Mtitu's Blog

Mtitu's Blog

Share

Mtitu family

25/03/2025

U T E U Z I.🧠✍️

25/03/2025

Huyuu msemajii anakumbushia wakati tulishasahau😁😁

25/03/2025

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa Palamagamba Kabudi amepanga kukutana viongozi wa Shirikisho la Soka la chini (TFF), Bodi ya Ligi Kuu ya Tanzania (TPLB) na Klabu ya Yanga ili kutatua mgogoro unaoendelea kuhusu kusogezwa mbele kwa mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Jumatatu Machi 24, 2025, kikao hicho kitafanyika jini Dar es Salaam, Alhamisi na maofisa kutoka Yanga, Simba, TFF na Bodi ya Ligi Kuu wamejulishwa na watahudhuria.

"Ni kweli tutakutana na Waziri Kabudi kuhusu masuala mbalimbali, ikiwemo kusogezwa mbele kwa mchezo wetu dhidi ya Simba. Tumepokea barua na tutahudhuria," alisema afisa mmoja wa Yanga aliyeomba kutotajwa kwa jina.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa alithibitisha kikao hicho kitafanyika jijini Dares Salaam kikiongozwa na Waziri Kabudi. Msigwa pia alieleza maofisa wa Simba watashiriki katika kikao hicho.

Mchezo huo, ambao ulikuwa umepangwa kufanyika Machi 8 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, uliahirishwa baada ya Simba kudai makomandoo wa Yanga waliwakatalia kuingia uwanjani kwa ajili ya mazoezi yao ya kabla ya mchezo.

25/03/2025

Mambo ya mitandaoni🧠✍️Sasa Itakuwajee

24/03/2025

Nahodha wa kikosi cha Uganda Cranes (Timu ya taifa la Uganda), amepata majeraha akiwa kwenye majukumu ya timu ya taifa hilo wakati wakijiandaa na mchezo wa kuwania nafasi ya kushiriki michuano ya kombe la dunia 2026 dhidi ya Guinea mapema wiki hii.🧠✍️

24/03/2025

Watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa Al-Shabab, kundi lenye mafungamano na Al-Qaeda, wamevamia kambi ya polisi katika Kaunti ya Garissa, mashariki mwa Kenya, na kuwaua polisi sita huku wengine wanne wakijeruhiwa, mamlaka imethibitisha.

Kwa mujibu wa ripoti ya polisi iliyotumwa kwa vyombo vya habari, shambulio hilo lilitokea Jumapili alfajiri, ambapo washambuliaji waliwashambulia askari waliokuwa kambini kwa kutumia silaha mbalimbali na kufanikiwa kuiteka kambi hiyo kwa muda.

"Watu sita wamefariki dunia na wengine wanne wamejeruhiwa na wako hospitalini," ripoti ya polisi imeeleza.

Kundi la Al-Shabab mara kwa mara limekuwa likitekeleza mashambulizi katika maeneo ya mpakani kati ya Kenya na Somalia, likilenga jeshi, polisi na raia wa kawaida.

Katika hatua nyingine, Ubalozi wa Marekani nchini Kenya umetangaza tahadhari kwa raia wake Jumanne, ukiwataka kuepuka kusafiri katika maeneo yenye hatari ya ugaidi, yakiwemo Garissa na kaunti nyingine zinazopakana na Somalia.

Kwa miaka kadhaa, Al-Shabab imekuwa ikipambana na serikali ya Somalia kwa lengo la kuipindua na kuanzisha utawala wake katika eneo la Pembe ya Afrika.

Wakati huohuo, watu wasiopungua 44 wameuawa na wengine 13 kujeruhiwa vibaya baada ya wanamgambo kuvamia msikiti nchini Niger, mamlaka ya ulinzi imesema.

Shambulio hilo lilitokea siku ya Ijumaa wakati wa sala za alasiri katika kijiji cha Fombita, kilicho katika eneo la Kokorou, karibu na mpaka wa Niger, Burkina Faso na Mali.

Kwa mujibu wa Wizara ya Ulinzi ya Niger, washambuliaji walizingira msikiti huo na kuwaua waumini kwa ukatili wa hali ya juu, kabla ya kuchoma soko na nyumba za wananchi. Mamlaka ililaumu kundi la EIGS, tawi la Daesh lililo na mizizi katika eneo hilo, kwa kuhusika na shambulio hilo.

Uasi wa wanamgambo katika eneo la Sahel ulianza mwaka 2012 baada ya waasi wa Tuareg kuchukua udhibiti wa kaskazini mwa Mali. Tangu wakati huo, ghasia zimeenea hadi nchi jirani k**a Burkina Faso na Niger, pamoja na baadhi ya mataifa ya pwani ya Afrika Magharibi k**a Togo na Ghana.

Machafuko haya yamesababisha vifo vya mamia ya maelfu ya watu na mamilioni kuyahama makazi yao.

24/03/2025

: Ufaransa na Uhispania zimefanikiwa kufuzu hatua ya Nusi fainali ya UEFA National League, Ufaransa wakiiondosha Croatia kwa mikwaju ya penati 5-4, huku Uhispania nao wakiwapiga Uholanzi kwa mikwaju ya penati 5-4.

Timu hizi zitakutana katika hatua ya Nusu fainali baada ya kufanikiwa kuvuka kibabe katika hatua ya Robo fainali.

Huku yupo Mbappe kule Yamal nani atafanikiwa kutinga fainali?

FT: Ufaransa 2-0 Croatia (2-2)
FT: Spain 2-2 Netherlands (4-4)

EXTRA TIME:

120' Spain 3-3 Netherlands (5-5)
PENATI 5-4

120' France 2-0 Croatia (2-2)
PENATI (5-4)

24/03/2025

MKUU Majeshi wa Uganda, Muhoozi Kainerugaba, ambaye ni mtoto wa Rais Museveni, amesema kuwa vikosi vyake vitadhibiti mji wa Kisangani, iwapo waasi wa M23 watachelewa kuuteka mji huo.

Kupitia mtandao wake wa kijamii wa ‘X’ amezungumzia mengi kuhusu DRC, Kainerugaba amesema jeshi lake au waasi wa M23 wataingia Kisangani, kwa agizo la Rais Yoweri Museveni, ili kuwaokoa wakazi wa mji huo wakati wowote kutoka sasa.

Wanajeshi wa Uganda wamekuwa nchini DRC, wakishirikiana na jeshi la FARDC, kupambana na makundi yenye silaha wakiwemo waasi wa CODECO na ADF ambapo Kainerugaba ameonekana kuongelelea kuwa nia ya kulinda wakazi wa DRC.

Kainerugaba ameapa kuwa hataacha wakazi wenye asili ya Uganda k**a vile Alurs, Bahema, Banande na Batutsi wapitie changamoto na kusema ana haki ya kuwalinda huku akipedekeza Rais wa Marekani, Donald Trump, asiingie katika mkataba wowote wa madini Afrika Mashariki bila Uganda na Rwanda.

Licha ya waasi wa M23 kuchukua miji kadhaa ya mashariki mwa Congo, waasi hao hawajaonesha nia ya kutaka kudhibiti mji wa Kisangani huku M23 ikidai inapanga kujiondoa katika mji wa Walikale, ili kutoa nafasi ya mazungumzo na Serikali.

#🧠✍️

24/03/2025

MKUU Majeshi wa Uganda, Muhoozi Kainerugaba, ambaye ni mtoto wa Rais Museveni, amesema kuwa vikosi vyake vitadhibiti mji wa Kisangani, iwapo waasi wa M23 watachelewa kuuteka mji huo.

Kupitia mtandao wake wa kijamii wa ‘X’ amezungumzia mengi kuhusu DRC, Kainerugaba amesema jeshi lake au waasi wa M23 wataingia Kisangani, kwa agizo la Rais Yoweri Museveni, ili kuwaokoa wakazi wa mji huo wakati wowote kutoka sasa.

Wanajeshi wa Uganda wamekuwa nchini DRC, wakishirikiana na jeshi la FARDC, kupambana na makundi yenye silaha wakiwemo waasi wa CODECO na ADF ambapo Kainerugaba ameonekana kuongelelea kuwa nia ya kulinda wakazi wa DRC.

Kainerugaba ameapa kuwa hataacha wakazi wenye asili ya Uganda k**a vile Alurs, Bahema, Banande na Batutsi wapitie changamoto na kusema ana haki ya kuwalinda huku akipedekeza Rais wa Marekani, Donald Trump, asiingie katika mkataba wowote wa madini Afrika Mashariki bila Uganda na Rwanda.

Licha ya waasi wa M23 kuchukua miji kadhaa ya mashariki mwa Congo, waasi hao hawajaonesha nia ya kutaka kudhibiti mji wa Kisangani huku M23 ikidai inapanga kujiondoa katika mji wa Walikale, ili kutoa nafasi ya mazungumzo na Serikali.

24/03/2025

FULL TIME ⏰

France 🇫🇷 2️⃣ ➖ 0️⃣ Croatia 🇭🇷 (AGG 2-2)
⚽️ 52' Olise
⚽️ 80' Dembele (🅰️ Olise)
✅ PENATI 5-4

Spain 🇪🇸 3️⃣ ➖ 3️⃣ Netherlands 🇳🇱 (AGG 5-5)
⚽️ 8' Oyarzabal (P)
⚽️ 54' Depay
⚽️ 67' Oyarzabal
⚽ 79' Maatsen (🅰️ Xavi Simons)
⚽️ 103' Lamine Yamal (🅰️ Huijsen)
⚽️ 109' Xavi Simons (P)
✅ PENATI 5-4

Portugal 🇵🇹 5️⃣ ➖ 2️⃣ Denmark 🇩🇰 (AGG 5-3)
⚽️ 38' Andersen (OG)
⚽️ 56' Kristensen(🅰️ Eriksen)
⚽️ 72' Ronaldo
⚽️ 76' Eriksen (🅰️ Dorgu)
⚽️ 86' Trincao (🅰️ Nuno Mendes)
⚽️ 91' Trincao (🅰️ Goncalo Ramos)
⚽️ 115' Goncalo Ramos (🅰️ Jota)

Germany 🇩🇪 3️⃣ ➖ 3️⃣ Italy 🇮🇹 (AGG 5-4)
⚽️ 30' Kimmich (P)
⚽️ 36' Musiala (🅰️ Kimmich)
⚽️ 45' Kleindienst (🅰️ Kimmich)
⚽️ 49' Moise Kean
⚽️ 69' Moise Kean (🅰️ Raspadori)
⚽️ 90+5' Radpadori (P)

Nusu Fainali ya Uefa Nations League
🇫🇷 FRANCE vs SPAIN 🇪🇸
🇩🇪 GERMANY vs PORTUGAL 🇵🇹

Want your business to be the top-listed Realtor/realty Service in Njombe?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Category

Website

Address

148
Njombe