Bakela Apdates og
Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Bakela Apdates og, Women's clothes shop, Mwanza.
29/05/2026
Allan Okelo ni mchezaji wa mpira wa miguu kutoka Uganda anayejulikana kwa uwezo wake mkubwa wa kiufundi, pasi za mwisho, na ubunifu akiwa eneo la kati la uwanja. Amezaliwa Julai 4, 2000, na amekuwa mmoja wa vipaji vilivyoibuka kwa kasi Afrika Mashariki katika miaka ya hivi karibuni.
Mwanzo wa safari yake ya soka
Okello alianza kujitengenezea jina lake akiwa bado mdogo kupitia klabu ya KCCA FC nchini Uganda. Hapo ndipo alipoanza kuonyesha kipaji cha kipekee cha kucheza k**a kiungo mshambuliaji, akifunga mabao na pia kutoa assist nyingi kwa washambuliaji wenzake.
Uchezaji wake ulivutia macho ya watazamaji wengi na makocha, jambo lililosababisha kupanda kwake haraka kwenye soka la kulipwa.
Safari ya nje ya Uganda
Baada ya kufanya vizuri KCCA, alipewa nafasi ya kucheza nje ya nchi na kujiunga na klabu ya Paradou AC ya Algeria. Huko alikumbana na ushindani mkubwa zaidi, ambao ulimsaidia kuongeza uzoefu na uimara wa kimchezo.
Kurudi Afrika Mashariki na mafanikio mapya
Baada ya kipindi cha Algeria, Okello alirudi Afrika Mashariki na kuendelea kung’ara zaidi. Uchezaji wake uliendelea kuimarika akiwa kwenye klabu tofauti, ambapo uwezo wake wa:
kupiga pasi za mwisho (key passes)
kufunga kutoka umbali
na kuchezesha timu
ulizidi kuonekana wazi.
Kwa sasa anatajwa kuichezea Young Africans SC (Yanga SC) ya Tanzania, mojawapo ya klabu kubwa zaidi Afrika Mashariki, ambako anatarajiwa kuongeza nguvu kwenye safu ya kiungo.
Aina ya uchezaji wake
Allan Okello ni mchezaji mwenye sifa hizi:
⚽ Ubunifu mkubwa wa mashambulizi
🎯 Pasi za hatari (killer passes)
💥 Uwezo wa kufunga mabao ya mbali
🧠 Uelewa mzuri wa mchezo (game intelligence)
Huwa anacheza zaidi k**a “number 10”, yaani kiungo anayebeba mzigo wa kuunda nafasi za mabao.
Timu ya taifa ya Uganda
Okello pia ni sehemu ya timu ya taifa ya Uganda (The Cranes) ambapo amecheza mechi mbalimbali za kimataifa, akiwakilisha nchi yake katika mashindano ya Afrika.
Hitimisho
Allan Okello ni mfano wa mchezaji kijana
UPDATE
12/02/2026
Wananchi wakilia kwa uchungu Mahak**a Kuu baada ya Mhe. Tundu Lissu kutokula mchana wa leo baada ya mapumziko ya muda mfupi.
Wananchi wengine walizimia.
Lissu, Mwenyekiti wa Chadema anayekabiliwa na kesi ya Uhaini alilalamika leo kutopewa Chakula.
APDATES og
16/11/2025
"Taarifa zilizotufikia hivi punde zinaeleza kuwa mchekeshaji na mshereheshaji maarufu nchini Tanzania, Mathias, anayefahamika zaidi k**a MC Pilipili, amefariki dunia ghafla mchana wa leo, Novemba 16, 2025.
Chanzo cha taarifa kinasema kuwa MC Pilipili alikuwa safarini kuelekea jijini Dodoma, ambako alikuwa amepangiwa kufanya kazi ya ushereheshaji jioni ya leo. Hata hivyo, akiwa njiani alipatwa na umauti kabla ya kufika kwenye shughuli hiyo.
Aidha kupitia Global TV , Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya General, Dodoma, Dkt. Ernest Ibenzi, amethibitisha kifo hicho, akieleza kuwa MC Pilipili alifikishwa hospitalini hapo akiwa tayari ameshafariki dunia".
BAKELA APDATES og
08/11/2025
James Watson, Mshindi wa Tuzo ya Nobel wa Marekani na Mgunduzi katika utafiti wa DNA, amefariki akiwa na umri wa miaka 97.
Kazi yake katika Sayansi ilikumbwa na matamshi ya kibaguzi, ambayo yalimlazimu kujiuzulu wadhifa wake katika Maabara ya kifahari akiwa na umri wa miaka 80.
Akiwa ametengwa na sehemu ya Jumuiya ya Wanasayansi, aliamua mwaka 2014 kupiga mnada medali yake ya Nobel.
Watson alizaliwa huko Chicago mnamo Aprili 1928 kwa Jean na James, walowezi wa Kiingereza, Scotland na Ireland.
Alishinda udhamini wa kusoma katika Chuo Kikuu cha Chicago akiwa na umri wa miaka 15.
APDATES og
07/11/2025
Taarifa zilizotufikia zinasema, Aliyekuwa Mgombea wa nafasi ya Uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Tulia Ackson, ametangaza rasmi kujiondoa katika kugombea nafasi hiyo.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa Dkt. Tulia amefanya uamuzi huo leo Novemba 7 2025.
Apdates og
07/11/2025
RATIBA YA SIMBA SC LIGI YA MABINGWA🔥
Hii Ni Ratiba Ya Mnyama-Simba SC Kwenye Ligi Ya Mabingwa Afrika Msimu Wa 2025-2026.
APDATES og
07/11/2025
Meneja wa Manchester United, Ruben Amorim ameshinda tuzo ya kocha bora wa mwezi Oktoba 2025 wa Ligi Kuu England baada ya kuiongoza klabu hiyo kushinda mechi tatu mfululizo kwa mara ya kwanza tangu achukue mikoba ya kuinoa timu mnamo Novemba 2024.
Ndani ya Mwezi Oktoba, kocha huyo wa zamani wa Sporting Lisbon aliwaongoza Mashetani hao Wekundu kushinda 2-0 nyumbani dhidi ya Sunderland, kabla ya kuichapa Liverpool 2-1 ugenini na kuhitimisha mwezi Oktoba kwa ushindi mnono wa 4-2 nyumbani dhidi ya Brighton.
Amorim raia wa Ureno amewashinda Mikel Arteta wa Arsenal (mechi 3, ushindi 3), Unai Emery wa Aston Villa mechi 3, ushindi 3) na Andoni Iraola wa AFC Bournemouth (mechi 3, ushindi 2, sare 1) aliokuwa nao kwenye kinyang'anyiro cha tuzo hiyo.
APDATES og
05/11/2025
Mshambuliaji wa klabu ya Yanga Sc, Clement Mzize anatarajiwa kuwa nje ya uwanja kwa takribani wiki nane (8) mpaka kumi (10) baada ya kufanyiwa upasuaji kutokana na maumivu ya goti yaliyokuwa yakimkabili.
Hayo yameelezwa na Meneja wa Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo, Ally Shaban Kamwe leo Novemba 5, 2025 na kubainisha kuwa uamuzi huo umekuja baada ya kuona anaendelea kupata maumivu kwenye goti lake kila alipokuwa akirejea uwanjani huku jopo la madaktari wakishirikiana na benchi la Ufundi na Mchezaji mwenyewe wakishauri upasuaji ufanyike.
"Mara ya mwisho tuliwajulisha kuhusu hali ya majeraha ya mchezaji Clement Mzize. Baada ya ushauri wa jopo la madaktari wakishirikiana na benchi la Ufundi na Mchezaji mwenyewe tulikubaliana afanyiwe upasuaji.
"Maamuzi haya yalikuja baada ya kuona anaendelea kupata maumivu kwenye goti lake kila alipokuwa akirejea uwanjani. Nipende kuutangazia Umma kuwa, mchezaji Clement Mzize atakuwa nje ya uwanja kwa wiki nane mpaka kumi," — Ali Kamwe
Apdates og
25/10/2025
Ghana 🇬🇭 close your eyes, you will open them in 2026 when going to the World Cup.
25/10/2025
Kikosi kazi
Click here to claim your Sponsored Listing.