Mbeya on Focus
Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Mbeya on Focus, Public Figure, Mbeya.
26/12/2024
Ushauri kwa Wanaume Wanaotaka Kuoa: Kutafuta Mwenza wa Maisha Mwema
Kuchagua mwenza wa maisha ni uamuzi muhimu sana ambao unaweza kuathiri maisha yako yote. K**a mwanaume unayetaka kuoa, ni muhimu kutafuta msichana ambaye atakuwa mke na mama mzuri kwa watoto wako. Tabia za wanamke unayetoka naye ndio zinaweza kuwa tabia za mwanao wa kiume au wa k**e. Je ni changamoto gani wanazipata vijana wa kiume wanapotafuta mwenza?
Tupe maoni yako!
TAKUKURU NA WIZARA YA AFYA ICHUNGUZENI HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA MBEYA, UFISADI UMEZIDI
Viongozi wa Hospitali ya Mkoa wa Mbeya hawakomi, hawana hofu tena, wameota usugu, wameamua kwenda na falsafa ya liwalo na liwe ni mwendo wa chukua chako mapema sisi wafanyakazi wa kawaida tunateseka huku tukiona wakubwa wa hospitali kuiba mamilioni ya fedha na kugawana posho bila kujali usawa na haki kwa wafanyakazi wengine.
Leo nitaeleza madudu yanayofanyika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya bila kuwataja watu majina, ila kwa kuwa serikali ina mkono mrefu na taasisi zake zina D2 wataelewa ni nani wahusika na ufisadi huu, bila shaka serikali itachukua hatua.
1. Viongozi wa Utawala wa Hospitali wanachelewesha malipo kwa makusudi kwa makampuni yaliyopewa tenda mbalimbali hospitalini kwa lengo la kuwadai rushwa ili walipwe pesa zao kwa haraka. Kwa muda mrefu huu umekuwa mradi wa wakubwa wanaohusika na malipo za zabuni mbalimbali za hospitali. TAKUKURU njooni mjik**atie watu hapa wanavimbiwa kwa rushwa na wizi.
2. Ni miezi zaidi ya 6 hatujalipwa extra duty, kila Viongozi wa utawala wakiulizwa kulikoni kuhusu pesa za extra duty wanasema serikali haina hela. Ni kweli makusanyo ya hospitali yameongezeka inakuwaje pesa za kulipa extra duty hazipo?
Lakini kila siku watu wanalazimishwa kufanya kazi muda wa ziada.katibu wa hospital kawa k**a Mungu mtu amekuwa mtu wa kujilipa kwenye mambo yao tu ya utawala na ukifanya ukaguzi wao hawana shida maana wanajilipa mapesa mengi. Ila likija swala la kuwalipa watumishi ambao ndio wanao wajibika kila siku katibu anakataa na ndie afisa bajeti.
Pamoja na kutolipa extra duty ya watumishi ila kila mwezi wanatoa taarifa ya matumizi ya fedha na wanaandika wamelipa watumishi extra duty milioni 30 au zaidi hizi hela wamemlipa nani? Njooni muwaulize watumishi k**a kweli wamelipwa hizo hela! Wamegeuza hospital ni kijiwe cha kujipatia pesa hasa wale waliopo utawala yani ile top management serikali njooni mtusaidie tunaumia tunataka pesa zetu za extra duty zote za miezi 6 ili zitusaidie katika kipindi hiki cha maandalizi ya kuwapeleka watoto shule Wamekuwa watu wa kutishia wale watumishi wanao sema ukweli.
Mtumishi wa afya asipolipwa pesa zake akawa na stres unazani ataweza kumtibu mgonjwa vizuri? Madactari wanalia manesi wanalia ila utawala wanakula pesa kazi kujiandikia madokezo na kujilipa pesa wamejilipa pesa za vikao ambavyo hata hawajakaa mpaka wanamlipa mwenyekiti wa bodi milioni kadhaa ili ionekane nae alishiriki kikao wakati walioshiriki kikao hicho ni wakuu wa idara na hawajalipwa jamani inauma sana.
3. Tunadai pesa ya malipo ya BIMA kwa zaidi ya miezi 10 lakini wiki chache wametulipa Tsh 7,000 (Elfu 7) kwenye akaunti atm gani inatoa kiasi cha elfu saba😠watumishi wote wamelipwa hiyo hela. Morali ya kazi kwa watumishi hasa sisi manesi inapungua maana tunafanya kazi usiku na mchana kuokoa maisha ya wananchi lakini ujira wetu imekuwa k**a tone la maji jangwani.Hii ndio imetuvunja moyo kabisa.
5. Wapo wafanyakazi ambao hawajui majukumu yao wala hawaelewi nini wanafanya lakini kwa sababu wanakitu kinaitwa check namba basi wanadhani wamemaliza kila kitu. Wakifika ofisini ni kusoma magazeti, kunywa chai na kuweka dole gumba la kudanganya mwajiri kuwa walikuwa kazini. Kuna maboss hawajui hata kuijngiza taarifa kwenye mfumo. Masaa 24 wawapo kazini ni vikao vya majungu na kutishia wafanyakazi wasio na check namba kuwa watasitishiwa mikataba yao wakiendekea kudai fedha zao wakati hospitali imeshasema haina pesa.
Tunaomba msaada wa kupaziwa sauti kwa ili mamlaka za TAKUKURU na Wizara ya Afya ziweze kuchukua hatua za haraka.
Nesi MRRH
Plz Hide my ID
Halmashauri ya Jiji la Mbeya Ukurasa Maalumu Ofisi ya Waziri Mkuu Ikulu Mawasiliano Ofisi ya Rais - Tamisemi millard ayo Msemaji Mkuu wa Serikali Dr. Tulia Ackson Mwigulu Nchemba Takukuru.tz Juma Zuberi Homera Mbeya Region Referral Hospital Mbeya Zonal Referral Hospital Samia Suluhu Hassan
Wizara ya Afya Tanzania
POLISI WATEKA WAFANYABIASHARA NA KUPORA FEDHA
Jeshi la Polisi wilayani Mbarali mkoani Mbeya limewateka na kupora mamilioni ya fedha wakulima wawili ambao pia ni wafanyabiashara wa mpunga katika kijiji cha Ubaruku.
Tukio hilo limefanyika Julai mwaka 2023 na kundi la polisi wakiongozwa na Afisa Upelelezi wa Wilaya ya Mbarali OCCID Ndaki Abel ambaye alimteka mkulima na mfanyabiashara Magesa Charles Lugwisha akiwa kwenye shughuli zake za kununua mpunga maeneo ya Ifakara mjini na kusafirishwa hadi kituo cha polisi Rujewa.
Mfanyabiashara mwingine aitwaye Kumbusho Jonas Homange naye alitekwa akiwa kwenye shughuli zake Kijiji cha Ubaruku na kupelekwa eneo maalumu la mateso polisi na kushushiwa kipigo, wakamtishia kipigo zaidi k**a ambavyo mfanyabiashara mwenzie Magesa Charles Lugwisha amefanyiwa kwa lengo la kumshurutisha atoe fedha.
Baada ya wafanyabiashara hao kuona mateso yamezidi wakaamua kuchangishana fedha ili kuwapa askari kwa lengo la kuepukana na mateso makali waliokuwa wanayapata na waliambiwa kuwa wakitoa fedha hizo wataachiwa huru.
Awali askari walitaka wapewe milioni 60 lakini Magesa Charles Lugwisha akatoa kiasi cha shilingi Milioni 10 na Kumbusho Jonas Homange akatoa shilingi millioni 30 na wakapata jumla ya shilingi milioni 40 ambazo walimkabidhi Ndaki Abel ambaye alituma mtu wake wa karibu kuchukua fedha hizo kwa niaba yake.
Wafanyabiashara Kumbusho Jonas Homange na Magesa Charles Lugwisha wakati wote wakiwa mikononi mwa polisi hawajawahi kumwambiwa makosa yao zaidi ya kuwapigwa na kuwataka watoe fedha na kuwapa askari hao.
"Tulipigwa na polisi na wakatutishia ya kwamba tusitoe taarifa hizi mahali popote la sivyo tutafilisiwa mali zote na kuuwawa." alisema Kumbusho Homange
"Baada ya vipigo na kuumizwa niliendelea kutibiwa nyumbani kwa usimamizi wa Afisa Upelelezi wa Wilaya ya Mbarali OCCID aitwaye Ndaki Abel." alisema Magesa Lugwisha.
Gazeti la Mwanahalisi la tarehe 28 Machi 2024 liliripoti kwa kina juu ya sakata hili kwenye ukurasa wake wa 2 na 3 na kupelekea Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Homera kuunda Tume ya uchunguzi juu ya tukio hilo la uporaji wa fedha za wafanyabiashara.
Tume hiyo ilihusisha maafisa kutoka vyombo mbali mbali vya serikali ikiwemo Taasisi ya Kuzuia na Kukupambana na Rushwa (TAKUKURU) Idara ya Usalama wa Taifa (TISS) na Maafisa kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
Tume ilibaini ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu, kuvunjwa kwa maadili ya utumishi kwa maafisa wa jeshi la polisi na makosa mengine ya jinai ikiwemo utekaji, uporaji na shambulio lenye nia ya kudhuru mwili kwa askari na maafisa wengine wa jeshi la polisi.
Aidha tume hiyo ilibaini uwepo wa ushirikiano kati ya mfanyabiashara aitwaye Milele Dembalemba Kaponda ambaye alishirikiana na afisa upelelezi wa wilaya ya Mbarali OCCID Ndaki Abel kupora fedha kwa wafanyabiashara hao.
Hivyo tume iliagiza kesi ya zilizofunguliwa na Ndaki Abel zifutwe na askari waliohusika kwa utekaji na unyanyanganyi kwa kutumia nguvu wahamishwe na washushwe vyeo na fedha zilizoporwa kiasi cha shilingi milioni 40 zirejeshwe kwa wafanyabiashara.
Ni miezi sita sasa tangu agizo hilo la tume dhidi ya idara ya polisi halijatekelezwa na wafanyabiashara hao wanapojaribu kufuatilia fedha hizo wanatishiwa maisha pamoja na biashara zao.
Kuna mkanganyiko wa taarifa kutoka kwa mamlaka zinazoshughulikia suala hilo kati ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, TAKUKURU Mkoa wa Mbeya, Idara ya Usalama wa Taifa Mkoa wa Mbeya, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya na Wizara ya Mambo ya ndani ambapo ofisi zote hizi zinakwepa kushughulikia suala hili.
Hali hii imepelekea wahusika waliobainishwa na tume kuhusika na sakata hili kuendelea kutoa vitisho kwa wafanyabiashara walioumizwa na kuporwa fedha zao kuwa hakuna mamlaka inayoweza kuwasikiliza hivyo wanapoteza muda na fedha zaidi kuendelea kufuatilia fedha zao.
Bado kuna hofu imetanda kwa wakulima na wafanyabiashara wa mpunga wilayani Mbarali ambao wanafuatilia kwa karibu namna mamlaka za serikali zinavyoshughulikia sakata hili huku wakionyesha kutokuwa na imani namna mwenendo wa shauri hili unavyoendeshwa.
Hivi wizara imeshindwa kumaliza suala hili? Nini kinaendelea nyuma ya suala hili? Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya pamoja na vyombo vya ulinzi na Usalama vimeshindwa kuwawajibisha wahusika wa unyama huu unaofanywa na jeshi la polisi?
Mamlaka zinazohusika wanasubiri Rais Samia Suluhu Hassan aingilie kati sakata hili ili haki itendeke? Hivi hawa wafanyabiashara wangebainika kuwa wanafanya biashara haramu, Je mamlaka zingeendelea kukaa kimya?
Ni nani aliwatuma hawa polisi kuteka na kupora fedha? Kwanini hawa askari wamehamishwa na wengine kushushwa vyeo badala ya kufukuzwa kazi? Kuna nini Mbarali Mbeya?
Kwenye sakata hili kila mtu anashangaa! Waziri wa mambo ya ndani anashangaa! Mkuu wa Mkoa anashangaa! Jeshi la polisi linashangaa! Mamlaka za usalama mkoa wa Mbeya zinashangaa! wakulima na wafanyabiashara wa mpunga waliotekwa na kuporwa fedha zao wanashangaa! wananchi wameduaa na kuchanganyikiwa!
09/09/2024
Mbeya, Tanzania
08/07/2024
Mbeya ni moja ya Jiji lenye barabara mbovu na chafu kuliko hata baadhi ya halmashauri ya wilaya hapa Tanzania. Nini sababu ya barabara za Mbeya kutokutengenezwa?
Dondosha coment yako hapa chini.
Halmashauri ya Jiji la Mbeya Ukurasa Maalumu
Napendekeza WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO ifanye marekebisho madogo kwenye Bajeti Kuu k**a ifuatavyo:
1. Kwa kuwa Serikali imeshanunua Ndege ya Mizigo. Na kwa kuwa asilimia kubwa ya mizigo ya kutoka hapa Tanzania kwenda nje ya nchi ni HORTICULTURE; Napendekeza Kodi/Ushuru wa Forodha wa Uingizaji wa Magari ya Friji (Refrigerated Trucks) Kodi /Ushuru uondolewe kabisa ili kutoa nafasi kwa wafanyabiashara kuingiza magari haya kwa wingi yasaidie sekta ya kilimo.
Lengo la hatua hii ni kufanya mazao ya HORTICULTURE yaweze kuwasili kwenye viwanja vyetu vya ndege yakiwa katika ubora ule ule yakitokea mashambani.
2. Kupunguza umri wa kuagiza magari chakavu kutoka miaka 5 iliyo-pendekezwa na Wizara hadi miaka 10. Hii ni kwa sababu WATANZANIA walio wengi bado hatujafikia UCHUMI wa kununua gari za umri wa miaka 5. Gari za miaka 5 ni gari zenye hali nzuri sana ni ghali sana.
Athari za hili ni kusababisha watanzania waendelee kutumia magari machakavu yaliyopo nchini na kusababisha ajali nyingi kutokana na uchakavu wa magari hayo.
Dr. Tulia Ackson
Mwigulu Nchemba
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Culinary Team
Attire
Website
Address
Mbeya