Malenga Tazz
THOSE WHO ARE INTREST TO FIND A SONG WRITER CALL THIS NO 0799823984/0772164224:
EMAIL :[email protected]
For songwriter,poems, music teacher
wazima nyote humu
15/10/2025
SHAIRI:KWAHERI BABA
MTUNZI:MALENGA PANGA LA MOTO
-Zimetufika tanzia,machozi yatiririka
-Nguzo imetulemea,na ghafla kuanguka
-Wa Kenya twajililia,mtetezi akaondoka
-Kwaheri baba KWAHERI,taishi kukukumbuka,
-Hadi vyama vya mseto,ni mbali ulitutoa
-Umeuitika wito,alokuita JALIA,
-Kwa kweli hili ni zito,Wakenya lotuachia
-Kwaheri baba KWAHERI, Wakenya takukumbuka
-Umetuachia Giza,na simanzi so kifani
-Wanao mewatatiza,k**a kinda lo jangwani
-Wa Kenya umewaliza,mfuta chozi ni nani!?
-Kwaheri baba KWAHERI,utaishi mtimani
-Bila wewe kwa siasa,ni chai bila sukari
-Walia wanasiasa,kuipoteza ambari
-Baba awe nani Sasa?umemaliza safari
-Kwaheri baba KWAHERI,Kakuteua KAHARI
-Kweli CHEMA hakifumu,wahenga walishasema
-Hakuna wakulaumu,akiamuru KARIMA
-Siku Yako imetumu,ulale mahali pema,
-Kwaheri baba KWAHERI,akurehemu KARIMA
😭😭😭😭😭😭😭🙏🙏🙏🙏🌹🌹🌹🌹🌹🌹
All Round Entertainment & News
Citizen TV Kenya
KENYA POLITICS �
Hon. Ali Hassan Joho
ODM PARTY FORUM
PARTY COUNTY 001 SURPOTERS
KBC Channel 1 TV
K24 TV
NTV Kenya
25/09/2025
OLD MEMORIES REMINDS U ABT UA OLD FRIENDS .
CAN TELL ME UMEONA NINI KWA HYO PICHA 😜 ILA UFUMWENI KUNAPITA MENGI WALLAH 😜
23/09/2025
MSEMO WA LEO NA MALENGA PANGA
KUNGUNI MVIVU ,HUGANDAMA MFUMBATI
All Round Entertainment & News All Follower's friends
SHARI:NIKULIPE NINI?
MTUNZI:MALENGA PANGA LA MOTO
HAFSAH:Ewe mliwazi wangu,Nina jambo nikwambie,
HAFSAH:Uhimayani mwangu,kwani nikufichie!?
PANGA:Naam kipenzi changu,la moyo nifungulie.
P:Wewe kwangu ja zawadi,kukutunza ni wajib
P:Tusije ifanya ndoano,kwa kujaza ATI ATI,
H:Sijakuona mfano,we wakwangu tofauti.
P:Sinipambe kwa kangano,kaja nipiga kibuti
H:Huba lako so mfano,sijui nikulipeni!?
H: Nyongo lonithaminisha,Leo mke wa thamani.
P:Nyonda menifurahisha,ndimi Yako asmini
H:Likofishwa menivusha,najihisi nipeponi
P:Wewe kwangu ja zawadi, kukutunza ni wajib.
P: Mapenzi linikatili,kanipotosha Imani,
P:We kwako menikabili,kwa busara na hisani
H:Labda niseme kwa Siri,siniibie jirani
H:Wewe fundi so mfano,sijui nikulipeni!?
H:Umekuwa k**a tiba, hosipitali ya Nini!?
H:Nikiona nashiba,chakula Cha KAZI Gani!?
P:Kukuweka wa akiba !na wakwanza awe nani!?
P:Wewe kwangu ja zawadi, Kukutunza ni wajib.
P: Na wewe Najivunia,ubavu wangu wa kweli,
P: Heshima menitunzia ,lotangulia tapeli,
H:Bora ishirini so mia,ya simango na kejeli.
H:Wewe fundi so mfano,kwako komo mefikia.
H: Na ndoa nimeridhia, niwe wako wa milele,
H: Nyongo ushanikalia,zinawiri mbelewele
P: Ahsante maridhia,lobaki vigelegele,
P:Wewe kwangu ja zawadi, kukutunza ni wajib.
P:Wataarifu mandugu, rafiki na majirani,
P:Tumeuunga udugu,wasubiri mkekani,
H:Na mafisi Wala njugu, Panga yupo himayani
P:Menitunuku zawadi,H: YARABI nikulipeni!?
24/07/2025
Uzima wa nyavu matundu,UKIONA ikishonwa basi jua halikuwa tundu ni shimo hilo.laweza tongea waliomo na wasiomo kuenda kwa MUUMBA wakiwa na huzuni. Tafakari ya panga kabla jembe HALIJATIWA makali
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Contact the public figure
Website
Address
Moshi