Tanapa Updates

Tanapa Updates

Share

The Official Page for Tanzania National Parks (TANAPA) News and Updates.

Photos from Tanapa Updates's post 06/08/2026

TANAPA TUPO NANE NANE- NJIRO

Karibu utembelee Banda la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) katika Viwanja vya Nanenane Njiro, jijini Arusha yanapofanyika maonesho ya 32 ya Kilimo maarufu k**a *NaneNane* yakiwa na Kauli mbiu isemayo *”Tambua Soko; Ongeza Tija kutekeleza Dira 2050”*

Ndani ya banda letu utapata elimu ya Uhifadhi, Utalii pamoja na fursa za kede kede za Uwekezaji katika Hifadhi za Taifa.

Aidha, tutajifunza pamoja mchango wa Hifadhi za Taifa katika maendeleo na ukuaji wa sekta ya Kilimo na Umwagiliaji . Namna vyanzo vya maji vinavyotunzwa ambayo kwa kiasi kikubwa huanzia katika maeneo ya Hifadhi.

Photos from Tanapa Updates's post 05/08/2026

Hivi, unajua kuna ishara ambazo wanyamapori huonyesha kabla ya kukasirika?

Wanyamapori wengi hawaanzi kwa kushambulia ghafla, mara nyingi huonyesha mabadiliko ya mwili, mikao au tabia ambazo hutofautiana kutoka mnyama mmoja hadi mwingine.

Lakini swali ni... je, unazijua?

👉 Swipe hadi mwisho ujifunze baadhi ya ishara hizo, kisha utuambie kati ya tembo, simba, kiboko, nyati na nyoka, ni ishara ipi uliijua?, na ukiiona ishara hiyo ukiwa safarini, ungefanya nini?

04/08/2026

Mhe. Chande: “Retreat iwe Chachu ya Kutekeleza Mikakati ya Wizara ya Maliasili na Utalii”

Cc,
Ukurasa Rasmi wa Wizara ya Utalii - Tanzania🇹🇿
Nyerere National Park

Photos from Tanapa Updates's post 04/08/2026

MHE. CHANDE AHITIMISHA MKUTANO WA KIMKAKATI WA VIONGOZI WA WIZARA 2026

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb) amehitimisha Mkutano wa Kimkakati wa Viongozi wa Wizara na Taasisi zake wa mwaka 2026 uliofanyika katika Hifadhi ya Taifa Nyerere. Mhe. Chande amewasisitiza viongozi hao kutumia mafunzo na maarifa waliyoyapata k**a chachu ya kuimarisha utendaji kazi na utekelezaji wa mikakati ya Wizara kwa maendeleo ya Sekta ya Maliasili na Utalii.

Aidha, Mhe. Chande ameeleza kuwa mafanikio ya mkutano huo yataonekana kupitia mabadiliko chanya katika utendaji wa viongozi na taasisi zao. Pia amesisitiza umuhimu wa ushirikiano, mawasiliano na kuzingatia taratibu ili kuendelea kujenga taswira nzuri ya Wizara, taasisi zake na Serikali kwa ujumla.

Mkutano huo wa siku nne umetoa fursa kwa viongozi kutathmini utendaji, kubadilishana uzoefu na kuweka mikakati ya kuimarisha utekelezaji wa majukumu. Pia viongozi walifanya utalii wa gari na boti ndani ya Hifadhi ya Taifa Nyerere na kujionea vivutio mbalimbali vya utalii na shughuli za uhifadhi.

04/08/2026

Kundi la Watalii 16 kutoka nchini Africa Kusini linatarajiwa kupanda Mlima Kilimanjaro Agosti 5, 2026 mara baada ya kuwasili leo Agosti 4, 2026 majira ya saa 6 usiku katika uwanja wa kimataifa wa ndege Kilimanjaro (KIA) mkoani kilimanjaro.

Kundi hilo lilipokelewa na uongozi wa TANAPA, kupitia Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi na Mkuu wa Hifadhi ya Taifa Kilimanjaro Angela Nyaki akiambatana na wawakilishi kutoka ofisi ya Makao Makuu ya Shirika na Kanda ya Kaskazini.

Safari ya hiyo ya hisani inayofanyika kila mwaka kupanda Mlima Kilimanjaro maarufu k**a *Trek4Mandela* hufanyika kila mwaka kumuenzi Hayati Nelson Mandela na kusaidia programu ya *Caring4Girls*

Kwa kuhimiza na kuhamisha jamii na wadau kuchangia fedha kwaajili ya kumuinua mtoto wak**e aweze kujikwamua kitaaluma, kiuchumi na kijamii kutoka katika mazingira hatarishi anayoyapitia pamoja na kuhamasisha watu kukusanya fedha za kusaidia kupambana na changamoto ya ukosefu wa taulo za k**e. Kupitia misaada mbalimbali kwa wasichana wenye uhitaji

Photos from Tanapa Updates's post 04/08/2026

Viongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii leo Agosti 4, 2026 wamehitimisha mapumziko yao maalum ya kikazi (Retreat) ndani ya Hifadhi ya Taifa Nyerere kwa kufanya utalii wa gari na boti, wakiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Hassan Abbasi.

Katika ziara hiyo, viongozi walipata fursa ya kutembelea na kujionea vivutio mbalimbali vya utalii vinavyopatikana ndani ya hifadhi hiyo.

Utalii wa boti ulifanyika katika Mto Rufiji, ambao ni mto mkubwa unaopitia ndani ya Hifadhi ya Taifa Nyerere na kumwaga maji yake katika Bwawa la Kufua Umeme la Julius Nyerere. Wakati wa safari hiyo, viongozi hao walishuhudia jamii mbalimbali za wanyamapori wakiwemo swala, twiga, tandala mkubwa, nyani pamoja na aina mbalimbali za ndege.

Ziara hiyo ililenga utembelea vivutio vya utalii na kujionea shughuli za uhifadhi zinazoendelea ndani ya Hifadhi ya Taifa Nyerere, ambayo ni hifadhi kubwa zaidi nchini Tanzania iliyobarikiwa kuwa na wanyama adimu wakiwemo mbwa mwitu wa Afrika pamoja na mandhari ya kuvutia ya maziwa matano yenye mchango mkubwa katika kuhifadhi na kuendeleza makazi ya viumbe hai ndani ya hifadhi hiyo.

04/08/2026

S02 EP02 - Ujirani Mwema na Faida Zake kwa Jamii
Katika episodi hii utasikia simulizi, uzoefu na ushuhuda kutoka kwa wataalamu wa uhifadhi pamoja na wanufaika wa programu za ujirani mwema, wakieleza namna uhifadhi unavyochangia maendeleo ya wananchi na ustawi wa jamii.
📍 Eneo: Arusha
🎤 Mwongoza Kipindi:
Afisa Uhifadhi Daraja la Pili, Happiness Sam
👥 Wageni:
• Afisa Uhifadhi Mwandamizi Lameck Matungwa – Kitengo cha Ujirani Mwema, Hifadhi ya Taifa Milima Mahale
• Rose Machange – Mwenyekiti, Kikundi cha Umoja wa Maendeleo Ngurdoto (UMANGU)
▶️ Tazama sasa kupitia YouTube na usisahau ku-like, ku-comment, kushare na ku-subscribe ili usipitwe na episodi zijazo.
TANAPA PODCAST – HIFADHI ZETU, SAUTI YETU.

Photos from Tanapa Updates's post 03/08/2026

VIONGOZI WA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII WAJENGEWA UWEZO KATIKA MKUTANO WA KIMKAKATI

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi, leo Agosti 3, 2026 ameongoza viongozi wa Wizara katika Mkutano wa Kimkakati unaoendelea kufuatia ufunguzi wake uliofanyika Agosti 2, 2026.

Katika siku ya pili ya mkutano huo, viongozi wamepatiwa mafunzo yenye lengo la kuimarisha uongozi na kuongeza tija katika utendaji wa Wizara. Mada zilizowasilishwa ni pamoja na “Emotional Intelligence in Leadership, Adopting a Selling Mindset to Maximize Value, pamoja na Transforming Tanzania’s Tourism through a Unified Digital Destination Ecosystem: Unlocking Growth, Visibility and Seamless Visitor Experience”.

Mkutano huo umebeba kaulimbiu isemayo: “Kugeuza Fursa Kuwa Matokeo Yenye Thamani Kubwa,” ikisisitiza matumizi ya uongozi thabiti, ubunifu na ushirikiano katika kuongeza thamani ya rasilimali za maliasili na kukuza sekta ya utalii nchini.

Cc,
Ukurasa Rasmi wa Wizara ya Utalii - Tanzania🇹🇿

03/08/2026

Ufunguzi wa Mkutano wa Kimkakati wa Viongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii 2026.

Cc,
Ukurasa Rasmi wa Wizara ya Utalii - Tanzania🇹🇿

Photos from Tanapa Updates's post 02/08/2026

TANAPA YASHIRIKI MKUTANO WA KIMKAKATI WA VIONGOZI WA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII 2026

Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) linashiriki Mkutano wa kimkakati wa Viongozi wa Wizara 2026 uliofunguliwa leo Agosti 02, 2026 na Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) ndani ya Hifadhi ya Taifa Nyerere.

Mkutano huo una lengo kufanya tathmini na kupitia mikakati ya Wizara itakayotekelezwa mwaka mpya wa fedha wa 2026/2027 katika kuendelea kuimarisha sekta ya uhifadhi na utalii ili kufanikisha malengo ya Serikali ya kuongeza idadi ya watalii na mapato kwa Taifa.

Mkutano huo wa Kimkakati wa Viongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii uliofunguliwa na Waziri Kijaji umejumuisha viongozi mbalimbali wa Wizara akiwepo Katibu Mkuu Dkt. Hassan Abassi, Naibu Katibu Mkuu Bw. Nkoba Mabula, Wakuu wa Idara Wizarani, Wakuu wa Vyuo vilivyopo chini ya Wizara, Taasisi zilizopo chini ya Wizara akiwemo Kamishna wa Uhifadhi TANAPA Massana Mwishawa.

Mkutano huo wa siku tatu umebeba Kaulimbiu isemayo “Geuza fursa kuwa matokeo yenye thamani kubwa” ambapo Dkt. Kijaji alisisitiza kendeleza kukuza utalii wenye ushindani kwa kuongeza thamani ya bidhaa za utalii, kuimarisha uhifadhi kwa kutumia sayansi, teknolojia, utafitina ubunifu. Pia ushirikishwaji wa jamii katika uhifadhi ili kuvutia uwekezaji wa kimkakati na ushirikiano na sekta binafsi, uboreshaji utendaji wa Taasisi pamoja na kuboresha mawasiliano kwa ajili ya kutangaza na kuhabarisha shughuli zinazofanywa na Wizara na taasisi zake.

Want your organization to be the top-listed Government Service in Arusha?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Address


Majengo
Arusha
23104