Yuzzo Jr
Asante kwa kutembelea ukurasa wetu wa habari za michezo za uhakika na makala kuhusu soka saa 24. sports
02/10/2026
🇹🇿 Tanzania U17 imeshinda bao 1-0 dhidi ya China 🇨🇳 kwenye mechi ya kirafiki pale Vertex Cup London siku ya jana. ✌️⚽
02/10/2026
Shirikisho la soka la Ghana limevunja mkataba na kocha wa timu ya taifa, Carlos Queiroz, baada ya timu hiyo kuanza vibaya kampeni ya kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027.
Ghana imepoteza mechi zake mbili za kwanza katika Kundi C, ikifungwa 2-0 na Ivory Coast na 4-2 na Gambia.
Matokeo hayo yameiacha timu hiyo mkiani mwa kundi na katika hatari ya kukosa AFCON kwa mara ya pili mfululizo.
Katika taarifa, Shirikisho hilo limesema limefikia uamuzi wa kusitisha mkataba huo kwa kuzingatia maslahi ya soka la Ghana.
Queiroz amesema alifika Ghana akiwa na lengo la kujenga msingi imara kwa ajili ya mustakabali wa timu hiyo, lakini matokeo ya hivi karibuni na mazingira yaliyokuwepo yamechangia uamuzi wa kumaliza ushirikiano huo.
02/10/2026
Rais wa Paris Saint-Germain (PSG), Nasser Al-Khelaïfi, ametangaza kuwa hatagombea urais wa FIFA katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Machi 18, 2027, mjini Rabat, Morocco.
Al-Khelaïfi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa European Football Clubs (EFC) na Mjumbe wa Kamati Tendaji ya UEFA, alikuwa ametajwa k**a mmoja wa watu walioweza kupewa nafasi ya kuwania urais huo dhidi ya Rais wa sasa wa FIFA, Gianni Infantino.
Akizungumza baada ya mkutano wa EFC mjini Copenhagen, Al-Khelaïfi alisema hana nia wala mpango wa kuwania nafasi hiyo, akisisitiza kuwa anataka kuendelea na majukumu yake katika PSG na soka la Ulaya.
“Sina kabisa nia, ajenda wala dhamira ya kuwa FIFA. Sidhani k**a mimi ndiye mtu sahihi kwa nafasi hiyo. Ninafurahia ninachokifanya. FIFA si kwa ajili yangu.”
Uamuzi huo unakuja wakati UEFA ikiendelea kutafuta mgombea wa kumpinga Infantino katika uchaguzi wa FIFA wa mwaka 2027. Rais wa UEFA, Aleksander Čeferin, ambaye pia amesema hatagombea nafasi hiyo, amekuwa akiongoza juhudi za kutafuta mbadala.
Infantino tayari amethibitisha kuwa atagombea tena urais wa FIFA, huku uchaguzi ukitarajiwa kufanyika katika Mkutano wa 77 wa FIFA tarehe 18 Machi 2027 huko Rabat, Morocco.
02/10/2026
Mchezaji wa Hull City, Lucas Gourna-Douath, amehusika katika ajali ya gari asubuhi ya leo wakati akielekea katika uwanja wa mazoezi wa klabu hiyo.
Gari la Gourna-Douath lilipinduka katika barabara iliyo karibu na eneo la mazoezi la Hull City.
Tukio hilo linakuwa la pili kwa mchezaji wa Hull City kupata ajali ya aina hiyo ndani ya kipindi cha wiki chache, baada ya mwenzake Sorba Thomas kuhusika na ajali katika barabara hiyo hiyo, ambapo gari lake aina ya Land Rover Defender lilipinduka.
Kwa mujibu wa taarifa za awali, Gourna-Douath pamoja na watu wengine waliohusika katika tukio hilo hawakupata majeraha makubwa.
02/10/2026
•MATOKEO YA SOKA JANA•
Alhamisi, October 01,2026
🌍NATIONS LEAGUE
Azerbaijan 0-0 Liechtenstein
Germany 2-0 Serbia
Denmark 2-4 Portugal
Greece 2-2 Netherlands
Wales 2-1 Norway
Ireland 2-2 Austria
Israel 0-0 Kosovo
Malta 1-1 Gibraltar
🌍AFRICA CUP OF NATIONS QUALIFIERS
Guinea 1-0 Kenya
🗺️INTERNATIONAL FRIENDLY
Maldives 0-6 Lebanon
Uzbekistan 4-1 Syria
🌍U21 EUROPEAN CHAMPIONSHIP QUALIFIERS
Greece 4-2 Latvia
North Macedonia 1-1 Montenegro
Armenia 0-1 Italy
Hungary 2-1 Lithuania
San Marino 0-13 Spain
Northern Ireland 1-1 Georgia
🇬🇭GHANA - PREMIER LEAGUE
Asante Kotoko 1-0 Karela United
🌍WOMEN'S CHAMPIONS LEAGUE
Austria Vienna 1-1 Inter
Koge 5-1 Servette
Manchester City 1-1 Real Madrid
PSG 5-0 Leuven
02/10/2026
MWANETU WAZIR JR ANAITAOA AFCON 2027:
Full Time
Mombasa United 2 : 1 Kariobangi Sharks
⚽️ Dennis Toeri
⚽️ Waziri Jr
⚽️Wyne Dalvine
Mombasa United wamepata ushindi kwenye mechi ya kwanza ya Playoffs ya kupanda au kushuka daraja ligi kuu soka nchini Kenya chini ya Kocha Adlhamid Moalin pale Mombasa.
Mechi ya marudiano itapigwa Nairobi siku ya jumanne.
01/10/2026
NGAO YA JAMII WANAWAKE 2026
Nusu fainali 1
FT’ JKT Queens 1️⃣-0️⃣ Mashujaa Queens
⚽️Fatuma Said
Nusu fainali 2
FT’ Simba Queens 3️⃣-0️⃣ Yanga Princess
⚽️Vivian Corazone
⚽️Senaf Demise
⚽️Mary Siyame
01/10/2026
•MATOKEO YA SOKA JANA•
Jumatano, September 30,2026
🌍AFRICA CUP OF NATIONS QUALIFIERS
Eritrea 0-5 South Africa
🗺️INTERNATIONAL FRIENDLY
Papua New Guinea 1-1 Solomon Islands
Fiji 2-1 New Caledonia
Seychelles 0-2 Sri Lanka
Lithuania 3-0 Andorra
🌍U21 EUROPEAN CHAMPIONSHIP QUALIFIERS
Faroe Islands 0-1 Luxembourg
Malta 1-4 Germany
Poland 3-0 Sweden
Czech Republic 1-0 Bulgaria
Romania 0-2 Finland
Kosovo 2-1 Cyprus
Scotland 5-2 Azerbaijan
Portugal 4-0 Gibraltar
🇳🇬NIGERIA - PREMIER LEAGUE
Enyimba 4-2 Shooting Stars
Katsina United 1-1 Rivers United
Sporting Lagos 0-0 Ikorodu City
Warri Wolves 0-1 Rangers International
🇬🇭GHANA - PREMIER LEAGUE
Medeama 1-0 Port City
🌍WOMEN'S CHAMPIONS LEAGUE
Roma 0-6 Barcelona
Hacken 0-3 Juventus
Paris 2-2 Arsenal
Benfica 0-3 Bayern Munchen
Lyon 0-0 Chelsea
01/10/2026
Kocha wa timu ya taifa ya Portugal, Jorge Jesus, alifika uwanja wa ndege pamoja na Rais wa Shirikisho la Soka la Portugal katika jaribio la mwisho la kumshawishi Cristiano Ronaldo abaki na timu hiyo. Ronaldo alikuwa ameondoka kwenye kambi ya Portugal nchini Denmark baada ya kutokubaliana na uamuzi wa kocha kuhusu nafasi yake kwenye kikosi.
Kwa mujibu wa taarifa hizo, Jorge Jesus na Rais huyo walimfuata Ronaldo hadi uwanja wa ndege wakijaribu kumshawishi abadili uamuzi wake na kurejea kambini. Hata hivyo, Ronaldo alisimamia uamuzi wake na kuendelea na safari yake, huku akipanda ndege na kuondoka Denmark.
Kuondoka huko kumetokea wakati ambapo Ronaldo amekuwa sehemu muhimu ya timu ya taifa ya Portugal kwa miaka mingi, hivyo tukio hilo limeibua maswali kuhusu mustakabali wa uhusiano wake na timu hiyo, hasa chini ya uongozi mpya wa Jorge Jesus.
Hadi sasa, Ronaldo hajatangaza rasmi kustaafu soka la kimataifa. Hata hivyo, mazingira ya tukio hili yameongeza mjadala kuhusu iwapo huu unaweza kuwa mwanzo wa mwisho wa Cristiano Ronaldo katika enzi yake ya Portugal, huku mashabiki wakisubiri maelezo zaidi kutoka kwake.
01/10/2026
Kagera Sugar imemtambulisha Frank Domayo kuwa kocha msaidizi namba mbili wa timu hiyo ambapo anaungana na kocha mkuu, Cedric Kaze aliyetangazwa Septemba 21, 2026 kuchua mikoba ya Juma Kaseja na Amri Kiemba aliyetangazwa leo kuwa kocha msaidizi namba moja.
Domayo anaungana na timu hiyo ikiwa tayari imecheza mechi sita za Ligi Kuu ya NBC msimu huu, ikipoteza nne na sare mbili, ikishika nafasi ya 15 kwenye msimamo ikivuna pointi mbili.
Domayo licha ya kuwa na taaluma ya ukocha pia amewahi kucheza mpira wa miguu kwa mafanikio katika klabu za Yanga, Azam FC, Namungo, JKT Ruvu, Taifa Stars na Twalipo Academy.
Pia Kagera Sugar imemtangaza Kefa Mabala kuwa mchambuzi wa video (Video analyst) wa klabu hiyo.
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Contact the business
Telephone
Website
Address
Bukoba
P.O.BOX1652BUKOBA
Alerts
Be the first to know and let us send you an email when Yuzzo Jr posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.