De Opera
Tanzanian and East African record Producer, Songwriter. Tanzanian & East African musician.
“You never win by defending — and only sometimes by attacking.
Calm is your weapon!
So keep calm.” ✍️💭
Quote of the day!
20/01/2026
Hakuna aliyemkamilifu ila kuna mambo hayana budi kukamilika abadani.
De Opera/
on social networks.
Siraj Kingi
15/01/2026
Hakuna lililo dahari, kila hatua ina kingo.
De Opera/
on social networks.
Siraj Kingi
15/01/2026
Mambo yanaweza kuwa mengi ila mengi yakawa si mambo!
De Opera/ on social networks.
Siraj Kingi
11/01/2026
Tatizo linauliza tatizo!
De Opera/ on social networks.
20/12/2025
Huwezi kukosoa. Shida na matatizo ndivyo vimefanya wafikie hapa.
Kuna watu wanapitia changamoto kubwa sana kiasi cha kwamba ukipewa moja tu unakufa, kila njia walishapita. Ni heri hata huyu awapaye udongo pengine kwa imani zao watapona kuliko yule anayewahukumu kuwa wamekosa maarifa. K**a una njia nyingine ya kuwasaidia, jitokeze hadharani. Wasaidie! Ushauri hautoshi kwa mtu mwenye hamu ya kupona.
11/12/2025
KABLA HAMJAWEKA AGANO, NG'AMUA HILI.
Kiapo ni nini?
Hii ni ahadi ya kuonesha ukweli au uaminifu, inayotamkwa mbele ya mtu, watu, au mamlaka fulani. Ni maneno yanayoweza kutamkwa kwa sababu yoyote, hata bila ukweli wa moyoni.
Agano ni nini?
Ni kubaliano maalum kati ya pande mbili au zaidi, lenye masharti, ahadi, na wajibu ambao kila upande unakubali kuufuata. Ni k**a mkataba, lakini mara nyingi huwa na uzito wa kiroho, kiimani, au uaminifu wa juu.
Kuna mtu mmoja aliniuliza, "Wanandoa hula kiapo au hufanya Agano?"
Jibu langu ni kwamba:
Soma hapa... https://deoperahub.blogspot.com/2025/12/kabla-hamjaweka-agano-ngamua-hili.html
10/12/2025
NAMNA YA KUJITOA KWA WATU SAHIHI (A true selfless sacrifice)
Mwenye njaa hawezi kukaa ndani, hata akizuiwa lazima atatoka tu. Akitaka kutoka akaambiwa rudi ndani, lazima atauliza 'mpaka muda gani'? 'Nitatoka saa ngapi?', 'Mi sijazoea kukaa ndani' na mara nyingi utamkuta yupo dirishani anachungulia nje. K**a hawezi kulifikia dirisha, basi yeye hukaa mlangoni akisikiliza k**a kuna mtu anakuja kufungua na hapo ukienda kufungua mlango ghafla, atapata umemng'oa kucha.
Hii inatufunza nini?
kuna baadhi ya watu wakiwa na nia huwa hawana subira, na mara nyingi huonekana wasumbufu na ndio hufanikiwa. Unaweza ukaminya mwisho wa siku utakubaliana.
Watu wengi wenye mipango thabiti, huwapima watu kwa nia na uwajibikaji.Hii ni k**a kumpa au kumuahidi chakula aliyeshiba. Hawezi kuona kinachelewa, hata ukimuambia atakula wakati mwingine, yupo tayari kusubiri. Hawezi kukusumbua. Unaweza dhani ni mtulivu, la hasha! hakuna utulivu penye njaa. Kwa hiyo k**a ni mtu mwenye malengo huangalia mwenye njaa kwa sababu huyo atakuwa na moyo wa kupambana na mwenye kuleta mipango mipya njinsi ya kuidhibiti njaa.
SOMA ZAIDI... https://deoperahub.blogspot.com/2025/12/namna-ya-kujitoa-kwa-watu-sahihi-true.html
14/11/2025
Habari mwana DoHub, natumaini unaendelea vizuri na
Karibu tena katika makala hii.
Leo nitazungumza kuhusu mawasiliano. Jinsi ya kukuza, kujenga na kuimarisha.
Mawasiliano ni kitu muhimu sana katika maisha yetu. Mawasiliano yanaweza kukuinua kutoka hatua fulani, kuipima hekima/busara yako, au kutengeneza uaminifu kati ya mtu na mtu au kikundi.
Kuna aina mbili za mawasiliano:
Mawasiliano ya Vifaa (Devices) — hususan simu
Mawasiliano ya Kijamii (Social Communication)
Nianze na mawasiliano ya vifaa(simu).
Kuna baadhi ya watu huchukulia tu mawasiliano ya simu k**a ni kitu cha kawaida tu na hayana maana sana.
Sasa, ngoja niseme! Mawasiliano ya simu yanaweza kukufanya uonekane wewe ni mtu mwenye hekima na busara sana kwa namna unavyoitumia. Mtu anaweza kukushusha hadhi na kukuondelea thamani endapo utatumia simu vibaya.
Mfano, ni namna mtu unavyoweza kumuuliza, kumjibu, kuzungumza.
Mtu anashushwa thamani au kupandishwa thamani wakati gani?.
Soma zaidi.. 👇
https://deoperahub.blogspot.com/2025/11/njinsi-ya-kujenga-kukuza-na-kuimarisha.html
02/09/2025
Habari za muda huu mpwa wangu? Natumaini unaendelea vizuri na tunakutana tena kwenye blog hii ya DOHub.
Leo nitaenda kuzungumza kuhusu urafiki kati ya jinsia mbili tofauti, jinsi unavyoweza kuharibu/kubomoa uhusiano uliokwisha jengwa au kuzuia/kukwamisha ujenzi wa uhusiano mpya.
Si jambo baya kujenga urafiki, lakini tazama urafiki unaokuwa nao unakupa faida ama hasara?.
Soma zaidi..
https://deoperahub.blogspot.com/2025/09/jinsi-urafiki-wa-jinsia-mbili-tofauti.html
07/08/2025
Maisha hutusogeza mbali na wapendwa wetu, lakini moyo hubaki uleule. My appreciation!
Mohamed Hussein "Zimbwe Jr" .
Mungu akikupandikizia upendo kwa watu hakuna mtu atakuchukia, bali kila mtu ataupeza uwepo wako. Haijalishi hujawafanyia chochote cha kushangaza bali ni kibali tu ulichonacho.
Hata mtu afikapo kukuchukia, baadaye hujiwazia yeye mwenyewe na kuona hakuna anachofaidika na hivo hulifungua tabasamu.
Yule akutengaye kwa tamaa, mpe kheri. Mpe kheri kila awaye kando yako na hata asiye kando yako.
Usibague watu wa kuongea nao, bali chagua watu wa kuwaeleza changamoto zako.
Na katika kuongea na watu, tambua kila kundi/mtu unapaswa kuongea maneno ya namna gani.
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Website
Address
Mwanza