Mbeya Fm Redio
MBEYA FM 89.3 MHz
COVERING AREA;
✅️MBEYA AND HIS AREA,
✅️NJOMBE
✅️IRINGA
✅️SONGWE
✅️RUKWA.
Polisi wanachafuliwa na watu wasiokuwa waaminifu ndani ya jeshi na sisi wakati wetu polisi tunamuanzia kwenye kata, sasa hivi sijuwi k**a kuna veting kwa sababu k**a hamfanyi veting au humjui askari kutoka kijijini kwake.
Omar Mahita ameyazungumza hayo kwenye M&S Podcast na kutoa mtazamo wake mpana kwa kile kinachofanyika kwa sasa katika jeshi la polisi.
📻Tufuatilie Mbeya Fm kupitia 89.3 Mhz au online kwenye Radio Box kwa jina la Mbeya FM Radio.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini ( (IGP), Camillius Wambura katika kipindi cha uongozi wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan jeshi hilo limepiga hatua kubwa ikiwemo maboresho ya makazi kutoka kwenye vibanda vya mabati hadi nyumba za kisasa za askari hao.
IGP Wambura amesema makazi ya askari yalikuwa katika mazingira magumu ikiwemo kuishi katika vibanda vilivyojengwa kwa mfumo wa mabati mithili ya nyumba za wavuvi wa samaki.
Wambura amesema hayo leo katika hafla ya kufunga mafunzo ya kozi namba 1/2025/ 2026 ya maofisa na wakaguzi wasaidizi wa Jeshi la Polisi iliyofanyika Chuo cha Taaluma ya Polisi Kurasini jijini Dar es Salaam yaliyohudhuriwa na Dkt Samia.
" Mheshimiwa Rais yale yamejengo ulioyaona pale kwenye slide si kambi za wavuvi, bali ni makazi ya polisi ambayo askari walilala humo na kwenda kulinda raia na mali zao.Majengo hayo yameisha kwa muda mrefu, lakini wewe umeyakataaa.
" Umetoa fedha na kuhakikisha majengo ya kisasa ya makazi ya askari yanajengwa hasa maghorofa, hii imeondoa hata yale makazi ambayo hata wavuvi wasingeweza kukaa.
Amesema " sisi ni kina nani tusisimulie hadithi hii? Au kina nani tusiokuwa na roho ya shukrani ya kusimulia hadithi hii, mheshimiwa Rais asante sana," amesema IGP Wambura.
Mkuu huyo wa Jeshi la Polisi, amesema mabadiliko hayo yaliyofanywa na Dkt Samia yataachaa alama kubwa ndani ya jeshi la polisi na vizazi vijavyo sambamba na kuweka kumbukumbu ndani ya jeshi hilo.
Ameeleza kuwa uongozi wa Dkt Samia umewezesha pia Jeshi la Polisi kupata vyombo mbalimbali vya usafiri, yakiwemo magari ya kisasa sambamba ajira mpya katika jeshi hilo, upandishaji wa vyeo kwa askari na ujenzi wa vituo vya kisasa vya polisi.
📻Tufuatilie Mbeya Fm kupitia 89.3 Mhz au online kwenye Radio Box kwa jina la Mbeya FM Radio. Like, comment na share ili kupata updates za kila siku!
📌 Mbeya Fm – Radio yako, Radio yangu, Radio yetu.
Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, amemtaka Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Camilius Wambura, kuangalia namna jeshi hilo litakavyojenga imani yake kwa wananchi, sekta binafsi na jumuiya za kimataifa zilizopo hapa nchini.
Mkuu huyo wa nchi ametoa kauli hiyo, akirejea utafiti uliochapishwa na Shirika la Afrobarometer hivi karibuni, ukihusisha wananchi wa Afrika na imani kwa Jeshi la Polisi.
Kupitia utafiti huo, wananchi hao walihojiwa endapo watapata shida ya kisheria, imani yao ikoje kwa Jeshi la Polisi na ripoti imeonyesha asilimia 12 pekee ya Watanzania waliohojiwa walisema watakimbilia polisi.
Katika nchi 38 za Afrika zilizohusishwa kwenye utafiti huo, moja pekee ndiyo ilikuwa na alama za juu yaani asilimia 25, kwamba raia wakipata shida watakimbilia polisi.
Rais Samia ametoa maelekezo hayo kwa IGP Wambura, leo Mei 28, 2026 wakati akihitimisha Mafunzo ya Maofisa na Wakaguzi Wasaidizi wa Polisi, Kurasini, Dar es Salaam leo Mei 28, 2026.
Amesema taarifa hizo si za kuzibeza, bali ni kuangalia changamoto zilipo hadi wananchi wajibu hivyo na zifanyiwe kazi.
“Tunataka kuona namna Jeshi la Polisi linavyojenga imani yake kwa wananchi na sekta binafsi na jumuiya za kimataifa zilizopo nchini. Hapa tunaangalia legitimacy (uhalali) ya polisi,” amesema.
📻Tufuatilie Mbeya Fm kupitia 89.3 Mhz au online kwenye Radio Box kwa jina la Mbeya FM Radio. Like, comment na share ili kupata updates za kila siku!
📌 Mbeya Fm – Radio yako, Radio yangu, Radio yetu.
19/03/2023
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe, Juma Zuberi Homera amesema mkoa wa kimadini Chunya unafanya vizuri sana katika sekta ya madini jambo linalopelekea uzalishaji wa madini kuongezeka kutoka kilograma 20 mpaka kufikia kilogramu 330 kwa mwezi ambapo zaidi ya Bilioni thelathini hupatikana kupitia sekta hiyo ya madini
Homera amesema hayo Mapema jana wakati akifunga maonesho ya kwanza ya Teknolojia ya Madini yalitofanyika kuanzia tarehe 14/03/2023 katika viwanja vya Chunya kati vilivyopo halmashauri ya wilaya ya Chunya ambayo hutambulika k**a mkoa wa kimadini Chunya
“Kwakweli Chunya mnafanya vizuri sana katika sekta ya madini kuanzia wachimbaji wakubwa na wachimbaji wadogo hakika kwakweli tunastahili kuwapongeza sana sana wanachunya wote kwa kazi kubwa mnayoifanya”
Homera amesema maelekezo aliyoyatoa Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan ya kulegeza mashariti katika sekta ya uchimbaji ndiyo yanayopelekea kuwa na wawekezaji wengi wilayani chunya Huku wawekezaji wazawa kuongezeka katika sekta ya Madini
“Tumeshuhudia wawekezaji wengine wamewekeza kwenye sekta ya madini hapa wilayani Chunya, tumejionea makampuni makubwa k**a vile Ramani Investment, kina Achimwene, Kindai Investment, Sunshine, Msigwa na mengine mengi, Yote haya ni kutokana na maelekezo aliyoyatoa Mhe. Rais ya kulegeza mashariti ya kuingiza vifaa vya uchimbaji hivyo ni lazima tumpongeze sana Mweshimiwa Rais kwa kuamua kuwekeza kwenye sekta ya Madini”
Kwakukumbuka kifo cha Rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Mhe. Dkt John Joseph Magufuli, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya amewaongoza wananchi waliojitokeza katika maonesho hayo kutulia kwa dakika moja ikiwa ni ishara ya kumkumbuka, kuenzi na kumwombea kheri apumzike kwa amani huko aliko
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Telephone
Website
Address
Mbeya