GALOD TZ

GALOD TZ

Share

Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from GALOD TZ, Sports, Moshi.

16/09/2026

Timu ya Taifa ya Tanzania πŸ‡ΉπŸ‡Ώ, Taifa Stars, imezindua rasmi jezi mpya ya nyumbani, ikiwa ni sehemu ya mwonekano mpya wa timu hiyo kuelekea michezo ijayo ya kimataifa.

Jezi hiyo imekuja ikiwa na muonekano unaobeba utambulisho wa Tanzania, huku rangi ya taifa ikiendelea kuwa sehemu muhimu ya muonekano wa Taifa Stars. πŸ‡ΉπŸ‡Ώβš½

πŸ”₯ Je, umeipokeaje jezi mpya ya Taifa Stars?

πŸ‘‡ ITOLEE ALAMA 1–10!

16/09/2026

Mshambuliaji wa Inter Miami, Lionel Messi, ameendelea kuandaa ukurasa wa mwisho wa safari yake akiwa na Timu ya Taifa ya Argentina, huku akitarajiwa kupewa heshima maalum mbele ya mashabiki wa nchi hiyo.

Shirikisho la Soka la Argentina (AFA) limetangaza kuwa Argentina itacheza dhidi ya Benin Oktoba 6, 2026, katika Uwanja wa Estadio Monumental, Buenos Aires β€” mchezo unaotarajiwa kutumika k**a sehemu ya kumuaga Messi.

Messi, ambaye ni mshindi wa Ballon d’Or mara nane, ameacha historia kubwa akiwa na Argentina. Katika safari yake ya kimataifa, ameitumikia nchi hiyo kwa zaidi ya miaka 20 na kushinda mataji makubwa yakiwemo:

πŸ† Kombe la Dunia 2022
πŸ† Copa AmΓ©rica 2021
πŸ† Copa AmΓ©rica 2024

Pia anaondoka akiwa mfungaji bora wa muda wote wa Argentina, akiwa amefikisha mabao 125 katika mechi 207 kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa kuhusu rekodi yake ya kimataifa.

πŸ”₯ AFA na kocha Lionel Scaloni pia wamewaalika wachezaji waliokuwa sehemu ya kikosi cha Argentina kilichotwaa Kombe la Dunia 2022 pamoja na familia zao, kwa ajili ya kushiriki katika tukio hilo maalum la kumuenzi Messi.

πŸ“… Ratiba ya mechi za Argentina:
πŸ‡¦πŸ‡· Argentina πŸ†š Bolivia β€” Septemba 30, 2026
πŸ‡¦πŸ‡· Argentina πŸ†š Burkina Faso β€” Oktoba 3, 2026
πŸ‡¦πŸ‡· Argentina πŸ†š Benin β€” Oktoba 6, 2026

Baada ya kumaliza safari yake ya kimataifa, Messi ataendelea na soka la klabu akiwa na Inter Miami nchini Marekani.

πŸ‘€ Je, unadhani Messi anastahili kupewa heshima gani kubwa zaidi katika mchezo wake wa mwisho akiwa Argentina?

πŸ“² GALOD TZ β€” Michezo na Burudani
πŸ‘‰ Like πŸ‘ | Comment πŸ’¬ | Share πŸ”„ | Follow βœ…

15/09/2026

Arsenal leo, Jumanne Septemba 15, 2026, inashuka dimbani kwenye Mzunguko wa Tatu wa Carabao Cup dhidi ya Ipswich Town, huku kocha Mikel Arteta akifanya mabadiliko kadhaa kwenye kikosi chake.

🚨 KUMBE MAX DOWMAN ANAANZA!

Kijana mwenye umri wa miaka 16, Max Dowman, amepewa nafasi ya kuanza katika kikosi cha Arsenal, hatua inayoweka macho ya mashabiki wengi kwenye kiwango chake dhidi ya Ipswich.

πŸ”΄ ARSENAL XI:
Kepa Arrizabalaga; Marli Salmon, Gabriel MagalhΓ£es, Myles Lewis-Skelly, MartΓ­n Zubimendi; Bruno GuimarΓ£es, Mikel Merino, Max Dowman; Noni Madueke, Eberechi Eze, Viktor GyΓΆkeres.

πŸ”΅ IPSWICH TOWN XI:
Christian Walton; Darnell Furlong, CΓ©dric KiprΓ©, Jacob Greaves, Abdoul Ouattara; Florentino LuΓ­s, Marcelino NΓΊΓ±ez, Kasey McAteer, Anis Mehmeti; Jaden Philogene, Zian Flemming.

⏰ Muda: Saa 4:00 Usiku EAT
🏟️ Uwanja: Portman Road
πŸ“Ί Matangazo: Sky Sports+
πŸ† Mashindano: Carabao Cup – Mzunguko wa 3

πŸ“Œ Jambo lingine la kuzingatia: Mchezo huu hautakuwa na VAR, kwa mujibu wa utaratibu wa mashindano katika hatua hii.

πŸ‘€ Macho yote kwa Max Dowman! Je, kijana huyo mwenye miaka 16 ataweza kuonyesha uwezo wake kwenye jukwaa kubwa?

15/09/2026

Young Africans SC (Yanga) imeondoka na pointi zote tatu baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Geita Gold FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC.

⚽ Komara ndiye shujaa wa Wananchi, akifunga bao pekee la mchezo dakika ya 55, bao lililotosha kuipa Yanga ushindi muhimu.

Pamoja na kupata kadi nyekundu, Yanga haikuyumba. Kikosi hicho kilipambana hadi dakika ya mwisho na kufanikiwa kulinda bao lao na kuhakikisha pointi tatu zinatua Jangwani. πŸ’ͺπŸ”₯

πŸ“Œ MWISHO WA MCHEZO:
🟒 Yanga SC 1-0 Geita Gold
⚽ Komara β€” 55'

Pointi tatu zimepatikana! Wananchi wameendelea na safari ya kusaka mafanikio msimu huu. πŸ†πŸ’šπŸ’›

πŸ‘‡ Unaionaje Yanga ya msimu huu?

13/09/2026

Simba SC imeandika usiku mwingine wa kukumbukwa kwenye mashindano ya CAF Champions League, baada ya kuichapa vibaya Mighty Wanderers ya Malawi kwa mabao 6-1 katika mchezo wa marudiano!

Ushindi huo wa kishindo unaifanya Simba SC kusonga mbele kwa jumla ya mabao 7-1 (Aggregate) na kuendelea kusalia kwenye safari ya kuisaka nafasi ya kutwaa taji la Afrika! πŸŒπŸ†

⚽ MABAO YA SIMBA SC:
⏱️ 08' β€” Clatous Chama πŸ”₯
⏱️ 28' β€” Cheikhna Gueye πŸ’₯
⏱️ 34' β€” Clatous Chama πŸš€
⏱️ 70' β€” Cheikhna Gueye πŸ”₯
⏱️ 88' β€” Kaletso ⚑
⏱️ 90+3' β€” Morice πŸ’£

⚽ MABAO YA MIGHTY WANDERERS:
⏱️ 45' β€” Kaliati (Pen)

πŸ”₯ SIMBA SC 6-1 MIGHTY WANDERERS
πŸ† AGGREGATE: SIMBA SC 7-1 MIGHTY WANDERERS

Dakika 90 zimeisha, lakini Mnyama ameacha alama yake! 🦁πŸ”₯ Simba sasa inasonga mbele kwa kishindo baada ya kuonyesha uwezo mkubwa na kuifunga timu ya Malawi kwa jumla ya mabao saba katika michezo miwili.

🎯 SWALI LAKO:
Ni nani aliyestahili zaidi tuzo ya Mchezaji Bora wa Mechi (MOTM) leo? πŸ‘‘πŸ”₯

πŸ‘‡ Taja jina lake kwenye COMMENT!
❀️ LIKE | πŸ”„ SHARE | πŸ’¬ COMMENT

06/09/2026

Leo ni siku ya vita ya London! 😀πŸ”₯ Arsenal wanakuwa wenyeji wa Chelsea katika mchezo mkubwa wa Premier League, huku kila upande ukihitaji pointi tatu muhimu.

πŸ“… Leo
⏰ Saa 12:30 jioni (18:30 GMT)
🏟️ London
πŸ† Premier League

πŸ”΄ ARSENAL: Wapo kwenye kiwango cha juu, wakiwa wameshinda michezo 5 mfululizo. 🟒🟒🟒🟒🟒

πŸ”΅ CHELSEA: Wanaingia kwenye mchezo huu wakiwa na rekodi ya kuvutia pia β€” ushindi 4 na kipigo 1 katika michezo 5 iliyopita. πŸŸ’πŸŸ’πŸŸ’πŸŸ’πŸ”΄

Leo hakuna nafasi ya kujificha! πŸ”₯ Arsenal wanataka pointi zote tatu nyumbani, Chelsea nao wanataka kuondoka na ushindi kwenye uwanja wa wapinzani wao.

πŸ‘€ Je, Chelsea watawapiga barafu ya kuganda Arsenal?

πŸ‘‡ Dondosha utabiri wako wa matokeo kwenye COMMENT!

05/09/2026

GABORONE UNITED 1-1 YANGA SC 😱πŸ”₯

Wananchi wameonyesha roho ya kupambana hadi dakika ya mwisho! πŸ’ͺ🏾 Yanga SC wameibuka na sare muhimu ya 1-1 dhidi ya Gaborone United katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa CAF Champions League.

⚽ 32' | Amseb β€” Gaborone United wanatangulia na kuwatia presha Wananchi.

⏳ 90+6' | YANGA SC! πŸ’₯πŸ’₯
Dakika za lala salama! Yanga wanachomoa bao la kusawazisha katika sekunde za mwisho na kuondoka Botswana na sare muhimu! 😱πŸ”₯

πŸŽ™οΈ Kengele imegonga, lakini vita bado haijaisha!
Sasa mambo yote yanahamia Benjamin Mkapa Stadium πŸ‡ΉπŸ‡ΏπŸŸοΈ kwa mchezo wa marudiano.

πŸ”₯ Goli la dakika 90+6' limewasha moto! Benjamin Mkapa itakuwa habari nyingine!

Daima Mbele, Nyuma Mwiko! πŸ’šπŸ’›

05/09/2026

Gaborone United wanaenda mapumziko wakiwa mbele kwa bao 1-0 dhidi ya Yanga SC katika mchezo wa CAF Champions League.

Yanga wana kazi ya kufanya kipindi cha pili kusaka bao la kusawazisha.

05/09/2026

04/09/2026

Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Miguel Ángel Gamondi, ametangaza kikosi cha awali cha wachezaji 42 watakaoingia kambini kujiandaa na michezo ya kufuzu AFCON 2027. πŸ‡ΉπŸ‡ΏπŸ†

Taifa Stars inatarajiwa kukutana na Guinea-Bissau pamoja na Madagascar katika kampeni za kufuzu AFCON 2027, huku pia ikipanga kutumia mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Ghana k**a sehemu ya maandalizi.

Gamondi amechanganya wachezaji wenye uzoefu, damu changa na nyota wanaocheza nje ya Tanzania, akiwemo baadhi wanaokipiga Ulaya, Marekani na Afrika.

🧀 MAKIPA

β€’ Zuberi Foba β€” Azam FC
β€’ Aishi Manula β€” Azam FC
β€’ Yona Amos β€” Singida BS
β€’ Metacha Mnata β€” Singida BS
β€’ Hussein Masalanga β€” Young Africans

πŸ›‘οΈ MABEKI

β€’ Ibrahim Bacca β€” Young Africans
β€’ Bakari Mwamnyeto β€” Young Africans
β€’ Lameck Lawi β€” Azam FC
β€’ Twalib Nuru β€” Azam FC
β€’ Vedastus Masinde β€” Simba SC
β€’ Mohammed M***a β€” Young Africans
β€’ Danillo Maino β€” FK Panevezys, Lithuania
β€’ Haji Mnoga β€” Patro Eisden, Ubelgiji
β€’ Nickson Kibabage β€” Simba SC
β€’ Mohammed Hussein β€” Young Africans
β€’ Anthony Mligo β€” Simba SC
β€’ Pascal Msindo β€” Azam FC
β€’ Nathaniel Chilambo β€” Simba SC

βš™οΈ VIUNGO

β€’ Novatus Miroshi β€” GΓΆztepe, Uturuki
β€’ Himid Mao β€” Azam FC
β€’ Adolph Mtasingwa β€” Kaizer Chiefs, Afrika Kusini
β€’ Yusuf Kagoma β€” Simba SC
β€’ Mohamed Sagaf β€” Eastbourne Borough, Uingereza
β€’ Alphonce Mabula β€” JS Kabylie, Algeria
β€’ Charles Mmombwa β€” Zabbar, Malta
β€’ Mudathir Yahya β€” Young Africans
β€’ Feisal Salum β€” Azam FC
β€’ Sheikhan Khamis β€” Singida BS
β€’ Morice Abraham β€” Simba SC
β€’ Abdulkarim Kiswanya β€” Azam FC

πŸ”₯ WASHAMBULIAJI

β€’ Tarryn Allarakhia β€” Boreham Wood, Uingereza
β€’ Simon Msuva β€” Newroz, Iraq
β€’ Bernard Kamungo β€” FC Dallas, Marekani
β€’ Kelvin John β€” Aalborg, Denmark
β€’ Kibu Dennis β€” Al Nasr, Libya
β€’ Abdul Suleiman β€” Azam FC
β€’ Sabri Kondo β€” Hacken, Sweden
β€’ Cyprian Kachwele β€” HFX Wanderers, Canada
β€’ Said Khamis β€” Hana Timu
β€’ Selemani Mwalimu β€” Young Africans
β€’ Paul Peter β€” JKT Tanzania

🎯 LENGO LA GAMONDI

Kocha Gamondi anaonekana kuanza kujenga kikosi chenye ushindani, mchanganyiko wa uzoefu na vijana, huku lengo likiwa ni kuhakikisha Taifa Stars inafanya vizuri kwenye mbio za kufuzu AFCON 2027.

πŸ‘€ WEWE UNAONAJI KIKOSI HIKI?

Ni mchezaji gani unadhani ameachwa lakini alistahili kuitwa Taifa Stars? πŸ‡ΉπŸ‡ΏπŸ‘‡

πŸ’¬ Toa maoni yako kwenye COMMENT.

Want your business to be the top-listed Gym/sports Facility in Moshi?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Category

Website

Address

Moshi

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when GALOD TZ posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Subscribe

We will notify you when anything happens in Moshi.