VETA
This is an official account for the Vocational Education and Training Authority (VETA).
22/06/2026
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA AIPONGEZA VETA KWA KAZI NZURI YA UTOAJI MAFUNZO KWA MAKUNDI MAALUM
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Regina Qwaray, leo tarehe 22 Juni, 2026 ametembelea banda la VETA kwenye maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika viwanja vya Chinangali Park jijini Doma.
Naibu Waziri akiwa katika banda la VETA, ametoa pongezi kwa kazi nzuri na kubwa inayofanywa na VETA katika kutoa mafunzo kwa watu wenye mahitaji maalum pamoja na uzalishaji wa bidhaa mbalimbali kupitia kampuni Tanzu ya VETA ya Ujuzi.
“Niwapongeze kwa kuongeza ujuzi kwa vijana wetu kwani kupitia ujuzi huo wanaweza
kujiajiri wenyewe, kwasasa Serikali imewekeza kwa vijana zaidi kujiajiri, sasa ile hoja ya vijana kujiajiri itafanikiwa k**a tutafanya uwekezaji mkubwa kwenye vyuo vya VETA,” amesema Qwaray.
Naibu Waziri ameongeza kuwa kijana anapohitimu kidato cha nne au elimu ya juu anaweza Kwenda VETA akapata ujuzi unaomuwezesha kujiari bila kusubiri ajira za Serikali.
Ameongeza kuwa pia ujuzi kwa wananchi una mchango mkubwa katika kufikia malengo ya Dira 2050.
VETA inashiriki katika maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yaliyoanza tarehe 16 Juni, 2026 nakufunguliwa rasmi tarehe 17 Juni, 2026 na Waziri wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwan Kikwete na yanatarajiwa kufungwa tarehe 23 Juni, 2026.
Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) inaendelea kuwakaribisha wananchi wa Dodoma kutembelea banda lake katika maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yaliyoanza tarehe 16 hadi 23 Juni, 2026 katika viwanja vya Chinangali Park.
Karibu kwenye banda la Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) tunashiriki Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yaliyoanza tarehe 16 hadi 23 Juni, 2026, katika viwanja vya Chinangali Park Dodoma.
17/06/2026
Mkurugenzi Mkuu wa VETA, CPA Anthony Kasore, akiwa katika hafla ya kutunuku vyeti kwa wakufunzi 30 waliopatiwa mafunzo ya teknolojia ya Uungaji Mabomba kwa Mzunguko (Orbital Welding). Hafla hiyo ilifanyika leo, tarehe 17 Juni 2026, katika Chuo cha VETA Dodoma, ambapo wakufunzi hao kutoka taasisi mbalimbali walitunukiwa vyeti baada ya kukamilisha mafunzo hayo maalum yanayowawezesha kupata tunuku za kimataifa katika Uungaji Vyuma.
17/06/2026
Mgeni rasmi katika ufunguzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma Waziri wa Ofisi ya Raisi- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Jakaya Kiwete, akikabidhiwa zawadi zinazolishwa na Kampuni Tanzu ya VETA ya Ujuzi, leo tarehe 17 Juni, 2026, alipotembelea banda la VETA kwenye maonesho hayo yanayofanyika katika viwanja vya Chinangali Park, jijini Dodoma.
17/06/2026
Mgeni rasmi katika ufunguzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma Waziri wa Ofisi ya Raisi- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Jakaya Kiwete akikabidhiwa zawadi zinazolishwa na Kampuni Tanzu ya VETA ya Ujuzi leo tarehe 17 Juni, 2026 alipotembelea banda la VETA lilipo kwenye maonesho yanayofanyika katika viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma.
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Telephone
Website
Address
VETA Head Office, 12 VETA Road, 41104 Tambukareli, P. O. Box 802, Dodoma Tanzania, Email: Info@veta. Go. Tz Telephone: +255 26 2963661 Fax: +255 22 2863408 Url: Www. Veta. Go. Tz
Dodoma
PLOTNO.18
Opening Hours
| Monday | 07:30 - 21:30 |
| Tuesday | 08:00 - 21:30 |
| Wednesday | 07:30 - 21:30 |
| Thursday | 07:30 - 21:30 |
| Friday | 07:30 - 21:30 |