Wasafi FM

Wasafi FM

Share

The leading radio station in Tanzania specializing in the latest music & entertainment news.

12/06/2026

AMBAO HAWAJARIPOTI JKT WAITWA KWA MARA YA MWISHO

Baadhi ya vijana waliochaguliwa kujiunga na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) lakini wakashindwa kuripoti kwa wakati kutokana na changamoto mbalimbali, wamepewa fursa ya mwisho ya kujiunga na mafunzo hayo kwa kuripoti katika makambi yaliyo karibu na maeneo wanayoishi.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mkuu wa Tawi la Operesheni na Mafunzo JKT Brigedia Jenerali Peter Mnyani, amesema utaratibu huo umeelekezwa na Mkuu wa JKT, Meja Jenerali Rajabu Mabele, ili kutoa nafasi kwa vijana ambao walikwama kufika katika makambi waliyopangiwa awali.

Afande Mnyani amesema vijana hao wanatakiwa kuripoti kuanzia Juni 12 hadi Juni 15, 2026, katika makambi ya JKT yaliyo karibu na maeneo yao ya makazi ili kuendelea na mafunzo k**a ilivyopangwa.

Hata hivyo, amefafanua kuwa utaratibu huo hauhusishi Kambi ya Ruvu JKT iliyopo Mlandizi mkoani Pwani, Kambi ya Makutupora JKT iliyopo mkoani Dodoma pamoja na Chuo cha Uongozi cha JKT kilichopo Kimbiji jijini Dar es Salaam.

Amesisitiza kuwa vijana wote ambao bado hawajaripoti wanapaswa kutumia fursa hiyo ya mwisho kufika makambini ndani ya muda uliotolewa, kwani baada ya Juni 15 hakutakuwa na muda mwingine wa nyongeza wa kuripoti.

Ngonya

12/06/2026

MKUU wa Wilaya ya Temeke, Sixtus Mapunda, amesema ameridhishwa na maandalizi ya Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF), maarufu k**a SabaSaba, yanayotarajiwa kuanza rasmi Juni 28 mwaka huu, huku akitoa wito kwa wananchi wa Jiji la Dar es Salaam na mikoa ya jirani kujitokeza kwa wingi kushiriki katika maonesho hayo ya kihistoria yanayotimiza miaka 50 tangu kuanzishwa kwake.

Mapunda alitoa kauli hiyo Juni 12 jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea mabanda mbalimbali katika viwanja vya maonesho, ambapo amesema maandalizi yanaendelea vizuri na yanaendana na hadhi ya maadhimisho ya jubilei ya miaka 50 ya Sabasaba.

Amesema maonesho ya mwaka huu yatakuwa ya kipekee kwa kuwa yatatoa fursa kwa wananchi kujionea maendeleo katika sekta za biashara, uwekezaji na utalii, sambamba na kusherehekea historia ya maonesho hayo ambayo yamekuwa chachu ya maendeleo.

Aidha, Mapunda amezitaka taasisi na ofisi zote za Serikali kuhakikisha mabanda yao yanakamilika ifikapo Juni 20 ili wageni na washiriki watakaofika kwenye maonesho hayo washuhudie maandalizi bora yanayoakisi hadhi ya maadhimisho hayo muhimu.

Kwa upande wake, Dkt Latifa Khamis Mkurugenzi Mkuu wa TANTARADE amesema taasisi hiyo imejipanga kuhakikisha maonesho ya mwaka huu yanakuwa makubwa na ya aina yake kwa kutoa fursa za biashara, uwekezaji, burudani na kujifunza kwa wananchi, wazalendo na wadau mbalimbali wa maendeleo.

Amesema hadi sasa nchi 23 zimethibitisha ushiriki wao katika maonesho hayo, huku makampuni 256 ya kimataifa yakionesha nia ya kushiriki na zaidi ya makampuni 2,776 ya ndani yakijiandikisha kushiriki, jambo linalotarajiwa kuongeza ushindani na fursa za kibiashara kwa washiriki kutoka ndani na nje ya Tanzania.

Aidha, maonesho hayo yatapambwa na programu mbalimbali zikiwemo “Usiku wa Kash Kash”, matembezi maalumu ya kuhamasisha matumizi ya bidhaa za Made in Tanzania pamoja na hafla ya Golden Jubilee itakayofanyika Julai 7 kwa ajili ya kutambua na kuwatunuku wadau waliotoa mchango mkubwa katika maendeleo ya Maonesho ya Sabasaba kwa kipindi cha miaka 50.

12/06/2026

Akizungumza na waandishi wa Habari leo Juni 12,2026, Katibu Mkuu wa Baraza la Taifa la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NaCoNGO), Francisca Damian, amesema maandalizi ya jukwaa hilo yanafanyika kwa ushirikiano na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum.

Amesema kaulimbiu ya mwaka huu ni “Fikra Mpya Kuhusu Uendelevu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali: Ubunifu, Ubia na Upatikanaji wa Rasilimali Fedha Kupitia Vyanzo vya Ndani,” ikilenga kuhimiza ubunifu, ushirikiano na kuongeza uwezo wa mashirika hayo kujitegemea kifedha.

Kwa mujibu wa Francisca, jukwaa hilo litawakutanisha viongozi na watendaji wa mashirika yasiyo ya kiserikali, taasisi za serikali, sekta binafsi, washirika wa maendeleo, taasisi za utafiti, vyombo vya habari na wananchi kujadili namna ya kuifanya sekta hiyo kuwa imara, yenye uwajibikaji na mchango mkubwa katika utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

Amesema mjadala utaweka mkazo katika kupunguza utegemezi wa ufadhili wa nje kwa kuimarisha vyanzo vya ndani vya mapato, kukuza ubia na sekta binafsi, kutumia teknolojia na ubunifu pamoja na kuendeleza mifumo madhubuti ya uwazi na uwajibikaji.

Mbali na mijadala, jukwaa litatoa fursa ya kuonesha mafanikio yaliyofikiwa, changamoto zinazoikabili sekta na fursa mbalimbali za kuimarisha shughuli za mashirika yasiyo ya kiserikali nchini.

Washiriki wanatarajiwa kutoka ndani na nje ya Tanzania, ikiwemo ukanda wa Afrika Mashariki, ambapo maazimio na mapendekezo yatakayopatikana yanatarajiwa kuboresha mazingira ya utendaji wa mashirika hayo na kuimarisha ushirikiano wa kimkakati kati ya wadau.

Francisca amesema kabla ya jukwaa la kitaifa kutafanyika majukwaa ya ngazi ya wilaya mwezi Juni na Julai, pamoja na ya mikoa kati ya Agosti na Septemba 2026, kwa lengo la kukusanya maoni na mapendekezo yatakayowasilishwa katika mkutano mkuu.

Aidha, NaCoNGO imetoa wito kwa mashirika yasiyo ya kiserikali, taasisi za serikali, sekta binafsi, washirika wa maendeleo, vyombo vya habari na wananchi kushiriki kikamilifu katika jukwaa hilo, ikisisitiza kuwa sekta hiyo imeendelea kuwa mshirika muhimu wa Serikali katika elimu, afya, uwezeshaji wa wanawake na vijana pamoja na ustawi wa jamii.

Francisca amehitimisha kwa kueleza kuwa Jukwaa la Mwaka la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali 2026 litakuwa fursa ya kutafakari mafanikio yaliyopita, hali ya sasa na mwelekeo wa baadaye wa sekta hiyo, huku NaCoNGO ikiendelea kushirikiana na wadau kuhakikisha maandalizi yanafanyika kwa weledi na kufanikisha malengo yaliyokusudiwa.

12/06/2026

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeomba kuendelezwa kwa ushirikiano kati ya Tanzania na Ireland kupitia utekelezaji wa Awamu ya Pili ya Mradi wa Maziwa Faida kuanzia mwaka 2027 hadi 2032, ili kuendeleza mafanikio yaliyopatikana katika kuongeza uzalishaji wa maziwa, kuboresha tija na kuinua maisha ya wafugaji nchini.

Ombi hilo limetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dkt. Fabian Madele, wakati akifungua rasmi Maonesho ya Ubunifu na Teknolojia katika Sekta ya Maziwa (TALIRI Open Day 2026) yaliyofanyika katika Kituo cha Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) Kanda ya Mashariki, jijini Tanga.

Dkt. Madele alisema Mradi wa Maziwa Faida unaotekelezwa kwa ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania kupitia TALIRI na Taasisi ya Maendeleo ya Kilimo na Chakula ya Ireland (TEAGASC), kwa ufadhili wa Serikali ya Ireland kupitia Ubalozi wake nchini Tanzania, umeleta mabadiliko makubwa katika sekta ya maziwa, hasa Mkoa wa Tanga.

Alieleza kuwa kabla ya kuanza kwa mradi huo, wafugaji wengi walikuwa wakizalisha wastani wa lita tatu hadi tano za maziwa kwa ng’ombe mmoja kwa siku. Hata hivyo, kupitia matumizi ya teknolojia bora za ufugaji, malisho ya kisasa, huduma za ugani zilizoimarishwa pamoja na mafunzo kwa wafugaji, uzalishaji umeongezeka hadi wastani wa lita 15 kwa ng’ombe mmoja kwa siku katika maeneo mengi yaliyofikiwa na mradi.

“Matokeo haya yanaonesha wazi mchango mkubwa wa utafiti, ubunifu na ushirikiano wa kimataifa katika kuongeza tija, kuboresha kipato cha wafugaji na kuimarisha usalama wa chakula na lishe nchini,” alisema Dkt. Madele.

Aidha, alisema Tanzania kwa sasa inazalisha takribani lita bilioni 4.1 za maziwa kwa mwaka huku mahitaji ya taifa yakikadiriwa kufikia lita bilioni 13 kwa mwaka, hali inayoashiria uwepo wa fursa kubwa ya kuwekeza zaidi katika sekta ya maziwa ili kupunguza pengo la uzalishaji na kuongeza mchango wa sekta hiyo katika uchumi wa taifa.

Kwa upande wake, Mwakilishi wa Balozi wa Ireland nchini Tanzania, Bi. Suzanne Keatinge, aliipongeza TALIRI kwa utekelezaji mzuri wa mradi huo na kuwatambua watafiti, maafisa ugani pamoja na wadau mbalimbali waliochangia mafanikio yake.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa TALIRI, Prof. Erick Komba, aliishukuru Serikali ya Ireland kwa ufadhili wake na kueleza kuwa mafanikio yaliyopatikana katika Awamu ya Kwanza ya Mradi wa Maziwa Faida (2021/2022–2025/2026) yameweka msingi imara wa kuendelea kuleta mageuzi chanya katika sekta ya maziwa nchini.

Prof. Komba alisema TALIRI itaendelea kuhakikisha kuwa matokeo ya tafiti, ubunifu na teknolojia zilizozalishwa kupitia mradi huo zinawafikia wafugaji wengi zaidi ili kuongeza uzalishaji, tija na ushindani wa sekta ya maziwa.

Aliongeza kuwa mradi huo uliogharimu zaidi ya Euro milioni 3, sawa na zaidi ya Shilingi bilioni 7 za Kitanzania, umenufaisha zaidi ya wanawake na vijana 3,000 katika ukanda wa pwani ya mashariki, hususan Wilaya ya Muheza mkoani Tanga.

Kwa mujibu wa Prof. Komba, mafanikio mengine ya mradi huo ni pamoja na kufanya tafiti za malisho bora yanayostahimili mazingira ya ukanda wa pwani, kubaini aina bora za ng’ombe wa maziwa, kuwajengea uwezo maafisa ugani, kutoa mafunzo kwa wafugaji, kuimarisha vyama vya ushirika vya wafugaji, kuboresha miundombinu ya utafiti na kuanzisha mashamba darasa yanayotumika kusambaza teknolojia za kisasa za ufugaji.

Mradi wa Maziwa Faida umetajwa kuwa mfano wa mafanikio wa ushirikiano wa maendeleo unaochochea matumizi ya utafiti, ubunifu na teknolojia katika kutatua changamoto za uzalishaji wa maziwa na kuchangia ukuaji endelevu wa sekta ya mifugo nchini Tanzania.

12/06/2026

KOMBE LA DUNIA FIFA 2026 LASOGEZWA KARIBU NA MASHABIKI TANZANIA

12/06/2026

Mfanyabiashara maarufu nchini na mmiliki wa Simba Logistics, Azim Dewji, amesema kuwa ulipaji wa Tozo ya Maendeleo ya Miundombinu ya Bandari ni hatua muhimu inayowezesha serikali kuendelea kuwekeza katika kuboresha na kupanua miundombinu ya usafirishaji na uchukuzi nchini.

Akizungumza kuhusu umuhimu wa tozo hiyo, Dewji alieleza kuwa maendeleo ya bandari yanahitaji uwekezaji mkubwa wa fedha ambao hauwezi kutegemewa na serikali pekee k**a ilivyokuwa katika miaka ya nyuma. Alibainisha kuwa katika mazingira ya sasa ya uchumi wa soko, ni muhimu kuwepo kwa vyanzo endelevu vya mapato vitakavyosaidia kufadhili miradi ya kimkakati ya maendeleo.

Alitolea mfano maboresho yaliyofanyika katika Bandari za Tanga na Mtwara, ambapo yameongeza uwezo wa kuhudumia mizigo na kuchochea ukuaji wa biashara. Kwa mujibu wake, mafanikio hayo yameonyesha kuwa uwekezaji katika miundombinu ya bandari una matokeo chanya kwa uchumi wa taifa na ukuaji wa sekta binafsi.

Dewji alisema kuwa ongezeko la biashara na mizigo inayopita katika bandari za Tanzania linaendelea kuongezeka kwa kasi, jambo linalohitaji uwekezaji wa mara kwa mara katika upanuzi wa miundombinu ili kukidhi mahitaji ya sasa na ya baadaye. Alisisitiza kuwa mapato yatokanayo na tozo hiyo yanaweza kusaidia kujenga na kuboresha bandari mpya, kupanua zilizopo pamoja na kuimarisha miundombinu inayounganisha bandari na maeneo ya uzalishaji na matumizi.

“Bandari pekee haitoshi k**a hakuna barabara, reli na miundombinu mingine ya kuiwezesha kufanya kazi kwa ufanisi. Hivyo, mapato yanayotokana na tozo hizi yana mchango mkubwa katika kuimarisha mifumo yote ya usafirishaji na uchukuzi ambayo ndiyo msingi wa ukuaji wa uchumi,” alisema.

Aidha, alieleza kuwa manufaa ya tozo hiyo hayaishii katika sekta ya bandari pekee, bali yanaweza kuchangia pia kuboresha huduma za jamii k**a afya, elimu na maendeleo mengine ya kijamii kupitia mapato yanayoongezeka kutokana na ukuaji wa biashara na ukusanyaji wa kodi.

Kwa ujumla, Tozo ya Maendeleo ya Miundombinu ya Bandari ni uwekezaji wa muda mrefu unaolenga kuongeza ushindani wa bandari za Tanzania, kukuza biashara ya ndani na nje ya nchi, kuvutia uwekezaji na kuimarisha ustawi wa wananchi kupitia maendeleo ya uchumi wa taifa.

12/06/2026

Vijana wametakiwa kutumia fulsa ya tamasha la kuinua vipaji la Twenzetu kwa Yesu 2026 ili kusaidia kubadili mitazamo yao yakubaliane na matarajio na matakwa juu ya mungu na watu bila ya kujali itikadi zao za kidini.

Akizungumza hayo leo Juni 11, jijini dar es salaam, Naibu Katibu Mkuu wa Kanisa la KKKT DMP, mchungaji Wilbroad Mastai amesema katika tamasha hilo wanaoalikwa sio wakristo ila ni jamii kwa ujumla kwakuwa vijana ni nguvu ya taifa.

Kwa upande wa Mkuu wa Idara ya Mission Uinjirist wa Diak**a KKKT DMP, Henry Mwinuka ameomba wazazi na walezi kuwaleta watoto katika tamasha hilo ili waweze kufahamiana na kuonesha vipaji vyao.

12/06/2026

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, ameagiza Jeshi la Polisi Wilaya ya Kigamboni kumk**ata kwa kumshikilia Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Lingato, Kata ya Kisarawe II, Cosma Kulwa maarufu k**a Kalimanzira, kwa tuhuma za kuuza viwanja mara mbili na kusababisha migogoro ya ardhi kwa wakazi wa eneo hilo.

Chalamila alitoa agizo hilo leo wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo, kusikiliza na kutatua kero za wananchi katika Wilaya ya Kigamboni.

Akiwa katika Mtaa wa Kichangani akitatua mgogoro wa ardhi unaohusisha zaidi ya familia 23 na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA), mwananchi mmoja aliyefahamika kwa jina la Hassan alijitokeza na kutoa malalamiko dhidi ya mwenyekiti huyo, akimtuhumu kumuuzia eneo la ekari moja ambalo baadaye lilidaiwa kuuzwa kwa mtu mwingine.

Kwa mujibu wa madai yaliyotolewa na wananchi, mwenyekiti huyo amekuwa akihusishwa na uuzaji wa viwanja vyenye migogoro pamoja na viwanja ambavyo tayari vilikuwa vimeuzwa kwa wanunuzi wengine, hali inayodaiwa kuchangia kuongezeka kwa migogoro ya ardhi katika eneo hilo.

Baada ya kushindwa kutoa maelezo ya kuridhisha kuhusu nyaraka za mauziano zinazodaiwa kuhusika katika sakata hilo, Chalamila aliamuru ak**atwe mara moja na kuwekwa mahabusu.

"Ak**atwe na akawekwe mahabusu mpaka kesho. Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, kesho itisha mkutano wa hadhara wa wananchi. Huyu mwenyekiti kesho atoke mahabusu akiwa na pingu ahudhurie mkutano huo. Amesema Chalamila

11/06/2026

Tanzania imeendelea kuimarisha nafasi yake katika soko la utalii Afrika baada ya kupokea kundi la watalii 50 kutoka nchini Nigeria waliokuja nchini kwa ajili ya kutembelea na kufurahia vivutio mbalimbali vya utalii.

Madina Mwaibula, Mkurugenzi Msaidizi wa Utalii na Utamaduni katika Taasisi ya Maendeleo ya Utalii na Utamaduni (DITEC), amesema ujio wa watalii hao ni sehemu ya jitihada za kuendelea kuitangaza Tanzania k**a eneo salama na lenye vivutio vya kipekee kwa wageni kutoka mataifa mbalimbali.

Amesema watalii hao watapata fursa ya kutembelea maeneo mbalimbali ikiwemo Hifadhi za Ngorongoro na Tarangire pamoja na visiwa vya Zanzibar, ambako watajionea mandhari, utamaduni na uzuri wa asili wa Tanzania.

Mwaibula amesisitiza kuwa Tanzania ni salama kwa wageni na wataendelea kutumia mikakati mbalimbali kuwavutia watalii wengi zaidi kutoka ndani na nje ya Afrika.

11/06/2026

ZANZIBAR YAWASILISHA BAJETI YA KIHISTORIA YA SHILINGI TRILIONI 8.5 KWA MWAKA WA FEDHA 2026/2027

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imewasilisha makadirio ya Bajeti Kuu ya Serikali ya shilingi trilioni 8.5 kwa mwaka wa fedha 2026/2027, kiwango kinachotajwa kuwa cha kihistoria kutokana na ongezeko kubwa la fedha zilizotengwa kwa utekelezaji wa shughuli za maendeleo na huduma za kijamii.

Bajeti hiyo iliyowasilishwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Juma Malik Akil, katika kikao cha Baraza la Wawakilishi, imeongezeka kwa asilimia 22.1 ikilinganishwa na bajeti ya mwaka wa fedha 2025/2026 iliyokuwa shilingi trilioni 6.9.

Akiwasilisha bajeti hiyo, Dkt. Akil amesema Serikali imejielekeza katika kuimarisha ustahamilivu wa uchumi kupitia ongezeko la mapato ya ndani, matumizi ya teknolojia za kidijitali na kuendelea kutekeleza mageuzi yatakayochochea ukuaji wa uchumi na kuboresha maisha ya wananchi.

Amesema bajeti ya mwaka huu imebeba kaulimbiu isemayo “Kuimarisha Ustahamilivu wa Uchumi kupitia Mapato ya Ndani na Mageuzi ya Kidijitali”, ikilenga kuongeza ufanisi katika ukusanyaji wa mapato, kuimarisha mazingira ya biashara na uwekezaji pamoja na kuharakisha utoaji wa huduma kwa njia za kidijitali.

Waziri huyo ameeleza kuwa Serikali itaendelea kuwekeza katika sekta za uzalishaji, miundombinu, huduma za kijamii na mifumo ya kidijitali ili kuimarisha uchumi wa Zanzibar na kuhakikisha wananchi wananufaika zaidi na matunda ya maendeleo.

Bajeti hiyo sasa itajadiliwa na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kabla ya kupitishwa kwa ajili ya utekelezaji katika mwaka wa fedha unaoanza Julai Mosi, 2026.

cc:

Want your business to be the top-listed Media Company in Dar es Salaam?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Category

Address


Mbezi Beach
Dar Es Salaam