BHEU

BHEU

Share

Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from BHEU, Casino, Bucharest.

24/03/2023
24/03/2023

📻Tunayokuandalia katika matangazo yetu Mchana huu ni pamoja na:
👉Rais Tshisekedi wa Kongo afanya mabadiliko makubwa ya baraza lake la mawaziri. Miongoni mwa mawaziri 57 ni pamoja na Jean-Pierre Bemba kuteuliwa kuwa waziri wa Ulinzi na muana siasa Vital Kamerhe kuwa waziri wa Uchumi. Utasikiliza pia uchambuzi wa kina kuhusu mageuzi hayo kabla ya uchaguzi mkuu wa Desemba.

👉Tanzania imetoa msaada wa fedha Dola za Marekani milioni $1,000,000 kwa Uturuki kama msaada wa kibinadamu kufuatia taifa hilo kukumbwa na janga la tetemeko la ardhi. Hatua hiyo imeibua mjadala mkubwa miongoni mwa jamii huku baadhi wakionekana kupongeza lakini wengine wanalaumu wakisema msaada huo unatolewa wakati maeneo mengi ya nchi yanakabiliwa na hali ngumu.

👉Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ameapa kukabiliana na mpasuko uliopo katika taifa hilo lililogawanyika pakubwa kufuatia mapendekezo yake juu ya mageuzi kwenye mfumo wa mahakama nchini humo. Haya yanakuja wakati upinzani dhidi ya mageuzi hayo ukiongezeka na ukizuwa wasiwasi wa mpasuko kwenye taifa hilo la Mashariki ya Kati.

👉Na utasikia pia uchambuzi kuhusu klabu ya bayern Munich kumfuta kazi kocha wake Julian Nagelsmann usiku wa kuamkia leo na kumteua Thomas Tukheri, aliekuwa kocha wa Chelsea na mshindi wa ligi ya mabindwa barani Ulaya kuchukua nafasi.

Want your establishment to be the top-listed Arts & Entertainment in Bucharest?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Category

Telephone

Website

Address


Bucharest