Moshi Poultry

Moshi Poultry

Share

Wauzaji Wa Vifaranga wa chotara na vifaranga wa kuku wa mapambo mfano kuchi,brahma, silkies na bantam

The moshi poultry farm is concerned with production of chick's, chicken, beekeeping and irrigation system in farms.

24/12/2025

Black australop
0754 469 193

27/09/2025
27/09/2025

Follow this link to join my WhatsApp group: https://chat.whatsapp.com/CPCd3PIUAUG6bq5yovjSbr

26/09/2025

Ooops

18/09/2025

Vifaranga wa brahma 45,000 @1
0710469193/0754469193
Moshi

14/09/2025

UELEKEO WA BANDA LA KUKU 🏡
Uelekeo wa banda la kuku ni jambo la msingi sana kwa ufugaji bora. Ukitengeneza banda bila kuzingatia uelekeo, unaweza kusababisha matatizo ya joto, baridi na hata magonjwa.

📌 Kanuni za uelekeo wa banda la kuku:

1. Uelekeo wa mlalo (East–West)
Yaani upepo utokee mashariki kwenda magharibi

Banda bora hujengwa likielekea mashariki – magharibi.

Hii inasaidia kuepuka jua kuingia moja kwa moja ndani ya banda muda mwingi wa mchana, hivyo kupunguza joto na kuepusha kuku kuathiriwa na mwanga mkali.

2. Uingizaji hewa (Ventilation)

Kuta za kaskazini na kusini zibaki wazi au zifungwe na waya wa wavu (mesh) kwa ajili ya hewa.

Hii inaruhusu upepo kuvuka moja kwa moja kwenye banda, kuku wakapata hewa safi na unyevu usikae ndani.
3. Mvua na upepo mkali

Eneo lenye upepo mkali, banda lipandikwe kiasi cha miti ya kukinga upepo upande unaobeba upepo zaidi.

Paa liwe na mteremko mzuri kuzuia maji ya mvua kuingia ndani.
4. Mazingira ya eneo

Banda lijengwe sehemu kavu, isiyo na maji kusimama.

Epuka kujenga sehemu ya chini/mabwawa kwa kuwa unyevu huleta magonjwa.

🏡 Kwa ufupi: Uelekeo bora wa banda la kuku ni mashariki–magharibi, kuta za kaskazini na kusini ziwe wazi kwa hewa, na banda lijengwe sehemu kavu yenye kinga dhidi ya upepo na mvua.
_______________________
FOMULA NZURI YA CHAKULA CHA KUKU WA MAYAI NI 10,000 TU.

FOMULA YA PELLETS NI
25,000

SAMAKI NI 12,000

0754 469 193

13/09/2025

🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥
🔥🐓🐓🐓🐓🐓🐓🐓🐓🐄🐐

FORMULA NZURI YA KUTENGENEZA CHAKULA .......

KUKU 10,000 /=

NG'OMBE 7500/=

SAMAKI 10,000/=

Ninakutumia unalipia ✅

(Only serious people)

0754 469 193 ☎️📞

09/09/2025

🤧 🤧 🤧 🤧 🤧 🤧 🤧 🤧 🤧

TAFADHALI NAOMBA UPITIE HAPA KIDOGO....

Mzunguko wa hewa bandani ni muhimu sana hivyo kukiwa na mzunguko hafifu upumuaji wa kuku huwa ni shida ni sawa na wewe unapokua toilet huwa unatoka haraka maana huwezi vumilia ile hewa au harufu,,,

Okay sikia hii....Hewa ya amonia huzalishwa na kinyesi cha kuku ikikaa muda mrefu au kuoza hivyo mapafu ya kuku hayawezi kuhimili hali iyo na huvuta amonia na kuleta mafua ya kuku (respiratory diseases) huwa na uhusiano mkubwa sana kwenye banda la kuku.

✍️ Chanzo cha hewa ya amonia
Hutokana na kinyesi cha kuku kinapooza na kutoa gesi ya ammonia.

Banda lisilokuwa na ventilation (hewa ya kutosha) hufanya gesi hiyo kujikusanya.

Banda lenye unyevu mwingi (maji kumwagika, manyasi/chaff mbovu) huchochea uzalishaji wa ammonia.
✍️ Madhara ya hewa ya amonia kwa kuku

1. Husababisha macho ya kuku kutoa machozi na kuvimba.
2. ✍️Hupunguza kinga ya mwili → kuku wanashambuliwa kirahisi na magonjwa ya mafua.

3. ✍️Hujeruhi njia ya hewa (mapafu, pua, koo) → kuku wanapiga chafya, wanakoroma.

4. ✍️Hupunguza kasi ya kukua na uzalishaji wa mayai.
🤧 Mafua bandani (respiratory diseases)
Hutokea zaidi pale banda lina hewa chafu, baridi na unyevu. Magonjwa yanayochochewa na amonia ni pamoja na:

CRD (Chronic Respiratory Disease)

Infectious Coryza

Bronchitis

Newcastle (huwa mbaya zaidi k**a kinga imeshuka kutokana na amonia).
💉Namna ya kudhibiti hewa ya amonia na mafua
1. 📌Usafi wa banda – toa kinyesi mara kwa mara, badilisha kitanda (litter) kilichooza.
2. 📌Ventilation nzuri – hakikisha banda lina madirisha au nafasi za hewa, bila kuingiza upepo mkali.
3.📌 Epuka unyevu – maji yasimwagike, tumia drinkers zisizomwagika kirahisi.
4. 📌Tumia dawa za kupunguza harufu ya kinyesi (k**a zeolite, lime/ chokaa, EM solutions).
5. 📌Chanjo na dawa – hakikisha ratiba ya chanjo inafuatwa; ukiwa na dalili za mafua unaweza kutumia antibiotics (k**a oxytetracycline, tylosin) kwa ushauri wa daktari wa mifugo.

6. 📌Vitamini na madini – toa multivitamin au dawa za kuongeza kinga (vitamin A, C, E) kusaidia kupunguza madhara.
👉 Kwa ufupi, amonia ndicho chanzo kikuu cha kuibua mafua bandani, hivyo tiba ya kweli ni kuimarisha usafi na hewa safi kabla ya dawa.
=====================
KWA FOMULA NZURI YA KUTENGENEZA CHAKULA CHA KUKU 10,000 TU
0754 469 193 📞☎️

26/08/2025

Mafua ya kukoroma kwa kuku mara nyingi husababishwa na magonjwa ya mfumo wa hewa (respiratory diseases). Hali hii hufanya kuku wapumue kwa shida na kutoa sauti za kukoroma au kufoka.

Vyanzo vya mafua ya kukoroma kwa kuku 🐓

1. Newcastle Disease (NCD) – homa kali inayoambatana na kupumua kwa shida, kikohozi, na wakati mwingine kupooza.

2. Infectious Bronchitis (IB) – virusi vinavyoshambulia mapafu na figo, kuku hupiga chafya na kutoa k**asi puani.

3. Chronic Respiratory Disease (CRD) – husababishwa na bakteria Mycoplasma gallisepticum; kuku hukoroma, kutoa mak**asi na kupungua uzito.

4. Infectious Coryza (Homorona) – ugonjwa wa bakteria unaosababisha harufu mbaya, kuvimba usoni na kukoroma.

5. Mazingira duni – vumbi, baridi, unyevunyevu au msongamano huongeza mafua na kusababisha kukoroma.

---

Dalili kuu

Kuku kukoroma au kutoa sauti k**a ngurumo wanapopumua

Kupiga chafya na kutoa mak**asi puani

Macho kuvimba au kutoa machozi

Kushindwa kula vizuri na kupungua uzito

Vifo endapo ugonjwa ni mkali (hasa Newcastle au Bronchitis)

---

Hatua za kuchukua

✅ Toa huduma ya haraka:

Watenge wagonjwa (isolation).

Safisha na hemea banda, epuka vumbi na baridi.

✅ Matibabu (kwa yale yanayotibika):

Dawa za antibiotic kwa CRD na Coryza (mfano: Tylosin, Oxytetracycline, Doxycycline – kwa ushauri wa daktari).

Vitamin na dawa za kuongeza kinga (multivitamin, stress pack, glucose).

Chanjo kwa magonjwa ya virusi (NCD, IB) kwani hayana tiba bali kinga.

✅ Kinga:

Ratibu chanjo mapema (mfano Newcastle kila wiki 3–4 kulingana na umri).

Usafi na uingizaji hewa mzuri.

Epuka msongamano na unyevunyevu kwenye banda.

0754 469 193

Want your public figure to be the top-listed Public Figure in Moshi?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Category

Telephone

Website

Address


Moshi

Opening Hours

Monday 09:00 - 17:00
Tuesday 09:00 - 17:00
Wednesday 09:00 - 17:00
Thursday 09:00 - 17:00
Friday 09:00 - 17:00
Saturday 11:00 - 17:00