Benjamin the seer
BOWL OF DIVINE HEALING,REVIVAL AND RESTORATION MINISTRY
25/12/2025
Katika ulimwengu wa roho,amekwisha kuwa MKIMBIZI anayekimbia hata pasipo kufuatiwa na mtu.Nalimuona akijificha na kuviziavizia akiwa katika mavazi ya kawaida sana.
Amekwisha kuwa RAIA wa daraja la kawaida asiye kuwa na ulinzi wowote.
Danieli 2:47
Mfalme akajibu, akamwambia Danieli, Hakika Mungu wenu ndiye Mungu wa miungu, na Bwana wa wafalme, awezaye kufumbua siri, kwa kuwa wewe uliweza kuifumbua siri hii.
The king answered unto Daniel, and said, Of a truth it is, that your God is a God of gods, and a Lord of kings, and a REVEALER OF SECRETS, seeing thou couldest reveal this secret.
Patience is the key
Subra ni ya muhimu
Kutoka 14:14
BWANA atawapigania ninyi, nanyi mtanyamaza kimya.
The LORD shall fight for you, and ye shall hold your peace.
A dream remains a dream until it becomes a plan
UJUMBE ZAIDI BAADA YA MFUNGO
Ay 4:12-13
Basi naliletewa neno Kwa siri,sikio langu likasikia manong'ono yake.Katika mawazo yaliyotoka katika maono ya usiku, hapo usingizi mzito uwaangukiapo wanadamu.
Nikaona katika maono mtumishi wa Mungu akiniambia,
"K**a njia ya kwanza itashindwa tunaenda kwenye phase nyingine ya ARMED UPRISING".
Tuombe sana kwa ajili ya taifa letu maana nyakati tulizopo ni za hatari sana k**a Bwana Mungu asipoingilia kati.
"Bwana asipoulinda mji,waulindao wakesha bure"
MAONO
Na nilipoingia kuutafuta uso wa Bwana kwa siku nne Kwa kufunga na kuomba kwa ajili ya TAIFA langu,
Bwana akanionyesha,
Maji yenye nguvu yakiwa yanafurika juu ya daraja,watu wakawa hawawezi kuvuka.
Tena nikaonyeshwa kundi la Wachawi wakifanya mambo Yao ya giza.
Bwana akanionyesha tena NYOKA mkubwa akiwa AMEKATWA KICHWA kinachuruzika DAMU nyingi mpaka ililowesha mavazi yangu na watu wengi wakawa wameenda kumshangaa yule NYOKA.
Kitabu cha Ufunuo kimeeleza JOKA k**a ni ufalme wa Rumi uliotaka kumwangamiza Yesu katika utoto wake lakini Mungu akamtoroshea nyikani yule mwanamke aliyetoka kujifungua na lile Joka kubwa jekundu likatema nyuma yao MAJI mfano WA MTO Ili uwagharikishe,Mungu akampa yule mwanamke uwezo
wa kuruka kwa mbawa Hadi nyikani alikolishwa kwa muda wa miaka mitatu na nusu mpaka adui yao(HERODE) alipokufa.
Yeremia 33:3 inasema, Niite nami nitakuitikia,nami(Mungu) nitakuonyesha mambo makubwa magumu usiyoyajua.
Joka kukatwa kichwa ni ishara ya ushindi.
LIPO TUMAINI.
Stay tuned
Usiondoke endelea kufuatilia updates
UJUMBE TOKA KWA MUNGU
Baada ya kushuhudia yote yaliyotokea katika taifa letu siku chache zilizopita.
Nikiwa k**a MWONAJI(SEER),niliamua kuutafuta uso wa Mungu nakuomba kwa ajili ya taifa letu na kwa damu zilizomwagika.
Ndipo Mungu akanijibu kwa ndoto ifuatayo.
Naliona maji(mafuriko) yameizingira NYUMBA Moja ambayo mlango wake ulikuwa wazi na usingeweza kufungwa kutokana na Yale maji.Nje ya ile NYUMBA kulikuwa na gari ambalo nalo lilikuwa limezingirwa na maji pia.
Nikaona Kwa mbali MAMA mmoja ambaye alikuwa k**a mzungu kwa mwonekano akaniomba nimsaidie kulitoa lile gari kwenye yale maji na lilikuwa ni gari la kubonyeza button(vitufe fulani).LAKINI kitu cha ajabu ni kwamba yule MAMA licha ya kumsaidia akasema nikiligongesha gari lake itabidi tuchangie gharama ya kulitengeneza mimi na yeye.Nikamshangaa sana ana moyo wa namna gani huyu!
Wakati natafakari kuhusu hayo maji ikiwa ni mafuriko au laa!Roho mtakatifu akanipa tafsiri kupitia Ufunuo 17:15 ya kwamba Yale MAJI ni WATU wa jamaa,makutano na lugha anapoketi yule MAMA.
Nilimfikishia yule MAMA gari lake akaondoka nalo.
Mwenye kuelewa NENO hili alilonifunulia BWANA na aelewe.
LIPO TUMAINI,JIPENI MOYO ENYI TAIFA LA MUNGU.
Ufunuo wa Yohana 6:9-10
[9]Na alipoifungua muhuri ya tano, nikaona chini ya madhabahu roho zao waliochinjwa kwa ajili ya neno la Mungu, na kwa ajili ya ushuhuda waliokuwa nao.
And when he had opened the fifth seal, I saw under the altar the souls of them that were slain for the word of God, and for the testimony which they held:
[10]Wakalia kwa sauti kuu, wakisema, Ee Mola, Mtakatifu, Mwenye kweli, hata lini kutokuhukumu, wala kuipatia haki damu yetu kwa hao wakaao juu ya nchi?
And they cried with a loud voice, saying, How long, O Lord, holy and true, dost thou not judge and avenge our blood on them that dwell on the earth?
DAMU INALILIA HAKI
UJUMBE
Bwana kanikumbusha Tena usiku wa leo habari za Nebukadneza,mfalme wa Babel na namna alivyochukuliwa kwenda uhamishoni mbali na makao ya wanadamu akaishi na wanyama wa mwituni.
Akapoteza kiti chake Cha ufalme ingawa Mungu alimrudisha Tena.Kilichompoza Nebukadneza ilikuwa ni KIBURI.
Mara ya mwisho Bwana kunisemesha habari za Nebukadneza ilikuwa ni mwaka 2020 February na nilipost kwenye ukurasa wangu na siku chache zilizofuata Mungu akamwadhibu Nebkadneza.
Mwenye akili na afahamu jambo hili alilosema Bwana Mungu wa majeshi.
CODED.
Hiki alichonionesha Bwana ni majibu ya maombi niliyoyafanya kwa siku kadhaa nikiwa sili chakula mchana na usiku kwa siku kadhaa.
Amosi 3:7
Hakika Bwana MUNGU hatafanya neno lo lote, bila kuwafunulia watumishi wake manabii siri yake.
Surely the Lord GOD will do nothing, but he revealeth his secret unto his servants the prophets.
Sikujua itaendelea mpaka leo
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Website
Address
Kibwabwa
Iringa