SEPRO
Ni mpango wa kuelimisha vijana ili kuweza kujitambua katika kufanya mambo mbalimbali ya kijamii,kiuc
31/08/2024
*Mzazi unakumbuka utotoni mwako wakati anakwenda shuleni uliambiwa nini* ?
Mtoto anayesoma hutegemea vyanzo vitatu vya malezi. Ambavyo ni
👉mzazi
👉walimu na
👉jamii inayomzunguka.
Katika malezi hayo yote, malezi ya wazazi huwa na nguvu kubwa kwa mtoto ulikinganisha na vyanzo vingine vyote. Maisha ya wazazi yanachangia mtoto kukua katika njia iliyonjema au mbaya.
Watoto hupenda sana kuwaiga wazazi kwa sababu huwa wanaamini kuwa mzazi ndiyo Mwalimu sahihi. Kwa hiyo kwa njia yote ile mtoto hutafuta kuwafanana wazazi wake. Hapa ndipo methali isemayo, samaki mkunje angali mbichi, mtoto wa nyoka ni nyoka, mama ni Mama hata k**a ni rikwama nk. Hutufundisha.
Mzazi anatakiwa kumlea mtoto katika malezi ya kiutu, kielimu, na kiroho.
Tukianza na elimu, mzazi anawajibu wa kufanya kila linalowezekana ili kumsaidia mtoto aweze kufanikiwa katika ndoto ya elimu. Ufuatao ni ushauri wa kumsaidia mtoto ili afaulu mtihani:
👉Mzazi mwambie mwanao, furahia kusoma na penda kujisomea Kwa bidii
👉Lengo la kwanza la elimu ni kumkomboa mtu kifikira, ndiyo maana tunasikia elimu ni ukombozi.
Itashangaza pale ambapo mtu msomi anafanya vitu ambavyo kwa jamii ni chini ya kiwango; wizi, uasherati, madawa ya kulevya nk.
👉Wasomi ni wengi lakini ajira ni chache, hakikisha usomi wako haujitenganishi na shughuli za kila siku za jamii mfano kilimo, ufugaji, biashara, nk.
👉Ingia darasani na sikiliza kwa makini anachofundisha Mwalimu
👉 Hakikisha unaandika alichofundisha Mwalimu kwa mwandiko mzuri
👉Kuwa na ratiba ya kusoma nje ya ratiba ya shule inayotumiwa na walimu kufundishia
👉Baada ya masomo, jikumbushe mlichosoma kwa njia ya kukiandika katika mhitasari
👉baada ya kusoma penda kuwashirikisha wenzako ulichoelewa
👉Kuwa na vikundi vya kujisomea ( group discussion)
👉Jenga urafiki na walimu, usiogope kuuliza ambapo hujaelewa
👉Penda kwenda maktaba kujisomea vitabu
👉 Jiamini kuwa unaweza fanya vizuri, usikubali kukata tamaa
👉rudiarudia mlichosoma darasani
👉k**a mwanafunzi waza masomo
👉Usiwe chanzo cha makundi maovu au kujiunga na makundi maovu
👉 Epuka maisha ya kujitenga na wenzako
👉 Kumbuka kutunza afya, fanya mazoezi, kula, kunywa na maji nk.
👉Kuwa na mahusiano mema na wanafunzi wenzako
👉Usipende kuhairisha mambo k**a kutofanya mazoezi ya darasani na kazi wanazotoa walimu darasani
👉Heshimu na ishi karidi ya sheria na taratibu za shule
👉Tambua vipaji vyako na uvitumie
👉 Kumbuka kusali/ kumtanguliza Mungu katika masomo yako.
👉Acha kuchagua masomo kutokana na sababu zisizo za maana
Mengine k**a mzazi jisemee kadiri unavyomfahamu mtoto wako.
ujana waleo ni uzee wakosho.
..
16/08/2024
25/09/2022
*SIRI ZA KUFANIKIWA*
*1. Jiamini*
✍🏻Mafanikio ya kweli yanaanza na wewe. Hivyo, kujiamini ni msingi mzuri utakaokufanya utambue uwezo wako katika kufanya jambo fulani.
✍🏻Amini uwezo wa kufanya jambo hilo uko mikononi mwako.
✍🏻 Usijishushe, jipime kwa mengi mazuri unayoweza kufanya, ikatae roho ya kujiona huwezi.
*2. Thubutu*
✍🏻Neno hili pia ni msingi wa pili mkuu wa mafanikio. Uoga wa kuthubutu ni kikwazo kikuu kinachowarudisha wengi nyuma na kujikuta hata kuanza safari ya mafanikio hawawezi.
✍🏻 Jambo lolote zuri na kubwa huwa gumu kufanya na ni rahisi kuhisi haliwezekani. Usikubali kushindwa bila kujaribu.
✍🏻Thubutu kwa dhati na weka nguvu yako na akili yako yote katika uthubutu huo. Hata hivyo, katika uthubutu huu, unapaswa kupima vizuri ili uchukue *‘calculated risk’* na sio kuthubutu pasipo kujua risk yake ikoje. Not just a Risk.
*3. Panga na tekeleza kwa vitendo*
✍🏻Kumbuka, ukishindwa kupanga ujue umepanga kushindwa *If you fail to plan, you plan to fail.* Kuwa na mipango inayopimika na kutekelezeka kwa kiwango cha juu.
✍🏻Usiwe na mipango tu mikubwa ambayo hata utekelezaji wake hauwezekani *Not just a plan*.
✍🏻 Unapopanga fikiria wapi utapata rasilimali na jinsi ya kutelezeka, lakini pia mpango wako ukupe uwezo wa kuutathmini na kujipima mwisho wa kazi hiyo.
✍🏻 Hata hivyo, mipango haitakuwa na maana k**a hautaitekeleza kwa ufanisi.
✍🏻Ukishindwa kutekeleza mpango wako, rudi angalia ulipoteleza ili urekebishe na sio kuufuta mpango mzima bila sababu ya msingi
08/09/2022
*Wazee wanasema, "kipindi cha mafuriko, mwenye hekima hujenga daraja lakini mpumbavu huchimba bwawa." Ingawa madaraja na mabwawa ni vitu vya muhimu, daraja ndilo linalopaswa lijengwe kwa haraka panapotokea mafuriko. Lazima tuanze kwanza na daraja kwa ajili ya kuokoa watu kwanza. Wengi wanafikiri ni sifa njema pale unapofanya au kuvumbua jambo tofauti na wenzako. Na baadhi wanakazana wafanye kitu chao cha pekee. Wengine wanaona furaha kutenda kinyume na wengine-wakijidai kwamba wana misimamo yao tofauti. Ati hawataki mambo yao yafanane na ya wenzao. Kufanya hivi wakati mwingine ni ishara ya kiburi, majivuno na ukatili. Kutenda jambo linalokaribiana kufanana na mwenzako sio vibaya. Majivuno ya kutaka uonekane wa tofauti yatakugeuza uwe mtu wa kubomoa madaraja na kuchimba mabwawa kipindi cha mafuriko. Acha kujiona kuwa binadamu wa pekee sana, wewe ni mwanadamu kati ya wanadamu.
05/09/2022
*Wazee wanasema "Usimtese mtu ili umfurahishe rafiki yako unayempenda." Rafiki yako akija kwako akikuambia anamchukia mtu fulani, na ikiwa unayeambiwa una mamlaka na yule anayechukiwa, usiende kumtesa anayechukiwa ili rafiki yako afurahi. Wasaidie wapatane. Usisahau machozi ya anayeteswa hugeuka mafuriko yakukusomba baadae. Kuwa makini na kujaribu kuwazika watu kwenye matope, wengine wanachipua k**a mbegu iliyopandwa kwenye matope. Usisahau wanyonge hutetewa na Mungu. Goliati alikuwa na nguvu lakini hakuwa na Mungu, Daudi hakuwa na nguvu ila Mungu alikuwa nguvu yake. Epuka kupigana na malaika waliowekwa na Mungu kati ya watu.
11/08/2022
Zifanye ziwe Kanuni za Maisha Yako katika Mafanikio.
Watu wengi tumekua na ndoto za baadae juu ya maisha yetu lakini tunajilaumu nahatujuwi nini chakufanya juu yamaisha yetu.Ili uweze kufanikiwa unahitaji utengeneze kanuni ambazo zitakuongoza kutekeleza jambo lako.Hivyo kila mmoja ana kanuni zake za maisha ambazo humuongoza katika kufanya mambo yake mbali mbali.Kanuni hutegemeana na lengo lako linataka mafanikio yapi na katika kiwango kipi.
Fikiri nini kipaumbele chako.(Think about what you want)
Kila mmoja anakipaumbele cha jambo analotamani kulifanya.Yawezekana yapo mambo mengi lakini lipo jambo moja huwa unalipa kipaumbele sana na unatamani kulifanya ili liweze kukuletea manufaa katika maisha yako.Katika hatua hii ya awali unachotakiwa ni kubadilisha fikra zako kwa kuzingatia kupata furaha na usalama kwa jambo unalotaka kulifanya ambalo ni kipaumbele chako.K**a mafanikio yako yanalenga kuwa na furaha basi fikra zako ni vyema kutambua kipaumbele gani kitakachokupa furaha.Fikra zako ni zamsingi mno hupaswi kuzipuuza.Katika kanuni ya kufikiri kipaumbele chako itakusaidia kujua nini ufanye na kujua hatima ya msimamo wa jambo utakalofanya juu ya lengo lako ulilokusudia.
Fikiria kuhusu wakati ujao.(imagine your future)
Hapa ni lazima ujijengee kanuni ya kujiuliza maswali k**a vile ;
▶Muda gani wa kuamka asubuhi?
▶unahitaji nini katika maisha yako?
▶Unataka uishi mjini au vijijini?
▶Unataka umilika biashara gani?
▶Unataka uwe nafamilia ipi?
▶Unataka vyanzo vipi vya pesa?
Kanuni ya kujiuliza maswali k**a haya itakusaidia kufikiria wakati ujao wa maisha yako ambao utakusaidia kujindalia malengo na mipango ya kutimiza mikakati yako lakini pia majibu ya maswali haya yatakupa mwanga wa kutengeneza ndoto moja ambayo itajengwaa na lengo kuu ulilonalo.
Kumbuka kutoa upatapo mafanikio.
03/08/2022
WEKA NAFASI NDANI YAMOYO WAKO
Chuki unayoijenga ndani yamoyo wako juu yamtu hakikisha unaipa nafasi kwani ipo siku utahitaji uwepo wa unayemchukia hapo ndipo utajenga mapigano yanafsi.Binadamu tumeumbiwa kukosea,kusamehe nakusahau ukitambua hivi upendo utaupa nafasi,chuki utazipa nafasi na hasira pia utazipa nafasi kwakutambua uthamani wamtu hauna ukomo ukiukosa leo si kwamba hautauhitaji milele.
12/06/2022
HITAJI LA MAFANIKIO
Nini hitaji la mafanikio yako?
Kila mmoja anahitaji la mafanikio yake ya kimaisha lakini kuna hitaji kuu ambalo ni lamsingi katika maisha yetu pale tulikosapo tu basi huwa ndiyo mwisho wa maisha yetu.Wapo wataalamu mbali mbali walioweza kuchunguza na kuchambua maisha ya mwanadamu tangu hatua ya kutunga mimba hadi hatua ya kifo.Mfano wa wachunguzi hao juu ya maisha ya wanadamu ni Abraham Maslow,
Mwana saikolojia Abraham Maslow ameweza kuainisha baadhi ya mahitaji muhimu ambayo ni yamsingi kwa mwanadamu kuyapata.Kuna ngazi kuu tano za mahitaji ya mwanadamuna ngazi hizo zilifanyiwa utafiti na Abraham Maslow mwaka 1907 mpaka mwaka 1970 na kuzipa jina la Maslow Hierarchy of needs, yaani ngazi za mahitaji ya mwanadamu. Lengo kuu ilikuwa ni kutaka kujua ni nini kinachofanya mtu afanye jambo au kitu fulani.Ngazi hizo tano ni :
1. Mahitaji muhimu (Biological and physiological needs) mfano chakula, Malazi, afya na hewa.
2. Hitaji la kiusalama (Safety needs) mfano ulinzi.
3. Hitaji la kijamii (Social needs) mfano upendo nakupendwa.
4. Hitaji la heshima (esteem needs)
5. Hitaji kujitosheleza na kujitambua (Self actualization needs).
Hitaji la mafanikio yetu kwa ujumla ni kwaajili ya kutimiza hitaji kuu la mwili ili uwe imara katika kutekeleza shughuli ya nyingine za uzalishaji mali.Tunatakiwa kuutimizia mwili mahitaji hayo matatu ndipo tuweze kuzalisha ziada kwaa ajili ya kusaidia wengine ambao hawajuwi wapi pakuanzia na wale ambao wanamahitaji maalumu ambayo ni yakuzaliwa nayo yanayowafanya wasiweze kuzalisha chochote.Baada ya kutimiza hitaji la mwili ndipo mahitaji mengine huchukua nafasi ya maisha ya mtu hadi kufikia hatua ya kuwa na familia au kuwa na uwezo wa kumiliki watu kwa ajili ya kutafuta upendo, hadhi na usalama.
08/06/2022
UTAJENGAJE HISTORIA YAKO ?
Watu wengi tumekua tukijisahau kutafakari jambo la kifo pale mmoja kati yetu anapotoweka katika ulimwengu wa duniani.Muda husogea na ndivyo siku za kuwepo duniani hupungua siku hadi siku.Kipi tunajifunza na kipi tunatarajia kuacha baada ya kifo ili kije kua ni cha kihistoria kwako na kwa vizazi vijavyo?
Mara nyingi tumekua ni watu wa kutazama, kusikia na kusoma historia za wengine bila kutafakari historia zetu tunaziachaje? Tunawakumbuka watu k**a vile Hayati Mwl.Jk nyerere, Nelson Mandera,
Lucky Dube na wengine kutokana na;
○Hekima, busara na utu wao wa kujali wengine,uzalendo wa nchi na jamii inayowazunguka.
○Pia kutoa shauri na kukemea maovu.
○Utu wa kujali matatizo ya wengine k**a sehemu ya matatizo yao.
SWALI JE,
Mimi na wewe tunajengaje historia yetu kabla ya kutoweka katika huu ulimwengu ili ije kua kumbukumbu kwa vizazi vya nyuma yetu? Nafasi bado unayo tuanze sasa kujenga historia zetu za baadae kwakuzingatia kusudi la mola wetu kwa kutuumba kwake.
K**a unataka kujenga historia ya maisha yako na kujiweka katika nafasi ya watu wenye thamani ulimwenguni huna budi kutambua kwanza nafasi ya historia yako itajengwa na jambo gani la kipekee.Wapo wagunduzi wa kanuni, vitu na vifaa mbali mbali vya kiteknolojia ambavyo hurahisisha kazi hao wote historia zao zilijikita katika ubunifu wa kiutendaji.
Wapo ambao historia zao waliziweka katika mageuzi ya kisiasa na kuwa viongozi mbali mbali wa nchi ulimwenguni na wapigania haki mashuhuri duniani kote.
UNAJENGAJE HISTORIA YAKO?
05/06/2022
Suala la ndoa na talaka limekuwa likijadiliwa mara kwa mara, na jambo hili linaleta utata mkubwa maana pindi wanadoa wanapotengana, mgogoro mkubwa kuhusu kugawana mali hutokea. Lakini je, ni mali pekee ambayo inapaswa mwanamke kufidiwa? Vipi kuhusu muda wake alioutumia katika kutunza familia?
Katika kipindi cha Ukumbi wa Wanawake siku ya leo tutaangalia suala hili la talaka na haki za mwanamke pindi anapoachana na mume wake.
sikiliza
Haki za Wanawake wanapotengana na wenzi wao Suala la ndoa na talaka limekuwa likijadiliwa mara kwa mara, na jambo hili linaleta utata mkubwa maana pindi wanadoa wanapotengana, mgogoro mkubwa kuhusu kugawana mali hutokea. Lakini je, ni mali pekee ambayo inapaswa mwanamke kufidiwa? Vipi kuhusu muda wake alioutumia katika kutunza familia?
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Telephone
Website
Address
Morogoro