PrGiven Sanga
📖 Gospel Preacher
🎤 SDA Evangelist
🫂Christian Counselor
🌍 Winning Souls for Christ
⬇️ Sermons & Teachings
ACHA, TUBU, OGOPA, KIMBIA DHAMBI.
"UPATE UZIMA WA MILELE" MWISHO WA DHAMBI NI AIBU NA MAUTI YA MILELE."
1 Yohana 3:4 & WARUMI 6:23"
14/07/2026
Yohana 16:8
Naye akiisha kuja, huyo atauhakikisha ulimwengu kwa habari ya dhambi, na haki, na hukumu.
Yohana 16:13
Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake.
06/07/2026
Mkristo mwenzangu, Shetani anajua udhaifu wako; kwa hiyo ambatana na Yesu. Kaa katika pendo la Mungu ndipo utashinda kila jaribu. Haki ya Kristo peke yake yaweza kukupatia uwezo wa kupinga mawimbi ya uovu yanayofurika ulimwenguni. Uwe mwenye imani. Imani hufanya mizigo kuwa miepesi, na kukupa utulivu katika wasiwasi. Siri ya kutatulia matatizo ni kudumu kumtegemea Mungu. Tembea kwa imani katika mapito aliyokuagiza. Majaribu yatakuja, lakini usitishwe, endelea mbele. Majaribu yataimarisha imani yako, na kukufanya ufae kwa kazi yake. Maandiko matakatifu yameandikwa, si kwamba tuyasome tu, na kushangaa, lakini imani waliyokuwa nayo watumishi wa Mungu wa zamani, hata sisi tuwe nayo. Bwana atatenda mambo kwa wenye imani wa sasa, k**a alivyotenda kwa wale wa zamani bila kupungua.
KITABU: MASHUJAA WA IMANI.
Sura ya 13, Uk.140.1
By Ellen G. White
30/06/2026
ACHA, TUBU, OGOPA, KIMBIA DHAMBI. "UPATE UZIMA WA MILELE" MWISHO WA DHAMBI NI AIBU NA MAUTI YA MILELE.
Kila atendaye dhambi, afanya uasi; kwa kuwa dhambi ni uasi. 1Yohana 3:4
Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu. Warumi 6:23
23/06/2026
Mpendwa,
Mshukuru Mungu kwa hapo ulipofika leo.
Kuna watu wengi sana wanatamani wafike hapo ulipo wewe sasa hivi.
Kumbuka kipindi cha nyuma ulikuwa unaomba Mungu angalau ufike hapo.
Kwa hiyo acha kulalamika. Punguza tamaa, Shukuru kwa kidogo ulichonacho leo, huku ukiendelea kupambana kwa kesho iliyo bora zaidi.
Shukrani, huleta amani moyoni na hufungulia milango mingi ya baraka
Malalamiko huleta chuki, wivu, ubinafsi pamoja na kufunga milango yote ya baraka kisha hufungulia milango mingi ya kupoteza vyote ulivyonavyo.
Bwana Mungu akuzidishie na akuinue zaidi leo unapoAmua kubadili Mtazamo wako. Amina.
1 Wathesalonike 5:18
shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu.
21/06/2026
CHAGUA KUMTUMIKIA MUNGU KATIKA UJANA WAKO, UTAPATA FURAHA YA KUDUMU.
KUMBUKA: Mungu huchagua Watu Ambao wamekamilika tayari bali ni wadhaifu k**a wewe ila waliotayari kuacha uovu na kutumika, Kisha Yeye (Mungu) Anawapa Uwezo wa kufaa kwa utumishi wake, kwahiyo huchelewa kumtumikia Mungu, Anza hatua ya kwanza Leo.
Je, Unatamani kumtumikia Mungu na hujui utaanzaje, nipo hapa nikusaidie 0758017166
Pr. Shukuru Mswete From Njombe, with
Pr. Given Sanga From Mbeya.
26/05/2026
Sijui unapitia hali gani kwa Sasa katika maisha yako, Lakini nikutie Moyo Mpendwa katika hali yako hiyo Muite Mungu naye atakusikia.
Haijalishi Hali yako imedumu kwa muda mrefu kiasi gani, usikate tamaa, huenda Leo ndio mwisho wa jaribu lako.
kwa imani Omba tena muda huu, utapata ushindi.
Je, ni Ndoa ina changamoto, Yesu ataingilia kati.
Je, ni Ugonjwa, Yesu Kristo ni Mponyaji.
Je, Uchumi Wako ni changamoto, Mwite Yesu Anakusikia.
Ndiyo Anakupenda na kukujali sana, usichoke jipe Moyo, Mwambie haja ya Moyo Wako, Yeye ni Baba Yako Mwenye Upendo mwingi kwako. Atakuweka huru Leo.
Ninakuombea Ushindi kwa Jina la Yesu kristo, Amina.
08/05/2026
Jiandae kubarikiwa, Mualike na Jirani yako.
Panga kushiriki, Andaa kituo chako.
Mimi nitashiriki nikiwa kituo cha Kanisa la Mji Mwema Sda Church-Arusha, Wewe je?
01/03/2026
Hatimaye Uzinduzi wa ONEVOICE27 TRVF, umekamilika.
Sasa Kazi ya utume inaendelea.
Kushoto ni Paul Ndaro Mkuu wa Huduma, Kulia ni Gidion Mazengo Mkurugenzi wa Shule ya Sabato, na katikati ni Given Sanga Mzee wa Kanisa, Mji Mwema Sda Church Arusha.
Uzinduzi ulifanyikia Njiro Sda church Arusha, 28February2026.
Bwana Atupatie Roho Mtakatifu tumalize kazi.
Click here to claim your Sponsored Listing.