HASCAVELA

HASCAVELA

Share

SAYANSI NA TEKNOLOJIA NI MISINGI YA TAIFA BORA. KAULI MBIU
“SAYANSI NA TEKNOLOJIA MISINGI YA TAIFA BORA."

DIRA (VISION)
Kuwa kampuni namba moja Tanzania inayochochea na kutumia vyema maendeleo ya SAYANSI na TEKNOLOJIA ili kupambana na UJINGA, UMASIKINI na MALADHI. DHIMA (MISSION)
Kuhakikisha tunatumia vyema maendeleo ya SAYANSI na TEKNOLOJIA katika mfumo chanya na wenye tija kwa jamii na nchi kwa ujumla.

08/08/2026

Ukwaju una faida zifuatazo kwa jamzito:

Ukwaju unapunguza kichefuchefu na kutapika:
Moja ya sababu kwanini wajawazito wanakula sana ukwaju ni kwasababu unasaidia kupunguza hali ya kichefuchefu na kutapika wakati wa mimba changa.

Ukila ukwaju kwa kuchanganya na chumvi kidogo itakusaidia kujihisi vizuri.

Husaidia kushusha shinikizo la damu:
Kwa wanawake ambao kenye familia zao kuna watu ambao wanasumbuliwa na presha wana uwezekano wa presha zao kupanda wakati wa ujauzito.

Ukwaju unasaidia kukukinga presha yako isipande kipindi cha ujauzito kwasababu ya madini ya potassium kwenye ukwaju.

Husaidia kutibu matatizo mbalimbali ya tumbo:
Moja ya matatizo ya tumbo yanayowasumbua wajawazito ni kupata choo kigumu.

Ukwaju una wingi wa nyuzi lishe ambazo ni muhimu kwa kutibu tatizo la kupata choo kigumu kwa wajawazito.

Husaidia kumkinga mjamzito asijifungue kabla ya muda:
Kwa mujibu wa taasisi ya ujauzito ya marekani ulaji wa madini chuma kwa wingi inasaidia kumkinga mjamzito asijifungue mapema kabla ya muda.

Ukwaju una wingi wa madini chuma hivyo inamsaidia mjamzito kuongeza madini chuma mwilini.

Husaidia ukuaji wa mtoto tumboni:
Ukwaju ni chanzo kizuri cha vitamin B3 na B4, vitamin hizo husaidia ukuaji wa mtoto tumboni hasa kwa kuimarisha mfumo wa fahamu wa mtoto.

Pia ukwaju una wingi wa madini ya calcium, zinc na magnesium pamoja na protini ambayo husaidia kuimarisha mifupa ya mtoto, na kusaidia kuimarisha kinga ya mwili na kudhibiti shinikizo la damu.

Ukwaju husaidia kuondoa maumivu ya misuli na kuvimba miguu hasa miezi ya mwisho ya ujauzito.

Je kula ukwaju ukiwa mjamzito ni salama?
Ndiyo ni salama kwa mjamzito kula ukwaju akiwa na mimba ila kula kwa kaisi.

08/08/2026

Hizi hapa Faida za Kula Ukwaju kwa Mama Mjamzito.

04/08/2026

Ni hali ya kawaida kwa mwanamke kutoka majimaji ukeni kwasababu mbalimbali za kiafya kwa wanawake.

Majimaji hayo yanasaidia kuweka uke safi na kumkinga mwanamke dhidi ya maambukizi ya magonjwa mbalimbali ukeni.

Majimaji hayo hutofautiana kwa rangi, muonekano wake na kiwango kinachotoka ukeni na inategemeana na umri wa mwanake na wakati wa hedhi.

Unapoona mabadiliko yoyote kwenye majimaji hayo yanayotoka ukeni inaweza kuwa ni ishara ya ugongwa.

Mabadiliko hayo yanaweza kuwa rangi au harufu ya majimaji hayo yanayotoka ukeni.

Ni muhimu kufahamu utofauti huo uliopo kwenye majimaji ya ukeni k**a ni kawaida au si hali ya kawaida.

Katika makala hii tufahamu kuhusu utofauti uliopo kwenye majimaji ya ukeni ili kujua k**a ni hali ya kawaida au si hali ya kawaida.

Uteute mweupe mzito:
Uteute mweupe mzito na unaonata ila usiotoa harufu kali ni hali ya kawaida kwa mwanamke hasa mwanzoni au mwishoni mwa hedhi.

Uteute msafi na mwepesi k**a maji:
Kwa mwanamke anapokuwa katikati ya mzunguko wake wa hedhi hasa muda ambao yai hushuka kwaajili ya kutunga mimba ni kawaida kuona ukeni unatoka uteute msafi na mwepesi k**a maji.

Uteute msafi na unaonata:
Endapo ukeni utatoka uteute mzito, msafi na unaonata ambao si mwepesi k**a maji ni ishara ya kuwa upo kwenye siku za hatari endapo utashiriki tendo la ndoa una uwezekano mkubwa wa kupata mimba.

Uteute wa rangi ya kahawia au nyekundu:
Uteute wa aina hii huonekana kipindi cha hedhi au mara baada ya kumaliza hedhi, pia kuna muda ambao mwanamke anaweza kuiona katikati ya mzunguko wake wa hedhi.

Ni kwasababu inaweza kutokea vidone vya damu kutoka katikati ya mzunguko wa hedhi hasa siku za hatari kwa mwanake.

Muda mwingine hali hiyo huwa ni ishara ya mimba changa k**a umetoka kushiriki tendo la ndoa siku zako za hatari.

Uteute wa njano au wa kijani:
Uteute wa njano iliyokoza au kijani inaweza kuwa ni ishara ya magonjwa kwenye viungo vya uzazi kwa mwanake hasahasa ukiwa ni uteute mzito na unaotoa harufu mbaya.

Ukiona hali hiyo ni vizuri kumuona daktari kwa uchunguzi zaidi.

Muda mwingine unjano kwenye uteute inaweza kuwa kawaida kwasababu ukikaa kwenye hewa muda mrefu unabadilika rangi.

04/08/2026

Kutokwa na Uchafu/Harufu sehemu za Siri kwa Mwanamke, Ni Ishara ya nini?

04/08/2026

Karibu Asilimia 90 ya wajawazito katika wiki 12 za mwanzo hupata hali ya kuhisi kichefuchefu na kutapika mara kwa mara.

Baada ya wiki 12 wengi hali hii hupotea kabisa na kuna wengine hali hii huendelea kipindi chote cha ujauzito.

Baadhi ya tafiti zimeonesha hali hiyo kwa wajawazito inasababishwa na mabadiliko ya homoni mwilini, mabadiliko ya shinikizo la damu na mabadiliko kwenye umeng’enywaji wa vyakula vya wanga tumboni.

Hali hii huwa kero kwa wajawazito wengi inapokuwa ni hali endelevu na ya mara kwa mara.

Hali hiyo ni ya kawaida kwa mjamzito.

Ila inapotokea mjamzito kutapika sana kiasi cha kusababisha kupungua uzito au kupungukiwa na maji mwilini ni hatari na ni muhimu kwenda hospital kwa msaada zaidi.

Pia unapoona dalili hizi zikiambatana na kutapika ni muhimu kumuona daktari.

👉 K**a unapitiliza masaa zaidi ya nane hujakojoa au unakojoa mkojo uliokelea sana rangi.
👉 Unajihisi zaifu, unahisi kizunguzungu, au k**a unajihisi kuzimia ukiwa unataka kusimama.
👉 Unapata maumivu ya tumbo.
👉 Joto la mwili linapanda.
👉 Au k**a unatapika damu.

Na haya ni baadhi ya mambo mjamzito anashauriwa kuyafanya kumsaidia kupunguza hali ya kuhisi kichefuchefu na kutapika katika hali ya kawaida.

👉 Jitahidi kupata mapumziko ya kutosha kwasababu kuchoka sana kunachochea hali ya kuhisi kichefuchefu.
👉 Jitahidi kuchunguza vyakula au harufu vinavyokuchefua na uviepuke.
👉 Asubuhi unapoamka kula vitu vikavu k**a vile biskuti.
👉 Kula kidogo kidogo na mara kwa mara vyakula vyenye wanga kwa wingi kuliko mafuta.
👉 K**a harufu ya chakula cha moto inakuchefua ni vyema usubiri kipoe ndiyo ule.
Jitahidi kunywa maji, kunywa maji kidogo kidogo na mara kwa mara inasaidia kuzuia kutapika.

Na tafiti mbalimbali zimeonesha kuwa kula chakula au kunywa vinywaji vilivyochanganywa na tangawizi inasaidia kupunguza kichefuchefu na kutapika kwa mjamzito.

Na k**a utatumia tangawizi hakikisha matumizi yako hayazidi robo ya kijiko cha chai kwa siku kwa tangawizi iliyosagwa.

04/08/2026

Tiba ya Mama Mjamzito kuzuia hali ya Kichefuchefu na Kutapika wakati wa Ujauzito.

01/08/2026

Shinikizo la Juu la Damu (Presha ya Kupanda) Mambo hatarishi na Jinsi ya kujilinda

08/07/2026

Wanawake wengi wanaweza kupitia changamoto ya kupata maumivu wakati wa tendo la ndoa katika kipindi flani kwenye maisha yao.

Wanaweza kupata maumivu kabla ya tendo la ndoa, wakati wa tendo la ndoa au baada ya tendo la ndoa.

Tuzifahamu sababu mbalimbali ambazo zinaweza kusababisha maumivu wakati wa kufanya tendo la ndoa kwa wanawake.

Kutokuwa na uteute wa kutosha ukeni:
Moja ya sababu ni kutokuwa na uteute wa kutosha ukeni, hali hii inaweza kusababishwa na kushuka kwa kiwango cha homoni ya Estrogen kwa mwanamke.

Kushuka kwa homoni ya Estrogn kunaweza kusababishwa na mwanamke kufikia ukomo wa hedhi, k**a ametoka kujifungua au akiwa ananyonyesha.

Pia kuna baadhi ya madawa mwanamke akiyatumia yanaweza kusababisha kupungua kwa uteute ukeni.

Majeraha ukeni.
Sababu nyingine ni majeraha ukeni ambayo yanaweza kuwa yametokana na ajali au alifanyiwa upasuaji kwenye viungo vya uzazi.

Pia k**a mwanamke alishawahi kufanyiwa ukeketaji au alichanwa ili kuongeza njia wakati wa kujifungua.

Yote yanaweza kusababisha maumivu wakati wa tendo la ndoa kwa mwanamke.

Magonjwa ukeni au magonjwa ya ngozi.
Magonjwa ukeni au magonjwa kwenye njia ya mkojo pia yanaweza kusababisha maumivu wakati wa kufanya tendo la ndoa kwa wanawake.

Pia kuna sababu za kisaikolojia ambazo zinaweza kusabaisha maumivu wakati wa kufanya tendo la ndoa kwa mwanamke.

Sababu hizo ni k**a vile msongo wa mawazo, wasiwasi, uwoga na matatizo ya kimahusiano yanaweza kusababisha mwanamke kutokuwa na msisimuko wakati tendo na kumsababishia maumivu

Pia baadhi ya wanawake ambao wameshawahi kufanyiwa unyanyasaji wa kingono wanaweza kuhisi maumivu wakati wa tendo la ndoa.

Mara nyingi maumivu haya huwa ni ya muda mchache.
K**a utaona maumivu wakati wa tendo yanaendelea kwa muda mrefu ni vizuri kumuona daktari kwa uchunguzi zaidi.

08/07/2026

Yafahamu Mambo haya Kuhusu Maumivu Wakati wa Tendo la Ndoa.

Want your business to be the top-listed Media Company in Mbeya?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Category

Address


Mbalizi
Mbeya