Daniel awack
MBUNGE WA JIMBO LA KARATU
12/05/2026
KARATU IKO MIKONO SALAMA
18/04/2026
TANZANIA KWANZA
KARATU IMEPOTEZA WATU MAKINI SANA
MBUNGE KARATU ATOA MSAADA WA MORAM KUREKEBISHA DARAJA LILILOHARIBIKA
Mbunge wa Jimbo la Karatu, Mhe. Daniel Awack, ametoa msaada wa malori ya moram kwa ajili ya kurekebisha miundombinu ya daraja lililoathiriwa na mvua kubwa katika barabara ya G/Arusha – Lambo.
Hatua hiyo imekuja kufuatia uharibifu uliosababishwa na maji mengi yaliyosomba sehemu ya daraja hilo, hali iliyosababisha usumbufu mkubwa kwa watumiaji wa barabara hiyo muhimu inayounganisha maeneo mbalimbali ya G/Arusha .
Akizungumza wakati wa utoaji wa msaada huo, Mhe. Awack amesema kuwa lengo ni kuhakikisha mawasiliano ya barabara yanarejea haraka iwezekanavyo ili kurahisisha shughuli za kiuchumi na kijamii kwa wananchi.
Wananchi wa eneo hilo wamepongeza juhudi hizo, wakieleza kuwa msaada huo umekuja kwa wakati muafaka kwani daraja hilo ni kiungo muhimu kwa usafiri wa watu na bidhaa.
Ukarabati unaendelea kufanyika kwa kushirikiana na wadau mbalimbali, huku jitihada zikielekezwa kuhakikisha daraja hilo linakuwa salama na kudumu kwa muda mrefu licha ya changamoto za mvua zinazoendelea kunyesha.
10/03/2026
Nimeshiriki kikao cha 52 cha Bodi ya Barabara ya Mkoa kilichofanyika tarehe 9 Machi 2026, ambapo pamoja na agenda nyingine muhimu, kikao hicho kimeridhia kupandisha hadhi ya barabara ya Rhotia – Kambi ya Simba – Slahhamo – Kitete – Upper Kitete – Lositete hadi Selela, Monduli. Barabara hiyo ambayo hapo awali ilikuwa inahudumiwa na Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA), sasa inapendekezwa kuhamishiwa kuhudumiwa na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) ili kuboresha zaidi miundombinu yake na kuongeza ufanisi wa huduma kwa wananchi.
Hoja ya kupandisha hadhi ya barabara hiyo iliwasilishwa mapema tarehe 6 Machi 2026 mbele ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mwigulu Lameck NCHEMBA, wakati wa ziara yake Wilayani Karatu, mkoani Arusha. Kupitishwa kwa pendekezo hilo kunatarajiwa kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa wananchi wa maeneo ya Rhotia, Kambi ya Simba, Slahhamo, Kitete, Upper Kitete, Lositete na Selela, kwa kurahisisha usafiri na usafirishaji wa bidhaa pamoja na huduma muhimu.
Hatua hiyo inaenda sambamba na juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan za kuendelea kuboresha miundombinu ya barabara nchini kwa ajili ya maendeleo ya wananchi.
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Website
Address
Karatu