LINDA AFYA YAKO

LINDA AFYA YAKO

Share

Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from LINDA AFYA YAKO, Health/Beauty, Mwanza, Mwanza.

21/01/2024

Shout out to my newest followers! Excited to have you onboard!

Hassani Sikinino, Isaya Mgata

10/01/2024

Madhara ya PID moja wapo ni kutoa UCHAFU mweupe mzito sehemu za SIRI ZA MWANAMKE usikubali uteswe na Hali hii njoo upate ushauri na TIBA

Photos from LINDA AFYA YAKO's post 17/10/2019

*JE, UNAJUA UGONJWA WA BAWASIRI (HEMORRHOIDS) NI NINI????!!*

~Ni ugonjwa unaotokana na kuathirika kwa mishipa ya damu ya ndani na nje ya sehemu ya haja kubwa na wakati mwingine mishipa hiyo huweza kupasuka/kuteleza na kuvuja damu kwenye njia ya haja kubwa na kasababisha kutoka kinyama au uvimbe.

~ugonjwa huu wa bawasiri kwa lugha ya kitaalamu unaitwa HEMORRHOIDS ilhali kwa lugha ya kingereza unafahamika k**a PILES. Katika jamii yetu ya KiTanzania ugonjwa huu unatambulika kwa majina tofautitofauti yakiwemo *bawasiri, mgolo, mang'ondi n.k*

~tatizo hili huwaathiri watu wote ila zaidi huwaathiri watu wazima kuliko watoto na inakadiriwa kuwa _karibu 50%ya watu wote wako katika hatari ya kupata tatizo hili katika umri wa miaka 30_50_

*AINA ZA BAWASIRI*
~Kuna Aina mbili za bawasiri

*(A) BAWASIRI YA NDANI*
~Aina hii ya bawasiri hutokea ndani ya mfereji wa haja kubwa huwa haiambatani na maumivu na wengi huwa hawajitambui kuwa Wana tatizo hili

~Aina hii hutokana na kuvimba na kuharibika kwa mshipa wa artery za ndani ya mfereji wa haja kubwa

~Aina hii imegawanyika katika madaraja manne

(1)DARAJA LA KWANZA ~Hii ni bawasiri ambayo haitoki mahali pale panapohusika

(2)DARAJA LA PILI ~hii hutokea wakati wa haja na kurudi yenyewe ndani baada ya kujisaidia.

(3)DARAJA LA TATU :hii hutokea wakati wa haja kubwa na mtu kuweza kurudisha ndani yeye mwenywe.

(4)DARAJA LA NNE : hii ni bawasiri inayotoka na huwa ngumu kurudi.

*(B)BAWASIRI YA NJE*
~Aina hii ya bawasiri hutokea katika eneo la mwisho kabisa la mfereji wa haja kubwa na huambatana na maumivu makali na kuwashwa kwa ngozi katika eneo la tundu hilo. Pia husababisha mishipa ya damu (vena) kupasuka na damu kuganda na kasababisha aina ya bawasiri iitwayo _THROMBOSED HEMORRHOIDS_

*NINI CHANZO CHA BAWASIRI?*

Bawasiri ni tatizo linaloanzia kwenye mfumo wa mmeng'enyo wa chakula. Huu mfumo ukishakua mbovu una kupelekea kutokupata choo vizuri.

Mfumo mbovu wa mmeng'enyo wa chakula unasababisha chakula kisimeng'enywe vizuri kwenye utumbo mdogo na hivyo kupelekea chakula kupitiliza kwenda moja kwa moja k**a kilivyo kwenda kwenye utumbo mkubwa ambapo maji maji kutoka kwenye chakula hufyonzwa na kuacha chakula kikiwa kikavu. Inapofikia wakati wa kupata choo; choo kinakua kikavu hivyo unatumia nguvu nyingi kukisukuma choo kitoke.

Sasa kitendo hicho kinapelekea misuli & mishipa ya haja kubwa kutanuka na kupelekea kukwanguliwa na choo kigumu na hivyo kinyama kuanza kujitengeneza, na hapo ndipo utaanza kusikia maumivu na miwasho kwa ndani, na mara nyingine kupata choo chenye damu.

Kadri unavyoendelea kupata choo kigumu mishipa inaendelea kukwanguliwa na kinyama kuongezeka mpaka kinatokezea nje na hicho kinyama kinaitwa Bawasiri (Hemorrhoids).

Mtu mwenye afya nzuri anapata choo kulingana na milo anayopata kwa siku. K**a anauwezo wakupata milo mitatu kwa siku, anastahili kupata choo mara tatu kwa siku, tena choo chako kitoke na urefu sawa wa ndizi mbivu, bila kujikatakata k**a kile cha mbuzi.

_VIFUATAVYO NI MIONGONI MWA VITU VINGINE VICHANGIAVYO MTU KUPATA UGONJWA HUU WA bawasiri:_
👁 Kufanya mapenzi kinyume na maumbile.
👁 Kuharisha kwa muda mrefu·
👁 Tatizo la kutopata choo laini au kujisaidia kinyesi kigumu *(Constipation)*
👁 Umri mkubwa·
👁 Uzito kupita kiasi (Uzito uliopindukia)
👁 Ujauzito (kwa baadhi ya wajawazito)
👁 Matumizi ya vyoo vya kukaa kwa muda mrefu.

*DALILI ZA UGONJWA WA BAWASIRI*
–CHUKUA TAHADHARI MAPEMA, uonapo dalili hizi:
⚠ kuwashwa katika ngozi ya eneo la tundu la haja kubwa. Huu muwasho unakuja kwa kujirudia mara kwa mara baada ya muda fulani.
⚠ Kukatishwa kwa haja kubwa na kurudi ndani wakati wa kujisaidia.
⚠ Kuhisi kutomaliza haja (kuhisi kitu kigumu kubaki ndani) baada ya kujisaidia haja kubwa.
⚠ Kujitokeza kwa uvimbe katika eneo la tundu la haja kubwa . Uvimbe huu unaanza kuota k**a upelepele.
⚠ Kujitokeza kwa kijinyama katika tundu la haja kubwa. Kinyama hiki kinaanzia ndani ya tundu la haja kubwa. kikitokea nje, ujue kwamba una hili tatizo la bawasiri kwa muda mrefu.
⚠ Kujisaidia kinyesi chenye damu mbichi na chenye kunuka harufu mbaya sana.

❗ *MADHARA YA UGONJWA HUU:*
Hebu tupitie angalau kwa uchache madhara ya bawasiri, ili upate sababu za msingi za KUCHUKUA TAHADHARI NA HATUA YA KULISHUGHULIKIA MAPEMA:
😣 Kupata *maumivu makali wakati wa kujisaidia* haja kubwa na kusababisha mishipa ya sehemu ya haja kubwa kukwanguliwa.
😣 Kuna uwezekano mkubwa wa kupata *saratani ya utumbo (Cancer)* kwa sababu kile kinyama kinakaa k**a kidonda
😣 *Kutopata hamu ya tendo la ndoa* _kwa jinsia zote._
😣 *Upungufu wa nguvu za kiume* kwa mwanamume , ikiwemo *uume kushindwa kusimama kwa muda unaotakiwa* hivyo kupelekea kupotea kwa heshima ya ndoa.
😣 Kuathirika *kisaikolojia*
😣 *Kutojiamini/kutokuwa na amani katika hadhara ya watu* kutokana na adha zake ikiwemo ile ya kujikuna kutokanako na kuwasha kwa ngozi ya eneo la tundu la haja kubwa (puru).

💡 *JINSI YA KUJIEPUSHA (Kwa wewe usiyenalo bado KABLA HALIJAKUPATA) NA KUDHIBITI (Kwa yeye aliye tayari analo) TATIZO HILI LA BAWASIRI:*

👉🏽Jitahidi kupata mlo kamili kila siku. Tumia _matunda na mboga za majani kwa wingi (kila mlo)_,
👉🏽 Kunywa maji ya kutosha. _Angalau lita 3 kwa siku_ (kulingana pia na uzito wako),
👉🏽 Epuka kukaa chooni kwa muda mrefu,
👉🏽Jifunze mkao sahihi & salama wa kutumia Choo cha kukaa ili kujiepushia na tatizo hili,
👉🏽Jiepushe na vilevi,
👉🏽 K**a usafishavyo mwili wako mzima kwa kuoga, tena zaidi ya mara moja kwa siku, _Jenga pia utaratibu wa kusafisha ndani mwili wako mzima_ kwa kutumia program za kilishe za kusafisha mifumo ya mwili mzima yaani *Whole Body Cleansing Program*, na _*hii huhusisha na usafi wa mfumo mzima wa usagaji chakula)*_
ili utoe taka mwili zote _*(zikiwemo za utumboni),*_ na uondoe sumu mwilini. Hii huepusha sana tatizo hili.

(Wasiliana nasi kwa uhitaji wa program hii ya kusafisha mwili mzima, kuondoa sumu na kupunguza mafuta mwilini), *UKIHITAJI!*

💡 *MATIBABU:*
Ugonjwa huu unatibiwa kwa namna mbalimbali kuu zikiwa za kihospitali ambapo kuna upasuaji (surgical operations) na kwa dawa bila upasuaji. Pia zipo za kiasili/kijadi (Traditional).

⚠ *NB:* Una dukuduku, swali au jambo lolote kuhusu tatizo hili au tatizo lingine lolote la kiafya? au umesumbuka/ kuna ambaye amesumbuka na kuutibu ugonjwa huu, _*kwa muda mrefu,*_ kwa njia hizo pasi mafanikio ya kuumaliza kabisa? au umekuwa ukijirudiarudia.

Utapata majibu/Utasaidika/Atasaidika maana kuna suluhu nyingine ya kudumu, salama na ya hakika ya hilo la bawasiri na mengine pia.

Kwa msaaada na ushauri piga +255758112230

07/07/2019

DALILI ZA UGONJWA WA PID
%Kutokwa na uchafu mzito sehemu za siri, yawezekana ukawa ni mweupe, njano, au maziwa
%Kuwashwa sehemu za siri
%Uke kutoa harufu mbaya
%Maumivu ya tumbo chini ya kitovu
%Uke kuwa wa ulaini sana
%Maumivu wakati wa tendo la ndoa
%Kuvurugika Kwa hedhi
%Kutokwa majimaji ukeni kupita kiasi
%Maumivu wakati wa kukojoa na wakati wa choo kubwa
%Homa, uchovu,kizunguzungu na kukosa hamu ya kula

MADHARA YA PID
•Ugumba
•Kansa ya shingo ya kizazi
•Mirija ya uzazi kuziba
•Majeraha kwenye mirija ya uzazi

TIBA
Tumia kirutubisho cha FEMININE WASH ni ya maji ambayo utatumia kuoshea kwa bibi
Pia Ipo COMPLETE PHYTO-ENERGIZER hii ni ya vidonge kwa wale ambao wamepata madhara tayari mpka kwenye kizazi
kwa maelezo,ushauri na jinsi ya kuipata
Usisite kunitafuta WhatsApp 0758112230
au nipigie au tuma ujumbe 0686044571
Nipo tayari kukuhudumia🙏🙏🙏

Photos from LINDA AFYA YAKO's post 09/05/2019

KUKOMESHA KISUKARI NI MIMI NA WEWE
Ndugu msomaji nikukaribishe tena katika mwendelezo wa makala haya ya ugonjwa hatari wa kisukari kwa leo tukiangazia athari kubwa zinazowezasababishwa na kisukari karibu.

TULIPOISHIA MAKALA YALIYOPITA
Kwani kwa mujibu wa ripoti ya shirika la afya duniani(WHO)inadai magonjwa yasiyo ya kuambukiza ndio chanzo kikubwa cha vifo duniani yakifanya ongezeko ya vifo vyote kwa kila mwaka.
Inakisiwa kuwa mwaka wa 2020 magonjwa haya yasiyo ya kuambukiza yatasababisha asilimia 73 ya vifo vyote duniani na asilimia 60 ya ukubwa wa tatizo la magonjwa duniani.
SONGA MBELE ZAIDI..............

Kutokana na kuwepo kwa athari mbalimbali ambazo husababishwa na ugonjwa huu usiowa kuambukiza wa kisukari ni pamoja na kuwepo kwa uwezekano mkubwa kwa mgonjwa aliyekwisha kuathiriwa na kisukari wenda akapatwa na tatizo la figo .Japo ni vigumu kujua ni mgonjwa yupi wa ugonjwa wa kisukari anawezakukumbwa na tatizo hili la figo japo zipo ishara kadha wa kadha.
Ieleweke kuwa ugonjwa huu wa kisukari ni chanzo kikuu cha ugonjwa wa figo ulio katika hatua ya mwisho kutokana na walio wengi hupatwa na tatizo hili ,hata hivyo kwa mgonjwa wa kisukari ni vigumu sana kupatwa na tatizo la figo hasa katika kipindi cha miaka kumi ya kwanza kabisa ya tatizo la ugonjwa wa kisukari.
Ikumbukwe kuwa ugonjwa huu wa kisukari huorodheshwa na shirika la afya ulimwenguni kuwa ni moja ya sababu kuu za watu kufariki mapema ikiwa ni pamoja na kupatwa na matatizo ya upofu,figo kushindwa kufanya kazi inavyotakiwa ,mtu kukatwa mguu na kupatwa na ugonjwa wa kiharusi,kwani hali hii yote huchochea athari kubwa za kiuchumi hasa kwa mtu na hata familia kwa ujumla.
WHO katika kuangazia athari ya tatizo la ugonjwa huu hatari wa kisukari hasa kwa jamii za kimataifa katika kusaidia kinga uchunguzi na usimamizi unaotakiwa kwa ugonjwa huo ambao ulisababisha vifo vya takribani watu milioni 1.6 kwa mwaka 2016 pekee kote ulimwenguni.
Kuendelea kujitokeza kwa matatizo mbalimbali hasa haya yote huchochewa na kuwepo kwa tatizo hili la kisukari ambalo limekuwa tishio kubwa kwa maisha ya wanajamii mabalimbali,hata hivyo jitihada za haraka zinatakiwa kuendelea kuchukuliwa kutokana na hali halisi ya tatizo kuendelea kushika kasi kwa kuenea ulimwenguni kote.
Aidha, athari kubwa ya kiuchumi itokanayo na ugonjwa huu wa kisukari kuna uwezekano mkubwa kutokea kwa mtu yeye mwenyewe na familia kwa ujumla kwani gharama hiyo ya kupanda hali ya maisha yawezasababishwa na sindano ya Insulini na ufuatiliaji pekee ambao waweza kutumia nusu ya mapato kwenye familia hali inayowafanya walio wengi kushindwa kupata dawa za kisukari mara kwa mara na huduma husika hali inayochochea tatizo kubwa na kuendelea kuongeza idadi ya walioathiriwa na ugonjwa hatari wa kisukari.
Kutokana na tatizo hili kuendelea kushamiri na kuwa kubwa kwa kiasi chake hali inayoendelea kuleta athari kubwa kwa jamii ya kitaifa na kimataifa kwani ni wakati sasa kwa kila mmoja wetu kutambua ugonjwa huu kwa undani ikiwa ni pamoja na kufuatilia ushauri wa kitaalamu kuhusu afya yako ili kuanza kuchukua hatua za kukabiliana na ugonjwa huu ikiwa umebainika kuathiriwa.
Daktari mgeta anaeleza kwa ujumla jinsi ya kuepukana na tatizo hili kwa kuchukua tahadhari mapema ikiwa ni pamoja na jamii kuwa na utamaduni wa kujali afya kwa ujumla hapa anasema;
"Kwa ujumla jamii ijipe mtazamo wa kuwa inapima na kuchunguza afya baada ya muda fulani hasa baada ya mwezi unapashwa kuangalia afya yako kwa ujumla,pia mazoezi yapewe kipaumbele sana hali itakayoufanya mwili kuwa na kiwango cha sukari iliyo na uwiano sawa" alisema Mgeta.
Kutokana na hali halisi ya mambo yanayozidi kujitokeza kwa kasi sana kutokana na kuwepo kwa tatizo hili la ugonjwa wa kisukari ni hakika kwa pamoja kushirikiana kwa kiasi kikubwa na kwa nguvu moja katika kulitokomeza tatizo hili.licha ya tatizo hili kuendelea kuwa pana na lenye nguvu katika kukatiri uhai wa maisha ya watu walio wengi ulimwenguni wewe na mimi bado tunayo nafasi ya kutumia dawa katika kuondokana na hilo tatizo ikiwa ni pamoja na kuendele kuchunguza afya zetu kwa pamoja.

ENDELEA KUFUATILIA MWENDELEZO WA MAKALA MBALIMBALI ZA AFYA ZIJAZO...............
Suluhisho la tatizo ulilonalo kiafya ni hapa>>>> Katunzi Abdul

Want your business to be the top-listed Beauty Salon in Mwanza?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Category

Website

Address

Mwanza
Mwanza
112230