The Same Qualities Foundation

The Same Qualities Foundation

Share

we value the qualities of all kids

04/08/2026

Mwenyekiti wa Chama cha Waendeshaji wa Utalii Tanzania (TATO), Wilbard Chambulo, amesema Tanzania inaweza kuongeza ushindani wake katika sekta ya utalii kwa kuondoa vikwazo vinavyochelewesha safari za watalii, hususan kupitia uwekezaji katika miundombinu na kurahisisha huduma za uhamiaji.

Akizungumza katika uzinduzi wa nyenzo za utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, Chambulo alisema sekta ya utalii inategemea zaidi urahisi wa safari na uzoefu wa mgeni kuliko taratibu ndefu zinazoweza kumkatisha tamaa kabla hajafika katika vivutio vya utalii.

Alitolea mfano watalii wanaotembelea Maasai Mara nchini Kenya na baadaye kutaka kuingia Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, akisema wengi wao hulazimika kupitia Nairobi, kisha Kilimanjaro na Arusha kwaajili ya taratibu za uhamiaji kabla ya kufika Serengeti. Alisema mlolongo huo huongeza gharama na muda wa safari, hali inayoweza kuwafanya baadhi ya wageni kuahirisha au kuacha kabisa safari yao ya Tanzania.

Kwa maoni yake, kujengwa kwa Kiwanja cha ndege katika eneo la Mugumu, Mkoani Mara pamoja na kuweka huduma huduma za uhamiaji kutawezesha watalii hao kuingia moja kwa moja Serengeti kutoka Maasai Mara, hatua ambayo itapunguza usumbufu na kuongeza ushindani wa Tanzania katika soko la utalii la Afrika Mashariki.

Akihitimisha, Chambulo alisema Tanzania tayari ina vivutio vinavyotambulika kimataifa, ikiwemo Serengeti na Zanzibar, na kwamba kuboresha miundombinu pamoja na kurahisisha taratibu za kuingia nchini kutasaidia kuongeza idadi ya Watalii na mapato yatokanayo na sekta hiyo.

04/08/2026

Unaweza kufikiria duniani mtoto anaweza kumfanyia ukatili mkubwa wa kumsababishia ulemavu wa kudumu tena wenye mateso mama yake mzazi?

Simulizi hii itakutoa machozi lakini ndio ukweli halisi.

Hayo yamemtokea Sophia Hussen Amuli (72), mkazi wa Kijiji cha Chiungutwa wilayani Masasi mkoani Mtwara.

04/08/2026

MISAADA YA NJE YASHUKA HADI ASILIMIA 0.9
Katika taarifa iliyowasilishwa mbele ya Rais Samia Suluhu Hassan, ilielezwa kuwa mchango wa misaada ya nje kwenye Bajeti ya Serikali umeshuka hadi asilimia 0.9. Hii inaashiria kuwa sehemu kubwa ya bajeti ya Tanzania sasa inagharamiwa na **mapato ya ndani, badala ya kutegemea misaada kutoka kwa wahisani.

Kwa mujibu wa Serikali, hatua hii imechangiwa na kuongezeka kwa ukusanyaji wa mapato ya ndani, kuimarika kwa usimamizi wa fedha za umma na ongezeko la mapato kutoka kwa taasisi na mashirika ya Serikali.

Kupungua kwa utegemezi wa misaada ya nje kunaweza kuipa Serikali nafasi kubwa zaidi ya kupanga na kutekeleza vipaumbele vyake vya maendeleo kwa kutumia rasilimali zake. Hata hivyo, ni muhimu kufahamu kuwa hii haimaanishi Tanzania imeacha kupokea fedha kutoka nje, kwani nchi bado inaendelea kushirikiana na washirika wa maendeleo kupitia mikopo ya maendeleo, mikopo yenye masharti nafuu na uwekezaji wa nje.

Kwa kifupi, takwimu ya asilimia 0.9 inaonyesha kuwa misaada ya wahisani imebaki kuwa sehemu ndogo sana ya bajeti, huku mzigo mkubwa wa kugharamia matumizi ya Serikali ukibebwa na vyanzo vya mapato ya ndani.

Je, unaona kupungua kwa utegemezi wa misaada ya nje ni ishara kwamba Tanzania inaelekea kujitegemea zaidi kiuchumi, au bado kuna changamoto zinazopaswa kushughulikiwa?

04/08/2026

Kathmandu, Nepal 🇳🇵
Maandamano yanayoongozwa na vijana nchini Nepal yameendelea kushuhudiwa katika siku ya hivi karibuni huku kukiwa na mvutano wa kisiasa na kijamii.

Tofauti na maandamano ya mwaka 2025 yaliyolenga kupinga rushwa na marufuku ya mitandao ya kijamii, safari hii makundi ya wazalendo wa Kihindu pamoja na wanaharakati vijana yamekuwa yakiandamana na kufanya migomo ya njaa yakitaka Nepal irejee kuwa taifa la Kihindu (Hindu Rashtra) na kuondoa dini ya kislamu sababu iliyopelekea waandamaji kuchoma nyumba za ibada za waislamu.

Pia wameibua wasiwasi kuhusu uhamiaji haramu na uwepo wa miundombinu inayodaiwa kujengwa kinyume cha sheria.

Mwishoni mwa Julai 2026, mapigano ya kijamii katika eneo la kusini mwa Nepal yalisababisha vifo vya watu kadhaa na kuwalazimu viongozi kuweka amri za kutotoka nje baada ya mivutano wakati wa maandamano ya kidini kugeuka vurugu, huku misikiti, nyumba na biashara zikishambuliwa.

Mamlaka zilipeleka vikosi vya usalama kurejesha utulivu, huku viongozi wakitoa wito wa wananchi kudumisha amani. Serikali inaendelea kufuatilia hali hiyo na kufanya mazungumzo na makundi ya Kihindu kuhusu madai yao.

04/08/2026
04/08/2026

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imeteketeza hekari 3,117.9 za mashamba ya bangi na kukamata watuhumiwa 12 katika operesheni maalum ya siku 16 iliyofanyika katika vijiji vinne vya Kata ya Kandawale na Kipatimo, Wilaya ya Kilwa, mkoani Lindi.

Akizungumza kuhusu operesheni hiyo, Kamishna Jenerali wa DCEA, Aretas Lyimo, amesema mafanikio hayo yametokana na ushirikiano mkubwa kati ya Mamlaka, wananchi na viongozi wa maeneo husika katika mapambano dhidi ya kilimo cha bangi.

Amesema operesheni hiyo ni sehemu ya mkakati endelevu wa DCEA wa kudhibiti uzalishaji wa dawa za kulevya nchini hususan bangi, ambayo imeendelea kulimwa katika baadhi ya maeneo nchini.

04/08/2026

ASKARI 60 WA ZIMAMOTO WANOLEWA UWEZO WA HUDUMA ZA DHARURA ARUSHA

Askari 60 wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kutoka mikoa mbalimbali nchini wameanza rasmi mafunzo maalumu ya First Responder Resiliency, Support and Knowledge Training (FIRST) Program for Prehospital Care yanayofanyika kwa muda wa wiki mbili katika Hospitali ya JKCI-ALMC, jijini Arusha.

Mafunzo hayo yanatolewa na wakufunzi kutoka Marekani (USA) kwa lengo la kuwaongezea uwezo askari hao katika utoaji wa huduma za matibabu ya dharura kabla ya mgonjwa kufikishwa hospitalini, pamoja na kuwajengea ujuzi wa kukabiliana na changamoto zinazojitokeza wakati wa uokoaji.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo, Mkurugenzi wa The Same Qualities Foundation, ambaye pia ni mwanzilishi na msimamizi wa mafunzo hayo, Dr. Peter Mabula, amesema washiriki wanapaswa kutumia kikamilifu fursa hiyo kwa kusikiliza na kujifunza kwa umakini ili kuongeza ubora wa huduma wanazozitoa kwa wananchi.

Dr. Mabula amesema matarajio yao ni kuona askari hao wanaporejea katika vituo vyao vya kazi, mbali na kuendelea kutoa huduma bora za matibabu ya dharura, pia wawe mabalozi wa elimu kwa kuwafundisha wenzao na jamii kuhusu umuhimu wa huduma za kwanza na mbinu sahihi za uokoaji.

Baadhi ya askari wanaoshiriki mafunzo hayo wameeleza kuwa mafunzo hayo yatawaongezea ujuzi na kujiamini zaidi wanapokabiliana na matukio mbalimbali ya dharura, wakisema maarifa watakayopata yataongeza ufanisi katika kuokoa maisha ya wananchi.

Mafunzo ya FIRST Program for Prehospital Care yanatarajiwa kuendelea kwa wiki mbili, yakihusisha vipindi vya nadharia na vitendo, huku yakilenga kuimarisha uwezo wa askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji katika kutoa huduma za haraka na salama kwa waathirika wa ajali na majanga mbalimbali.

Kupitia mafunzo hayo yanayotolewa na wakufunzi kutoka Marekani, washiriki wanatarajiwa kurejea katika maeneo yao ya kazi wakiwa na ujuzi wa kisasa utakaosaidia kuboresha huduma za dharura na kuokoa maisha ya wananchi kwa ufanisi zaidi.

Photos from The Same Qualities Foundation's post 03/08/2026

ASKARI 60 WA ZIMAMOTO WANOLEWA UWEZO WA HUDUMA ZA DHARURA ARUSHA

Askari 60 wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kutoka mikoa mbalimbali nchini wameanza rasmi mafunzo maalumu ya First Responder Resiliency, Support and Knowledge Training (FIRST) Program for Prehospital Care yanayofanyika kwa muda wa wiki mbili katika Hospitali ya Seliani, jijini Arusha.

Mafunzo hayo yanatolewa na wakufunzi kutoka Marekani (USA) kwa lengo la kuwaongezea uwezo askari hao katika utoaji wa huduma za matibabu ya dharura kabla ya mgonjwa kufikishwa hospitalini, pamoja na kuwajengea ujuzi wa kukabiliana na changamoto zinazojitokeza wakati wa uokoaji.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo, Mkurugenzi wa The Same Qualities Foundation, ambaye pia ni mwanzilishi na msimamizi wa mafunzo hayo, Peter Mabula, amesema washiriki wanapaswa kutumia kikamilifu fursa hiyo kwa kusikiliza na kujifunza kwa umakini ili kuongeza ubora wa huduma wanazozitoa kwa wananchi.

Mabula amesema matarajio yao ni kuona askari hao wanaporejea katika vituo vyao vya kazi, mbali na kuendelea kutoa huduma bora za matibabu ya dharura, pia wawe mabalozi wa elimu kwa kuwafundisha wenzao na jamii kuhusu umuhimu wa huduma za kwanza na mbinu sahihi za uokoaji.

Baadhi ya askari wanaoshiriki mafunzo hayo wameeleza kuwa mafunzo hayo yatawaongezea ujuzi na kujiamini zaidi wanapokabiliana na matukio mbalimbali ya dharura, wakisema maarifa watakayopata yataongeza ufanisi katika kuokoa maisha ya wananchi.

Mafunzo ya FIRST Program for Prehospital Care yanatarajiwa kuendelea kwa wiki mbili, yakihusisha vipindi vya nadharia na vitendo, huku yakilenga kuimarisha uwezo wa askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji katika kutoa huduma za haraka na salama kwa waathirika wa ajali na majanga mbalimbali.

Hayo ni mafunzo yanayotarajiwa kuwa chachu ya kuboresha huduma za dharura nchini kupitia askari waliopata ujuzi wa kisasa kutoka kwa wakufunzi wa kimataifa.

Photos from The Same Qualities Foundation's post 03/08/2026
Want your organization to be the top-listed Non Profit Organization in Arusha?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Telephone

Address


P. O BOX 11641
Arusha