mbele katika Bwana, anajikuta kila wakati wanatubu juu ya dhambi hiyo hiyo. Na wanakosa ujasiri wa kusimama mbele za Mungu, mbele ya shetani na mbele za watu.
Kila wanapotaka kufanya kitu, shetani anawaletea wazo kuwa, bado hawajasamehewa kosa alilolifanya jana au ju*i. Na kwamba haitakuwa rahisi kwako kupokea baraka toka kwa Mungu. Kwa hiyo watu hawo anaanza kutubu tena upya!
Watu wengi hata sasa hawana uhakika k**a Mungu amewasamehe juu ya makosa waliyoyafanya.
Uhakika utaupata katika Neno la Mungu.
Mungu ameahidi kuwa ukitubu katika Roho na Kweli, unasamehewa.
(1Yohana 1:9)
Paulo alifahamu siri hiyo ya kuyasahau mambo ya nyuma aliyomkosea Kristo, kwa kuwatesa wafuasi wa Yesu, kabla ya kuokoka kwake. Hii ilimsaidia kulitangaza Jina la Yesu bila yeye kujisikia vibaya moyoni mwake.
Kwa hiyo Paulo aliweza kusema:
"...... ila natenda neno moja tu; nikiyasahau yaliyo nyuma, nikiyachuchumilia yaliyo mbele, nakaza mwendo niifikilie mede ya thawabu ya mwito mkuu wa Mungu katika Kristo Yesu" (Wafilipi 3:13,14)
Ili uweze kusonga mbele katika wokovu, ni budi ujifunze kujisamehe na kuyasahau uliyoyafanya zamani.
Tabia hii unayo ndani yako:
Kuyafuta makosa na kutoyakumbuka tena ni tabia ya Mungu ambayo imo ndani yako sasa.
Ulipompokea Kristo moyoni mwako na kumkiri kuwa ni Bwana wa maisha yako, pia ulipokea ndani ya moyo wako tabia hii ya Mungu ya kufuta makosa na kutoyakumbuka.
Hii ndiyo tabia inayotakiwa ionekane katika maisha yako unapokosewa na mtu.
Tatizo la wengi ni kwamba wamekuwa viumbe vipya, lakini wanataka kutumia tabia yao ya zamani. Katika tabia ya zamani, walisamehe lakini hawakusahau walichokosewa. Tabia mpya ni kufuta makosa na kutoyakumbuka kabisa. Kwa hiyo na sisi tukikosewa tunatakiwa kusamehe na kusahau!
Hatua zifuatazo katika mfululuzo wa masomo yanayofuata wiki zijao zitakusaidia kuijenga na kuitumia tabia hiyo ya Mungu iliyo ndani yako. Tunaamini utakuwa pamoja nasi wiki ijayo ili kuendelea na somo hili - katika kipengele kinachosema: "Hasara za kulipiza kisasi"
KANAANI MPYA WhatsApp Group Invite
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Contact the public figure
Telephone
Website
Address
Around The World
Mwanza