Amos Msuli
mwandishi wa habari, na mtangazaji
JUHUDI za serikali za katazo la uuzaji wa pombe za viroba nchini huenda likakwama kutokana na baadhi ya wamiliki wa baa na grocer wilayani Rungwe mkoani Mbeya kuendelea kuuza pombe hizo kwa kificho huku wakivibatiza jina la ‘Dawa au Samaki mchanga.
Serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania,imepiga marufuku uuzaji na usambazaji wa pombe hizo,kwenye karatasi za naironi ikihitaji pombe hizo ziuzwe kwenye chupa,hali ambayo imeleta Taharuki kwa wafanyabiashara huku wengine wakijipiga risasi hadi kufa.
Siku ya tarehe 1/3/2017 gazeti hili lilishuhudia fuso moja likiwa na shehena za viroba likitua wilayani humo,lengo likiwa ni kuviuza maeneo ya grocer zilizopo vijijini na kwenye maeneo ya mipakani.
Baada ya katazo hilo,gazeti hili lilifanya uchunguzi kwa siku kadhaa katika wilaya mbili ambapo kwa wilaya ya Kyela wamekuwa wakiuza kwa kificho na kubatiza jina la ‘’Chapati’’kwa viroba vya Malawi na vya Tanzania wakiviita ‘’Kichwa’’ambavyo wamekuwa wakiuza kwa kificho kwa wateja wanao wafahamu.
Kwa Upande wa wilaya ya Rungwe gazeti hili lilipita katika baa nne na groser sita na kushuhudia pombe hizo zikiuzwa kwa majina ya ‘’Ng’ombe’’ kwa viroba vya Malawi na’’Dawa’’ au ‘Dagaa mchanga’’kwa viroba vya Tanzania.
Akizungumzia hali hiyo,mwenyekiti wa wamiliki wa nyumba za kulala wageni yaani hotel.gest na baa wilayani Rungwe,Christopher Mwakanyamale,alisema huenda uuzaji huo unafanyika kweli kutokana na serikali kutoa muda mfupi na kuwa ipo haja ya kuongeza siku 30 mbela ili waviondoe.
Alisema zoezi ni zuri lakini serikali ilitoa muda mfupi huku ikijua wajasilia mali wengi wakiwemo wanawake wamekopa fedha kwenye taasisi mbalimbali ambazo wanarejesha kila baada ya siku saba na biashara waliyokuwa wakiitegeme ni viroba na ndiyo maana wanauza kwa kificho.
‘’Ndugu mwandishi,wafanyabiashara wengi walinunua mzigo mkubwa wa viroba na kulipia mapato yote ya serikali ikiwemo,TRA na bidhaa yenyewe inanembo ya TBS,ilitakiwa serikali isitishe kwenye viwanda na kutoa muda kwa walionavyo ili waviuze na kuanza kununua vya kwenye chupa.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya wafanyabiashara wilayani humo,Lumage Mwivaha,alisema kitendo cha serikali kuviondoa viroba hivyo ni jambo la kupongezwa licha ya kuwa walitoa muda mfupi uliopelekea hasara kubwa kwa wafanyabiashara.
Alisema vijana wengi kutokana na bei kuwa ndogo ya viroba walikuwa wakinywa hovyo huku afya zao zikidhorota na kuwa kitendo cha kubadirisha jina la viroba hivyo halina tija na kuwa suala la kupambana na wauzaji hao wanaiachia serikali
Mbeya
Ucheleweshaji wa tafsiri ya Tangazo la Serikali namba 28 - GN28, kuhusu mipaka baina ya Hifadhi za taifa -TANAPA na Vijiji 21 katika Halmashauri ya wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya, umedaiwa kuchelewesha mipango na maendeleo ya wananchi wa vijiji hivyo.
Baadhi ya wananchi wa wilaya ya Mbarali vikiwemo Vijiji vya Kata ya Msangaji, wamemweleza Mkuu wa mkoa wa Mbeya AMOS MAKALA kuwa maendeleo yao katika maeneo yao yamesimama wakisubiri serikali kutoa tafsiri ya haraka ili wajue mipaka ya maeneo yao wanayoishi.
Kwa taarifa zaidi na Hosea Cheyo
Ni miaka kumi sasa tangu serikali imewaahidi wananchi wa Vijiji 21 vya wilaya ya Mbarali ambao wamepisha na kusimamishwa kufanya shughuli yoyote katika maeneo yao, mpaka pale serikali itakapo toa tafsiri ya GN28 juu ya mipaka ya hifadhi na vijiji.
LWITIKO MWAKATOBE-MKAZI WA MBARALI MBEYA
MARCUS KALINGA-MKAZI WA MBARALI MBEYA
Pia Viongozi waandamizi wa wilaya ya Mbarali nao wanasema kucheleweshwa kwa utekelezaji wa tangazo la serikali namba 28, juu ya hatima ya mgogoro wa wananchi na Hifadhi za taifa,unasababisha serikali kuchukiwa kwa kiasi kikubwa.
FRANCIS MTEGA-M/KITI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MBARALI
ABDALLAH MSANGI-MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MBARALI
Akizungumza na wawakilishi wa wananchi wakati wa kikao maalum cha baraza la madiwani wa wilaya ya Mbarali, Mkuu wa mkoa wa Mbeya AMOS MAKALA, amesema hatua ya kuwalipa fidia wananchi imeanza kinachofuata ni kutoa tafsiri.
AMOS MAKALA-MKUU WA MKOA WA MBEYA
EZEKIEL KILEMILE-KATIBU TAWALA WA WILAYA YA MBARALI
SONGWE;
Wakazi wa Chitete Wilayani Momba Mkoa mpya wa Songwe wametakiwa kuwa na ushirikiano na viongozi wao ili waweze kutatua changamoto wanazokutana nazo kwa wakati.
Hayo yamesemwa na Kamanda wa umoja wa vijana wa CCM (UVCCM) Twist Masoud wilayani humo, katika ziara iliyofanyika katika kijiji hicho baada ya kuona kwamba lawama nyingi zinaelekezwa kwa viongozi wa kijiji hicho.
Aidha,Masoud amesema kuwa,Ziara hiyo imefanyika ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa irani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kwa lengo la kusikiliza kero ambazo zinawakabili wanakijiji wa kijiji hicho ikiwa ni pamoja na kutoa Elimu kwa wasiojua kusoma na kuandika namna ya kushiriki katika chaguzi bila kurubuniwa.
Hata hivyo, amewataka Wananchi kubadilisha viongozi ambao wameona wanalega lega kuwaletea maendeleo ili kuwapanafasi wengine wenye uwezo wa kutatua kero zao kwa wakati bila kuangalia itikadi za chama.
Click here to claim your Sponsored Listing.
Telephone
Website
Address
Mbeya
95