Nactvet

Nactvet

Share

Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi

Photos from Nactvet 's post 16/06/2023

NACTVET kupitia Kurugenzi ya Udahili, Utahini na Utunuku imeendesha mafunzo ya siku mbili kwa maafisa mitihani wa kanda ya Kati na Kaskazini, kuanzia tarehe 15 na 16 Juni, 2023,Jijini Dodoma na Arusha.

Mafunzo hayo yamelenga kuwajengea uwezo Maafisa Mitihani wa Vyuo vya Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi ili kuwaongezea umahiri katika utendaji wa kazi zao. Mafunzo pia yalilenga kutatua changamoto mbalimbali zinazohusu uendeshaji wa mitihani.

Mkurugenzi wa Udahili, Utahini na Utunuku , Dkt. Marcelina Baitilwake, ameongoza mafunzo hayo akishirikiana na Meneja, Bw. Twaha Twaha na wakuu wa vitengo vya Kurugenzi hiyo.

Mafunzo hayo yameratibiwa kwa kuzingatia kanda na Bodi za Masomo.

Mafunzo k**a hayo yanatarajiwa kufanyika katika kanda ya Mashariki mwishoni mwa mwezi Juni, 2023 na baadae kwenye kanda zilizobaki.

Photos from Nactvet 's post 12/06/2023

*Dkt.Rutayuga awataka wakuu wa vyuo binafsi kuanzisha programu zinazokidhi mahitaji ya jamii*

Katibu Mtendaji wa NACTVET, Dkt. Adolf Rutayuga amewataka wakuu wa vyuo binafsi vya elimu na mafunzo ya ufundi stadi kuanzisha programu zinazokidhi mahitaji mbalimbali kwenye jamii.

Dkt. Rutayuga ameyasema hayo wakati akifungua awamu ya pili ya mafunzo kwa wamiliki na wakuu wa vyuo binafsi vya Mafunzo ya Ufundi Stadi kutoka Kanda ya Kusini na Kanda ya Nyanda za Juu Kusini leo tarehe 12 Juni, 2023 mjini Morogoro.

‘’Lengo la mafunzo haya ni kuwajengea uwezo wakuu na wamiliki wa vyuo binafsi katika utoaji wa mafunzo ili kusaidia katika kukidhi mahitaji ya jamii na kutoa wataalam wenye ujuzi na umahiri’’alisema Dkt. Rutayuga

Aliongeza kuwa, nia ya Baraza ni kuvisaidia na kuvilea vyuo hivyo ili viweze kufikia malengo huku akiwasihi wamiliki/wakuu wa vyuo kufuata sheria, kanuni na taratibu za NACTVET ikiwa ni pamoja na kufanyia kazi mapungufu yaliyoainishwa vyuoni mwao ili kuendana na ubora unaohitajika.

Naye Bw. Nurudini Nhuva,(Mkurugenzi - Quality Development College) kwa niaba ya washiriki, amepongeza NACTVET kwa kuandaa mafunzo hayo yaliyowaleta pamoja na kusikiliza changamoto zao kwa maendeleo ya Elimu ya Ufundi Stadi nchini huku akiwashauri washiriki wengine kufuata Kanuni na taratibu zilizowekwa na NACTVET.

Miongoni mwa watumishi wa NACTVET walioshiriki katika kutoa mafunzo hayo ni pamoja na Dkt. Alex Nkondola, Mkurugenzi(Huduma za Taasisi),Dkt.Amani Makota, Mkurugenzi(Huduma za uendeshaji vyuo),Dkt. Hirst Ndisa(Meneja Kanda ya kusini) na Bw. Joha Fugutilo(Meneja Kanda ya Nyanda za Juu Kusini).

NACTVET ina jumla ya vyuo 1329 (VET- 805, TET- 465, FDC- 55) vya elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi inavyovisimamia nchini.

Photos from Nactvet 's post 11/06/2023

with .repost
・・・
WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA VYUO VYA KATI

Wanafunzi 58,298 wakiwemo wasichana 18,166 na wavulana 40,132 sawa na asilimia 31 wamepangiwa kujiunga kwenye kozi mbalimbali za stashahada katika vyuo vya kati vinavyosimamiwa na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTVET).

Wanafunzi 1,645 wakiwemo wasichana 646 na wavulana 999 wamechaguliwa kujiunga na vyuo vya Ualimu ngazi ya Stashahada ya Sayansi, Hesabu na TEHAMA

Wanafunzi 1,877 wakiwemo wasichana 757 na wavulana 1,120 wamechaguliwa kujiunga na fani mbalimbali katika vyuo 04 vya Elimu ya Ufundi ambavyo ni Chuo cha Ufundi Arusha (ATC), Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST) na Chuo cha Usimamizi na Maendeleo ya Maji (WDMI).

Wanafunzi 1,842 wakiwemo wasichana 943 na wavulana 899 wamechaguliwa kujiunga na Vyuo vya Afya ngazi ya Stashahada.

Wanafunzi 52,934 wakiwemo wasichana 15,820 na wavulana 37,114 wamechaguliwa kujiunga kwenye kozi mbalimbali zikiwemo za Kilimo, Ufugaji, Utawala, Biashara na zinginezo za Stashahada katika vyuo vya kati mbalimbali nchini.

11/06/2023

Tujikumbushe maonesho yetu

Photos from Nactvet 's post 10/06/2023

Mafunzo yanaendelea…

08/06/2023
27/05/2023

Dirisha la udahili kufunguliwa rasmi

Photos from Nactvet 's post 11/05/2023
Want your school to be the top-listed School/college in Dodoma?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Telephone

Website

Address


17007 Mwangosi Road
Dodoma
41110