JAMII Helper media

JAMII Helper media

Share

Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from JAMII Helper media, Public Figure, Sing'isi, Arusha.

👋 Welcome to Jamii Helper Media!
🌟 Spreading inspiration and knowledge 📚
🌍 Join us in community development!
🎥 TikTok: @jamiihelpermedia
📷 Instagram: @jamiihelpermedia

#Education #CommunityDevelopment
We Spread Education Based On Gender And Norms.

01/05/2026

JAMII HELPER recognizes You 🤞🤞🤞

27/03/2026

Mikono 🤝 Kwa Mikono 🤝 Tusimame Pamoja Tuzifikie Ndoto 🤝
❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️✨

11/03/2026

🎒 BACK TO SCHOOL SUPPORT DRIVE 📚

Kupitia JAMII Helper, tunaungana kuleta tabasamu kwa watoto wenye uhitaji kwa kuwasaidia kupata mahitaji ya shule.

📅 25 Aprili 2026
📍 Simanjiro – Manyara

Unaweza kuwa sehemu ya mabadiliko haya kwa kuchangia:
• Fedha
• Mahindi na Maharage
• Mafuta ya kupikia na Chumvi
• Sare za shule
• Vifaa vya michezo

🤍 Kila mchango wako unaweza kumbadilishia mtoto maisha.

💳 Lipa Namba: Halopesa 24016520
(Jina: JAMII Helper)

📞 Mawasiliano:
0624 188 209 | 0612 419 023
0692 729 000 | 0622 285 196

Nijuze • Nijue • Nimjuze
Let’s Get Inspiration Together 💪

Simanjiro InspireChange

03/01/2026

JODIC YATUNUKIWA CHETI CHA SHUKRANI KUTOKA JAMII HELPER

Kituo cha Huduma Tandaa na Ubunifu wa Kidijitali (JODIC) cha Chuo cha Maendeleo ya Jamii Tengeru kimetunukiwa cheti cha Shukrani kutoka kwa taasisi ya “Jamii Helper” ikiwa ni katika kutambua mchango wa kituo hicho kwa kuwezesha kuanzishwa kwa taasisi hio.

Akizungumza wakati wa kukabidhi cheti hicho Bw. Kukwaja Kilaja, Mwenyekitii wa taasisi hio alisema “ Tumeamua kuja kukabidhi cheti hiki cha shukrani kwa uongozi wa Chuo kupitia JODIC kwa kutulea kipindi ni wanafunzi na kutuwezesha kuanzisha taasisi yetu ambayo imejikita katika kusaidia jamii”.

Naye Bw. Mejoel Kirika, Meneja wa kituo cha JODIC alikuwa na haya ya kusema “Tumefurahi kuona wanafunzi tuliopewa kazi ya kuwalea wanafanikiwa, na leo wamerudi kuonesha matunda ya kazi waliyoifanya wakati walipokuwa wanafunzi”.

“Natoa rai kwa wanafunzi wanaoendelea na masomo na wanajamii waje katika kituo, tuwape elimu ya ujasiriamali na ubunifu watakayoweza kuitumia hata baada ya kumaliza masomo yao” alielezea Bw. Kirika.

Kituo cha Huduma Tandaa na Ubunifu wa Kidijitali kilichoanzishwa mwaka 2019 kikiwa na lengo la kuibua, kukuza na kuendeleza ubunifu, Uanagenzi na Ushirikishwaji wa Jamii ndani na nje ya Taasisi. Kituo hiki kinahudumia wanafunzi waliosajiliwa kusoma kwenye Taasisi hii lakini pia wananchi wanaozunguka maeneo ya jirani na chuo katika wilaya ya Arumeru na Mkoa wa Arusha kwa ujumla.
#2026

Photos from JAMII Helper media's post 29/12/2025

Thanking God 🙏.

Photos from JAMII Helper media's post 28/12/2025

🕊️ REST IN PEACE 🕊️
JAMII Helper inaomboleza kuondokewa na
Bw. Douglas Augustine Magombola,
ambaye alikuwa mdau mzuri na mshirika wa karibu wa JAMII Helper. Kupitia ushirikiano wake, alichangia kwa namna kubwa maendeleo ya jamii na kuimarisha malengo ya taasisi yetu. Moyo wake wa kujitolea na mshik**ano utaendelea kukumbukwa.

Tunatoa pole za dhati kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki. Tunaungana nanyi katika maombi, tukimuomba Mungu awape faraja, nguvu na amani katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.

📖 “Heri waliolazwa katika Bwana tangu sasa.”
— Ufunuo 14:13
🕯️ Pumzika kwa amani. Mchango wako kwa JAMII Helper na jamii kwa ujumla hautasahaulika.

Photos from JAMII Helper media's post 24/12/2025

JODIC YATUNUKIWA CHETI CHA SHUKRANI KUTOKA JAMII HELPER

Kituo cha Huduma Tandaa na Ubunifu wa Kidijitali (JODIC) cha Chuo cha Maendeleo ya Jamii Tengeru kimetunukiwa cheti cha Shukrani kutoka kwa taasisi ya “Jamii Helper” ikiwa ni katika kutambua mchango wa kituo hicho kwa kuwezesha kuanzishwa kwa taasisi hio.

Akizungumza wakati wa kukabidhi cheti hicho Bw. Kukwaja Kilaja, Mwenyekitii wa taasisi hio alisema “ Tumeamua kuja kukabidhi cheti hiki cha shukrani kwa uongozi wa Chuo kupitia JODIC kwa kutulea kipindi ni wanafunzi na kutuwezesha kuanzisha taasisi yetu ambayo imejikita katika kusaidia jamii”.

Naye Bw. Mejoel Kirika, Meneja wa kituo cha JODIC alikuwa na haya ya kusema “Tumefurahi kuona wanafunzi tuliopewa kazi ya kuwalea wanafanikiwa, na leo wamerudi kuonesha matunda ya kazi waliyoifanya wakati walipokuwa wanafunzi”.

“Natoa rai kwa wanafunzi wanaoendelea na masomo na wanajamii waje katika kituo, tuwape elimu ya ujasiriamali na ubunifu watakayoweza kuitumia hata baada ya kumaliza masomo yao” alielezea Bw. Kirika.

Kituo cha Huduma Tandaa na Ubunifu wa Kidijitali kilichoanzishwa mwaka 2019 kikiwa na lengo la kuibua, kukuza na kuendeleza ubunifu, Uanagenzi na Ushirikishwaji wa Jamii ndani na nje ya Taasisi. Kituo hiki kinahudumia wanafunzi waliosajiliwa kusoma kwenye Taasisi hii lakini pia wananchi wanaozunguka maeneo ya jirani na chuo katika wilaya ya Arumeru na Mkoa wa Arusha kwa ujumla.

Chanzo

Photos from JAMII Helper media's post 22/12/2025

JAMII Helper ✊ ni wakati wa VISION na MISSION.

18/12/2025

Happy Birthday Director! ✊✊

Photos from JAMII Helper media's post 11/08/2025

Katika picha ni viongozi watendaji wa JAMII Helper Kukwaja Kilaja Funuki & Nishary Juma Kapanga

Wakitoa semina elekezi iliyofanyika kwa wanachama na viongozi wa vikundi vya VICOBA wasiopungua 35 kijiji cha kilombero kata ya Rahaleo, Nachingwea mkoa wa Lindi

Miongoni mwa masuala waliyofundishwa ni pamoja na:-
1. Somo la hisa.
2. VICOBA
3. Katiba
4. Marejesho
5. Gawio
6. Uanachama
7. Ujasiliamali
8. Fursa
9. Namna ya kuwalinda watoto wao.

Mara baada ya semina hiyo kuna tuliyo yabaini kutoka kwenye VICOBA hivyo.

1. Mazoea ya kuendeleza masuala yasiyo na tija kwao (kufanya kwa mazoea bila uthibitisho).
2. Kutokuwa na elimu pamoja na uelewa wa kitosha kuhusiana na masuala ya kifedha hususani VICOBA.
3. Hawajui nini wanatakiwa wafanye.
4. Hawana maono ya kuwa wafanikiwa zaidi ya kukopeshana wao kwa wao.
5. Hawana kiu na shauku ya kutaka kujifunza kutoka kwa wataalamu wa fedha pamoja na maendeleo ya jamii.

Tuwasaidie watu hawa ili wafanikiwe. Tupo tayari kuja kwako.

08/08/2025

*Safari ya maisha ni safari ambayo kiubinadamu haina mpangilio maalum-life is not static it's dynamic.👇👇*
Nilianza kwa idadi ya mtu mmoja kufolo akaunti yangu,ila kufikia leo ni zaidi ya watu elfu moja wamefika na kupenda kile nafanya.

Mungu ni mwema huenda wewe ni miongoni mwa idadi hii na k**a sio basi siku moja naamini utakuwa miongoni mwa idadi kubwa ya watu zaidi ya *milioni 15-15M followers*

Nilishirikisha watu tofauti tofauti kuwaelezea maono yangu, wapi nataka kufika,nani nataka kumfikia ikiwemo mawaziri kafhaa wa hili taifa hususani *Waziri Dorothy Onesphora Gwajima* nakumbuka alisema *"anza na kile ulicho nacho kisha nitakuona na kusimama upande wako"*

Niliafiki na sasa Mungu amemleta kwa upya na kutembea sambamba, ukiona mtu ametulia kimya zifi kumuombea kuna mpito anaupitia. Omba juu yake ili avuke akuvushe usitake kushindana nae.

Leo naishia hapa tukutane wakati mwingine kunako majaaliwa.

Want your public figure to be the top-listed Public Figure in Arusha?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Category

Telephone

Address

Sing'isi
Arusha