imacrobot

imacrobot

Share

Ujue ulimwengu wa sasa na ujao.

10/08/2021

DALILI ZA CYBERATTACKS KATIKA MAGARI YANAYOTUMIA UMEME.
K**a nilivyosema katika post iliyopita kuwa ni kweli magari yanayotumia umeme yanaweza kudukuliwa na kusababisha madhara makubwa.Miaka ijayo yatakuwa ni sehemu ya maisha yetu ila changamoto kubwa tutakayokabiliana nayo ni cyberattackers.

Mpaka sasa kuna taarifa nyingi tu zinazoelezea matukio ya udukuzi wa magari ya umeme unaoendelea katika mataifa makubwa mfano nchini Marekani moja ya magari yanayotengenezwa na kampuni ya TESLA yanayofahamika k**a Tesla model x yalidukuliwa na si mara moja kwa magari hayo kudukuliwa. Lakini pia nchini Israel katika chuo cha ben, walifanya uchunguzi wa magari hayo kwa kubadilisha tu mfumo wa picha na alama za barabarani na mwisho wa siku gari walilolifanyia jaribio hilo lilipoteza mwelekeo.

Wataalamu wa teknolojia ya magari haya wamekuwa wakitoa tahadhari kubwa kwa watumiaji kuhusu uhalifu huu ambao unaweza kupelekea maisha yao kuwa hatarini.Bwana Jin Ye ambaye ni mtaalamu wa magari na teknolojia aliwahi kutoa viashiria viwili vikuu vitakavyomfanya mtu kutambua kuwa gari lake limeingiliwa na cyberattackers (wadukuzi/ hackers).
Kwanza kabisa charge ya gari huwa inaisha kwa muda mfupi sana.Cyberattackets wanauwezo wa kupunguza uwezo wa charge ya gari kwa 50% kwa kutumia mbinu za kisasa hivyo basi unapohisi charge ya gari lako inapungua kwa haraka basi anza kufanya uchunguzi.
Pili speed ya gari hupungua na kuwa ndogo sana pale unapokuwa barabarani.
Hivi ni viashiria viwili vikuu vitakavyokufanya uhisi kuwa mfumo wa ulinzi wa gari yako wajanja wameuingilia.

Lakini pia hata katika vituo vya hadhara vya kuchaji navyo pia vipo hatarini kuingiliwa na wajanja hawa.

๐Ÿ™Like
๐Ÿ™Follow

10/08/2021

CYBERSECURITY.
Cybersecurity ni jaribio la kulinda mifumo ya kidigitali, networks pamoja na program zisiingiliwe au kuharibiwa na mashambulizi ya kidigitali ambayo tunayaaita cyberattacks.Mashambulizi hayo hufanyika kwa lengo la kuharibu au kubadili taarifa muhimu zilizopo katika mfumo wa network au kuhamisha fedha toka katika account ya mtu bila yeye mwenyewe kujua.kwa kifupi kitendo hichi ndio hufahamika k**a udukuzi au ku-hack.

Cybersecurity ilikuwepo kwa lengo la kudhibiti uhalifu huo wa kimitandao ila sasa changamoto kubwa iliyopo na inayosababisha mpaka leo kuendelea kuwepo kwa ripoti za udukuzi wataalamu wanasema kuwa, kutengeneza ulinzi madhubuti kabisa wa kukomesha vitendo hivyo ni changamoto kwa sababu kwa sasa vifaa ni vingi sana na pia kila siku kadri teknolojia inavyozidi kukua, ndivyo jinsi washambulizi wa kimitandao wanazidi kuongeza na kuvumbua mbinu mpya.Ni vigumu kuwazuia wasiendelee na uhalifu huo.

Mafanikio yanayolenga kufikia ulinzi madhubuti wa cybersecurity una matabaka mengi ambayo yamejigawanya katika sehemu nyingi k**a vile katika kompyuta, networks, programmes au data, hivyo basi itakuwa bora zaidi kuunganisha na kutengeneza mfumo mmoja tu madhubuti ambao utazuia mashambulizi hayo.Tuchukulie mfano katika makampuni itakuwa bora zaidi k**a watu wote watakaa na kuamua kutengeneza mfumo mmoja wa ulinzi ambao utakuwa madhubuti kabisa, hii kwa kiasi fulani itasaidia kudhibiti uhalifu huu.

Mfumo huu unapaswa kutumika kikamilifu kabisa katika miaka ijayo baada ya magari ya umeme kusambaa sehemu kubwa ya dunia.Ndio, ni kweli magari ya umeme yanatunza mazingira ila je, vipi k**a mfumo wake wa cybersecurity utaingiliwa na wadukuzi?.
Hili ni swali ambalo unapaswa kujiuliza kwani kitu chochote kile kitakachounganishwa tu na internet ni rahisi sana kushambuliwa na wadukuzi.
Unaweza ukawa upo ndani ya gari yako na ukashambaa ghafla mifumo ya utendaji kazi ndani ya gari inabadilika bila wewe mwenyewe kugusa sehemu yoyote ile, hii ni hatari kubwa sana kwani ajali huweza kutokea.
Japo unaweza kupata viashiria vitakavyokufanya uhisi kuwa gari yako imeingiliwa na cyberattackers.๐Ÿค”

Next time nitakupa viashiria hivyo.

๐Ÿ™Like
๐Ÿ™follow

10/08/2021

JE, UNAWEZA KUNUNUA GARI LA KUCHAJI NNJE YA NCHI, ILHALI UNAISHI KATIKA NCHI ISIYO NA VITUO VYA KUCHAJI GARI HILO?.
Hivi karibuni tumekuwa tukishuhudia makampuni mengi ya magari yanayotumia mafuta kutangaza kuachana na biashara ya utengenezaji wa magari hayo na badala yake magari mengi yatakayokuja miaka ijayo ni yale yanayotumia umeme.Sababu kuu iliyopelekea uamuzi huu ni kutokana na uchafuzi mkubwa wa mazingira duniani kwani, magari yanayotumia petroli yamekuwa yakizalisha kiwango kikubwa cha hewa ya ukaa (CO2) ambayo imekuwa ikiharibu tabaka la ozon kwa muda mrefu sana.
Mataifa mbalimbali duniani kwa sasa yamekuwa yakiwekeza nguvu nyingi katika kujenga miundombinu itakayosaidia magari hayo kutumika katika nchi zao mfano ni ujenzi wa vituo vya kuchaji.

Watu wengi wanaoishi katika mataifa ambayo bado hayajaanza kuwekeza katika mabadiliko haya wamekuwa wakijiuliza je, itawezekana kwao kumiliki magari haya ilhali bado hakuna vituo vya chaja katika nchi zao?.
Bahyad Jafari ambaye ni CEO wa ELECRIC VEHICLES COUNCIL, alipokuwa anatoa maelezo kuhusu magari haya alisema kuwa, "wamiliki wa magari ya kuchaji hutumia magari hayo tofauti na yanayotumia petroli kwani wataweza kuyachaji wakiwa nyumbani au kazini endapo tu k**a kutakuwa na kifaa maalum cha kuchaji".Mfano ni hapo juu katika picha ambayo inaonyesha gari la umeme likichajiwa nyumbani katika chaja yake.
Ni sawa na unavyounganisha simu yako na chaja yake iliyoweka katika soketi.
Hivyo basi utatakiwa kuwa na soketi yake ambayo utaiweka nyumbani au ofisini.
Dr. Whitehead alisema kuwa "ukiongelea kuhusu chaji ya nyumbani basi unapaswa kufahamu kuwa ni chaji inayochukua saa moja kila usiku", akimaanisha kuwa, utatakiwa kuchaji gari lako kwa muda wa saa moja kila usiku.

Vituo vya bararani hivi vitakuwa maalum kwa magari yatakayohitaji kiwango kikubwa sana cha nishati hii, mfano ni k**a magari yatakayotembea kilomita 270 kwa muda wa nusu saa.

Huu ndio ulimwengu ujao na inatabiriwa mpaka kufikia mwaka 2040 hakutakuwa kabisa na magari yanayotumia nishati ya mafuta. Makampuni mengi kwa sasa yameona kuwa hili ni fursa kubwa ya biashara na kuamua kuanza mipango ya kuzalisha magari haya mfano mzuri ni kampuni ya APPLE.

10/08/2021

DISNEY, YOUTUBE PAMOJA NA NETFLIX ZAUNGANA KWA PAMOJA NA KUWA SEHEMU YA BURUDANI KATIKA MAGARI YA TESLA.
kwa muda mrefu kampuni ya utengenezaji wa magari yanayotumia umeme nchini Marekani ijulikanayo k**a TESLA MOTORS, imekuwa ikijiboresha mpaka kufikia hatua ya kuwa miongoni mwa kampuni bora zaidi za utengenezaji wa magari nchini marekani.Kampuni hiyo imekuwa ikitengeneza magari yenye sifa za kipekee ambazo huchochea ukuaji wa soko lake kwa kupendwa na watu wengi sana nchini Marekani na mataifa mengine mengi nnje ya bara la Marekani.
Miongoni mwa vitu vinavyowavutia watu ni muonekano wa magari hayo na pia, magari hayo ni rafiki wa mazingira tofauti na kampuni nyingine za magari kwani magari hayo hutumia umeme tu katika kujiendesha.

Hivi karibuni kampuni ya DISNEY ambayo ni maarufu kwa utengenezaji na usambazaji wa filamu duniani iliungana na mitandao ya NETFLIX pamoja na YOUTUBE na kuwa k**a sehemu ya burudani ndani ya magari ya TESLA.
Watumiaji wa magari hayo watakuwa na uwezo wa kutazama video mbalimbali pamoja na kupakua filamu,miziki na burudani mbalimbali zitakazokuwa zinapatikana ndani ya magari hayo.Hatua hii imetajwa kuongeza mvuto na thamani kwa kampuni hiyo kwani burudani hizo zitaongeza hamasa ya watu kutaka kumiliki magari hayo.

Please follow

10/08/2021

KIPIMO CHA TOZO ZA MATANGAZO KATIKA AKAUNTI ZA MITANDAO YA WATU MAARUFU.
Watu wengi maarufu duniani wamekuwa na kawaida ya kupokea matangazo mbalimbali ya kibiashara toka kwa kampuni au watu binafsi.Matangazo hayo huwekwa katika akaunti zao za mitandao ya kijamii na kuwafikia wafuasi wao.Mara nyingi hapa Tanzania watu wengi wanaangalia wingi wa wafuasi(followers) alionao mtu k**a kigezo kikuu cha mtu huyo kupata biashara nyingi za kupost matangazo.Hiyo inaweza kuwa moja ya sababu lakini je unafahamu kuwa wingi wa followers si kigezo kikubwa sana cha akaunti ya mtu kupata tenda nyingi za kutangaza biashara za watu mbalimbali ?.

ENGAGEMENT RATE, hiki ndio kitu pekee kinachofanya akaunti ya mtu kupendwa na wafanyabishara na kupokea tenda nyingi za matangazo.Engagement rate, hii ni hesabu ambayo inapima kiasi gani wafuasi wako na hata ambao sio wafuasi wako wana shiriki katika post zako unazoweka katika akaunti yako kwa ku-like,kukoment,kushea,kur-reply n.k.
Endapo k**a post zako zinapata ushirikiano mkubwa toka kwa wanaokufuatilia basi hali hiyo inamfanya mtu kuaminiwa kuwa na ushawishi na kupata tenda za matangazo katika akaunti yake.

ENGAGEMENT RATE huwa katika mfumo wa asilimia, endapo k**a akaunti yako itapata asilimia nyingi hii itakufanya kuaminika na kupata biashara nyingi za ku-post katika akaunti yako.
Akaunti zenye ENGAGEMENT RATE kuanzia 3% na kuendelea hizi ndizo mara nyingi hupendwa na wamiliki wa biashara na kuzipa nafasi ya kutangaza biashara zao.
Kwa kutumia ENGAGEMENT RATE tutafahamu ni kiasi gani cha fedha kitahitajika kwa mtu mwenye ushawishi kupost post moja ya tangazo la kibiashara.

Tafadhali follow

10/08/2021

NEBULA, KIWANDA CHA NYOTA ANGANI.
NEBULA ni eneo linalopatikana umbali wa miaka ya mwanga 1,500 kutoka duniani ambapo eneo hili ndipo mahali nyota huzalishwa.
Katika eneo hili maelfu ya nyota huzalishwa ambazo baadhi ni kubwa na nyingine ni ndogo sana kiasi kwamba hatuwezi kabisa kuziona kwa kutumia macho yetu tukiwa huku duniani.

photo:NASA

Tafadhali like,comment pamoja na ku-follow ukurasa huu

10/08/2021

MWEZI NI MALI YA NANI HAPA DUNIANI?๐Ÿค”
Mnamo mwaka 2020 aliyekuwa rais wa Marekani Donald Trump, alitoa ruhusa kwa taifa la USA kuanza harakati za kutafuta rasilimali zilizopo mwezini.
Miaka michache iliyopita taifa la CHINA lilifanya utafiti wa kilimo cha viazi katika ardhi ya mwezi.
Mwaka 2024, shirika la anga la Marekani NASA, linatarajia kufanya safari yake ya kurudi mwezini.
Je, MWEZI ni mali ya nani hapa duniani??๐Ÿค”.

Mnamo tarehe 27/01/1967, mataifa ya USA, UNITED KINGDOM (UK) pamoja na umoja wa nchi za kisovieti(SOVIET UNION), kwa pamoja walisaini mkataba uliojulikana k**a OUTER SPACE TREATY.Mkataba huu ulikuwa na sheria pamoja na miongozo yote ya safari na tafiti za anga pamoja na matumizi sahihi ya rasilimali zinazopatikana angani.
Ndani ya mkataba huu ulielezea kuwa, haijalishi ni bendera ya taifa gani itakayowekwa mwezini, hakuna taifa lolote hapa duniani lenye mamlaka ya kuumiliki mwezi pia, mkataba huo ulielezea kuwa matumizi ya mwezi yanapaswa kufanyika kwa manufaa ya taifa zima.
Mpaka kufikia mwaka 2019, mataifa 109 yalikuwa tayari yameshaingia katika mkataba huo.

Mkataba huo haukuzuia mashirika pamoja na watu binafsi kumiliki vipande vya ardhi vilivyopo mwezini kwani, mnamo mwaka 1980, kampuni ya MOON REAL ESTATE COMPANY LUNAR EMBASSY inayomilikiwa na Dennis Hope, ilianza kuuza vipande vya ardhi mwezini, ambapo, kampuni hiyo iliuza eka moja ya mwezi kwa thamani ya dola za kimarekani 25.Mpaka sasa kampuni hiyo imeshafanikiwa kuuza ekari milioni 611 za ardhi ya mwezini.

Tafadhali like, comment pamoja na ku- follow page yetu ๐Ÿ˜ƒ๐Ÿ‘๐Ÿ’ช

10/08/2021

FAHAMU KUWA WHATSAPP SIO MTANDAO WA KIJAMII.
Kuna baadhi ya watu wanapopewa fursa ya kutaja mitandao ya kijamii wanayoipenda na kuifuatilia basi, hawatoacha kuutaja mtandao wa WhatsApp k**a miongoni mwa mitandao ya kijamii.
Ifahamike kuwa WhatsApp si miongoni mwa mitandao ya kijamii bali WhatsApp ni application maalum kwa ajili ya kutuma na kupokea jumbe mbalimbali(chatting site).

Mitandao ya kijamii k**a instagram, facebook,twitter, Pinterest na mingineyo ilitengenezwa kwa ajili ya watu kushea maoni yao, fikra zao, picha zao pamoja na mifumo yao mbalimbali ya kimaisha ambayo huitoa kwa jamii kubwa ya watu waliopo nao na hata ambao hawapo nao karibu.
Ukija kwa upande wa WhatsApp pamoja na application mbalimbali za kutuma na kupokea jumbe k**a iMessage na messenger hizi zilitengenezwa maalum kwa ajili ya mawasiliano baina ya watu wawili au pengine hata kundi dogo la watu ambao hushea fikra na mawazo mbalimbali.
Kwa kifupi application za mitandao ya kijamii hujumuisha jamii kubwa ya watu, wakati application za kutuma na kupokea jumbe mbalimbali(chatting sites), hujumuisha watu wawili tu au kundi dogo la watu.

Please like, comment and follow our page for more contents๐Ÿ˜€๐Ÿ’ช๐Ÿ‘

10/08/2021

SIKU AMBAYO MWANADAMU ATATAWALIWA NA KUWA MTUMWA WA TEKNOLOJIA.
Kwa dunia ya sasa tuliyopo sayansi na teknolojia zinazidi kukua kwa kasi kubwa sana.
Nadhani umewahi kusikia habari za SINGULARITY na k**a bado, basi twende pamoja.

Katika elimu ya fizikia, neno SINGULARITY linamaanisha sehemu katika shimo jeusi ambapo, endapo kitu chochote kile kitaingia ndani ya shimo hilo, kitu hicho kitasambaratishwa na kupotea milele.
Baadae neno SINGULARITY likaanza kutumika kuelezea mabadiliko makubwa sana ya teknolojia, ambapo, kompyuta zinazofahamika k**a ARTIFICIAL INTELLIGENCE (A.I) zitakuwa na uwezo mkubwa sana wa kiakili kuliko mwanadamu.

Kwa mara ya kwanza, SINGULARITY ilianza kuelezewa na mwanasayansi aliyefahamika kwa jina la VENNA VINCI katika kitabu chake cha THE COMING TECHNOLOGOCAL SINGULARITY.Katika kitabu hicho, VENNA alielezea mambo manne muhimu, yatakayomfanya mwanadamu kuunda kiumbe mwenye uwezo mkubwa wa kiakili, kabla ya mwaka 2030.
VENNA aliendelea kwa kusema kuwa, kati ya mwaka 2030 mpaka mwaka 2045, hapo ndipo dunia itakuwa imeshaingia rasmi katika kipindi cha singularity, na kompyuta za A.I zitakuwa na uwezo mkubwa sana wa kufikiri na kutoa maamuzi k**a wanadamu.

RAY KURZWELL, mwanasayansi na muandishi wa maono ya kiteknolojia, katika kitabu chake cha THE SINGULARITY IS NEAR, yeye anakubaliana na VENNA kuhusu ujio wa teknolojia hii, ila, kwa mtazamo wake yeye anaona teknolojia hii itakuwa na manufaa makubwa kwa wanadamu.Anasema kuwa, teknolojia hii itamsaidia mwanadamu kuongeza ujuzi wake, pia, itamsaidia kutafuta dawa za maradhi mbalimbali pamoja na kutibu magonjwa k**a kupooza na msongo wa mawazo.

Marehemu STEPHEN HAWKING, aliyekuwa mwanasayansi wa nchini Marekani, yeye aliipinga teknolojia hii na kusema kuwa, endapo haitodhibitiwa itaweza kuchukua nafasi kubwa na kuwatawala wanadamu.

Mpaka sasa kuna kila dalili inayoonyesha mwanadamu atatawaliwa na A.I kwani katika baadhi ya makampuni na viwanda leo hii, kazi nyingi hufanywa na ROBOTS.

Wacha tuone jinsi wanadamu watakavyopambana na teknolojia hii pale itakapofika hichooo kipindi cha 2030.

10/08/2021

MLIMA MREFU KULIKO YOTE KATIKA MFUMU WA JUA UNAOONGEZA HAMU YA MWANADAMU KUTAKA KWENDA KUISHI MARS.
Bila shaka ukizungumzia mlima mrefu duniani wote tunafahamu kuwa ni mlima EVEREST, mlima ambao ndipo mahali palipo kilele cha dunia, lakini je, umewahi kusikia habari za mlima mrefu kuliko yote katika mfumo wa jua ?๐Ÿ˜ฎ

Ndio, OLYMPAS MONS, ndio mlima mrefu kuliko yote katika mfumo wetu wa jua, yaani, ukianza sayari ya kwanza mpaka ya tisa, OLYMPAS MONS ndio mlima mrefu zaidi wenye urefu wa kilomita 22 ambapo ni mara tatu ya mlima EVEREST.

Mlima huu unapatikana katika sayari ya MARS ambayo ni sayari ya nne kutoka jua lilipo.
Mlima huu ni aina ya volcano ambapo tafiti zinasema kuwa, uliwahi kulipuka takriban miaka 25 iliyopita,na kurusha mawe makubwa katika anga la sayari ya mars.

Wengi wanajiuliza, kwanini mlima huu ni mrefu kiasi hiki, na je, itawezekana kwa mwanadamu kuupanda mpaka kufika juu ya kilele chake ??๐Ÿค”
Mlima huu umekuwa mrefu kutokana na kani ndogo ya uvutano (low gravity)iliyopo mars na pia kuupanda mpaka kufika kileleni ni changamoto kubwa sana kutokana na mawe mengi yaliyopo katika mlima huo.

Kwa sasa tutegemee selfie za kutosha ifikapo mwaka 2022 ambapo kampuni ya space x inatarajia kufanya safari yake ya kwanza,kwenda katika sayari ya mars kwa lengo la kuanzisha maisha hukoo.๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€

Please like comment and follow our page for more contents๐Ÿ˜€๐Ÿ’ช๐Ÿ‘

NB:picha haina uhusiano na taarifa

10/08/2021

DUNIANI TUNAISHI KATIKA NDOTO ZA WATU WALIOKWISHAFARIKI MIAKA MINGI ILIYOPITA.
Endapo k**a leo hii utamfufua mtu aliyefariki miaka 100 iliyopita na kumrudisha duniani,basi mtu huyo anaweza kustaajabu na kushangaa jinsi ulimwengu ulivyobadilika, kutokana na mapinduzi makubwa ya sayansi yaliyotokea na yanayoendelea kutokea duniani.
Maisha tunayoishi sasa yalikuwa ni ndoto kwa watu walioishi miaka ya zamani sana,na pia ni maisha ambayo yalionekana kuwa hayatowezekana kabisa kuwepo kwa ulimwengu wa sasa.
Katika ulimwengu wa sayansi kuna aina ya taaluma ijulikanayo k**a BUNILIZI YA KISAYANSI, ama kwa lugha ya kitaalamu hujulikana k**a SCIENCE FINCTION.
Hii ni aina ya fasihi,filamu,michezo ya video au sanaa iliyokuwepo toka miaka ya zamani sana ambapo watu walikuwa wakiandika na kutabiri habari za sayansi na teknolojia ambayo itakuja kutokea kwa miaka ijayo,pamoja na kuchukua nafasi kubwa katika maisha ya mwanadamu.Waswahili husema lisemwalo lipo na k**a halipo basi linakuja,hapa waswahili hawakukosea kabisa๐Ÿ‘.
Mara nyingi bunilizi ya kisayansi huelezea vifaa na sayansi ambayo haipatikani leo hii,bali itakuja kuwepo miaka ya mbeleni.
Mtu wa kwanza aliyewahi kuandika bunilizi yake ni mwandishi kutoka Ufaransa aliyejulikana k**a JULES VERNE, ambaye aliwaza matumizi ya bunduki kubwa itakayomwezesha mwanadamu kufika mwezini.Wakati anaandika haya,watu wengi walimshangaa na kuona kuwa ni kitu kisichowezekana kabisa, ila miaka ya sasa hilo limekuwa ni jambo linalowezekana na pia tunatarajia mwaka 2024 taifa la USA litafanya safari yake kwenda mwezini.
Nadhani sasa umeanza kunielewa kidogo.
Yupo mtu aliyefahamika k**a H.G.WELLS,ambaye aliwaza kuwa miaka ya mbeleni kutakuwa na mashine yenye uwezo wa kupaa angani (aeroplane),pia aliwaza kuwepo kwa mashine za kivita k**a vifaru lakini pia,aliwaza kuwa miaka ijayo kutakuwa na runinga.Hivi sasa vitu vyote alivyowaza mtu huyu vipo, wakati kipindi anayesema haya watu waliona ni ndoto za mchana.
Mtu mwingine ni ISAAC ASIMOV profesa wa masuala ya biokemia ambaye pia alikuwa mwandishi wa bunilizi za kisayansi,yeye aliandika kuhusiana na matumizi ya roboti.
Tusishangae kuona siku moja ELON MUSK akafanikiwa kumfanya mtu aishi milele.๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€

10/08/2021

MNARA MPYA WA DUBAI.
Ukizungumzia mji wenye majengo marefu duniani huwezi acha kuitaja DUBAI.
Dubai ndipo mahali panapopatikana jengo refu duniani, BURJ KHALIFA lenye urefu wa mita 828.
Miaka iliyopita Dubai ilitangaza rasmi kuanza ujenzi wa jengo lingine refu zaidi ya BURJ KHALIFA ambalo litakuwa na shape inayofanana na rocket.Taarifa kamili za urefu wa jengo hilo bado hazijatolewa ila inatajwa kuwa na urefu unaozidi mita 828.
Kwa taarifa zisizo rasmi zinasema kuwa jengo hilo litakuwa na urefu wa takriban mita 1300 ๐Ÿ˜ฎ๐Ÿ˜ฎ๐Ÿ˜ฎ
Engineer maarufu SANTIAGO CALATRAVA ndie mchoraji wa ramani ya jengo hilo na pia ndie aliechora ramani ya burj khahila.
Kwa matarajio jengo hilo lilikuwa likamilike mwaka 2020 ila kutokana na COVID19 ujenzi wake ulisitishwa.
Nako pia nchini Saudi Arabia wanaendelea na ujenzi wa jengo refu kuliko yote nchini humo litakaloitwa JEDDAH TOWER,ambalo litakuwa na urefu wa mita 1007.

Please like, comment and follow our page for more contents๐Ÿ˜€๐Ÿ’ช๐Ÿ‘

Want your school to be the top-listed School/college in Arusha?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Category

Telephone

Website

Address


Arusha