Iaa_tz

Iaa_tz

Share

Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Iaa_tz, College & University, Arusha.

Institute of Accountancy Arusha is a Public Owned Institute offering courses in Accountancy, Finance, Banking, Computing, Procurement and Other business courses in levels from Certificate, Diploma, Bachelor and Masters Degree

05/06/2026
04/06/2026

Dirisha la maombi kwa ngazi ya Shahada ya Uzamili (Masters) na Stashahada (Diploma) ya miaka miwili na miaka mitatu kwa mwaka wa masomo 2026/2027 limefunguliwa. Jinsi ya kutuma maombi yako tafadhali tembelea tovuti ya chuo www.iaa.ac.tz au tupigie kupitia namba 0742833444, 0781803490

Pia unaweza kupiga bure kabisa kupitia namba 0800110505 na 0800110506.
#

Photos from Iaa_tz's post 03/06/2026

UONGOZI WA AMUCTA WATEMBELEA IAA KUJIFUNZA MIFUMO YA UTOAJI ELIMU KIDIJITALI.

Uongozi kutoka Chuo Kikuu Kishiriki cha Askofu Mkuu Mihayo Tabora (AMUCTA) umetembelea Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) kwa lengo la kujifunza mifumo mbalimbali ya utoaji wa elimu kwa njia ya kidijitali (E-Learning and Blended Learning).

Katika ziara waliyofanya leo Juni 03, 2026 wakuu wa idara pamoja na wataalamu wa TEHAMA kutoka AMUCTA wamepata fursa ya kufahamishwa kuhusu sera na miongozo inayotumika katika utoaji wa elimu kwa njia ya mtandao, mifumo ya upimaji wa wanafunzi, uunganishaji wa masomo ya mtandaoni na ya ana kwa ana, huduma za msaada kwa wanafunzi, pamoja na hatua za ulinzi na usalama wa taarifa.

Uongozi wa AMUCTA umeeleza kuwa IAA imeonyesha mafanikio makubwa katika utoaji wa elimu kwa njia ya mtandao na mfumo wa mchanganyiko (Blended Learning), hivyo kutokana na mafanikio hayo, AMUCTA imeona umuhimu wa kujifunza kutoka IAA ili kuimarisha na kufanikisha malengo yake ya kutoa elimu bora kupitia mifumo ya kidijitali.

Photos from Iaa_tz's post 01/06/2026

Wanafunzi wa Shahada mwaka wa tatu Chuo Cha Uhasibu Arusha-IAA kutoka fani sita za TEHAMA wamepatiwa elimu kuhusu utambuzi na uendelezaji wa wataalamu wa TEHAMA hapa nchini.

Katika mafunzo yaliyotolewa leo Juni 1, 2026 katika ukumbi wa PGB3 na Mtaalamu wa huduma za TEHAMA kutoka Tume ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano-ICTC Mhandisi. Sadath Kalolo, wanafunzi hao wamejifunza namna na umuhimu wa kujisajili katika mfumo wa utambuzi, kujua kazi za tume pamoja, maadili na sheria zinazoongoza sekta ya TEHAMA.

ICTC imeanzishwa na kuanza kufanya kazi mwaka 2016 ikiwa na kazi mbalimbali ikiwemo kupanga na kuendeleza miradi ya TEHAMA, kutambua na kuendeleza wataalamu, kutoa mwelekeo wa maendeleo na kusimamia utekelezaji wa sera ya TEHAMA nchini.

Photos from Iaa_tz's post 29/05/2026

WANAFUNZI IAA WASHIRIKI JUKWAA LA TUYAJENGE TALKS

Wanafunzi wa Chuo Cha Uhasibu Arusha IAA wameshiriki Jukwaa la Tuyajenge Talk lililoandaliwa na Clouds Media kuelekea msimu wa kumi wa Malkia wa nguvu lililofanyika ndani ya Chuo cha Uhasibu campus ya Arusha

Akifungua Jukwaa hilo Mhadhiri mwandamizi IAA Dkt. Mohamed Mwanga amewashukuru Clouds kwa kuichagua IAA na kuwahakikishia kuendeleza ushirikiano kati ya taasisi hizi mbili

Kwa upande wake Mtangazaji kutoka Clouds media Najma Paul amewataka wanafunzi kuhakikisha wanajiamini na kumtanguliza mwenyenzi Mungu kwenye kila jambo ili kuweza kufikia malengo yao

Nao wanafunzi walioshiriki katika jukwaa hili wameushukuru Uongozi wa Chuo cha IAA na Taasisi ya Clouds kwa kuwasogezea fursa Hii kubwa na kuahidi kuwa wanakwenda kufanyia kazi vyote walivyojifunza.

Photos from Iaa_tz's post 29/05/2026

IAA NA UNDP TANZANIA KUFUNGUA FURSA ZA AJIRA KWA WANAFUNZI

Uongozi wa Chuo Cha Uhasibu Arusha-IAA umeingia makubaliano na UNDP Tanzania yanayolenga kuendelea kuboresha ubora wa elimu na kuwajengea wanafunzi uwezo wa kushindana katika mazingira ya ajira yanayobadilika kwa kasi ndani na nje ya nchi.

Makubaliano hayo yamesainiwa leo Mei 29, 2026 Jijini Dar es Salaam na Naibu Mkuu wa Chuo Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaalam, Dkt. Grace Temba, yakiwa yamelenga kuongeza fursa za mafunzo, tafiti na programu zitakazochochea maendeleo ya kitaaluma na kijamii kwa wanafunzi.

Aidha, makubaliano hayo pia yatasaidia wanafunzi kukuza fani na vipaji walivyonavyo, kuimarisha ubunifu pamoja na kuibua suluhisho za changamoto mbalimbali za jamii, ikiwa ni chachu ya kuwawezesha wanafunzi kutumia maarifa yao katika kuleta mabadiliko chanya na kuchangia maendeleo endelevu ya taifa

28/05/2026

Application Window for Master's Degree Programmes (October Intake) for the Academic year 2026/2027 is now open.
Master's Degree Programmes Offered are:

1. Master of Business Administration in Corporate Management (MBA-CM)
2. Master of Business Administration in Information Technology Management (MBA-ITM)
3. Master of Business Administration in Leadership & Governance (MBA-LG)
4. Master of Business Administration in Procurement & Supply Management (MBA-PSM)
5. Master of Business Administration in Policy Development and Ex*****on (MBA-PDE)
6. Master of Arts in Peace and Security Studies (MA-PSS)
7. Master of Accountancy (MA)
8. Master of Accounting and Finance (MAF)
9. Master of Science in Finance and Banking (MSc-FB)
10. Master of Finance and Investment ( MFI)
11. Master of Human Resource Management (MHRM)
12. Master of Project Planning Management (MPPM)
13. Master of Education Management (MEM)
14. Master of Science in Economics and Finance (MSc.EF)
15. Master of Information Security (MIS)

*Apply now*
Arusha, Babati, Bukombe, Dar es Salaam, Dodoma and Songea Campuses.

For more details please call: 0742833444 or visit www.iaa.ac.tz

28/05/2026

Application Window for Two years and Three years Diploma Programmes (September/October Intake) for the Academic year 2026/2027 is now open.

Diploma Programmes Offered are:

1. Diploma In Accountancy
2. Diploma In Finance &Banking
3. Diploma In Procurement & Supply Chain Management
4. Diploma In Business Management
5. Diploma In Business Management with Chinese
6. Diploma In Computer Science
7. Diploma In Information Technology
8. Diploma In Computer Networking
9. Diploma In Mobile Applications
10. Diploma In Multimedia
11. Diploma In Library & Information Studies
12. Diploma In Records & Information Management
13. Diploma In Accountancy with IT
14. Diploma In Economics & Finance
15. Diploma In Insurance & Risk Management
16. Diploma In Marketing & Public Relations
17. Diploma In Human Resources Management
18. Diploma In Clearing and Forwarding
19. Diploma In Agriculture Value Chain Management
20. Diploma in Cyber Security

*ENTRY QUALIFICATION:*
*THREE-YEAR DIPLOMA*
Form four (IV) with at least four (4) passes excluding religious subjects.

*TWO-YEAR DIPLOMA*
a) NTA Level 4 in the related field of study;

b) Form Six
At least One Principal Pass and One Subsidiary Pass excluding religious subjects

*Apply now*
Arusha, Babati, Bukombe, Dar es Salaam, Dodoma, and Songea Campuses.

For more details please call: 0742833444 or visit www.iaa.ac.tz

Want your university to be the top-listed University in Arusha?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Telephone

Website

Address


Arusha