STL MEDIA

STL MEDIA

Share

STL RECORDS
STL TV TANZANIA
STL FM
STL VIDEO/PHOTO STUDIO
0754974891/0761047785
[email protected]
Located at USA-River Arusha Tanzania

07/01/2026

Kajala afunguka kwa mara ya kwanza...
"Harmonize alianza kumlipia Paula ada ya shule tangu Form 2!" 💛

Uhusiano wao haukuanza jana... ulikuwa wa muda mrefu! 😱

Je unaweza kumlipia ada mtoto wa mwenzio?
Cc:

Photos from STL MEDIA's post 07/01/2026

Baada ya mechi zote za mtoano (Round of 16) kukamilika, timu nane zilizofuzu hatua ya quarter-finals ni hizi:
Senegal 🇸🇳
Mali 🇲🇱
Morocco 🇲🇦 (wenyeji)
Cameroon 🇨🇲
Egypt 🇪🇬
Côte d'Ivoire 🇨🇮 (mabingwa watetezi)
Nigeria 🇳🇬
Algeria 🇩🇿

mechi za robo fainali (Quarter-finals):
Mali vs Senegal
Cameroon vs Morocco
Egypt vs Côte d'Ivoire
Algeria vs Nigeria
Mechi zitachezwa kuanzia Januari 9, 2026.

Je, unadhani nani atafika nusu fainali au hata kushinda kombe? Toa maoni yako chini! 👇
Cc:

06/01/2026

KUTANA NA SAM NUJOMA RAIS ALIYEONGOZA BILA MIKOPO YA IMF WALA BENKI YA DUNIA 🌍🇳🇦

Sam Nujoma, rais wa kwanza wa Namibia, aliheshimika kwa msimamo wake imara na maono ya uhuru wa kweli. Katika miaka yake 15 madarakani, alifanya uamuzi wa kipekee wa kutokuchukua mikopo kutoka Benki ya Dunia wala Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF).

Aliamini kuwa Namibia inaweza kujijenga bila kutegemea sana taasisi kubwa za kifedha duniani. Uongozi wake unakumbukwa k**a ishara ya kujitegemea na fahari ya bara la Afrika. 🖤

Cc:✍🏾

06/01/2026

Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, ametoa wito kwa mataifa ya Afrika kuungana kijeshi na kimkakati ili kulinda usalama wa bara. Akizungumza jana na vijana nchini Uganda, Museveni alisema kuwa huku mataifa k**a Marekani yakitawala anga, bahari na nchi kavu, Afrika inaweza kujikita zaidi kwenye vita vya nchi kavu k**a faida yake ya kiistratejia.

Museveni alikosoa viongozi wa zamani wa Afrika kwa kukosa maono ya umoja, akisema wengi walitaka kuwa "samaki wakubwa kwenye kidimbwi kidogo," badala ya kuunganisha nguvu kwa manufaa ya bara zima.

Amesisitiza kuwa kukosekana kwa ushirikiano wa kijeshi na uwekezaji katika rasilimali k**a anga na bahari kunaifanya Afrika kuwa dhaifu kijeshi na kuathiri usalama wa siku zijazo.

Photos from STL MEDIA's post 06/01/2026

Kupitia maneno yaliyojaa hisia, mke wa Mkubwa Fella amefunguka kuhusu maumivu ya moyo yanayotokana na hali ya mumewe kuumwa na ukimya wa waliowahi kusaidiwa naye. Akiwa na huzuni, ameonesha kusikitishwa na namna watu waliokuwa karibu na kufaidika kupitia Fella, hawajachukua muda hata kuulizia afya yake.

Amesisitiza kuwa licha ya ukimya huo, wamejifunza kuwa nyakati ngumu hufunua sura halisi za watu, na kwamba imani yao iko kwa Mungu, wakitegemea maombi na shukrani kwa wale wachache waliobaki kuwa nguzo ya faraja.

Ujumbe huu ni mwito wa tafakari kuwa ukaribu wa kweli hupimwa nyakati za majaribu. Mkubwa Fella bado anakumbukwa k**a mhimili wa vipaji Bongo Fleva, na mchango wake hautafutika.

Photos from STL MEDIA's post 06/01/2026

Msanii wa hiphop kutoka Tanzania, Young Lunya, amewapa mashabiki wake ladha mpya kupitia Insta Story yake, akisikiliza ngoma yake mpya Session 7. Hii ni sehemu ya msururu wa kazi zake binafsi alizoanza tangu Session 1, ambazo mara nyingi huonesha uwezo wake wa kisanaa kwa dakika moja. Safari hii, *Session 7* inatarajiwa kuwa na dakika 7:20 ikiashiria ukuaji, ubunifu na kujiamini kwake katika game ya rap. Mashabiki wajiandae kwa lyrical fire! 🔥

Cc:✍🏾

05/01/2026
Photos from STL MEDIA's post 05/01/2026

Tafiti mbalimbali za afya ya akili zimebainisha kuwa kulala pamoja na mwenza au mpendwa (yaani “wajifunikao shuka moja”) kunaweza kuwa na manufaa kadhaa kwa afya ya akili. Hapa ni muhtasari wa yale utafiti unasema:

1. Hupunguza Msongo wa Mawazo (Stress):
Watafiti wamegundua kuwa kugusana kimwili k**a vile kukumbatiana au kulala karibu kunaongeza kiwango cha oxytocin ("love hormone"), homoni inayosaidia kupunguza msongo wa mawazo na kuleta utulivu.

2. Huimarisha Hisia za Usalama na Amani:
Kuwa karibu na mtu unayemwamini huongeza hisia za usalama, jambo ambalo linaweza kusaidia ubongo kupumzika vizuri na kulala usingizi wa kina jambo muhimu kwa afya ya akili.

3. Huboresha Ubora wa Usingizi:
Kwa baadhi ya watu, usingizi huimarika wanapolala na wenzi wao kutokana na uthabiti wa upumuaji, mapigo ya moyo, na kiwango cha joto la mwili vitu vinavyochangia usingizi bora unaoathiri moja kwa moja afya ya akili.

4. Huongeza Muunganiko wa Kihisia:
Kuwa karibu na mpendwa usiku huchochea mawasiliano na ukaribu wa kihisia, hali inayosaidia kupunguza upweke, huzuni au hata dalili za sonona.

5. Huimarisha Kinga ya Mwili:
Kupitia kupunguza stress na kuleta furaha ya kihisia, watu wanaolala pamoja huweza kuwa na kinga bora ya mwili, ambayo inahusiana pia na ustawi wa akili.

Kwa ujumla, “wajifunikao shuka moja” si tu ishara ya mapenzi, bali pia ni fursa ya kuimarisha afya ya akili kwa njia ya upendo, ukaribu, na utulivu wa kihisia.

Cc:,✍🏾

Bruce Melodie (Rwanda) Diamond Platnumz (Tanzania) na Brown Joel (Nigeria), wameandika historia baada ya wao wa pamoja kufikisha views milioni 1 ndani ya siku tatu tu. Ushirikiano huu unaunganisha Afrobeat, Afro-R&B na Bongo Flava, ukithibitisha nguvu ya muziki wa Afrika kimataifa.

Cc:✍🏾

Want your public figure to be the top-listed Public Figure in Arusha?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Category

Address

NAPOCO
Arusha