Injili Mtandaoni

Injili Mtandaoni

Share

Injili Mtandaoni ni huduma inayolenga kuhubiri injili ya Yesu Kristo katika mitandao ya kijamii.

29/10/2025

Wafilipi 4:8 BHN
Hatimaye, ndugu zangu, zingatieni mambo mema na yanayostahili kusifiwa; mambo ya kweli na bora; mambo ya haki, safi, ya kupendeza na ya heshima.

27/10/2025

Yakobo 5:13 SUV
Mtu wa kwenu amepatikana na mabaya? Na aombe. Ana moyo wa kuchangamka? Na aimbe zaburi.

26/10/2025

Zaburi 31:24 SUV
Iweni hodari, mpige moyo konde, Ninyi nyote mnaomngoja BWANA.

24/10/2025

Yohane 14:6 BHN
Yesu akamjibu, “Mimi ni njia, na ukweli na uhai. Hakuna awezaye kwenda kwa Baba ila kwa kupitia kwangu.

23/10/2025

Wafilipi 2:3 SUV
Msitende neno lo lote kwa kushindana wala kwa majivuno; bali kwa unyenyekevu, kila mtu na amhesabu mwenziwe kuwa bora kuliko nafsi yake.

22/10/2025

Zaburi 34:18 BHN
Mwenyezi-Mungu yu karibu na waliokufa moyo; huwaokoa wote waliokata tamaa kabisa.

21/10/2025

2 Wakorintho 12:9 BHN
Lakini akaniambia: “Neema yangu inatosha kwa ajili yako; maana uwezo wangu hukamilishwa zaidi katika udhaifu.” Basi, ni radhi kabisa kujivunia udhaifu wangu ili uwezo wake Kristo ukae juu yangu.

20/10/2025

Waefeso 2:8-9 BHN
[8] Maana, kwa neema ya Mungu mmekombolewa kwa njia ya imani. Jambo hili si matokeo ya juhudi zenu, bali ni zawadi ya Mungu. [9] Wala halitokani na matendo yenu wenyewe, asije mtu akajivunia kitu.

19/10/2025

Zaburi 51:10 BHN
Uniumbie moyo safi, ee Mungu, uweke ndani yangu roho mpya na thabiti.

18/10/2025

Wafilipi 1:6 SUV
Nami niliaminilo ndilo hili, ya kwamba yeye aliyeanza kazi njema mioyoni mwenu ataimaliza hata siku ya Kristo Yesu.

17/10/2025

Yeremia 33:6 SUV
Tazama, nitauletea afya na kupona, nami nitawaponya; nami nitawafunulia wingi wa amani na kweli.

16/10/2025

Yohana 6:35 NEN
Yesu akawaambia, “Mimi ndimi mkate wa uzima. Yeye ajaye kwangu, hataona njaa kamwe na yeye aniaminiye, hataona kiu kamwe"

Want your public figure to be the top-listed Public Figure in Arusha?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Category

Telephone

Website

Address


Arusha