Thinker Genius
Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Thinker Genius, Education, Geita.
03/05/2026
Watu wengi wanachanganya kazi na maisha binafsi.
Unaanza kuona boss k**a rafiki… kampuni k**a familia…
Lakini ukweli ni huu:
Biashara inaangalia faida, sio hisia zako.
Ukifanya kazi vizuri, wanakulipa.
Ukishindwa, wanakubadilisha.
Hakuna loyalty ya kweli k**a unavyodhani.
Ndio maana:
Usijisahau kwa ajili ya kazi.
Usitoe kila kitu mpaka ubaki bila kitu.
Fanya kazi yako kwa akili.
Lipwa unachostahili.
Linda muda wako, afya yako, na maisha yako binafsi.
Kazi ni sehemu ya maisha… sio maisha yako yote.
02/05/2022
Kataa maumivu katika nafsi yako karibisha furaha na amani, hauwezi kuwa na furaha na amani kwa mtu asiyejali wala kuthamini chozi lako.
Hauwezi kuona raha na furaha ya mahusiano ndoa ikiwa unanyanyasika na kudharaulika.
Ni ngumu kuachana na mtu unayempenda, ila kuendelea kuishi na unayempenda halafu hakupendi ni kukubali kwa hiyari maumivu na karaha.
K**a ulivyokuwa humjui anza hatua za kumsahau katika maisha yako leo, kuwa nae mbali kwani anakudhoofisha kiakili pia anakufanya usipate nafasi ya kuwa na mtu sahihi kwako atakaekupenda, kujali na kukuthamini.
Yupo wa aina hiyo achana na mawazo kuwa wote ni k**a huyo, labda hakuna atakae kutesa na kukuumiza k**a yeye.
Yupo bora zaidi yake mwenye heshima, upendo na hadhi ya kuwa mumeo.
Kubali maumivu ya muda mfupi ya kuachana naye.
Wengi ni waoga kukubali maumivu ya muda mfupi na matokeo yake wanakuwa na maumivu muda wote.
Amua kuwa na furaha Leo, Maisha ni yako ni wewe unaweza kuyapa Thamani, pia ni wewe unaweza fanya yasiwe kila kitu.
Thinker Genius
28/04/2022
Welcome to join us
23/04/2022
Ukiona mtu ameyashikiria mahusiano yenye mateso makubwa basi itakuwa ameishi katika matumaini na imani kuwa ipo siku yatakuwa sawa au aliwaza vitu atakavyopoteza akiyaacha hayo mahusiano mpaka muda wa kujinasua ukampita.
Maamuzi sahihi yasipofanyika kwa wakati sahihi huwa si sahihi tena, basi ameamua kuyaishi makosa katika maisha yake yote.
Follow link hii kujifunza Mengi kuhusu njoo
+255742527159
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Contact the school
Telephone
Website
Address
Geita