Kasherente TV
Professional youtube coach
11/06/2026
TAHARUKI ARUSHA! GARI LA WATALII LASHAMBULIWA, MWENYEKITI CHAMBULO ALALAMIKIA USALAMA
Mkoa wa Arusha umeingia kwenye mjadala mkubwa wa usalama baada ya kuripotiwa tukio la kushambuliwa kwa gari lililokuwa limebeba watalii na watu wasiojulikana, hali iliyozua hofu kwa wadau wa sekta ya utalii.
Kwa mujibu wa taarifa zinazosambaa, Mwenyekiti wa Chama cha Waendeshaji wa Utalii Tanzania (TATO), Wilbard Chambulo, ametoa tamko kali akieleza wasiwasi wake kuhusu hali ya usalama katika baadhi ya maeneo ya Arusha. Inadaiwa Chambulo amesema kuwa baadhi ya vituo vya polisi vilivyokuwa vinahudumia maeneo ya utalii vimepunguzwa au kuachwa, jambo ambalo linaweza kuongeza mianya ya matukio ya kihalifu dhidi ya wageni na watalii.
Arusha ndiyo lango kuu la utalii wa kaskazini mwa Tanzania, ikihudumia watalii wanaoelekea maeneo maarufu k**a Serengeti National Park, Ngorongoro Conservation Area na Mount Kilimanjaro. Hivyo, tukio lolote linalohusisha usalama wa watalii huibua taharuki kubwa ndani na nje ya nchi.
Taarifa zilizopo zinaonyesha kuwa wadau wa utalii wamekuwa wakisisitiza umuhimu wa kuimarishwa kwa ulinzi kupitia Polisi wa Utalii, kitengo ambacho kwa miaka mingi kimekuwa kikihusika na kulinda wageni wanaotembelea vivutio vya Tanzania.
Hata hivyo, hadi sasa haijaonekana taarifa rasmi ya kina kutoka Jeshi la Polisi ikieleza mazingira kamili ya shambulio hilo, idadi ya waliojeruhiwa au kuk**atwa kwa watuhumiwa. Uchunguzi zaidi unaendelea kusubiriwa kutoka kwa mamlaka husika.
Swali kubwa linaloulizwa na wengi ni hili: Je, tukio hili ni tukio la kawaida la uhalifu au ni ishara kwamba usalama katika njia za watalii unahitaji kuimarishwa haraka zaidi?
11/06/2026
๐จ MANENO YA KIDUKU YAZUA MJADALA MKUBWA BAADA YA HASARA YA HASSAN! ๐ณ๐ฅ
Baada ya Hassan kupoteza pambano lake, bondia maarufu Kiduku amevunja ukimya na kutoa ujumbe uliogusa hisia za wengi.
Kiduku amesema hakuna bingwa wa kweli ambaye hajawahi kuonja machungu ya kushindwa, akisisitiza kuwa makovu na maumivu ndiyo sehemu ya safari ya mafanikio. Amesema kupoteza pambano si mwisho wa ndoto, bali ni nafasi ya kujifunza, kujipanga upya na kurudi akiwa imara zaidi.
"Champion wa kweli lazima awe na makovu. Hakuna bingwa ambaye hajawahi kuanguka," amesema Kiduku.
Kauli iliyowavutia wengi zaidi ni pale alipomhimiza Hassan kutokata tamaa, akisema huu ndio wakati wa kuwaonyesha Watanzania na dunia nzima kuwa bado ana uwezo wa kurudi juu zaidi kuliko awali.
๐ฅ Je, unaamini Hassan anaweza kurejea kwa nguvu zaidi na kutwaa ushindi katika pambano lijalo?
๐ฅ๐น๐ฟ
11/06/2026
Habari za Papo kwa Papo ๐ฅน๐ฅน๐ฅน๐ณ๐ฌ๐
Msanii maarufu wa Nigeria, Davido, alionekana akiwa amevaa koti lililoandikwa majina ya watoto 26 waliotekwa nyara na majambazi nchini Nigeria wakati wa maonyesho yake ya kuhesabu muda kuelekea FIFA.
Kupitia kitendo hicho, Davido alitumia jukwaa lake kuonyesha dunia mateso na changamoto wanazopitia watu wa nchi yake. Nyuma ya koti hilo kulikuwa na maandishi makubwa yaliyosomeka: โBring Back Our Girlsโ (Warudisheni Wasichana Wetu).
Davido ameonyesha mfano wa kipekee wa kutumia umaarufu wake kutetea masuala ya kijamii na kuhamasisha watu kuhusu matatizo yanayoikabili jamii yake.
Tunaendelea kumuombea na kuamini kwamba Mungu atambariki kwa kitendo hiki cha kugusa mioyo ya wengi.
Funzo: Inashangaza kuona bado kuna watu wasiompende Davido baada ya hatua hii ya kuonyesha mshik**ano na huruma kwa wahanga wa tukio hilo. โค๏ธ๐๐พ
11/06/2026
HUYU NDIO "SLEEPINGBEAUTY": MWANAMKE ALIYELALA MILELE JUU YA MLIMA HATARI ZAIDI DUNIANI
Katika ukimya wa kutisha wa Mlima Everest, mita zaidi ya 8,500 kutoka usawa wa bahari, kuna simulizi moja ambalo huwafanya hata wapandaji hodari zaidi kushtuka.
Wanaliita "Sleeping Beauty".
Jina hilo halikutokana na hadithi za kufikirika, bali lilitokana na mwili wa mpandaji mlima kutoka Marekani, Francys Arsentiev, ambaye alifariki mwaka 1998 akiwa njiani kushuka kutoka kileleni mwa Everest.
Francys alikuwa ametimiza ndoto yake kubwa ya kufika kilele bila kutumia oksijeni ya ziada. Lakini ushindi huo uligeuka kuwa jinamizi la kutisha.
Akiwa amechoka kupita kiasi na kukosa nguvu za kuendelea, alibaki peke yake ndani ya ukanda unaoitwa "Death Zone" โ eneo ambalo mwili wa binadamu huanza kufa polepole kutokana na ukosefu mkubwa wa oksijeni.
Asubuhi iliyofuata, wapandaji wengine walimkuta akiwa bado hai lakini akiwa ameganda vibaya na kushindwa kusogea. Kwa sauti ya huzuni iliyovunja mioyo ya wengi, alisikika akiomba msaada huku akisema:
"Msiniache peke yangu..."
Lakini katika mazingira hayo ya kifo, hata kujaribu kumuokoa kulihatarisha maisha ya waokoaji wenyewe.
Hatimaye, Francys alifariki akiwa amelala upande mmoja wa njia kuu ya kuelekea kileleni.
Kwa miaka mingi, mwili wake uliendelea kuonekana na maelfu ya wapandaji waliopita eneo hilo. Uso wake wa amani na mavazi yake yaliyoganda kwenye barafu vilimfanya apewe jina la kutisha lakini la kusikitisha โ Sleeping Beauty.
Leo hii, simulizi yake bado ni mojawapo ya hadithi zinazoumiza na kutisha zaidi kuwahi kutokea kwenye Everest. Ni ukumbusho kwamba juu ya mlima huo hakuna ushindi wa bure, na kosa dogo tu linaweza kugeuza ndoto kuwa safari ya mwisho.
โ๏ธ Je, wewe ungeendelea kupanda kuelekea kileleni ukijua mbele yako kuna miili ya watu waliopoteza maisha wakifuatilia ndoto hiyo hiyo? :::
11/06/2026
โTumekuwa tukiiba sana mafuta ya Iran ๐ฎ๐ท tuna Mamillion ya mapipa tumechukua Iran ila ilikuwa siri sana na wakati huu Iran wameshagundua nimeona niseme tu kwakuwa sihofii kusema na bei ya mafuta itashuka sana hakuna shidaโ
- Donald Trump, Rais wa Marekani ๐บ๐ธ
11/06/2026
๐จ TETESI NZITO: Klabu ya Pyramids FC ya Misri imeanza mazungumzo ya siri ya kumuwania nyota wa Yanga, Pacome Zouzoua. ๐จ๐ฎ๐ฅ
Taarifa zinaeleza kuwa mabingwa hao wa Afrika wamevutiwa na kiwango bora cha Pacome msimu huu na wako tayari kutoa dau kubwa ili kupata saini yake.
Inadaiwa Pacome anaonekana k**a mbadala sahihi wa Fiston Mayele ambaye hatma yake ndani ya Pyramids bado haijawa wazi. ๐
Je, Yanga wataweza kumzuia nyota wao muhimu kuondoka au Pyramids watafanikisha dili jingine kubwa kutoka Jangwani? ๐ฐ๐ข๐ก
11/06/2026
Mchambuzi nguli wa Michezo Edo Kumwembe amehoji kwanini baadhi ya Watanzania wanashangilia baada ya Hassan Mwakinyo kupoteza pambano lake dhidi ya Michael Soro wa Ivory Coast.
"Hiki kitu kimeniuma, lakini sina cha kufanya. Watanzania wengi wanashangilia mjomba wangu, Hassan Mwakinyo Jr, kupoteza pambano lake. Nimemuita mjomba kwa sababu mama yangu anatokea Tanga."
"Tatizo ni mjomba Hassan au Watanzania? Tufungue mjadala. Ingekuwa ni pambano la ndani, isingekuwa shida. Lakini sisi na yule jamaa Soro, ilipaswa kuwa ni pambano la SISI dhidi ya YEYE."
"Hili limekuwa tofauti. Imekuwa k**a vile SISI na Soro dhidi ya Mjomba Hassan. Labda kuna mahali Anko amekosea wakati akijenga maisha yake katika mchezo huu."
"Vyovyote ilivyo, yeye ndiye bondia bora zaidi Tanzania kwa sasa. Hata hivyo, kuwa na mahusiano mazuri na jamii yako ni jambo muhimu katika maisha ya kila siku."
"Nani anamchukia Mbwana Samatta kiasi cha kufurahia akikosa goli? Sidhani. All the best, Anko Hassan. We will rise again..." - Ameandika Edo Kumwembe.
10/06/2026
Kuna Ukweli hapa?
10/06/2026
๐จ IRAN YARUHUSIWA KUINGIA MAREKANI KABLA YA MECHI ZA KOMBE LA DUNIA! ๐ฎ๐ทโ
๐บ๐ธ
Baada ya sintofahamu iliyotawala siku za hivi karibuni, mamlaka za Marekani zimethibitisha kuwa kikosi cha Iran kitaruhusiwa kuingia nchini siku moja kabla ya mechi zake za Kombe la Dunia 2026.
โ๏ธ Timu hiyo, ambayo imeweka kambi yake nchini Mexico, itasafiri kwa ndege maalum kuelekea miji itakayocheza mechi zake za Kundi F dhidi ya New Zealand, Belgium na Misri.
Hata hivyo, baadhi ya maafisa wa ujumbe wa Iran bado wanakabiliwa na changamoto za visa, jambo ambalo limeendelea kuzua mjadala kuelekea mashindano hayo.
10/06/2026
Huo hapo ujumbe Wa muigizaji Nicole, amesema hawakubali wanaume kwanza ni watu wanao jiona Bora kuliko.
Nicole ameanza kampeni ya kupinga ndoa na amejipa cheo Cha Mwenyekiti Wa Wapinga Ndoa nchini.
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Contact the business
Telephone
Website
Address
Moshi