Agri Smart TV

Agri Smart TV

Share

Official onlineTv Dealing with Agriculture.Promoting Agribusiness ,Food safety,opportunities and info

09/08/2024

Kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa mapema mwaka huu pamoja na uchaguzi mkuu mwaka 2025,wanawake waliopo kwenye sekta ya kilimo,wametakiwa kujitokeza kwa wingi kushiriki katika mchakato mzima wa kupata viongozi bora pamoja na wao pia kugombea nafasi mbali mbali ili kuweza kusaidia kwa urahisi kutatua changamoto wanazokutana nazo katika shughuli zao za kilimo.
Usisahau ku SUBSCRIBE kwenye YouTube channel yetu ya Agri Smart Tv

25/01/2024

Congratulations .We are proud of you 👏🏽 cc

16/12/2023

Genesi 1:27-28. Lord i thank you for a Gift of Life.

14/10/2023

Happy Nyerere Day Fam

13/10/2023

Mbole ya Ruzuku ni moja kati ya mkakati wa serikali kuwasaidia wakulima kupunguza gharama za kilimo kwa kupunguza bei ya mbolea nchini.Je hali ya upatikanaji wa mbolea hiyo upoje katika maeneo yako? Tumzungumza na baadhi ya wakulima mkoani Arusha kuhusu upatikanaji wa mbolea hiyo na tumezungumza pia na afisa kilimo ambaye ameelezea namna ya kupata mbolea hiyo.Video iko hapa chini.

13/10/2023

Ili kuweza kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi yanayoendelea kuikumba dunia ,wataalam wa kilimo wanashauri wakulima kujikita kwenye kilimo Ikolojia ambacho ni rafiki kwa mazingira,afya na uchumi pia.Je kilimo ikolojia ni nini?

Full video ipo hapa na majibu yote

25/09/2023

Kutokana na hali ya upungufu wa mvua inayoendelea nchini,wakulima wameshauriwa kufanya kilimo cha umwagiliaji wa matone ili kupata uhakika wa chakula.Agri smart tv tumekuwekea video yenye mafunzo kuhusu umwagiliaji wa matone.

22/09/2023

Watanzania wengi bado wanatumia kuni k**a chanzo kikuu cha nishati ya kupikia?Nini madhara ya matumizi hayo makubwa kwa mazingira na binadamu?Nini kifanyike kupunguza matumizi hayo?Fuatilia video yetu upate kujifunza mengi

22/09/2023

Maharage yanatajwa k**a moja ya vyakula vyenye virutubisho vingi sana katika mwili wa binadamu, pia ni chakula kinachopatikana kwa urahis na bei yake pia ni rafiki. Yafahamu maharage lishe yanayoongeza damu pamoja na kusaidia kuongeza nguvu za kiume.
Tumekuwekea hapa video kamili yenye maelezo kuhusu umuhimu wa maharage katika lishe.

21/09/2023

Zao la tangawizi ni moja kati ya mazao yenye matumizi mengi lakini pia ni moja kati ya zao ambalo halilimwi kwa wingi hapa nchini hivyo kufanya soko lake la ndani na nje liwe kubwa kutokana na uhitaji wa zao hilo.
Tumekuwekea simulizi nzima ya zao la tangawizi kwenye video hapo chini.

17/09/2023

Tafiti zimeendelea kuonyesha uwepo wa mabaki ya kemikali katika mboga mboga na matunda hali inayosababishwa na matumizi makubwa ya viuatilifu katika mboga mboga na matunda. Teknolojia sasa inarahisisha kila mtu kuweza kulima mboga mboga safi na salama Kwa matumizi ya nyumbani hata kwa watu wasiokuwa na maeneo ya kulima.
Agri Smart tv tumekuwekea teknolojia hizo tofauti tofauti za kulima mboga popote hata kwa watu wanaoishi maghotofani.

Want your public figure to be the top-listed Public Figure in Arusha?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Category

Telephone

Address


15883
Arusha
0000