Mlewa Electronics
-ICT Expert
-Economist
-Karibu ndani ya familia ya "Christopher Mlewa" 🙏
04/10/2026
Leo usilalamike, leo usilia, leo ni siku ya kusema ASANTE tu.
Asante Mungu kwa pumzi, kwa afya, kwa familia, na kwa fursa nyingine ya kuanza upya.
Wengi walitaka kuiona leo, hawakuiona, wewe umeiona sio kwa nguvu zako, bali kwa NEEMA tu familia.
Nenda kanisani, mwabudu Mungu kwa moyo, acha Mungu akupambanie vita zako wiki hii, kamwe usiingie kwenye mtego wa kupambana mwenyewe kwenye vita zako, tafadhali.... muachie aliyekuumba, yeye atamaliza.
JUMAPILI NJEMA FAMILIA! 🙏
03/10/2026
Sisi binadamu tusio na AKILI, tukaamua kumuomba Mungu atupe maarifa, Mungu hakuwa mchoyo kabisa, akatupatia.
Sasa maarifa tuliyopewa yameanza kugeuka yenyewe ndio Mungu, SO SAD!!!💔 Amini nakuambia AI haitakuja kuchukua kazi yako tu, bali inakuja kuchukua nafasi ya Mungu moyoni mwako.
Unamwambia AI Siri zako zote kuliko unavyomwambia Mungu, hatari SANA, hii vita mwisho wake ni nini? Mimi sijui, japo najua mshindi atakuwa ni mmoja tu... naye ni huyu👇
"Ambaye hajawahi kutengenezwa, bali ndiye aliyetuumba." unakubaliana na mimi? nijibu hapo chini.
_
_
03/10/2026
Ndani hakufai mkuu, tutoke nje! Amini nakuambia siku yako itakua nzuri sana, USISAHAU kuiombea simu yako.💪
-
-
02/10/2026
KUSHINDWA kudhibiti HOFU ya kuchelewa imetufanya wengi tuko kwenye kazi tusizozipenda, wachumba tusiowapenda na biashara za hasara.
Tuliogopa kuchelewa, tukakimbilia chochote kilichokuja mbele yetu. INAUMA😞
Swali kwako:
Ni kitu gani ULIKUBALI kukifanya kwa haraka kwa sababu uliogopa kuchelewa, na leo unakijutia?
Andika hapa chini👇 na comment yako inaweza kumsaidia mtu mwingine leo.
FOLLOW kwenye INSTAGRAM
02/10/2026
Kwani mwenzetu kifo umetoka wapi? mbona unatufanyia ukatili? tazama unavyokula maskini wenzetu.
Tazama ambavyo unapenda kuchukua matajiri wetu, wamekukosea nini?
Mbona pesa za matibabu walikua nazo, si ungewaambia waende lini India? k**a ulitaka rushwa basi ungesema.... mbona Sir Wicknell Chivayo na Lowasa wa Monduli wangekupa tuu, Kanumba angeshindwa? na JPM wa Chato je? aaah....!
Kifo unatuudhi sana, mbaya zaidi ukituua basi unatuweka kwenye shimo lefu sana, kwani tulikukosea wapi? mbaya zaidi hata ndugu zetu wa karibu wanatuwahisha kwenye hilo shimo la futi 6 kwa kusema eti mochwari ni gharama sana sisi kulala.
Tazama sasa ndugu tuliowapenda ndio wataongoza kutufukia udongo kaburini, na baada ya dakika 20 wataondoka kuwahi chakula nyumbani na wakituacha bila kujali uzito wa mchanga tulioubeba kaburini.
Kifo wewe ni katili sana, sawa sisi watu wazima tumekubali huenda tulikoseana mahali flani, vipi hawa malaika unaokula..! mtoto wa miezi miwili, na mwingine wa mwaka mmoja amekukosea nini ndugu yangu KIFO? aaah unakera sana.
FOLLOW Christopher Mlewa
-
-
01/10/2026
PUMZIKA KWA AMANI TAJIRI Sir Wicknell Chivayo (1982-2026) 🙏
Jana Zimbabwe imepoteza mmoja wa wafanyabiashara wake wakubwa kwenye ajali ya helicopter huko Marondera. Ameondoka na mkewe na watu 4 wengine, hakuna aliyenusurika.
Watu wengi wameuona msiba tu, lakini mimi k**a Mchambuzi wa Uchumi na Mifumo, nauliza swali kubwa zaidi...
NINI KINAENDA KUTOKEA KWENYE MALI ZAKE BAADA YA MMILIKI HUYU KUONDOKA?
Chivayo alikuwa na kampuni ya Intratrek, mradi wa Solar wa 100MW, na mitandao ya biashara kwenye nchi nyingi sana za Afrika, hata hapa kwetu tunamfahamu, ni taarifa mbaya sana kuwa bilionea huyu alikua hana utaratibu mzuri wa kulinda mali zake kwa siku ambayo hatokuepo duniani, HAKUJIHAMI.
Somo kwa wafanyabiashara wa Tanzania.
1. MALI BILA DIGITAL SUCCESSION NI BOMU.
Leo akaunti zake, tender zake, na hata mitandao yake ya kijamii - nani ana password? Familia nyingi za matajiri wa Afrika hupoteza 70% ya mali ndani ya mwaka 1 baada ya kifo kwa sababu hakuna mfumo.
Tajiri jiulize hivi, siku ukifa na biashara zako zitakufa? jibu ni ndio zitakufa, kwa sababu tu huna mfumo wa kidigitali wa urithi (Digital Succession System).
2. MALI NYINGI BILA MFUMO wa kisheria wa kidigitali ni hatari sana.
Ndugu tajiri wa kitanzania, tazama sasa kuna ripoti zinaonyesha hata akaunti zake za pesa, zilikuwa na kesi mahak**ani Afrika Kusini, kipi kitaenda kutokea na yeye hayupo na hakuna mwingine wa karibu anayejua pakuanzia, hatari sana.
Kanuni ya kiuchumi inaamini kuwa biashara isiyo na mfumo sahihi, ni k**a ajali tu inayosubiri muda ufike.
K**a biashara yako inakufa ukiwa mgonjwa kwa siku 2 tu, basi hapo huna biashara bali una kazi. Chivayo alijenga himaya, lakini je, alijenga mfumo wa kuendesha himaya bila yeye? jibu hapa ni HAPANA.
Huyu blaza aligawa Maybach nyingi sana kwa watu, lakini kumbukumbu bora sio gari uliyompa mtu bure, bali ni kampuni inayoendelea kulipa mishahara hata baada ya wewe kuondoka..... INAENDELEA KWENYE COMMENT 👇
01/10/2026
Bonyeza hapa ili baadae usipitwe kabisa
30/09/2026
Bila shaka hii ni picha yangu BORA ya muda wote kwenye simu yangu, picha hii ilipigwa usiku wa tar 02/05/2011 ndani ya PENTAGON (wizara ya ulinzi ya Marekani), pichani anaonekana Rais wa wakati huo Barack Obama, makamu wake kipindi hicho Joe Biden, pamoja na viongozi wa juu wa "CIA"
Hapa walikua wanaangalia LIVE kwenye screen jinsi ambavyo wanajeshi wao wa Marekani walikua wanaendelea na oparesheni ya kumuua Osama Bin Laden huko PAKISTAN, Kuna mama hapo pichani ameziba mdomo, hii ni ishara kwamba kilichokua kinaendea hapo si cha kawaida kabisa, mama alijikaza sana kupiga kelele, baadae siri ikavuja kuwa huyu mama ni alikuwa..... INAENDELEA KWENYE INSTAGRAM YANGU.
HAKIKISHA UMEFOLLOW Instagram hii ili ujue Muendelezo na MENGINE MENGI👇
FOLLOW
FOLLOW
30/09/2026
Mkuu! ni kweli wenzetu waliofanikiwa kiuchumi wanayo tabia ya kutuona sisi ni wavivu, hatujitumi na wanafika mbali sana kutuona hatuna AKILI.
Tazama wanavyotulaumu kuwa tunachelewa sana kuamka, sasa tuamke twende wapi na michongo hatuna?
Tazama wanavyotulaumu kuwa hatusaidii ndugu zetu, sasa tutawapa nini na hatuna vya ziada?
Tazama wanavyotulaumu kuwa tunapoteza muda mwingi Kanisani & Masjid, sasa tufanyaje na wakati kete zote wametuibia na iliyobaki ni moja tu kwa MUNGU?
Tazama wanavyosema eti hatutunzi pesa, jamani tutatunza nini wakati tunachokipata kinaishia kwenye kututunza tu?
Wenzetu punguzeni kutulaumu, viatu tulivyovaa si k**a vyenu, vyetu vinatubana sana, tazama tulivyochubuka miguu.😭😭
Imani yetu ni kwamba siku yetu nzuri INAKUJA, tutakula meza moja na wakuu wa nchi💪💪Kwaherini.
-
-
29/09/2026
Wakuu tuache kuita mke wa mtu bila sababu ya msingi aise, atakuja atufungulie kesi mbaya sana huyu hayati ALEXANDEL G. BELL.
-
-
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Contact the school
Telephone
Website
Address
Iringa
Alerts
Be the first to know and let us send you an email when Mlewa Electronics posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.