Radio5tz
Radio 5 is one of Tanzania's most popular Swahili speaking radio station, broadcasting news and entertainment
News segment comprises of accurate; soft and hard local, international and national news. Entertainment segment encompasses Blues, Afro vibes and R&B, of both local (African) and international flavors that provide a rare source of relaxation in the hectic world we live in.
29/05/2026
🔥 Usikose! 🔥
Tuko na A.T ndani ya Funiko Base Serikalini kuanzia saa 7:00 mchana hadi saa 10:00 jioni. Karibu tushare vibe, 🎶✨
26/05/2026
Eid Al Adha njema!
25/05/2026
Mwenyekiti wa (CHADEMA) Taifa, Tundu Lissu, akiwasili katika Mahak**a Kuu, Divisheni ya Masijala, jijini Dar es Salaam leo, Mei 25, 2026, kwa ajili ya usikilizwaji wa shauri lake la maombi ya kujumuishwa k**a mdaiwa katika kesi ya mali za chama iliyofunguliwa na Saidi Issa Mohamed pamoja na wadai wengine wawili.
Na Semio Sonyo – Radio 5
Klabu ya Arsenal hatimaye imetangazwa mabingwa wa Ligi Kuu England baada ya kusubiri kwa miaka 22, kufuatia ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Crystal Palace katika mchezo wa mwisho wa msimu uliochezwa Uwanja wa Selhurst Park.
Baada ya Manchester City kupoteza dhidi ya Aston Villa, Arsenal walithibitisha ubingwa huo na kumaliza msimu wakiwa kileleni kwa tofauti ya pointi saba. Nahodha Martin Ødegaard aliliinua kombe hilo mbele ya mashabiki waliokuwa katika shamrashamra kubwa, huku kocha Mikel Arteta akiongoza sherehe za kihistoria.
Ubingwa huo ni wa kwanza kwa Arsenal tangu mwaka 2004, ukiwa ni mafanikio makubwa kwa Arteta na kikosi chake baada ya miaka mingi ya changamoto na presha ya ushindani.
Mbali na kutwaa ubingwa, Arsenal pia wameweka rekodi ya kuwa timu ya kwanza katika historia ya Premier League kumaliza msimu bila kuruhusu penalti wala kupata kadi nyekundu.
25/05/2026
Wananchi wa Jiji la Arusha leo wamekumbwa na changamoto kubwa ya usafiri kufuatia madereva wa daladala kusitisha huduma za usafirishaji katika maeneo mbalimbali ya jiji hilo, hali iliyosababisha mamia ya wakazi kulazimika kutembea kwa miguu kufika katika shughuli zao za kila siku.
Maeneo ya Mianzini, Sanawari na Ngulelo yalishuhudia idadi kubwa ya abiria wakisubiri usafiri kwa muda mrefu bila mafanikio, huku wengine wakiamua kutembea kutokana na ukosefu wa magari ya usafiri wa umma.
Madereva wa daladala waliohusika katika mgomo huo wameeleza kuwa hatua hiyo imetokana na kile walichodai kuwa ni ongezeko la faini kutoka Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA), pamoja na kupanda kwa gharama za uendeshaji wa magari, hususan bei za mafuta zinazozidi kuongezeka kila siku.
Aidha, madereva hao wameiomba serikali kupitia mamlaka husika kuruhusu marekebisho ya nauli za daladala kutoka kiwango cha sasa hadi angalau shilingi 1,000, wakieleza kuwa kiwango kilichopo hakikidhi gharama za uendeshaji na kinaendelea kuathiri shughuli zao katika kipindi hiki cha changamoto za kiuchumi.
24/05/2026
Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Miguel Gamondi, ametangaza kikosi cha Taifa Stars kitakachoingia kambini kwa ajili ya maandalizi ya michezo miwili ya kirafiki iliyopo kwenye kalenda rasmi ya FIFA.
Taifa Stars inatarajiwa kucheza dhidi ya Uganda na Rwanda katika michezo hiyo ya kirafiki yenye lengo la kuimarisha kikosi na kuongeza ushindani kuelekea mashindano yajayo ya kimataifa.
Kocha Miguel Gamondi amesema uteuzi wa kikosi hicho umezingatia kiwango cha wachezaji, nidhamu pamoja na mahitaji ya kiufundi kwa ajili ya kuijenga timu imara itakayoweza kufanya vizuri katika michezo hiyo muhimu ya maandalizi.
13/05/2026
Bia namba moja ya mabingwa Tanzania, Safari Lager, imeandika historia baada ya kutangaza udhamini wake wa Kombe la Dunia la FIFA 2026, na kuwa chapa ya kwanza ya bia kutoka Tanzania kupata nafasi kwenye jukwaa kubwa zaidi la mpira wa miguu duniani. Hii ni hatua kubwa inayomilikiwa na kila shabiki wa mpira wa Tanzania ambaye amewahi kuamini!
Kuna jambo kubwa linakuja tarehe 23 Mei – endelea kufuatilia pamoja na kurasa zetu za mitandao ya kijamii ili kugundua jinsi unavyoweza kuwa sehemu ya ukishirikiana na !
11/05/2026
Kesho ndani ya kipindi cha Good Morning Tanzania tutakuwa LIVE na,
Dr. Pascal Kang’ria
Mratibu wa Afya ya Akili – Arusha DC
🧠 Mada: Demografia ya Afya ya Akili
📅 Jumanne, Mei 12, 2026
⏰ 06:30 – 10:00 Asubuhi
🎤 Hosts
Wilson Exavery
04/05/2026
06/04/2026
Honoring the legacy of Abeid Amani Karume a symbol of unity, strength, and true leadership.
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Contact the business
Website
Address
Njiro Block J
Arusha
P.O.BOX15883