Ofisi ya Rais-UTUMISHI
Jukumu kubwa la OR-MUUUB ni kuimarisha Utawala Bora katika uendeshaji wa shughuli za Serikali kwa kubuni Sera, Sheria, Kanuni na Taratibu
13/06/2026
UFUNGUZI WA MAADHIMISHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA 2026 CHINANGALI PARK JIJINI DODOMA
08/06/2026
NAIBU KATIBU MKUU UTUMISHI AWATAKA WATUMISHI WA UMMA KUWA MABALOZI WA HUDUMA BORA KWA WANANCHI
Na Antonia Mbwambo-Dodoma
Tarehe 8 Juni, 2026
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Xavier Daudi amewataka Watumishi wa Umma kuendelea kuzingatia maadili ya kazi, kuwa na tabia njema na kuwahudumia wananchi kwa weledi ili kuongeza ufanisi wa huduma za umma utakaochangia katika utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.
Bw. Daudi ametoa rai hiyo wakati akihitimisha mada ya mafunzo kuhusu Usimamizi wa Utendaji Kazi yaliyotolewa kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kiutendaji watumishi hao Juni 8, 2026 katika eneo maalumu la Ofisi hiyo Mtumba jijini Dodoma.
Bw. Daudi alisema, mafanikio ya Taasisi za Umma hayapimwi tu kwa utekelezaji wa Mipango na Sera, bali pia kwa namna Watumishi wanavyowahudumia Wananchi wanaowategemea katika kupata huduma. Alisisitiza kuwa tabia njema, uadilifu na uwajibikaji ni sifa muhimu zinazopaswa kuonekana kwa kila Mtumishi wa Umma.
“Tunapaswa kutambua kuwa kila Mwananchi anayefika kupata huduma ni mteja muhimu wa Serikali. Jukumu letu ni kuhakikisha anahudumiwa kwa heshima, usikivu na kwa wakati. Hii ndiyo njia bora ya kujenga imani ya Wananchi kwa Taasisi za Umma na kuimarisha utawala bora,” Bw. Daudi alisema.
Aliongeza kuwa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 inalenga kuwa na taifa lenye maendeleo jumuishi, uchumi imara na huduma bora za kijamii, hali ambayo inahitaji Watumishi wa Umma kuwa sehemu ya mabadiliko hayo kwa kuzingatia maadili na kuongeza ufanisi katika kazi zao.
Kwa upande wake mwezeshaji kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Oswin Mkinga, alieleza kuwa usimamizi wa utendaji kazi ni muhimu katika kuboresha matokeo ya Taasisi za Umma kwa kuwa utendaji bora huanza kwa upangaji mzuri wa malengo, ufuatiliaji wa utekelezaji wake na tathmini ya mara kwa mara ili kubaini mafanikio na maeneo yanayohitaji maboresho.
Bw. Mkinga alisisitiza kuwa, usimamizi wa utendaji kazi ni chombo muhimu katika kuimarisha uwajibikaji wa Watumishi na kuongeza thamani ya huduma zinazotolewa kwa Wananchi hivyo, ni lazima kila mtumishi akaelewa mchango wake katika kufanikisha malengo ya taasisi na taifa kwa ujumla.
04/06/2026
UTAWALA BORA NA USIMAMIZI MAKINI WA RASILIMALIWATU NI MSINGI WA UTUMISHI WA UMMA WENYE MATOKEO – MHE. QWARAY
Na Antonia Mbwambo –Dodoma
Tarehe 3 JUNI, 2026
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray, amewataka Wakuu wa Idara na Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu Serikalini kuhakikisha wanakuwa mstari wa mbele katika kusimamia haki, uwajibikaji na uzingatiaji wa sheria katika Utumishi wa Umma ili kuongeza ufanisi wa utoaji wa huduma kwa wananchi.
Mhe. Qwaray ameyasema hayo Juni 3, 2026 wakati akifunga Kikao Kazi cha Wakuu wa Idara na Vitengo vya Utawala na Usimamizi waRasilimaliwatu Serikalini kilichowakutanisha viongozi kutoka Wizara, Wakala, Taasisi za Umma, Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa Jijini Dodoma.
Amesema, mafanikio ya Serikali yanategemea kwa kiwango kikubwa ubora wa usimamizi wa rasilimaliwatu.
“Rasilimaliwatu ndiyo injini ya maendeleo ya taifa; isimamiwe kwa weledi, haki na uwajibikaji.” – Mhe. Regina Qwaray alisema.
Aidha Mhe. Qwaray alibainisha kuwa Serikali imeendelea kupokea malalamiko yanayohusiana na ucheleweshaji wa kupandishwa vyeo, malipo ya stahili za watumishi na ukiukwaji wa taratibu za kiutumishi, hivyo kuwataka wataalamu wa Utawala na Rasilimaliwatu kuwa washauri waaminifu kwa viongozi wao na walinzi wa utawala wa sheria katika taasisi wanazozihudumia.
Pia alisisitiza umuhimu wa kuzingatia maadili ya utumishi wa umma, matumizi salama ya teknolojia na ulinzi wa taarifa za Serikali, huku akitoa wito kwa waajiri kuwajengea watumishi uwezo kuhusu matumizi sahihi ya Akili Unde (AI) na mifumo ya kidijiti.
Katika kuongeza ufanisi wa utendaji kazi, aliagiza utekelezaji wa Mfumo wa e-Utendaji usimamiwe kwa ukaribu zaidi, na kwamba wasimamizi watakaoshindwa kutekeleza wajibu wao wa kutathmini utendaji wa watumishi wachukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu za Utumishi wa Umma.
Ameongeza kuwa kufungwa kwa kikao hicho hakumaanishi mwisho wa juhudi za kuboresha Utumishi wa Umma, bali ni hatua ya kuanza kutekeleza kwa vitendo maazimio na maelekezo yaliyokubaliwa.
“Kumalizika kwa kikao hiki si mwisho wa kazi, bali ni mwanzo wa utekelezaji wa maazimio na maelekezo yaliyotolewa kwa lengo la kujenga Utumishi wa Umma sikivu, jumuishi, na wenye matokeo,” alisisitiza Mhe. Qwaray.
Kwa upande wake Katibu Mkuu-UTUMISHI Bw. Juma Mkomi amesema ni matarajio yake kuwa kikao hicho kitaleta matokeo chanya kwa viongozi hao yatakayoboresha utekelezaji wa majukumu na kuongea tija katika utumishi wa umma.
03/06/2026
Kikao kazi cha siku tatu cha Wakuu wa Idara na Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu Serikalini kinahitimishwa leo tarehe 3 Juni, 2026 jijini Dodoma na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray.
Kikao Kazi hicho kilifunguliwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete ambapo katika siku hizo tatu washiriki wamepewa uelewa wa namna ya kuimarisha utawala na usimamizi wa rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma.
02/06/2026
KIKAO KAZI CHA WAKUU WA IDARA NA VITENGO VYA UTAWALA NA USIMAMIZI WA RASILIMALIWATU KATIKA WIZARA NA IDARA ZINAZOJITEGEMEA, WAKALA WA SERIKALI, TAASISI NA MASHIRIKA YA UMMA, SEKRETARIETI ZA MIKOA NA MAMLAKA YA SERIKALI ZA MTAA
02/06/2026
WEBINAR JUNE 2, 2026
02/06/2026
IDHIWANI: SERIKALI YALIPA ZAIDI YA BILIONI 24 MADAI YA WATUMISHI
Aonya Watumishi wanaoghushi barua za uhamisho, Asema 6 mbaroni kesi uhujumu uchumi
Na. Jawadu Kinyobwa
Serikali imeendelea kuboresha ustawi wa watumishi wa umma kwa kulipa malimbikizo ya mishahara yenye thamani ya Tsh. Bilipni 24,699,256,645.7 na kulipa watumishi 1,249 waliokoma utumishi yenye thamani ya zaidi ya Tsh. Bilioni 5,548,386,177.90.
Hayo yamebainishwa Juni Mosi, 2026 Mabele Hall jijini Dodoma na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete (Mb) katika ufunguzi wa kikao kazi cha Wakuu wa Idara na Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Wizara na Idara zinazojitegemea, Wakala wa Serikali, Taasisi na Mashirika ya Umma, Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka ya Serikali za Mtaa.
Pamoja na maboresho hayo, Mhe. Ridhiwani amesema wapo baadhi ya waajiri ambao hawatekelezi ipasavyo wajibu wao katika kushughulikia madai ya aina hiyo ambapo hadi kufikia Mei 28,2026 madai ya watumishi 18,021 yenye jumla ya Shilingi 50,917,523,216 hayajawasilishwa Ofisini kwake.
“Baadhi ya waajiri wamekuwa wakiwasilisha katika Ofisi hii madai yenye kasoro ambazo walipaswa kuzibaini kabla hawajayawasilishwa. Vile vile, yapo madai ya malimbikizo ya mshahara yanayotokana na waajiri kutozingatia Sheria, Kanuni na Taratibu katika uendeshaji wa mashauri ya kinidhamu na hivyo kuzalisha madeni makubwa kwa Serikali” amesema.
Katika hatua nyingine, Mhe. Ridhiwani ametoa onyo kali kwa waajiri na viongozi wa taasisi za umma wanaokiuka sheria na taratibu za kiutumishi hususani kwa Waajiri kuchagua aina ya watu wa kufanya nao kazi, kutopokea watumishi wanaohamishiwa kwenye Taasisi zao, Waajiri kujimilikisha Taasisi na kuficha barua zenye maelekezo mahsusi ikiwemo barua za uhamisho.
Sambamba hayo, amesema Ofisi yake kwa kushirikiana na Taasisi za Haki Jinai imeanza kuchukua hatua mbalimbali kwa watumishi wanaojihusisha na ukiukwaji wa maadili ikiwemo kughushi barua za Ofisi hiyo ambapo hadi sasa jumla ya watuhumiwa Sita wamefikishwa mahakamani kwa makosa ya Uhujumu Uchumi na kesi zinaendelea.
Awali akizungumza Katibu Mkuu Ofisi hiyo Juma Mkomi, amesema kikao hicho kimeandaliwa mahsusi kwa lengo la kutathmini nafasi ya wasimamizi wa Utawala na Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma, kubadilishana uzoefu katika kuboresha ufanisi wa utekelezaji wa majukumu ya Serikali hususan katika Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma hasa tunapoelekea kwenye utekelezaji wa Dira Mpya ya Taifa ya 2050.
Pia, Mkomi amesema kikao hicho kitajikita zaidi katika kujadili masuala muhimu ya Usimamizi wa Utumishi wa Umma, Usimamizi na matumizi ya Mifumo ya TEHAMA Serikalini, changamoto zilizopo katika utekelezaji wa majukumu ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu na namna bora ya kukabiliana nazo.
Kikao kazi hicho kina kauli mbiu isemayo “Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma Sikivu, Jumuishi, Wenye Matokeo na Uwajibikaji kuelekea Dira 2050”.
28/05/2026
FAIDA ZA KUVAA BEJI KWA WATUMISHI WA UMMA
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Contact the organization
Telephone
Website
Address
670
Dodoma