Nuru ya Ulimwengu

Nuru ya Ulimwengu

Share

NURU YA ULIMWENGU | Light of the World Mission Experience🌍
Equipping believers for cross-cultural evangelism. Bridging faith, culture & mission.🙏🏿

21/04/2026

NuruYaUlimwengu

16/04/2026

Nuru ya Ulimwengu . Mafundisho ya Biblia.

16/04/2026

Nuru ya Ulimwengu
102.7.

13/04/2026

2 Wakorintho 9
⁶ Lakini nasema neno hili, Apandaye haba atavuna haba; apandaye kwa ukarimu atavuna kwa ukarimu.
⁷ Kila mtu na atende k**a alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa lazima; maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu.
⁸ Na Mungu aweza kuwajaza kila neema kwa wingi, ili ninyi, mkiwa na riziki za kila namna siku zote, mpate kuzidi sana katika kila tendo jema;

11/04/2026

NGUVU YA MSAMAHA - Uponyaji wa Kiroho.

KIFUNGU: Waefeso 4:31–32

LENGO: Bila uponyaji wa ndani, hasa katika eneo la msamaha, huwezi kukua kiroho.

UTANGULIZI:
Ndugu zangu, k**a vile mwili usiotibiwa unapokuwa na ugonjwa hushindwa kukua vizuri, ndivyo ilivyo pia kwa roho ya mwanadamu. Mtu anaweza kuwa anaenda kanisani, anaomba na kusoma Biblia, lakini ndani yake kuna majeraha, chuki, uchungu na kutokusamehe. Hali hii inazuia ukuaji wake wa kiroho. Leo tutajifunza kwamba msamaha ni tiba ya kiroho, ni dawa ambayo Mungu ametupa ili kuponya mioyo yetu. Ulimwengu unasema ukisamehe wewe ni dhaifu au mjinga, lakini Biblia inafundisha kwamba msamaha ni nguvu, si udhaifu.

MSAMAHA NI TIBA YA MOYO ULIOJERUHIWA

A. Waebrania 12:15

B. Mtu aliyefanyiwa mabaya alitegemea wema lakini akarudishiwa ubaya. Anaumia na anaweka maumivu moyoni. Maumivu yenyewe ni tatizo, lakini kuyashikilia moyoni ni tatizo kubwa zaidi. Ni k**a kidonda kilichopona lakini kovu bado lipo; ukikikuna kinaanza kuuma tena.

C. Wakristo wengi wanabeba uchungu wa zamani na kusema “nimesamehe lakini sitasahau.” Huu si msamaha wa kweli. Msamaha wa kweli ni kuachilia adhabu na haki ya kulipiza kisasi. Unaposhikilia uchungu unajiumiza mwenyewe na unazuia uponyaji wako. Msamaha unakuponya wewe kwanza.

MSAMAHA SI UDHAIFU, NI NGUVU YA KIROHO

A. Mathayo 18:21–22

B. Yesu akiwa msalabani alisema, “Baba, wasamehe, kwa kuwa hawajui watendalo.” Alikuwa katika maumivu makubwa lakini alichagua kusamehe.

C. Ulimwengu unasema ukisamehe wewe ni mjinga au dhaifu, lakini Yesu anaonesha msamaha ni nguvu ya juu ya kiroho. K**a msamaha ungekuwa udhaifu, Yesu asingetuambia tusamehe bila kikomo. Kadri unavyosamehe ndivyo unavyokuwa na nguvu zaidi kiroho.

MSAMAHA HUONDOA UDUMAVU WA KIROHO NA KULETA UKUAJI

A. Waebrania 8:12

B. Stefano alipokuwa anapigwa mawe alisema, “Bwana, usiwahesabie dhambi hii.” Hakuomba kulipiza kisasi bali aliomba msamaha kwa waliomuumiza.

C. Kutokusamehe kunapofusha macho ya moyo na kunazuia mtu kuona mapenzi ya Mungu. Kunazaa uchungu, hasira, chuki na fitina. Lakini msamaha hufungua macho ya moyo, huleta amani na ukuaji wa kiroho. Unaposamehe unafanana na Kristo na unaanza kuona njia ya Mungu katika maisha yako.

WITO.
Ndugu zangu, msamaha si chaguo bali ni Amri kwa Mkristo. Yesu alisamehe, Stefano alisamehe, na sisi tunaitwa tusamehe. Kumbuka kwamba msamaha ni tiba, ni nguvu na ni ufunguo wa ukuaji wa kiroho. Usiseme nimesamehe lakini sitasahau, bali sema nimeachilia na nimemwachia Mungu. Unapomsamehe mtu haumponyi yeye tu, bali unajiponya wewe mwenyewe. Leo chagua kuachilia, chagua kusamehe ili roho yako ipone na ukuaji wako wa kiroho uanze. Amina.

03/04/2026

“This is why we go. This is why we preach 🔥 ”
Nuru ya Ulimwengu.

28/03/2026

Nuru ya Ulimwengu.
Let it Rain....🌍

Photos from Nuru ya Ulimwengu's post 28/03/2026

Nuru ya Ulimwengu🌍
Mission Experience.
Evangelism in Kikatiti.

Photos from Nuru ya Ulimwengu's post 26/03/2026

Nuru ya Ulimwengu | Mission Experience
Spread the Good News 📖

15/03/2026

Lilolo kuu ni Upendo

Yohana 13
³⁴ Amri mpya nawapa, Mpendane. K**a vile nilivyowapenda ninyi, nanyi mpendane vivyo hivyo.
³⁵ Hivyo watu wote watatambua ya kuwa ninyi mmekuwa wanafunzi wangu, mkiwa na upendo ninyi kwa ninyi.

UPENDO NI KANUNI YA MBINGUNI NA YA MILELE
1 Yohana 4:8

UPENDO NDIO UTAMBULISHO HALISI WA KANISA
Yohana 13:34–35

UPENDO HUTOKA NDANI YA KANISA NA KUFIKA KWA JAMII
Luka 10:33–34

Kanisa linalokua halipimwi kwa sauti ya mahubiri,
bali kwa sauti ya upendo wake katika maisha ya watu.
"NGUVU YA UPENDO"

“Basi, sasa inadumu imani, tumaini, upendo, haya matatu; na katika hayo lililo kuu ni upendo.”
— 1 Wakorintho 13:13 🙏🏿

Kwa mafundisho zaidi, jiunge na WhatsApp Channel yetu:
https://whatsapp.com/channel/0029VbBFm8XAInPg0yIaiD1s
Tembelea ukurasa wetu wa Facebook:
https://www.facebook.com/share/p/1AdiNwVDrg/
📞 Jifunze zaidi kupitia WhatsApp:
+255 683 299526
Mw: Evance Momburi.

Photos from Nuru ya Ulimwengu's post 11/03/2026

ABS . JOURNEY TO THE TRUTH .

Want your school to be the top-listed School/college in Moshi?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Address

Kilimanjaro
Moshi