JAMII FM RADIO
JAMII FM ni kituo cha redio cha kijamii kilichoanza kutoa huduma mwezi Septemba 2016 kwa lengo la kuwapa jamii jukwaa la kuzungumzia maendeleo yao.
JAMII FM RADIO haitawajibika kwa maoni yatakayotolewa yenye kukiuka sheria za nchi. JAMII FM is a Community Radio that was launched in September 2016 for the purpose of giving community members particularly from rural areas access to information and means of communication. The programmes are basically focused on issues that directly or indirectly reflects community livelihood including people with
25/07/2026
Wanafunzi sasa ni mtelezo hasa inapofika muda wa kujisomea baada ya kuzinduliwa kwa umeme, Bonyeza hapo kwenye picha ili kusoma zaidi.....
Ndejembi awasha umeme Sekondari, Mtwara Waziri wa Nishati Deogratius Ndejembi amewasha umeme katika Shule ya Sekondari Mtiniko, Nanyamba, na kusema Serikali imewekeza zaidi ya Shilingi bilioni 203 kupeleka umeme katika vijiji na vitongoji vya Mkoa wa Mtwara Na Musa Mtepa Waziri wa Nishati, Mhe. Deogratius…
24/07/2026
Kikosi kazi cha kupambana na Uhalifu wa usafirishaji haramu wa Binadamu Mkoa wa Mtwara kimeaswa kuwajibika kwa vitendo ili kutokomeza kabisa tatizo hilo.
Akizungumza Leo Julai 24, 2026 kwenye ukumbi wa Hoteli ya Luwa wakati wakifunga semina ya siku mbili, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Mtaki Kurwijila amesema kikosi kazi hicho kinatarajiwa kufanya kwa vitendo yale waliyofundishwa wakati wa Semina.
ACP Kurwijila amesema kikosi kazi hicho, kinapaswa kwenda kuchukua hatua stahiki za usafirishaji haramu wa Binadamu kabla ya kusubiri matokeo ya tatizo kutokea.
Ameongeza kuwa, Kikosi kazi kiende kusaidia Jamii katika kupata elimu ya namna ya Kuzuia,kulinda na namna ya kushughulikia taarifa au matukio ya Usafirishaji haramu wa Jamii kwenye ngazi zao, ikiwemo kutoa taarifa kwa vyombo husika.
ACP Kurwijila amesema katika Mkoa wetu changamoto hizo za usafirishaji haramu zipo na Jamii inaweza ikawa inafanyaka kwa kujua au kwa kutokujua, hivyo wanapaswa kukemea na kuacha kabisa kufanya matendo hayo haramu.
Nao baadhi ya wajumbe wa kikosi kazi hicho cha Mkoa, wamesema wataenda kuwajibika ipasavyo kulingana na mafunzo waliyopata na wameomba ushirikiano kutoka kwa Jamii hasa pale wanapohitaji ufafanuzi au kuhitaji Taarifa kutoka kwao.
Semina hiyo ya siku mbili iliyoandaliwa na CVM kwa kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Sekretarieti ya kupambana na usafirishaji Haramu wa Watu (ATS) kwa ufadhiri wa serikali ya Itali, ambao umekutanisha wadau mbalimbali wa sekta za Serikali na Asasi za kiraia.
23/07/2026
Furaha zimetawala wilaya ya Newala kwa kuishukuru serikali kwa umeme wa kV 33
Wananchi Newala waishukuru serikali kwa umeme Wananchi wa Newala wameishukuru Serikali kwa kuzindua laini ya umeme wa kV 33 kutoka Masasi hadi Newala, wakisema itaimarisha shughuli za kiuchumi, kuongeza uzalishaji wa wajasiriamali na kuboresha huduma zinazotegemea umeme wa uhakika Na Musa Mtepa Wananchi wa Wilaya ya…
23/07/2026
Wadau kutoka Taasisi mbalimbali Mkoani Mtwara wameaswa kuimarisha ushirikiano katika kupambana na usafirishaji Haramu wa Binadamu, kupitia kutoa elimu kwa wananchi na utaratibu wa pamoja wa hatua za kisheria na utendaji.
Wito huo umetolewa Leo Julai 23, 2026 Mkoani Mtwara na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Dkt Benedicto Ngaiza wakati akifungua semina ya kuhusu Usafirishaji haramu wa Binadamu na Uhamiaji salama.
Dkt Ngaiza amesema, Usafirishaji haramu wa Binadamu ni uharifu mkubwa unaokiuka haki za Binadamu na kuvunja utu wa Mwanadamu.
Ameongeza kuwa uhalifu huu unathiri sana Wanawake, Watoto, vijana pamoja na makundi mengine yaliyo katika mazingira hatarishi.
Nao baadhi ya washiriki wa semina hiyo wamesema, imekuja kwa wakati muafaka na ni muhimu sana na ni mambo ambayo yamekuwa yakitokea kwenye Jamii zetu na Kuna wakati wananchi wanafanya kwa kujua na kutokujua.
"Kuna vijana waliletwa na kushawishiwa kutoka Dar es Salaam na walihaidiwa kuja kufanya kazi hapa Mkoani Mtwara, lakini walivyofika ile kazi waliyohaidiwa hawakupata, ndipo kijana mmojawapo, alimtumia ujumbe baba yake kuwa tangu wamefika hapa hakuna kazi yeyote inayoendelea naomba nitumie hela ya chakula, sababu aliyewashawaishi aliwaambia waje na hela zao na wakifika watarudishiwa, lakini baada ya kufika, aliwazungusha na bila kuwarudishia hela zaidi ya mwezi, ndipo baba wa kijana huyo alipiga simu na akatueleza sehemu alipo huyo kijana na tukampata huyo mtu aliyewaleta na tukamwambia awarudishe vijana wote 30 na kurudishwa Dar es Salaam" amesema Bahati Sendela Naibu Mkuu wa upelelezi Mkoa wa Mtwara.
Semina hiyo imeandaliwa na shirika la CVM kwa ufadhili wa serikali ya Italia kwa kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Sekretarieti ya kupambana na Usafirishaji Haramu wa Watu (ATS) ambao imewashirikisha wadau kutoka vyombo vya ulinzi na Usalama, Mahakama, Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Uhamiaji, Maafisa Ustawi wa Jamii, Viongozi wa Dini, Viongozi wa Serikali Wawakililishi wa Asasi za kiraia.
22/07/2026
Wilaya ya Newala sasa kuanza kwa fursa mpya zitokanazo na Umeme
Serikali yatatua changamoto ya umeme Newala Waziri wa Nishati Deogratius Ndejembi amezindua laini ya umeme ya kilovoti 33 kutoka Masasi hadi Newala, mradi utakaoboreshwa upatikanaji wa umeme wa uhakika na kuchochea shughuli za kiuchumi wilayani humo Na Musa Mtepa Waziri wa Nishati, Deogratius Ndejembi, leo Julai…
16/07/2026
KIPAZA CHA LEO 🎤
Kumekuwa na baadhi ya watu wenye ulemavu wanawatumia watoto wadogo katika kuomba misaada" Jamii Inazungumziaje ili swala.
MCHAKAMCHAKA SHOW
Thursday 😄
Host Buda 🎤
https://radiotadio.co.tz/jamiifm
Sikiliza Jamii FM Radio kupitia kiunganishi kilichopo hapo juu
15/07/2026
KIPAZA 🎤
Ebu tuambie ukweli kati ya muziki wa singeli na muziki wa hip-hop upi unafanya vizuri sana kwenye majukwaa makubwa hapa nchini.
MCHAKAMCHAKA SHOW
Host Buda
https://radiotadio.co.tz/jamiifm
Sikiliza Jamii FM Radio kupitia kiunganishi kilichopo hapo juu
14/07/2026
Wanachama wa MFICO’S Msangamkuu wameiomba serikali kukamilisha vifaa vya boti ya mkopo yenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 102, wakisema upungufu wa vifaa umewazuia kuanza uvuvi na kurejesha mkopo. Kusoma kwa undani wa habari hii bonyeza picha hapo chini.......
Wavuvi Msangamkuu wakwama kutumia boti ya mkopo Wanachama wa MFICO’S Msangamkuu wameiomba serikali kukamilisha vifaa vya boti ya mkopo yenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 102, wakisema upungufu wa vifaa umewazuia kuanza uvuvi na kurejesha mkopo Na Musa Mtepa Wanachama wa Chama cha ushirika cha msingi…
14/07/2026
KIPAZA 🎤
Unafahamu umuhimu wa kutunza mazingira ya bahari.
Twenzetu pamoja kitaa kimeongea kwenye kipaza 🎙️
MCHAKAMCHAKA SHOW
HOST Buda
https://radiotadio.co.tz/jamiifm
Sikiliza Jamii FM Radio kupitia kiunganishi kilichopo hapo juu
13/07/2026
Usikose kusililiza kipindi cha Dira ya Asubuhi tarehe 14.07.2026...Tuma maoni na ujumbe wako utasomwa kwenye kipindi
Children in Crossfire
Utpc TZ
Tanzania ECD Network
Ikulu Mawasiliano
Ofisi ya Rais - Tamisemi
Wizara ya Afya
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Contact the business
Telephone
Website
Address
Mtwara