BOMBA FM RADIO 104.1 Mhz MBEYA

BOMBA FM RADIO 104.1 Mhz MBEYA

Share

BOMBA FM RADIO broadcasting live from MBEYA CITY - TANZANIA.(Iringa,Mbeya,Rukwa,Njombe & Ruvuma). Tus

20/06/2026

Day -3 💥🔥
Burudani ni sehemu kubwa ya kongamano kubwa la operation washa taa kila mkoa ambapo kimsingi leo nfio siku ya mwisho kutoka ndani ya .

Nini unataka Mungu akutendee leo 🙌 mtumishi wa Mungu Mtume Boniface Mwamposa Bulldozer wa madhabau ya yupo tayari kukuhudumia.

19/06/2026

Msemaji wa Jeshi la Polisi, DCP David Misime, ametoa onyo kali kwa baadhi ya watu wanaotumia majukwaa mbalimbali kuhamasisha vitendo vya uhalifu nchini, akisema kuwa Jeshi la Polisi halitasita kuchukua hatua za kisheria dhidi ya mtu yeyote atakayebainika kujihusisha na vitendo hivyo.

DCP Misime amesema usalama wa nchi ni jukumu la kila mwananchi na kwamba ni muhimu wananchi kuzingatia sheria na kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama katika kuzuia na kutoa taarifa za vitendo vinavyoweza kuhatarisha amani, usalama na utulivu wa Taifa.

19/06/2026

Watu wasiojulikana wanadaiwa kuvamia na kuvunja Ofisi za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Nyasa jijini Mbeya na kuondoka na nyaraka mbalimbali za chama hicho.

Taarifa ya tukio hilo imetolewa na Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Mbeya, Hamad Mbeyale, ambaye amesema tayari wamelijulishaJeshi la Polisi kwa ajili ya uchunguzi huku akiomba wahusika watakapok**atwa wachukuliwe hatua za kisheria.

19/06/2026

Mbunge wa Jimbo la Ole, visiwani Zanzibar, Mhandisi Said Salim Hamad, amesema kuwa watu wanaotoa kauli za uchonganishi dhidi ya Muungano wa Tanzania wanafanya hivyo kwa misingi ya chuki binafsi, akisisitiza kuwa hatua hizo haziwezi kuuvunja wala kuudhoofisha Muungano uliodumu kwa miaka mingi.

Mhandisi Hamad amesema wapo Watanzania wengi walio tayari kusimama na kuutetea Muungano kwa gharama yoyote, akieleza kuwa Muungano umeendelea kuwa nguzo muhimu ya amani, umoja na maendeleo ya wananchi wa pande zote mbili za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

19/06/2026

Tazama hapa Mkuu wa mkoa wa Rukwa Makongoro Nyerere akimtania Mkuu wa wilaya ya Ileje Farida Mgomi katika kikao kuelekea maonesho ya Wakulima nanenane Kanda ya Nyanda za juu kusini kilichofanyika jijini Mbeya.

Katika ukurasa wake wa Instagram Mkuu wa wilaya ya Ileje Farida Mgomi ameonesha kufurahishwa na utani wa Bosi wake ambapo ameandika;


Pamoja na majukumu mazito ya seikali tuliyokuwa nayo kuna wakati inapendeza tukifurahi k**a hivi.

Mhe RC Makongoro Nyerere leo umetuvunja mbavu.

Tunakushukuru sana boss kwa kuongoza vema kikao cha nane nane Mbeya kwa wajumbe wa Nyanda za juu kusini leo.

19/06/2026

OPERATION WASHA TAA
KILA MKOA

19/06/2026

Ni wakati wa Sala ya Baba Yetu na

“Baba yetu uliye mbinguni,
Jina lako litukuzwe.
Ufalme wako uje.
Mapenzi yako yatimizwe duniani k**a huko mbinguni.
Utupe leo riziki yetu ya kila siku.
Utusamehe makosa yetu,
k**a sisi nasi tunavyowasamehe waliotukosea.
Usitutie majaribuni,
bali utuokoe na yule mwovu.
Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu, hata milele. Amina.”

Photos from BOMBA FM RADIO 104.1 Mhz MBEYA's post 19/06/2026

🔥 MAELFU YA WATU WAFURIKA KWENYE KONGAMANO LA MWAMPOSA DODOMA!

Umati mkubwa wa wananchi umejitokeza kushiriki mkutano wa Operation Washa Taa Kila Mkoa, kupitia huduma ya MTUME MWAMPOSA BULLDOZER.

18/06/2026

Tayari Mtumishi wa Mungu, MTUME MWAMPOSA BULLDOZER, yupo madhabahuni kwa ajili ya kufungua malango ya neema, mafanikio na ukombozi kwa wakazi wa Dodoma.

Ni katika mkutano mkubwa wa Operation Washa Taa Kila Mkoa, ambapo maelfu ya watu wamekusanyika kushuhudia nguvu za Mungu zikifanya kazi.

18/06/2026

Waziri Mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema huduma za afya hazibagui upande wa Muungano anaotoka mwananchi, bali kinachoangaliwa ni uwepo wa bima ya afya inayotambulika ili kumwezesha kupata huduma.

Amesema utaratibu huo unatumika kwa pande zote mbili za Muungano bila changamoto yoyote katika utoaji wa huduma.

Dkt. Nchemba ametoa kauli hiyo leo Juni 18, 2026 bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Segerea, Agnesta Kaiza, kuhusu utaratibu wa kisera na kisheria unaotumika kuwahudumia Watanzania wa pande zote za Muungano katika masuala yasiyo ya Muungano, ikiwemo huduma za afya.

Want your business to be the top-listed Media Company in Mbeya?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Category

Telephone

Address


P O Box 579
Mbeya
255