ROCK FM RADIO
ROCK FM RADIO
29/06/2026
KIJA MPUNZI AFUNGA PINGU ZA MAISHA
Mtangazaji Mahiri wa Hope Channel Tanzania,Awr Tanznia na Rock Fm radio Ndugu Kija Mpunzi amefunga pingu za maisha na Vumilia Kasili..
Tukio hili takatifu limefanyika tarehe 28/07/2026 Jijini Arusha.
Mch.Dr .David Mpwani mwenyekiti wa Kanisa la Waadventista wa sabato Union ya kaskazini mwa Tanzania alitangaza rasmi kuwa Kija Mpunzi na Vumilia ni Mke na mume.Tukio hili linafunga na kufungua ukurasa mpya kwa vijana hawa ambao Mungu amewapatia kibali cha kumtumikia ndani ya kanisa la Waadventista wa Sabato.
Sisi watumishi wa Hope Channel Tanzania Awr Tanzania na Rock Fm tunaungana kwa pamoja na Maelfu ya wana jamii wanaokupongeza na Kukuombea heri, amani na upendo kwenye ndoa yenu.
MAFUNDISHO YA NJOMBE NET EVENT KUPAMBANUA IMANI YA KWELI NA KANISA LA KWELI- MH.ANTHONY MTAKA.
Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Anthony Mtaka amesema Mafundisho ya Njombe Net Event yatapambanua ukweli na kanisa la kweli. Mheshimiwa mtaka ameyasema hayo leo May 09/05/2026 alipotembelea kituo kikuu cha mahubiri ya Njombe Net Event - Tumaini lenye Baraka unaondelea katika Kanisa la Waadventista wa Sabato Njombe Mjini. Amesema kuna Mahubiri kwenye baadhi ya vyombo vya habari na mitandao ya kijamii yanayoendana na ramli chonganishi mahubiri hayo hayafai na siyo muhimu katika maisha ya Mwanadamu mcha Mungu.
Sambamba na hilo, Mheshimiwa mtaka amewapongeza wahudumu kwa masomo mbalimbali ya afya na familia yanayotolewa katika mkutano huo na kurushwa kote duniani, akieleza kuwa yana faida kwa jamii na maisha ya watu wengi.
Aidha ameahidi kuchangia sehemu ya mkutano huo kwa kugharimia usafiri,malazi na chakula kwaya ya Kurasini,Galilaya Central na Magomeni ili kuongeza nguvu siku ya kuhitimisha
mkutano huo.
Mkutano huo ambao Mhubiri mkuu ni Mch.Baraja Butoke,Mnenaji wa masomo ya familia ni Mch. Thomas Bihene na Masomo ya afya ni Dakitari Magomere ulianza mnamo tarehe 09/05/2026 na unaendelea hadi tarehe 30/05/2026 ukirushwa mbashari kila siku saa 11:00 jioni hadi saa 02:00 usiku kwenye vyombo mbalimbali vya habari: Hope Channel Tanzania,Awr Tanzania,Rock fm na mitandao mbalimbali ya kijamii.
Na Abel Kinyongo
14/03/2026
🌍 Injili ya Milele Iwahi kwa Ulimwengu Wote
Leo tunaungana na Waadventista duniani kote katika Sabato Maalumu ya Adventist World Radio (AWR).
Kupitia redio na vyombo vya mawasiliano, injili inaendelea kufika mahali ambapo wahubiri hawawezi kufika — vijijini, milimani, jangwani, na hata katika maeneo ambayo kuhubiri hadharani ni vigumu.
✨ Watu wengi wamepata tumaini
✨ Vijiji vimebadilika
✨ Maelfu wamekubali Kristo
Na yote haya yanawezekana kwa sababu watu wa Mungu wameamua kushiriki katika utume huu.
🙏 Sadaka yako leo inaweza kusaidia mtu kusikia injili kwa mara ya kwanza.
Hebu tushiriki pamoja kupeleka tumaini kwa ulimwengu.
📻 AWR – Sauti ya Matumaini kwa Ulimwengu
07/03/2026
TANZIA
Mwenyekiti wa kanisa la Waadventista wa Sabato Nyanda za juu kusini mwa Tanzania Mch.Toto Ndege Bwire kusaga.Anatangaza kifo cha Mch.Joseph T Msambwa wa Mtaa wa Malangali Wilaya ya Rungwe mkoa wa Mbeya, kilichotokea tarehe 06/03/2026 mkoani Mbeya.
Mwenyekiti anaungana na familia,waumini na wote walioguswa na msiba huo.Mazishi yatafanyika siku ya Jumatatu tarehe 09/03/2026 Mkoani Njombe.
"Naye atafuta kila chozi katika macho yao"
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Website
Address
Mbeya