Isack Jonas Jr.

Isack Jonas Jr.

Share

Fashion Designer •||• Gospel Singer •||• Songs Writer •||• Models Trainer •||• Born

18/06/2022

KU-furahi,
KU-endelea mbele,
KU-jiamini,
KU-wa na amani,
KU-tabasamu
N.K...

04/06/2022

HESHIMA HUGHARAMIKIWA ila haupatikani kwa Fedha.

Nimejifunza kuwa, ukitaka kuheshimiwa kubali kuishi ndani ya kanuni kuu tatu.
1. Kwa wadogo zako Mara zote tafuta kuwa mfano mzuri, hakikisha hautengenezi mazingira ya walioko chini yako kiumri kujifunza au kukunukuu kwa mambo yasiyofaa. Penda kuwa taswira njema unayotaka kuiona kwao.

2. Kwa watu wa rika lako onesha utofauti. Mara zote usipendwe kubebwa na mambo, jenga misimamo yako itakayokutofautisha nao, wanapokuona wawe na jambo la kujifunza. Kuwa mtu anaetengeneza trend sio anaefuata trend zilizopo.

3. Kwa waliokuzidi umri kuwa msikivu. Kuna tofauti sana kati ya mtu mwenye ujuzi na mwenye uzoefu. Mwenye ujuzi atakuelezea kitu kilivyo ila mwenye uzoefu atakuelezea kunavyofanya kazi. Wazee hata k**a hawajui mengi ila wana uzoefu mwingi na huo uzoefu ni hazina yenye faida kubwa sana ukiweza kuipata na kuitumia. Jua sana ila usijue kupita wenye uzoefu.

Heshima HUGHARAMIKIWA.

01/06/2022

Kindly Support my good work.

31/05/2022

Imani ina uwezo wa kujenga vitu vikubwa sana na hofu huweza kubomoa kila kitu maishani mwako.
Chagua Imani

31/05/2022

UPENDO UNAJIPIMIA.
Kiwango cha upendo unachoweza kutoa kwa wengine ndicho kiwango cha upendo ulichonacho na unachoweza kuuelewa, na uzuri wa upendo ninkwamba tunaweza kuongeza kiwango muda wowote kwa namna nyingi sana.
Tujifunze kupenda wengine kwa viwango vikubwa ili tuweze kuelewa upendo kwa viwango hivyo.

30/05/2022

Uaminifu ni jambo linalokujenga wewe na pia kutendea vyema jamii.
Chagua UAMINIFU zaidi ya kitu kingine chochote...!

27/05/2022

KUWA NA STRESS KWENYE HAYA MAISHA NI LAZIMA

Unaweza kustress saivi ukashindwa kuanza unachotaka kufanya hizi ni stress mbaya ila ukianza saivi baadae utakuwa na stress ya jinsi ya kuendeleza ulichoanza hizo ni stress nzuri.

SASA Chagua unataka stress zipi.

26/05/2022

Kuna msemo wa Ijue Thamani yako ila kwangu nadhani kujua kusudi la kuwepo kwako duniani INA faida kubwa kwani thamani yako huletwa na wewe kuliishi kusudi lako duniani.

Tafuta kujua wito wako.

25/05/2022

Kuna furaha katika kufanikiwa kufanya mtu mwingine afurahi.

24/05/2022

Mche MUNGU
PENDA watu.
PERIOD.

24/05/2022

Mabadiliko in jambo muhimu sana kwa sababu hutusaidia kuwa bora zaidi yatulivyo sasa au hata kutuondolea hali tutusizofurahia. Kitu pekee cha kuepuka katika kujifanyia mabadiliko ni kubadilika kunakoweza kukudhuru au kubadilika kuwa usivyotaka kwa ajili ya kufurahisha mtu asiyedhamini kujitoa kwako kwa ajili yake.

Kubadilika kunakofaa ni k**a:
1. Kuacha tabia au mambo yanayowakwaza wazazi wako.
2. Kuboresha afya ya mwili wako k**a kupunguza unene.
3. Kuepukana na tabia zinazokupotezea sifa njema kwa Mungu na jamii yako.
4. Kuacha matumizi ya vitu vinavyokuletea madhara kiafya, kiimani au kijamii.

Wote tuna chumba cha kuwa bora kila wakati. Mabadiliko ni kuufungua mlango huo na kuingia.

23/05/2022

Ukuaji ni mchakato wa uhai wa kiumbe chochote lakini Ukomavu ni wa kipekee.
Umri unaonesha ukuaji, hekima na maamuzi huamua ukomavu.

Want your school to be the top-listed School/college in Arusha?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Category

Telephone

Address

Arusha