Simulizi Zetu
0784468229
group la whatsp
https://chat.whatsapp.com/EIfeKtRLbKsJTItXf1HqJc
HUKO KWENU NAULI SH NGAPI KITUO HADI KITUO?
ššš šš®ššš«šš¤šāØ
Ndugu zangu wote tupeane mihariko
NATAKA NIWATUMIE HELA YA SKUKUUUUU MASHABIKI ZANGU
WEKEN NAMBA ZENU HAPO
NIMENG'OA JINO NIMECHOKA KUWEKA PANALDO KILA SIKU
ANAEJUA DAWA YA JINO
TUTAENDELEA NA HADITHI MDA SIO MREFU
04/01/2026
SAPNA (NDOA YA KULAZIMISHWA)
# # # # # # # # # # # # #
SEHEMU YA 11
Nikapiga piga story na baba pale mpaka muda wa kupika ulipofika nikaenda jikoni kupika chakula cha mchana na k**a kawaida yangu nikipika nyumba nzima inanukia mahanjumati nikaliungurumisha pilau nyama maaan pale nyumbani Kila kitu kipo shida niwe nayo Mimi tu mpishi.
Nikapika pilau langu la nyama nikakaanga na nyama za kuku nik**aliza nikaenda kumuuliza baba wakina Ryan wanarudi saa ngapi Akanijibu sijajua kwani we hujampigia nikamwambia Mimi Sina simu baba alishangaa akasema sasa kwanini huna simu ulimwmbia mamaako mkwe nikamwambia hapana sijamwambia Bado ila haina ulazima Mimi simu ya Nini,akaniambia sasa wewe unawasirianaje na familia yako nikamjibu sijawai kuongea nao toka nimeondoka,baba alishangaa akasema ngoja niwapigie uongee nao maaanaake sio vizur siku zote hizo na hata hujawa tafuta .
Baba akanipa simu yake nikampigia mama,alifurahi nilivyomtafuta hadi akawa anapiga vigeregere akaniuliza vipi mwanangu unaendeleaje nikamwambia nipo vizur tuu sijui wewe akaniambia wao wapo salama kabisa hawana shida,mama akaniuliza vipi mambo yashaita au nikamuuliza mambo gani mama aaaaah mwanangu ndo kusema hujui, nikamwambia ndio mama sijui mama akarudia Yan nauliza tayari mshafanya michezo ya kutafuta mjukuu tumboni maaan uku kupiga kwako simu ghafla kumenishangaza.
Ila mamaangu jamn kwaiyo mtu akimpigia hadi awe na shida,nikamwambia kwanza mume wangu kaja Leo sasa hayo mapenz nafanya wapi mama,mama anachoniahauri eti ananiambia changamka mwanangu changamka uyo mumeo mpe zawadi.
Nikamuuliza sasa namnunulia zawadi gani mama akaanza kucheka namuuliza sasa unacheka Nini mama wakat nimemuuliza kuhusu iyo zawadi akasema we mtoto embu punguza mawenge kwanza ujue utaachika, Mimi namaanisha zawadi zingine wewe unatak ukanunue Aya nenda ukanunue mtoto kwaajili ya mume wakoš¤£.
Kumbe muda huo naongea na mama Wakina Ryan walikuwa wameshafika ndo wanaingia,sasa huko kwenye simu Mimi nataniana na mama namwambia bwan mama mie siwez kuzaa ntaenda kununua watoto naogopa kuzaa mama anacheka uyo Nilivyoona baba anarudi maan alitoka mara moja nikamuaga mama akasema sawa kwaheri msalimie na mkwe wangu nikamwambia usijali salamu zimefika,nakata tuu simu naskia Raymond anacheka nageuka nyuma yupo Raymond na Ryan nikawa Hadi naona aibu Kwa mambo ninayo yaongea.
Nikajikaza Kwa mara ya kwanza nikawakaribisha Kisha nikaanda chakula nimemaliza nikaenda kumuita mama ingawa alishangaa kwasababu hakuniambia nipike ila kanikuta nimeshapika alifurahi uyo akaanza kunisifia huku anamwambia Raymond Yan na wewe mtoto inabidi bababako Ako aende akakutafutie mke ukouko kijijini kwakina sapna.Mume wangu akashangaa Kisha akauliza wewe mama kumbe mke anaitwa sapna,hapo niseme ukwel Mimi mwenyw nikacheka maaan mume wangu hajui jina languš¤£.
Itaendelea....
Full 1000
WhatsApp 0784468229
02/01/2026
SEHEMU YA 10
SAPNA NDOA YA KULAZIMISHWA
Tukainuka huku amenishika bega na alivyo mrefu sasa,kanishika k**a mtoto wake tunatoka ananchekesha basi Nacheka kwaaibu tukiwa tunashuka ngazi kule kweny meza ya chakula wakaanza kupiga makofiš¤£,Raymond akaanza kuimba ujinga𤣠hadi aibu
Tukafika mezani tukakaa babamkwe akaniangalia anacheka tuu.
Mama akamuuliza mbona unamcheka mkwe wangu,baba akamwambia Yan nikiwambia nilipokutana na uyu Binti mtacheka, mama akauliza enhee wapi baba akaanza kuhadithia.wakt baba anahadithia Raymond anamsumbua kakaake na naskia anavyomwambia eti anamwambia kaka naona umeopoa chombo icho,alafu kaka unajua miaka ya shemeji,alivyosema hivo nikamkatisha nikamwambia Raymond mama anakuita akaelewa tu namkatishaš¤£.
Tuk**aliza kunywa chai mama akaenda chumbani kwake alafu Leo shangazi alikuwa anaondoka kwaiyo Ryan na Raymond wakampeleka nikabaki Mimi na baba tuu sebleni. Nikaamua kumuuliza ivi baba kwann ulinifanyia hivi,Kumbe sikuile ulikuwa unamaanisha ulivyoingealea kuniozesha Kwa mwanao babamkwe akajibu ndio na pia akasem yeye ni mwanaume wa maneno yake akisema kitu ujue k**aaanisha na lazima atakitimiza nikamuuliza Tena amepajuaje nyumbani kwetu, nilivyomuuliza ilo swali akacheka kwanza Kisha akasema Kuna siku ulikuwa unatoka shule nikakufatili mpaka kwenu na nakumbuka hiyo siku nilichokaa na nilipata shidaa maana sio kwaumbali ule kwenu ni mbali na shule.
Nikaanza kucheka nikamwambia siungesema tuu nikuelekeze baba,mmmmh we ungekubali kunielekeza wakti ulivyoambiwa tu kuhusu kuolewa ukaanza kulia hadi pale sebleni tukaskia,eeeh kumbe mlisikia babakasema ndio ndomaana tukawai kuondoka na wewe Yan iwe iweje ningekufata tuu uje kweny familia yangu maana unaakili sana na pia unahuruma.
Ndo maaan siku Ile ulivyokataa ela nikakwambia utaolewa na mwanangu.
Nikamwambia sawa baba ila Ile siku nilikuwa nakutania sasa ndo sinachakufanya sasahivi nshaolewa na ni mke wa mtu ambae ndo mwanao Tukaanza kuchekaš¤£
Itaendelea....
Full 1000
Whatsp 0784468229
31/12/2025
KEITH - MR ROMANTIC*
*__________________________________________*
*SEHEMU YA KUMI NA MOJA*
Basi wikiendi ikafika salama Nakumbuka ilikuwa siku ya Jumapili. Nilivaa gauni refu jekundu, lina mpasuo pembeni lilinikaa poa ajabu.
Kwa kweli nilikuwa nimependeza sana. Nilipojiangalia kwenye kioo nikagundua mimi ni pisi kali ni kwa vile Jua la bushi lilipausha sana
Baada ya kumaliza kujiandaa, nikatoka. chumbani nikamkuta Keith ananisubiri sebuleni.
Aliponiona mara ya kwanza alishtuka akawa k**a amepigwa na butwaa. lla ghafla tu mood yake ikabadilika akanikunjia sura
"Unaonaje, nimependeza eeeh??" Nilimuuliza kwa nia nzuri tu jamani
"Umependeza but sijui k**a umependeza ivi coz tunaenda kwa Aunt au kwakua unajua Rico atakuwa pale
Nikashangaa "Unamaanisha nimependeza hivi kwa sababu ya Rico?
"Au nimekosea??"
"Kwani Keith Ni kosa kupendeza?? Pia mbona story za Rico tulishamaliza Na mimi sina mda nae kabisa
"Usinielewe vibaya ila Sitaki watu ambao
hawana hatia waumie"
"Watu k**a nani?"
"Watu k**a K**a Maya. Anampenda Rico sana
"Atauumiaje sasa? Nachojua Mimi sifanyi chochote kibaya na Rico. Tumeenda tu kwa sababu wametualika. Na pia ulisema umewa miss Aunt na Uncle unataka kuwaona. Tatizo
liko wapi?"
Hakusema chochote, Alisimama, akachukua funguo za gari akatoka nje hata hakusema Twende. Ilibidi nijiongeze nimfuate nyuma nyuma lasivyo angeondoka aniache
Mnajaua Nikaanza kujiuliza, Kuna nini kinaendelea? Kwa nini ananifanyia hivi?" Ghafla
tu anaanza kuwa k**a mume mwenye Gubu
Au pengine Keith ananipenda? Namna anavyofanya inaonekana kabisa ana wivu. Weeh sikutaka kuamini ila nilijikuta nimefural.
Sio siri hata mimi kuna namna nahisi ninapo kua na Keith. Sijui ni mapenzi au vipi lakini sichoki kumtazama, kumsikiliza mpaka mda mwingine
hadi namwota
Nikajisemea ikitokea k**a Keith atanitongoza
wallah sikatai. Apo najiliwaza ndani ya moyo nikasahau kabisa nina mimba ya mtu mwingine, Ila mimi
Haya Tukafika nyumbani kwa Rico. Tulikaribishwa vizun, lakini baba yake Rico alikuwa safarini. Nyumbani kulikuwa na mama.
yake, Maya na Rico mwenyewe.
Mama Rico aliponiona alishangaa
"Huyu ndiye yule binti wa kijijini?"
Keith akajibu "Si binti kijijini Ana jina lake
Aunt, Anaitwa Lola"
"Amebadilika sana, now kawa mrembo. Ni umaskini tu ndio ulikuwa unamharibu binti wa watu. Angalia alivyo mrembooo...
Maya akaongezea
"Ndiyo si nilikuambia, Lola ni mrembo mno
Walinisifia pale hadi nikaona aibu nikawa
natizama chini tu.
"Sol Mnaendeleaje Kelth? Hujaja kwangu siku nyingi utadhani tuna ugomvi? Mama Rico
alilalamika
"No Aunt si unajua nina jukumu kubwa la Lola! So most of the time nakua busy ofisini, busy
nyumbani but hakuna kilicho aribika! Am sorry
kwa kufanya uni miss sana" alijibu Keith
"Naelewa dr, uzuri leo umekuja No problem So
k**a hamtajali acha niende na hawa warembo jikoni then nyie mka relax huko nje mkisubiri
msosi Mama Rico alituchukua mimi na Maya tukaenda jikoni kwaajili ya kuandaa mapocho pocho
Tukiwa jikoni niligundua mama Rico alikuwa
ananijali sana tofauti na siku ya mwanzo.
Alikuwa mpole mwenyewe nikahisi k**a
ameanza kunipenda
"Usiniogope Lola mimi sing'ati! Najua labda ni kwa sababu ya nilichosema mara ya kwanza
ulipokuja, sometimes mdomo wangu hauna break ila please usiniogope okay??"
Nikajibu "sawa Mama hakuna shida"
"Haya Tupike nini leo?"
"Pilau nyama, kachumban, chips na rosti la kuku alidakia Maya
Mama Rico akacheka "Vyote hivyo?
Maya akasema "Ndiyo, leo ni siku special familia
nzima ipo hapa
"Okay hakuna shida kipenzi tutapika vyote ivyo
Basi Tukaanza heka heka za kupika, ajabu Maya
aliondoka akaenda sebuleni kuchezea simu. Mama Rico hakupenda lakini hakusema.
chochote ili tu asije kukwazana na Maya.
Jikoni Tukabaki mimi, mama Rico na
wafanyakazi wawili waliokua wanatusaidia. Tulikuwa tunacheka na kupiga storil Kale ka
moment kalikua kazuri mno
Mda huo huko Nje upande wa Garden, Keith na
Rico walikuwa kimya kila mmoja na simu yake.
Toka walipandishiane kule restaurant kila mmoja
alikua kamkaushia mwenzake.
Rico alipoona hakuna cha kuongea, akaona ni
heri aje jikoni kuchukua angalau kinywaji. Lakini kabla hajafika jikoni alimuona Maya kakunja nne
sebuleni Akamfuata
"Babe Mmeshamaliza kupika?"
"Me Sijul, Nadhani itakua bado"
"K**a bado hawajamaliza, mbona uko hapa?"
"Unajua sipendi kupika pika nimewaachia wenyewe huko jikoni
Rico akakasirika "Angalau ungeenda kuwasaidia au ukae nao muongee. Hivi unajitenga unadhani
ni sawa?"
"Rico, siwezi hata kukaa kwa amani nyumbani
kwa wakwe wangu? Mama yako hajasema chochote also mimi sio housegirl hapa"
"What??? Maya.. please embua acha drama.
zakol Najua kabisa Mama hajapenda
"K**a hakupenda angeniambia. So please
niache"
Rico hakujibu Akampita akaja mpaka jikoni. Alipofungua mlango, akatuona tukicheka na
kufurahia.
All enjoy kuniona nipo nimejiachia sana na
mama yake. Akatamani ningekuwa mkwe pale
maana nilipatana na mama ake kushinda hata
huyo Maya
Akahairisha kuchukua kinywaji badala yake.
akaenda chumbani kwake na kukaa kitandani.
"Nimefanya nini sasa?? Best wife ni Lola na nilifanya makosa sana kumpuuzia. Najuta hata
kwanini nilipoteza mda wangu kwa Maya...! Daaahinabidi nifanye kitu ili nimpate Maya.
tena lasivyo Keith atanizidi kete"
Rico akawaza kidogo kisha akatoa simu yake, akatafuta namba aliyo isave k**a Patricia,
akaipiga.
Simu ikaita mara mbili then ikapokelewa na Sauti nyororo ya k**e.
"Ah Rico shemeji angu, Inaonekana umeni miss
sana
Rico akasema "Ndiyo, nimekumiss kinomal Unarudi lini?"
"Sijui. Niko bize sana na biashara yangu inaenda vizuri
"Mhhh hongera! Na Vipi kuhusu Keith?"
"Mimi na Keith tuliachana au ulisahau. Nilichagua kazi badala ya kuolewa na yeye
"Lakini bado unampenda
"Ofcourse, Na yeye pia ananipenda. Keith hawezi kumpenda mwanamke mwingine zaidi yangu"
akacheka
"Mambo yamebadilika sasa. Keith anaanza kumpenda mwanamke mwingine"
Patricia akasema kwa mshangao "Nini?
Impossible
"Ukweli ndo huo! Ukichelewa, utamkuta ameoa"
"My God kwanini lakini! Daah so inabidi nirudi haraka lasivyo itakula kwangu! Thanks Rico kwa
taarifal Byeee Patricia akakata simu na kumfanya Rico atabasamu.
Mpango wake ulikuwa kumrudisha ex wa Keith
ili kuharibu kila kitu. Rico alijua Keith alimpenda
Patricia sana.
Walikuwa wanapendana sana na Keith alikua
tayari kumuoa Patricia ila siku moja kabla ya harusi Paticia akapata taarifa kuwa kapata kazi huko Paris ya mitindo.
Kwaiyo harusi ikavunjika Patricia akaenda Paris akimuacha Keith na maumivu. Wallachana
Japo inasemekana bado walikua wanapendana.
Na Patricia alisema akishamaliza kazi zake zote huko Paris atarudi Tanzania kwaajili ya Keith.
Alikua na confidence kuwa hata akimpigia Simu Keith usiku wa manane akiomba warudiane
Keith hawezi kukataa. Yooh nimekwisha mimi
Unajua kitakachofuata? Nakuja
Chapters
Full 1000
Whatsp 0784468229
30/12/2025
8--9
SEHEMU YA 8
SAPNA
Nipo busy mwenyw mke napikia familia na hata sikuambiwa ni kiherehere changu tuu nikapka nilivyomaliza nikaenda kweny fridge kulikuwa na mikate na siagi nikawa napaka uku naimbaimba, Ghafla bila kutarajia nikaskia mtu kanishtua Kwanguvu sasa Ile kugeuka khanga ikanasa kwenye jiko ikanitoka nikabaki na nguo ya ndani tuu,naangalia sasa nimuone Alie nishtua ni mkaka hata simjui.
Nikavaa harakaharaka mamamkwe alikuwa kaaamka nae wakati uo nikaskia namuita Ryana mwanangu,uyo Ryan mwenyw macho yamemtoka ananiangalia Kwaaibu nikatoka jikoni hata mama sikumuona nikakimbia kuelekea chumbni.Aibu gani hii jamn mume kaniona uchi siku ya kwanza tuu nikabaki chumbni ata chai yenywe nikaiacha uko jikoni,aibu sasa nikaskia hodi chumba nilicho Mimi naenda kufungua namkuta Ryan kaleta mizigo yake akaniuliza kwani wewe ni mfanyakazi mpya au sasa aibu nikawa naongea uku naangalia chini,akaniuliza mbona unaongea ivo nikamwambia hamna akaniambia nipishe nataka nikaoge nikamwambia sawa alafu nikaondoka kwenda seblen.
Nafika sebleni namkuta mamamkwe anaanda chai akaniuliza mkwe vipi umemuona mme wako nikamwambia ndio ila kilichonikuta Hadi naona aibu ,aibu ya Nini sasa mkwe akauliza mama,nikamwambia kaja kanikuta jikoni akanishtua sasa nilikuwa nimevaa kanga ikanidondoka.
Mama alicheka uyo ni alinicheka Ikanibidi tu na Mimi nicheke Kisha akanisema Yan uyo kashazoea kunishtua basi alivyokusikia uko jikoni akajua ni Mimi ndo maaan akafanya ivo alafu kuhusu kukuona uchi si mume wako uyo chaaajabu ni nini hapo eti mkwe Kuna chaaajabu hapo nikabaki Nacheka tu.
Muda wa kunywa chai ukafika mama akanituma nikamuite Ryan,nikaenda kule chumbani nagonga hodi haniskiaa kule seblen nachungulia mama akawa ananionesha ishara niingie si chumba changu pia sasa nilikuwa nimeegemea mlango wakati naongea na mama kule ndani Ryana akaufungua mlango nikaingia mzima mzima na alikuwa kifua wazi sijui katoka kuoga akabaki kanikombatia,mmmmh ama kwel siku ya kufa nyani miti yote huteleza maana Leo hiyo nimekutana nae matukio yote haya yametokea.
Akaniangalia usoni uku anatabasamu k**a Raymond tuu ananiuliza vipi Kuna kitu umesahau Hadi nikashikwa na kigugumizi,akatbasamu Kisha akaniweka sawa maaan tulikuwa Bado tumeegemeana, nilivyosimama vizur ndo nikamwambia twende tukanywe chai mama anakuita Akanijibu sawa nakuja.
Nimetoka uko chumbani kwake natetemeka Yan miguu haifanyi kazi, pale sebleni alikuwepo Raymond shangazi baba hakuwepo mama yeye alikuwa Kwa nyuma kule mezani anaanda chai Raymond Hadi akauliza shemj vipi mbona hushuki nikamwambia Amna,akauliza Tena au kaka ndo tayari Tena kashafanya yakeš¤£
Nikabaki namshangaa tuu,baada ya k**a dakika mbili nikainuka nikamfata mama tukasaidizana kuandaa chai tulivyomaliza watu wakaitwa chai inywewe baba akaja akasalimiana na mwanae maaan nik**a miaka miwili alikuwa kusoma,tukakaa mie hata apertite ya kula sikuwa nayo Raymond akaanza anamuliza kakaake eti kaka unamjua uyo msichana,kakaake akajibu huyu mrembo au alivyosema hivo nilihisi aibu Hadi nikapaliwa, Raymond nianacheka mbavu Hanaš¤£š¤£.
Itaendelea...
SEHEMU YA 9
Kakaake akasema ntajuaje ni nan na hamjaniambia ni nan,sasa nikwambie kaka baba alikwambia anasurprise sasa huyo ndo surprise yako mkeo uyo nimekuolea Mimi.
Raymond alishtuka akamuangalia babaake k**a Kwa hasira Kisha akamuangalia mamaake Kwa hasira akauliza sasa ndo Nini mnanifanyia hivi Kwan niliwambia nataka kuoa si mngeni taarifu mapema Au kuniomba ruhusa.
Nilijiskia vibaya sana,nikainuka nikakimbilia chumbani nikaanza kulia mama Ryan uko akawa anamsema ryana sasa Yan we mtoto laaana kwel wewe unataka utuletee Vituko k**a ulivyotuletea mara ya mwisho,Hivi yule mwanamke gani yule mwanamke Hana hata stara anavaa uchiuchi,we ulikuwa unapenda ambavyo bababako anamuona vimapaja vyake eeeh maaan sikuelewe nimeenda sasa kukutaftia mwanamke mwenyw hofu ya Mungu mstaarabu Hana hata mambo mengi unaanza kumzodoa na nakwambiaje ukimpa talaka uyo Mimi sio mamaako Tena na kupa lazi.
Mamaake alivyoongea ivo akaondoka na chai akaisusa, Kwa jinsi Ryan anavyompenda mamaake akamfata chumbani kwake alipo Kisha akamuomba msamaha akambembeleza maaana alikuwa kanuna hatr,akamwambia kamkubali basi uyo mwanamke ambae ndo Mimi mamaake alivyosikia hivi alifurahi sana akarudi kunywa na chai, mambo yote hayo yakaendelea wakina baba , Raymond na shangazi wao hawakutia hata neno maana yule mama naskia ni mkalii akiongea ameongea hataki ushauri na ata Raymond utaniwake wote uko ila mamaake akiwa na hasira hajibu kitu Wala hachekicheki hovyo.
Walivyorudi mezani mama akamwambia Ryan anifate sasa maan nipo chumbani nilikuwa nalia Ryan akakubali kaja kanigongea mlango sikutaka hata kufungua nilikuwa nalia tuu,akaomba ufunguo wa ziada akafungua.Alinikuta nimekaa chini nalia akanifata na yeye akakaa chini akaanza kunipigapiga mgongoni k**a ananibembeleza,nikamwambi najua hunipendi usinipe moyo we niache tuu nitakuwa hata house girl wenu ila sirudi nyumban.
Ryan akanikiss mdomoni nilishangaaa š³maana nimambo mageni kwangu kabisa haya sikuwa hata najua kurudishia nikabaki tunimezubaaa k**a chizi nimetoa mijicho,alivyomaliza akaniambia mmh mke wangu unalips tamu nikawa naona aibu hata kumuangalia siwezi akaniambia sasa mke unataka kuondoka alafu Mimi unaniacha na nan au unataka nikucheat mkee wangu nikamwambia wewe ila hunitaki akanikiss Tena nikabaki namshangaa akaniambia Yan mke ukiongelea tuu mambo ya kukuacha nitakuwa nakunyamazisha Kwa kiss š,alafu ujue nimekupenda ghafla Toka Nilivyoona chupi yangu ya maua asubuhi š«£,kwaaibu nikaamka nikamwambia twende tukale maana ataanza kuongea na mengine huyuš¤£.
Itaendelea....
Full 1000
Whatsp 0784468229
29/12/2025
6--7
SAPNA (NDOA YA KULAZIMISHWA)
# # # # # # # # # # # # #
SEHEMU YA 6
Nilivyofika kwanza shemeji si aliamishwa akakaa pale mbele,akanigeukia uku anacheka akaniambia mkee karibu nyumbani kwetu utupikiage sasa 6
mama akampiga mkofi wa mgongo akamwambia Raymond na kakaako akija nakusemea unamtania mke wake.
Kumbe shemeji anaitwa Raymond,akamjibu mama eeeh kwanza mtu mwenyw hata hajui k**a kaolewa mke uyu mke mbona ataisoma namba uyu.Ningekuwa na uwezo ningeenda kumuuza shemeji Kwa waganga wa jadišmaana ni anakera ukiwa na hasira unaweza ukamroga ila ni kahandsome lakini sio Sanaa.
Tukashuka kweny gari maan tuliingia getini nyumba Yao ni kubwa Hadi nikawa nashangaaa haya ni Yale majumba nilikuwa nayaona kweny tv ni makubwaaa hayo kuangalia ivi mlango wa nyumba kubwa nikamuona babamkwe kasimama anatusubiri,kweny Ile familia watu wote siwajui na Wala sijawazoea ila yule mbaba nimeshamzoea na namchukulia k**a babaangu ingawa yeye ndo kasababisha yote haya kwaiyo nilivyomuona nilishangilia sana nikamkimbilia nikaenda kumkombatia uku nalia.
Raymond sasa akaanz kucheka katupita pale mlangoni Bado tumekombatiana akawa ananiambia aaaah mkee vipi unalia Tena 𤣠baba akamsukuma uko,wale washenga waliopanda gari nyingine wakashuka wakasalimia na babamkwe Kisha wakaondoka tukabaki sasa k**a familia,yule mmama aliekuwa akinibembeleza nikatambulishwa kumbe ni mamaake Raymond na mume wangu uyo mbaba ninaemwita babamkwe ndo baba wa mume wangu mmama mwengine ni shangazi wa bwana harusi wale wengine wote n majirani.
Nikawasikiliza walivyojitambulisha nikjua watasema jina la mtoto wao ila wapi nikavaa ujasiri nikamuuliza Kwan uyo mume wangu anaitwa nan alafu yupo wapi.Raymond alicheka Yan alicheka na safari hii sio Raymond tuu Hadi mamamkwe akawa anataka kucheka ila anajikaza tuu,babamkwe akasema wote nyamazeni Familia nzima ikanyamaza akaanza kuniambia sasa mwanangu mume wako yupo na anarudi kesho kutoka marekani kimasomo na kuhusu jina lake anaitwa anaitwa Ryan na anamiaka 27.
Nilidhan shemji Raymond ananitania kuhusu miaka nilivyoambiwa ni 27 nikamgeukia Raymond akanikonyeza Kisha akacheka𤣠Yan uyu shemeji sidhani k**a mzima huyu kwanza yeye nakucheka kucheka na yeye,kutania ndo usiseme sasa.
Baba akamwambia mama embu mpeleke mkweo chumbni Kwa mume wake apumzike kwanza maana ilikuwa ni mchana na nimechoka kwel,mama akanibebea mizigo yangu akanipeleka uko chumbani,Ile nyumba ni ya Ghorofa na chumba cha uyo mume wangu Ryan kipo juu.
Nikawa napiga story na mamamkwe wakati tunaenda ananiambia nisijali bwan niachane na Raymond nisimsikilize,na pia akaniambia mwanae ni wakawaida tu hatishi kiivo anakamwili kasize nisiogope,š³Kwan uyu mama anamaanisha Nini kusema ivo ama anadhan naogopa mambo niliofundishwa na shangaziš¤£.
Itaendelea....
SEHEMU YA 7
Nikamjibu sawa,akanifikisha chumbani nikaoneshwa bafu nikaenda kuoga Kisha nikarudi kulala. Nililala kuanzia mchana Hadi Hadi usiku saa mbili nimeamka tuu naangalia saa ni saa mbili aibu hii jamn Yan ukweni siku ya kwanza na nimeamka saa 2, nikaenda kuoga nikavaa kishati na kitenge ndani nilivaa taiti kwanza mwanzo nilivaa khanga ila nikavua baada ya kuona makalio yanajichora sana alafu Mimi sijui nijisifiaje maana nina mtako uo mixer mshepu Nina kasura kazuri sema tu ndo nimenyoa alafu Nina kamwili kadogo dogo.
Nilivyovaaa kitenge nikatoka njee nakuta shemeji ,shangazi wanaangalia tv baba hayupo seblen mama yupo jikoni nikaona Bora niende kumsaidia mama jikoni ila akili yangu yote ilikuwa kwenye tv,nikapitiliza kwenda jikoni sindoshemej akaniona akaanza kunitania Tena,eti shemeji MashaAllah MashaAllah, mke wa kaka uyo daaaaah baba kwanini hakunichagulia Mimi, shangazi akampiga kofi maana anaongea ujinga tuu.
Nikaenda jikoni nikamkuta mama yupo mwenyw jikoni nikaanza kumsaidia kazi ndogo ndogo k**a kukata nyanya,mama akaniambia mkwe embu nisaidie kupika mboga nataka nikaoge nikamwambia sawa usijali nikapika mboga,mimi kwenye mambo ya kupika nipo veryš,nikawapikia nyama rosti kwanz picha linaanza harufu ikaenda sebleni kote watu wanaguna tuu mmh mmh,Raymond akaropoka we mpishi we utatutoa pua wenzio ukuš¤£.
Nik**aliza kupika muda wa kuandaa nikaandaaa msosi mezani watu wakaja kula na babamkwe akaitwa, wamekula Raymond akaanza kusifia Yan baba chakula k**a hichi sijawai kula tangu nizaliwe mama akamkata jicho ilo Raymond mwenyw akabadilisha mada akasema alafu nimeongea na kaka kasema kesho atakuja mida ya asubuhi asubuhi mama akamuuliza umemwambia kuhusu mke,akajibu hapana,niseme ule ukwel alivyosema hivo nikajiskia vibaya maaana naolewa hata mume hanijui hata hajui k**a atakuta mke nyumbani kwaiyo niponipo tuu kimoyo najisemea ila sio mbaya hata hakinikata siondoki hapa ntakua ata dada wa kazi tuu.
š¤£.
Watu wak**aliza kula nikasaidizana na mama tukatoa vyombo,nilivyofika jikoni nikaosha kabisa nikaenda kulala nikakumbuka niliambiwa hamna kulala bila kuoga na shangazi,kwaiyo nikaamka nikaenda kuoga Kisha ndo nikalala usingizi mtamu,asubuhi na mapema nikaamka saa kumi na moja,nilishtuka muda uo kwasababu nishajizoesha kuwai kuamka kipindi kile naenda shule nilikuwaga naaamka saa kumi kamili.
Nilivyoamka nikaenda kuoga nikavaaa khanga kwasababu muda huo watu hawajaamka kwaiyo nikawa huru nikavaa khnnga na kishati hata kitop sikuwa nimevaa sababu najua watu hawawezi kuwai kuamka sababu ya uchovu nusu saa tuu ntakuwa nshamaliza kutengeneza chai.Nikaenda sebleni hamna mtu adi taa zimezimwa kwakua nilikuwa sijui sehemu ya kuwashia taa nikaenda moja Kwa moja jikoni nikawasha taa nikaanza kuandaa chai uku naimba zangu .
Itaendelea
Full 1000
Whatsp 0784468229
28/12/2025
9--10
Chapter 9
KEITH MR ROMANTIC
Baada ya Keith kufungua mlango, Rico akaingia ndani moja kwa moja
"Nimekupigia tangu asubuhi lakini hupokei"
Keith akajibu "Nilikuwa bize, sikupata muda wa kuangalia simu
"Sawa, lakini ulipaswa kupokea. Unajua hali tuliyo nayo sasa. Okay Vipi?? Ulisema utaenda kumwambia mama yangu. Natumaini umebadilisha mawazo...
"Yeah nimebadilisha mawazo...
Rico akapumua kwa furaha "Ah, asante Mungu Nilikuwa na stress siku nzima. Nilijaribu kupiga pia ofisini kwako lakini wakasema hukurudi baada ya chakula cha mchana"
"Ndiyo, nilikuwa bize"
Wakiwa wanaongea, mimi nilikuwa bado jikoni. Sikujua k**a kuna mgeni, Nilimfuata Keith nimwambie pilau linaungua bila kujua Rico yupo
pale
"Keith, pilau inaungua huku tutakula mkaa"
"Kweli Inaungua? Nakuja...."
Keith akaacha kuongea na Rico, akafuatana na mimi mpaka jikoni. Alifunua sufuria akakuta pilau imekakaukia akaongeza supu kidogoo tu.
"Halija ungua bhana! But Nimeongeza kasupu kadogo, acha nirudi nikaongee na Rico"
Nikamuuliza "Mnaongea nini?"
"Usijali, kila kitu kiko sawa" Akatoka jikoni akarudi sebuleni akamkuta Rico amekaa kwenye kochi kakunja uso.
"Bro, jana ulisema unataka aondoke, lakini leo hadi pilau mnapika? Nini kinaendelea?"
"Nifanye nini sasa? Tulale njaa?"
"Naona mmezoeana sana yani Ni siku moja tu lakini ni k**a mmejuana muda mrefu Rico
hakupenda
"Hakuna chochote kinachoendelea. Nimeongea na baba, amekubali tuoane mara Lola atakapo jifungua. Wakati huo, wewe leta mpango wa nini kitafuata baada ya mtoto kuzaliwa. Kwa kuwa
anaishi hapa, lazima nimjali. Unataka nifanye nini? Nisizungumze naye wakati tunaishi nyumba moja?"
"Nakuelewa lakini ni mapema sana nyinyi kuzoeana hivi
"Kwanini? Una wivu?"
"Mimi? Wivu? Hapana. Ninachokuambia tu ni
kwamba wasichana wa kijijini ni hatari. Wanatumia watu ili wapate pesa, usije ukaingia mtegoni Bro!"
"Lakini Lola si wa hivyo
Rico akauliza "Umejuaje? Mimi namjua Lola kuliko wewe. Wewe ume mjua kwa siku moja tu"
"Ndiyo nimemjua siku moja Lakini ndani ya lyo siku moja, alinionyesha yeye ni mtu wa aina gani. Wewe ulimjua kwa sababu ya kile ulichotaka kutoka kwake. usimhukumu dada wa watu" So please
Rico akamwangalia Keith kwa hasira akasema "Sawani Fanya unachotaka ila Bro tafadhali hakikisha hakuna mtu atajua hii issue"
"Ok"
Rico akanyanyuka amekasirika. Akaondoka akiwa
Aliingia kwenye gari lake akaanza kupiga kelele kwa hasira coz alikuwa na wivu.
Namna nilivyokuwa natoka jikoni nikimuita Keith na kutabasamu, ni kitu ambacho sikuwahi kumfanyia yeye. Pia muonekano wangu ulikuwa umebadilika, nilivaa vizuri na Hilo lilimvuruga
akili.
"Hapana, siwezi kuwa na wivu kwa ajili yake! No! No! Rico calm down Akavuta pumzi na kutoa mpaka alipokaa sawa ndipo Aliwasha gari na
kuondoka.
Sikujua kilichotokea, zaidi nilikuwa namtazama dirishani mpaka alipoondoka, Iliniumiza sana kwa sababu aliondoka bila hata kuongea na mimi. Nilidhani labda angeniuliza hali yangu, lakini hapana.
"Ulidhani atazungumza na wewe?" Keith akaniuliza aliporudi jikoni.
"Ndiyo!"
"Kwa nini?"
"Kwa sababu nataka kujua lengo lake la kunidanganya kiasi icho"
"Ni maelezo gani unayotaka Lola? Sorry kwa kusema hivi lakini tayari alishasema hakupendi"
"Najua, lakini angalau angeomba msamaha kwa kile alichonifanyia
"Rico si mtu wa hivyo. Na hata k**a ataomba msamaha, basi kwa mda wake. Hakuna haja ya kumlazimisha"
"Sawa"
"So acha kujistress kwa mambo ya Rico. Chakula kiko tayari, tule okay?"
"Okay"
Keith akapakua chakula pale tukaanza kula. Kwa kweli chakula kilikuwa kitamu sana asikuambie mtu jamaa anajua kucheza na mwiko sio mchezo. Huku mjini mnakula pilau mnapo jisikia Ila kule kijijini tunakula tu siku za sikukuu
Baada ya kula tulikaa sebuleni tukaanza kuangalia movie. Hata sikuangalia sana coz niliishia usingizi bila kujua ilikuaje kuaje.
Keith alivyo gentleman alinibeba mpaka
chumbani akanilaza vizuri kitandani. Aliniangalia sana jinsi nilivyo karembo then akajiuliza kwanini Rico alinipiga tukio kiasi kile??
Na jinsi alivyokua ananitazama ndo jinsi moyo wake ulikua ukimuenda mbio. Alitamani anipapase kidogo huku azichezee chezee па nywele zangu jambo ambalo hakulitarajia.
Alisimama haraka akatoka kule chumbani k**a mshale kabla hajafanya kitu cha ajabu
"Nini kinaendelea? Kwanini naashindwa kuji control.....??? Aaah My God..."
Je nini kitaendelea?
Nakuja.........
Chapter 10
Keith alijipa moyo labda alihisi vile kwa sababu alikuwa amekunywa wine kidogo wakati anaangalia movie. Akaona asifikirie sana, aende
kupumzika
Jamani niwaambie tu, tangu siku ile nilikuwa nikishi na Keith kwa furaha kabisa. Ananijall sana, Anahakikisha nakula, nakunywa na napata kila kitu ninachohitaji
Pia wekeeed tulikuwa tunaenda kwa baba Keith kushinda huko mpaka jioni. Apo Baba Keith alikuwa anamtumia mama yangu na pesa ya matumizi kwaajili yake na Lulu. Imagine upendo waliokua wananionyesha hawa watu daah sio
pos
Basi bhana Keith akaniambia nianze clinic na Siku ya kwanza ya clinic tulienda pamoja. Nilipokuwa najaza kadi ya clinic, Keith akataka niandike jina lake k**a baba mtoto, nyle ila huyu
kaka
Baada ya clinic akaniambia tukatembee kidogo. "I think nikonunulie simu. Nikiwa ofisini sina amani cause nashindwa kuwasiliana na wewe
"Hakuna haja jamani
"Kuna haja kabisa. Lazima nikununulle simu"
Haya Tukaenda zetu mall Akaninunulia simu mpya ya laki 9 k**a sijasahau. Akaninunulia pia na line then akasave namba yake na namba ya
Baba yake tul
"Hauhitaji namba ya mtu mwingine kwenye simu yako isipokuwa zetu, au unataka ya Rico??" "Hapana jamani"
"Hahaha sorry nilikua natania tu alicheka maana nilishaanza kununa
Sasa Tukiwa bado tunanunua vitu vingine, tukakutana na Maya na Rico! Na wao walikua wanafanya shopping kule kule kwenye mall.
Rico kwanza kutuona tupo pamoja akaanza ku
jam
"Mbona mko pamoja?"
"Bro, hatujaonana kwa wiki mbili alafu unaanza maswali bila hata salamu?" Keith akasema vile makusudi
"Sorry. Mnaendeleaje?"
Keith akajibu "Tuko poa
"Woow tungejua na nyie mko hapa basi tungefanya shopping pamojal Au mlikua
mipango mingine"
Maya akauliza aki smile
"Nimempeleka Lola clinic then nikaona ni vizuri
kumnunulia simu ili tuwe tunawasiliana" Keith
alimibu
"Aaaaaa so sweet, Napenda jinsi unavyomjail
Lola" Maya alifurai
"Kwa kuwa Lola ni jukumu langu sasa, lazima
nimjal
Maya akamwangalia Rico aliyekuwa kimya lakini
ana hasira ya wivu akamwambia,
"Baby, si unaona Keith anavyoniall Lola Mpaka
raha yaani
"Ndiyo Rico akajibu k**a hataki vile! tia Maya
hakujali, alinigeukia akanambia
"Lola, sikupata nafasi ya kukujua vizuri kwa sababu ya situation lilyokuwepo
Nikamjibu "Mimi pia
Akaserna "Hakuna kilichoharibika. So mnaonaje
tukale chakula cha mchana wote wanne? It will
be fun
"Sawa hakuna shida nilikubali maana
nisingeweza mkatalia dada wa watu alieonyesha
upenda
Tullingia wote kwenye restaurant ya pale pale mall Tukakaa meza moja karibu kabisa na
dirisha
Rico alikuwa ananiangalia hanimalizi. Wiki
chache nilizokaa na Keith zilinibadilisha sana.
Nilionekana mzuri zaidi na hilo likaanza kumpa
stress
Basi Tukaagiza chakula huku tunapiga ston. Maya ndiye alikuwa anauliza maswali mengi, hasa kuhusu jinsi nilivyokutana na Keith,
"Miijuana vipi? Nataka kujua kila kitu Lola.
Uljisikiaje ulipomuoma Keith kwa mara ya
kwanza?" Maya akauliza
Nikaanza kusimulla jinsi nilivyo kutana na Rico lakini apo Maya anajua ni Keith. Alafu kila nilipokua nasimulia nilikua nikimwangalia Keith
machoni, mara tushikane mikono ili tu ile hadithi
lonekane ya kweli
"Nilikuwa naenda kisimani kuchota maji, ndipo
nikakutana naye. Nilipomuona nilihisi kitu
ambacho sikuwahi kuhisi kabla. Ni handsome mno huwezi amini kijiji kizima kilikua
kinamgombania
Maya akauliza "na mwishoni akakuchagua
wewe??? Weeeeeeh! So sweets
"Ndio japo aliniumiza sana alivyo niacha
kijgini
"Ooh usijali Lola, now upo hapa anakuhudumia
hakuna kitakacho haribika! I wish you all the
best
"Asante" nilishukuru nikiendelea kumtazama
Keith machoni
Weeeh mjomba Rico alihisi moyo wake
unaungua ndani kwa hasira. Ghafla akapiga
meza kwa nguvu Wote tukashtuka
"Baby, uko sawa?" Maya akamuuliza
"Ndiyo niko sawa alijakaza sana
"Sasa mbona umepiga meza namna lyo??
Unajua umeniogopesha"
"Maya acha maswali mengi, chakula icho
kimefika
akasema ivyo makusudi kubadilisha mada na ili tusimuulize tena kwanini alifanya vile.
Basi Mhudumu akaleta chakula na vinywaji pale kila mtu akapewa alicho agiza Chakula kilionekana kitamu, lakini nilipokula kijiko kimoja
nikahisi harufu kali ya kitunguu.
Mnajua kabisa mimi na kitunguu tulikua
hatupatani eeeeh... Acha nisitoke spidi spidi kwenda kutapikia chooni Keith kuona vile na
yeye akasimama kutaka kunifuata huko huko
chooni uzuri Maya alimzuiae
"Huwezi kumfuata huko hujui k**a ni choo cha
wanawake
"Najua, lakini anatapika" Keith alikuwa na
wasiwasi
"Unadhani shida ni nini??" Maya akauliza
"Ni chakulal kuna harufu kali ya kitunguu. Kwa
hali yake hapatani navyo kabisa
"Sawa, ngoja nimwangalie we relax"
Maya akaja chooni kuniangalia akawaacha Keith
na Rico peke yao pale mezani
"Kwa nini una wasiwasi sana? Inaonekana
unamjali sana Lola Rico uvumilivu ukamshinda
"Kwalyo sipwasi kujali
"Unapaswa, lakini sasa imezidil Bro Inaonekana kuna kitu kingine kinaendelea
"Unamaanisha nini?
"Keith unaanza kumpenda Lola?"
"Kwanini unaniuliza swali k**a lo? Au una wivu?"
"Kwanini niwe na wivu?"
"K**a hauna wivu basi sawa, kwa sababu
nidiona ulivyopiga meza kwa hasira Keith
skacheka kwa dharau
"Unajua wewe ni binamu yangu na i respect you! But sitaki uwe karibu sana na Lola
"Una maanisha nini Rico??? Coz usingetaka niwe
karibu nae usingemsogeza kwangu"
"Unajua ninamaanisha nini, Sitaki tupigane
"Kupigana? Don't worry, kwaajili ya Lola niko
tayari kupigana
"Mimi pia
Wanaume Walitazamana kwa hasira kubwa
k**a wanataka kuvunjana meno. Sasa Mimi na
Maya tulipotoka chooni, tukawakuta
wanatazamana k**a mbwa mwitu.
Nilihisi kabisa hapa kuna hatari dangerous! Na
k**a tungechelewa kidogo zingepigwa ngumi
palee mpaka majogoo
"Mbona mnaangaliana
k**a mnataka
kuvunjana pua?" Maya akauliza
"Noool Ni story tunapigal By the way Lola
unaendeleaje??" Rico akauliza
"Yuko sawa ni harufu tu ilimsumbua"
"K**a yuko sawa nafikiri tuondoke Keith
akanik**ata mkono kwa nguvu
Maya alisikitika "Kwaiyo mnaondoka bila hata ya
kula jamani??
"Yeah I think ni vizuri k**a Lola atarudi
nyumbani kupumzika"
"Ok! Mraonaje hil weekend mkaja nyumbani tule
pamoja lunch! Unajua Keith since ile siku ya
engagement yangu hujawai kuja kabisal Also
Aunt yako analalamika kukumiss all the timel Au
Rico hajakuambia lio??" AƤuliza Maya
"I know ila usijali tutakuja
Keith hakutaka stori nyingi, alinivuta mkono
tukaondoka
Namna alivyokuwa ananivuta nilihisi kuna kitu
kinaendelea. Alikuwa na hasira sana, na
tulipofika kwenye gari ikabidi nimuulize
"Kuna nini? Kwa nini una hasira?"
Akasema "Niko sawa"
"Au sababu ya Ricol Inaonekana mmepisharia
kauli nyie sio kawaida
"Tuachane na ilo! Kwanini Maya alipokuuliza jinsi
tulipokutana kwanini ukamsimulia hadithi yako
na Rico? Keith alilalamika na wivu juu nyie
huyuu
"Sikuwa na hadithi nyingine sasa ningejibuje"
Keith akavuta pumzi then akatulta kidogo. Yeye mwenyewe akajishangaa na kujiuliza mbona
wivu na hasira vimemkaba viie?? Utadhani
mume mwenye wivu
"Sorry just Mood yangu haipo sawa
"Sawa Twende nyumbani tupumzike"
Akatabasamu kidogo, akawasha gari tukasepa
zetu
Full 1000
Whatsp 0784468229
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Contact the public figure
Telephone
Website
Address
Mbeya